Monday, 25 August 2014

KAMA HAMJUI VILE:::ONA PICHA ZA MKAUSHO WA RIHANNA KWA CHRISS

Rihanna ampigia mikausho Chris Brown kwenye mechi ya basketball

0
Chris Brown na Rihanna wamejikuta wapo karibu kwa umbali mdogo sana walipokua kwenye mechi ya basketball kwa ajili ya kuchangia taasisi ya CC Sabathia na Robinson Cano. Mechi hiyo ilikuwa ya mafanikio kwa kuingiza zaidi ya dola milioni 1 lakini story kubwa sio hiyo.
Kitu kilichotengeneza headline ni pale Rihanna alivyoonyesha mikausho mikali hasa wakati Chris Brown anapokuwa karibu yake wakati wa mechi hiyo. Kuna wakati Chris Brown alikuwa anawasalimia mashabiki waliokuwa wamekaa karibu na kiti cha Rihanna na picha zilipigwa Rihanna anaonekana ameweka mikausho na kuangalia pembeni.
Mechi iliisha vizuri na picha ya hapo juu imekuwa maarufu sana kwenye instagram hivi sasa.
1
2
3
4
5

Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana

Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana

 25 Agosti, 2014

Wapiganaji wa Renamo nchini Msumbiji
Habari kutoka Msumbiji zinasema serikali ya nchi hiyo imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo ili kumaliza uhasama kuelekea uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya chini kwa chini kati ya wafuasi wa Renamo wenye silaha na majeshi ya serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo walijitoa katika mkataba wa amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, mkataba ambao ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Wiki iliyopita ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza kuwaachilia wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi karibuni.
Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani.

KESI KIFO CHA KANUMBA, SURA MPYA!

KESI KIFO CHA KANUMBA, SURA MPYA!

 
Stori: Shakoor Jongo
Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea.
 
Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi (open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.
 
Wakili maarufu Bongo anayemtetea 'Lulu', Peter Kibatala.
YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.
ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa mahakamani.
 
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.
 
Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.
“Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

BURUDANI NA PICHA:Picha 8 mpya za P Square

Picha 8 mpya za P Square zinazoangaliwa sana kwenye internet hivi sasa.

ddd
Peter na Paul mapacha wa P Square wanakaribia kutoa album yao ya sita na hivi sasa wametoa picha zao mpya ikiwa ni moja ya promotion kuelekea uzinduzi wa album hiyo.
Kama wewe ni shabiki wa P Square enjoy kucheki hizi picha.
0
1
2
3

5
6
7

DIMPOZ AWACHANGANYA JOKATE, VENESSA MDEE!

DIMPOZ AWACHANGANYA JOKATE, VENESSA MDEE!


 Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money, Ijumaa Wikienda limeinyaka.
 
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akipozi kimahaba na Vanessa Mdee, 'V-Money'.
Kikizungumza na gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa Bongo, chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani.
“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema:
 
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akishow love na Jokate Mwengelo ‘Kidoti’.
“Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa mshikaji tu.”
Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.

Sunday, 24 August 2014

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JESHI

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JESHI
  August 24, 2014

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais…
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Oficer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli jana.
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.

AJALI:AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA COASTER MOROGORO

AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA COASTER MOROGORO

Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali.
Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa ndani ya gari.
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mgogo, ambaye ni dereva  wa bodaboda amegongwa gari na kufariki papo hapo, jioni hii mkoani Morogoro.Gari iliyomgonga dereva huyo ni aina ya Coaster  inayofanya safari ya Kihonda Mjini mkoani humo.

MPASUKO CCM IRINGA

MPASUKO CCM IRINGA


Mwenyekiti wa CCM Iringa, Jesca MsambatavanguJOTO la kuwania ubunge Iringa Mjini, katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani limeanza kuwagawa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa.
Mgawanyiko huo umekua zaidi baada ya kutangazwa kuwa sherehe za kumsimika kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa huo, zitafanyika Agosti 23 na Wilaya ya Iringa Mjini Agosti 29 mwaka huu.
Awali ilipangwa sherehe hizo zifanyike kwa siku moja lakini inadaiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa, Jesca Msambatavangu, ameingilia mchakato huo.
Inadaiwa anafanya hivyo kupunguza nguvu ya kujizolea umaarufu kamanda wa vijana wilaya ya Iringa Mjini atakayesimikwa Fredrick Mwakalebela anayetajwa kutaka kuwania ubunge kama inavyotajwa kwake.
Inaelezwa tishio la Msambatavangu ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ameshaanza maandalizi hayo na tishio kwake ni Mwakalebela.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Mwenyekiti huyo juu ya kuingilia mchakato wa sherehe hizo lakini hakuwa tayari kupokea wala kujibu ujumbe mfupi aliotumiwa.
Katibu wa CCM Iringa, Hassan Mtenga, alikana mkoa kuingiza mkono wake kwenye sherehe hizo kwakuwa kila kitu hufanywa na UVCCM.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Katibu wa UVCCM, mkoa Iringa Al Haidary Fumu, alisema wameamua kutenganisha sherehe hizo ili kutoa fursa ya kuzifanya kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa Kamanda wa UVCCM, Salim Abri Asas, akishaapishwa yeye ndiye atakuwa na jukumu la kumuapisha wa wilaya ambaye naye atawapisha wa kata.
“Mimi sijui kama kuna sarakasi za kuwania ubunge katika jambo letu, najua kufanya hivyo tutaongeza gharama lakini ni lazima tufunge mkaja,” alisema.
Naye Mwakalebela alisema kutenganishwa kwa sherehe hizo kutaongeza gharama kwakuwa maandalizi ya pamoja yalishafanyika.
“Haya mambo ya siasa yana vitu vingi, mimi naona wana CCM tuna kila sababu ya kuepuka kushughulikiana katika kuwania ubunge,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

MAMBO YA KATUNI HAYO:CHANGAMSHA AKILI KIDOGO

PICHA YA WIKI:VIPI KAJALA ALIPENDEZA?

Msanii wa Bongo Muvi Kajala akifuatilia shoo kwa karibu zaidi

HAYO NDO MAMBO YA SERENGETI FIESTA WAJA LEO(TANGA)

SERENGETI FIESTA YAFUNIKA MKOANI TANGA

Mshindi wa Serengeti Super nyota 2013, Edo Boy akifungua burudani.Young killer akikonga nyoyo za mashabiki katika Tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
Mr. Blue akiwapagawisha washabiki jukwaani katika tamasha hilo.Recho akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta mkoani Tanga.Tunda Man naye akifanya yake.Khadija Maumivu akifanya maajabu jukwaani.Shabiki akimkubali jux kwa shoo aliyoionyesha....Linnah naye akilishambulia jukwaa.
...Ni MO Music ndani ya usiku wa Tamasha la Fiesta mjini Tanga.Msanii wa Bongo Muvi Kajala akifuatilia shoo kwa karibu zaidi.Linnah akiwa na wanenguaji wake.Ommy Dimpoz akiwajibika mbele ya mashabiki zake.Madee akifanya makamuzi jukwaani.Vannesa Mdee akiliteka jukwaa usiku wa Fiesta mjini Tanga.

HUYO NDO MKUU WA WILAYA TANGA......HAPO VIP?


Ruge akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwenye Tamasha la Serengeti FiestaRuge akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya, Halima Omar Dendegu (kulia).