Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya
moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na
serikali za mitaa.
Msemaji wa chama hicho Antonio Muchanga amesema kwamba kumekuwa na
ukiukwaji wa taratibu katika upigaji kura huo na udanganyifu wa kura.
Matokeo ya awali katika uchaguzi huo zinaonesha kwamba chama cha FRELIMO
kinaongoza katika uchaguzi huo.Wakati haya yakitokea kumekuwa na
uvunjifu wa amani wakati polisi walipo ingia katika ghasia na
waandamanaji waliokusanyika nje ya vituo vya kupigia kura kufuatilia
zoezi la uhesabuji wa kura .
Ingawa wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Zimbabwe wanaeleza kuwa pamoja na
yote hayo,uchaguzi huo ulikua huru na wa haki.ikumbukwe kuwa chama cha
Renamo na chas Frelimo walipigana vita ya wenyewe kwa wenyewe
vilivyomalizika mnamo mwaka 1982.(BBC)
No comments:
Post a Comment