Wednesday, 3 September 2014

HII NDO KICHENI PATI YA LUCY KOMBA...FUNIKO...

Posted by GLOBAL on September 3, 2014
Stori: Imelda Mtema
NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.
Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.
Akiwa kwenye usafiri wa baiskeri ya matairi matatu maarufu kama 'Guta'.
Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.
Akiingia ukumbini kwa mbwembwe.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.

SAMAHANI KWA HIZI PICHA..AJALI AJALI..MTOTO AGONGWA NA GARI SOWETO MBEYA...

Wednesday, September 3, 2014
MTOTO AGONGWA NA GARI ENEO LA SOWETO LEO , DEREVA AKIMBIA.

Mtoto huyo ukiwa kando muda mchache baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Double Cabin ambayo ilikimbia baada ya kufanya tukio hilo
Baadhi ya wasamalia wema wakiwa wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa mtoto huyo 
Baadhi ya wasamalia wema wakimchukua mtoto huyo kwa ajili ya kuupeleka hospitali
 Mashuhuda

 Tukio hili limetokea mida ya saa Tano asubuhi leo ambapo chanzo cha ajali hiyo ni Mwendo kasi wa Gari hilo ambapo halikuchukua tahadhari na kusababisha kugongwa kwa Mtoto huyo 

Picha na Mbeya Yetu.

Tuesday, 2 September 2014

KWA MSAADA WA MUUMBA TU>>VITA DHIDI YA EBOLA YASHINDIKANA...

MSF:Vita dhidi ya Ebola vinashindikana

 2 Septemba, 2014
Nchini DRC watu 31 wamefariki kutokana na Ebola
Rais wa shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka, MSF Juliana Liu, ameambia mkutano wa umoja wa mataifa kuwa vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi vinashindikana.
Akiongea mjini New York, alisema kuwa miezi sita tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone, jamii ya kimataifa imeshindwa kukabiliana na tisho la kuenea kwa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 1500 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa huo kuwahi kuripotiwa tangu kugunduliwa kwake katika kanda ya Afrika ya kati karibu miaka 40 iliyopita.
Wakati huohuo kuna hofu kwamba, mlipuko wa Ebola unatishia mavuno ya wakulima mashambani katika kanda ya Afrika Magharibi.
Shirika la kimataifa la chakula na kilimo limeelezea wasiwasi kuhusu hali ya chakula nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, nchi tatu ambazo ziliathirika zaidi kutokana na Ebola.
Shirika hilo limesema mavuno ya Mchele na Mahindi yataathirika zaidi katika msimu huu unaokuja.
Upungufu wa chakula unatabiriwa kuwa mbaya zaidi katika miezi michache ijayo.

Mrembo akataa kurejesha taji lake

Mrembo akataa kurejesha taji lake

 2 Septemba, 2014
Mya Myat anataka aombwe msamaha na waandalizi wa shindano la taji hilo
Mshindi wa taji la urembo nchini Burma aliyenyang'anywa taji lake wiki iliopita ,amekataa kurudisha taji hilo kwa waandalizi wa mashindano hayo Korea Kusini.
Katika kikao na wanahabari,Mya Myat Noe amesema kwamba atarudisha tu taji hilo lenye thamani ya dola 100,000, ikiwa ataombwa msamaha na waandalizi wa mashindano hayo.
Bi May alishinda mashindano ya Miss Asia Pacific World mwaka 2014 iliyofanyika mwezi Mei mjini Seoul.
Wiki jana waandalizi walimshtumu kwa kukosa shukrani na kutokuwa mkweli.
Bi May ni mshindi wa kwanza wa shindano hilo nchini Burma , kulingana mwandishi wa BBC Jonah Fisher.
Waandalizi wanasema mshindi huyo aliwadaganya na kuwadharau madai aliyoyakanusha
Mrembo huyo alidaiwa kutoroka na taji hilo, madai ambayo ameyakanusha.
Bi May aliwaambia wanahabari kuwa alilazimishwa kudanganya kuhusu umri wake na waandalizi hao pia walimshurutisha kuwekwa matiti bandia.
Hata hivyo amekana madai ya kuwa alitoroka na taji hilo akisema kuwa aliabiri ndege kuelekea Myanmar bila kufahamu kuwa alikuwa ashavuliwa taji hilo.
Waandalizi walidai kuwa mwanadada huyo aliwadanganya na kuwadharau, ila hawakutoa maeleo zaidi.
Baadaye ilifahamika kwamba kulikuwa na mtafaruku kati ya mamake May na waandilizi hao kuhusiana na vipi Bi May anaweza kusimamiwa .
CHANZO BBC 

