Harakati
za kutetea haki za wanawake nchini Saudi Arabia kutaka na wao wapewe
haki ya kuendesha magari kama wanaume zashika kasi kubwa, sasa
wanaadhimisha mwaka mmoja wa kupinga amri ya kwatazo kwa wanawake
wasiendeshe magari na wanawake wanapinga na kuendesha magari kinyume na
amri waliowekewa.
Kwenye mitandao ya kijamii kumetolewa miito
kadhaa ya kuwataka wanawake wapinge amri hiyo kwa wingi na waendeshe
magari,wanaharakati wanaopinga amri hiyo wameiambia BBC kuwa harakati
zao zinaendelea vizuri na mwito umepokelewa vyema ingawa mwaka huu
utatumika kuongeza uelewa zaidi juu ya suala hilo.Nayo mamlaka ya Saudi Arabia imetoa onyo kali na kuwataka wasaudia wote wasijihusishe na mgomo huo,na mmoja kati ya wanaharakati ambaye ana ushawishi mkubwa ameelezea mgomo huo uloanza mwaka wa jana kuwa umeitia hofu kubwa serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment