Monday 6 October 2014

IRINGA::NAPE ; JIMBO LA IRINGA MJINI MPANGAJI WAKE KODI YAKE IMEKWISHA LAZIMA ATOKE

Kamanda wa UVCCM mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  akisalimiana na katibu wa itikadi na uenezi Taifa  Nape Nnauye  leo 
Vijana  wa CCM  wakijiandaa kumvisha skafu katibu mkuu wa CCM taifa Bw Kinana  leo baada ya  kuwasili  Iringa kwa ziara ya  siku 6 
Kinana  akivishwa  skafu  
Mbunge wa  jimbo la Isimani  Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu wa bunge  kulia akisalimiana na katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana lea  baada ya  kuanza  ziara yake  wilaya ya Iringa 
Mbunge wa  jimbo la Kilolo na Prof Peter Msolla  kulia akisalimiana na Kinana 
Kinana  akisalimiana na viongozi wa CCM wilaya ya Iringa 
Kamanda wa UVCCM mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  akisalimiana na katibu wa itikadi na uenezi Taifa  Nape Nnauye  leo 
Mdau wa matukiodaima Bi Shirima  akisalimiana na Kinana  leo 
kada wa CCM jimbo la Iringa mjini Dr Yahaya  akisalimiana na Kinana 
wana CCm wakiwa katika  viwanja vya CCM wilaya ya Iringa  vijijini leo 
Nape  kulia akiwa na  wana CCM Iringa  leo 
Wana CCM wakiwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini leo 

Askari  wakiwa katika  ulinzi mkali 
Kinana  akifungua ofisi ya  CCM wilaya ya Iringa  vijijini baada ya  kukarabatiwa  upya 

 

KATIBU  wa  itikadi na uenezi  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape  Nnauye  ambana mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amfananisha na mpangaji na  kuwa kodi yake ya  kuendelea kudumu katika  jimbo  hilo  imekwisha  hivyo ajiandae  kufungasha vilago ili  uchaguzi mkuu 2015 akabidhi jimbo hilo CCM.

Nnauye  alitoa kauli hiyo  leo  mara  baada ya  kuwasili katika  jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya  ziara siku 6 mkoani Iringa na  katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana

Alisema  kuwa CCM imekusudia  kuyarejesha majimbo  yote  yaliyochukuliwa na  wapinzani  mwaka 2010  likiwemo jimbo la Iringa mjini  linaloongozwa na mbunge  wake mchungaji Msigwa na  kuwa  uwezo na nia ya  kulikomboa jimbo  hilo  upo hivyo ni lazima wapangaji  wote kuanza kukaa mkao wa  kuondoka .

" Tutakuwa na  ziara  mkoa wa Iringa kwa muda wa  siku  6 na hadi  tukimaliza  ziara  yetu hapa  Iringa  chama  chetu  kitakua  juu  zaidi hivyo  nawaombeni fikisheni  salam kwa  wapangaji kuwa kodi yao  imekwisha  na  hivyo  tunahitaji watuajie jimbo  letu na  kwa sasa  hatuna mpango wa kupangisha   tena" alisema Nnauye  huku akishangiliwa na umati wa  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  waliokuwepo katika mapokezi hayo.

Akizungumza na  wanachama   hao  kabla ya  kuzindua  ofisi  ya CCM wilaya ya  Iringa  vijijini  Iliyofanyiwa  ukarabati upya katibu  mkuu  ,Abdulrahman Kinana alisema  kuwa CCM imeendelea  kukamilisha utekelezaji wa ahadi zake  ambazo ziliahidiwa  mwaka 2010  na  kuwa  hadi sasa  sehemu kubwa ya ahadi hizo  imetekelezwa na kilichobaki ni  kuwaomba  watanzania  kuendelea  kuwa na imani na CCM ili mwakani 2015  kuendelea kuchagua chama  hicho.

Kinana  alisema  kuwa  kazi  kubwa  imeendelea  kufanywa na  viongozi wa  CCM na  serikali yake  chini ya Rais Jakaya  Kikwete  katika  kuona  watanzania  wanaendelea kunufaika na matunda  ya serikali yao kwa kusogezewa  maendeleo karibu  zaidi na kutaja  miradi mkubwa ambayo imetekelezwa  kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara  za lami  kila kona ya nchi  hii.

" Tunazunguka  kuendelea  kukijenga  zaidi  chama lengo ni kuona  watanzania wanaendeleo kukiamini chama na  kuhamasisha  zaidi wananchi kujitokeza  kwa  wingi  katika chaguzi za  serikali za mitaa mwaka huu  ili  kuchagua  viongozi  wanaotokana na  CCM kwani ndicho chama  chenye mapenzi ya kweli ya  kuliongoza Taifa hivyo  hakuna  sababu ya  watanzania  kutokiamini  chama cha mapinduzi"

Pia alisema  kuwa mbali ya  CCM kuendelea  kukamilisha utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi bado chama  hicho kina mpango mzuri wa  watanzania  ili kuona mwakani 2015 chama  kinashinda na hapa  watanzania  wategemee  ahadi  nyingi  na kubwa zaidi  ya zile za mwaka 2010.

Awali  Kinana alimpongeza  aliyekuwa mjumbe wa  bunge la katibu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  kwa  jinsi  alivyowawakilisha  vema  wakazi wa mkoa wa Iringa na  watanzania kwa ujumla katika  bunge la katiba na  kuwa alikuwa akimfuatilia na kufurahishwa na uwezo wake mkubwa wa  kujenga  hoja.

Kwa upande wake Msambatavangu  akimkaribisha katibu mkuu  huyo alisema  kuwa  mbali ya  kuwa  ziara  hiyo inaanzia jimbo la Kalenga kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini ila mbunge  wake Bw Godfrey Mgimwa hatafanikiwa  kushiriki kutokana na heshima kubwa ambayo spika wa bunge Anne Makinda   amempa mbunge huyo kwa kumteua kuwa miongoni mwa  wabunge  wachache vijana kwenda  nje ya Tanzania  kushiriki mkutano mkuu wa dunia wa  wabunge  vijana.

No comments:

Post a Comment