HII NDO RIPOTI YA MADAWA YA KULEVYA KUTOKA KWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

OFISI YA MKEMIA MKUU YATOA TAARIFA YA DAWA ZA KULEVYA YA MWAKA 2013 NCHINI

Posted by GLOBAL on September 2, 2014
Kushoto ni  Mkuu wa kitengo cha Jinai Kemia, Elias Mulima pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Makosa ya Jinai na Vinasaba, Gloria Omary wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakimsikiliza Gloria Omary alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo.
Sehemu ya waraka huo
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali kupitia maofisa wake, leo imetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo uliopo Posta jijini Dar es Salaam.

Boko Haram wauteka mji muhimu Nigeria

Boko Haram wauteka mji muhimu Nigeria

 2 Septemba, 2014
Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.
Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.
Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.
Zana za kivita zinazotumiwa na wapiganaji wa Boko Haram
Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.

MAMBO YA NDOA HAYO>>>NDOA YA MWALIMU AIBU KANISANI

NDOA YA MWALIMU AIBU KANISANI

Posted by GLOBAL on September 2, 2014
Stori: Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
MWALIMU mmoja wa Shule ya Msingi Makurumla iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Maria Samuel Hoza, amejikuta akiaibika vibaya baada ya mumewe, Bryton Muhanje kumkuta akiwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa nyingine kwenye Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga, Jumamosi iliyopita.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Makurumla, Maria Samuel Hoza akiwa katika harakati za kufunga ndoa yake ya pili.
Gazeti hili lilimshuhudia Muhanje, akiingia kanisani na kwenda moja kwa moja mbele ya altare na kumzuia Padri Richard, ambaye alikuwa amemaliza kufungisha ndoa ya kwanza, asifanye hivyo kwa maharusi wanaofuata kwa vile ni batili.
Chanzo chetu makini cha habari kililidokeza gazeti hili juu ya kuwepo kwa mpango wa mwanamke ambaye yupo katika ndoa, kutaka kuolewa tena na mtu mwingine bila mumewe kujua. Kufuatia ‘tip’ hiyo, kikosi kabambe cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilifanikiwa kupata namba ya mwanaume huyo na kufanya naye mawasiliano ili kujua ukweli wa madai hayo.
Mume wa Maria Samuel Hoza, Bryton Muhanje (kulia) akitoa pingamizi la ndoa ndani ya Kanisa Katoliki la Kigogo Luhanga.
Muhanje alikiri kupata tetesi hizo, lakini alikuwa akihaha kujua sehemu itakakofanyika harusi hiyo na kwamba timu ya vijana wake ilijipanga kuhakikisha anafahamu eneo hilo.Baadaye aliwaeleza OFM kuwa alikuwa alisikia ndoa hiyo ingefungwa Magomeni, hivyo alikodi pikipiki sita zilizofanya doria katika makanisa yote yaliyopo eneo hilo ili kujua mkewe alikuwa kanisa gani.
Pamoja na hivyo, mwanaume huyo pia alikwenda hadi shule anayofundisha mwalimu huyo na kwa kuwa hawamfahamu, alijitambulisha kama ndugu yake na kwamba alikuwa anaomba kujua kanisa ambalo (mkewe) atafunga ndoa, kwani ameelezwa kuwa lipo Magomeni lakini hakuelewa ni lipi.
“Wanafunzi wa pale wakaniambia siyo Magomeni, bali ndoa inafanyika Kigogo Luhanga, ndipo nilipowasiliana na wenzangu na kuwaeleza habari hiyo, nikaongozana na baadhi ya wanafunzi ambao pia walikuwa wanakwenda kwenye harusi hiyo,” alisema.
Padri Richard akitoka nje ya kanisa hilo mara baada ya pingamizi la harusi kutokea.
OFM ikiwa tayari kwa kunasa tukio hilo, walikuwa wameshatinga kanisani hapo mapema na kushuhudia maharusi watatu tofauti wakijiandaa kufunga ndoa, wakiwemo Maria na mwenzake.
Ratiba ilionyesha kwamba ndoa ya wawili hao ilikuwa ya pili, hivyo mara tu zamu yao ilipofika na Padri Richard kuanza kutoa risala ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia, wote walionekana kuwa na bashasha ya siku hiyo muhimu ya kuungana.
Ghafla bila kutarajia, wakati wasaidizi wa padri wakimletea kibakuli chenye pete ya ndoa, Muhanje alijitokeza na kumuomba mchunga kondoo huyo kusitisha zoezi hilo kwa vile anayetaka kufunga ndoa, ni mke wake halali.
Makamanda wa Polisi wakiwa nje ya kanisa tayari ili kutuliza ugomvi.
Akiwa amepigwa na butwaa, padri huyo alilazimkika kwanza kumuuliza bibi harusi kama anamtambua mtu aliyesimama mbele yake, lakini akiwa mkavu alikataa akidai hajawahi kumuona maishani mwake.
Mume akiwa ameongozana na mpambe wake aliyesimamia ndoa yake, alimuomba padri atoe vielelezo kuthibitisha ukweli huo na baada ya kupewa nafasi hiyo, alionesha picha mbalimbali za siku ya harusi yao, nakala ya cheti cha ndoa na akaomba pia aruhusiwe atoe kompyuta yake mpakato ili achezeshe video ya siku hiyo ya Oktoba 29, 2009 alipofunga naye ndoa katika Kanisa la KKT Kimara Korogwe, Dar.
Kwa ushahidi huo, padri huyo alikubaliana naye na kusimamisha zoezi hilo na kuwataka kuongozana kwenda ofisini kwa mazungumzo zaidi. Baada ya mazungumzo marefu ofisini, padri huyo alikubaliana na hoja za mume na hivyo kusitisha zoezi hilo, akidai mwanamke huyo hawezi kuolewa kwa mara ya pili.
Ilifahamika baadaye kuwa Maria, ambaye amezaa mtoto mmoja na Muhanje, alitumia jina la Neema Stanley Hoza katika kusudio lake la kufunga ndoa ya pili.
Baadhi ya wapambe na wanandugu wakirudi makwao mara baada ya ndoa kubatilishwa.
Hata hivyo, wakati kukiwa na sintofahamu ya tukio hilo kanisani, ghafla kikosi cha askari polisi wakiwa katika ‘difenda’ kilitia timu kuhakikisha usalama unakuwepo.Askari hao walisema walipewa taarifa za kuwepo kwa tukio ambalo lingeweza kuhatarisha amani na ili kuhakikisha jambo hilo linatokea, waliondoka na maharusi wa pili baada ya taratibu za kikanisa kukamilika.
Baada ya tukio hilo, Muhanje alisema alimuoa mkewe mwaka huo, baada ya kuwa ameishi naye kinyumba kuanzia mwaka 2005.“Baada ya kukaa naye kwa miaka minne, tukaamua kufunga ndoa mwaka huo wa 2009 na baada ya hapo, yeye akaenda kufanya kazi ya ualimu Lushoto katika Shule ya Shambalai.
Picha ya ushahidi ikionesha ndoa ya halali kati ya Bw. Bryton Muhanje na Mwl. Maria Samuel Hoza.
“Mwanzo tulikuwa na maisha mazuri tu na katika kipindi hicho, nilijitahidi kumfanyia utaratibu wa uhamisho ili aje Dar na kufanikiwa kumleta mwaka 2012 na alipangiwa Shule ya Makurumla.“Baadaye kidogo hali yangu kifedha ikayumba, ndipo matatizo yalipoanza kwani kitendo cha kutegemea hela za mshahara wake katika maisha kikamshinda, akaanza kutafuta visa mbalimbali ili mradi mimi nimpige apate sababu ya kuondoka.
“Alifanya vituko vingi sana, wakati mwingine alifunga mlango na kuondoka na funguo na kwenda kwa dada yake na kulala huko huko, wakati mwingine aliamua tu kuvunja vitu bila kujali hadi mwaka jana mwezi wa nne alipoondoka moja kwa moja kwenda kusikojulikana.“Siku chache zilizopita ndipo nilipopata habari kwamba ana mpango wa kuolewa, ndipo nikaanza kufuatilia ili nijue.
“Nilipokuwa pale kanisani wakati wa kuzuia ndoa, yule mwanaume aliyetaka kumuona mke wangu, alinitishia kuwa atanikomesha, nimeenda polisi kuripoti maana siwezi kujua atafanya nini na nimefungua jalada lenye namba MAG/RB/8452/2014 KUTISHIWA KUUA KWA MANENO.”

UKATILI WA KIJINSIA HUO>>MUME NA MTOTO WAMWAGIWA MAJI YA MOTO MWILINI...

MUME: MKE WANGU KANICHOMA KWA MAJI YA MOTO NA MWANANGU

Posted by GLOBAL on September 2, 2014
Ni hali ya kusikitisha na kustaajabu kwa  jamii baada ya Tunu Kimaro kummwagia maji ya moto mumewe, William Mushi (32), mkazi wa Mabibo  jijini Dar es Salaam pamoja na mtoto wake mchanga.
Bw. William Mushi (32), aliyemwagiwa maji ya moto na mke wake, Tunu Kimaro.
Tukio hilo la kikatili lilitokea Agosti 15, mwaka huu nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam na lilishangaza majirani kutokana na Tunu kudaiwa kuchukuwa maji ya moto yaliyokuwa yanachemka na kuwamwagia bila huruma.
CHANZO NI MTOTO
Akisumulia mkasa huo Mushi alikuwa na haya ya kusema:
“Mke wangu anaitwa Tunu Kimaro ana miaka 23. Alinimwagia maji ya moto baada ya kumkuta mwanangu wa miezi saba hali yake ya kiafya ikiwa siyo nzuri, nilipokuwa naondoka asubuhi nilimuagiza ampeleke hospitali.
Mtoto mchanga wa Bw.William Mushi aliyeunguzwa pia na maji ya moto.
“Baada ya kufika nyumbani na kumkuta mwanagu Ivan amenyong’onyea, nilipomuuliza mke wangu sababu za kutompeleka hospitali alinijibu majibu ya kijeuri kama siyo mke wangu na mtoto siyo wake.
  “Niliendelea kumtaka anieleze sababu ya kutompeleka mtoto wetu hospitali ndipo aliposema ngoja anioneshe.
Shangazi wa mtoto mchanga akikiuguza.
“Alitoka nje kumbe alikuwa  anachemsha maji, alikuja nayo yakiwa kwenye sufuria aliloshika kwa kitambaa, akatumwagia mimi na mwanangu ambaye anajua hajui chochote,” alisema Mushi.
LENGO LAKE KUTUUA
Akaongeza: “Naamini lengo lake lilikuwa ni kutuua na si vinginevyo. Ni jambo la kusikitisha sana na majirani nao walisoneneshwa na tukio hili baya.
Muuguzi aliyejitambulisha kwa jina la Cristene Chilambo akimbeba mtoto huyo.
“Ni vyema angesubiri niwe peke yangu, lakini alitumwagia maji akijua kuwa nina mtoto tena mchanga. Nashukuru Mungu kwa sababu nilijitahidi kumkwepesha na maji yale ya moto, lakini yalimpata na kumuunguza kama unavyoona.”
AKIMBILIA POLISI
Mume huyo alisema: “Baada ya mke wangu kutufanyia kitendo kile alikimbilia polisi na kudai eti kuna mtu amemshambulia.
“lakini baadaye nilipopelekwa polisi kuchukua PF 3 (hati ya kuruhusu nitibiwe), askari walishangaa kuona nilivyounguzwa mimi na mwanangu na walipigwa na butwaa nilipowaeleza kuwa aliyefanya hivyo ni mke wangu.
Mtuhumiwa Tunu Kimaro.
“Askari polisi baada ya kupata ukweli ilibidi mke wangu awekwe ndani ili aweze kutoa maelelezo ilikuwaje. Nashindwa kuelewa kama sababu ni kumlaumu kwa kutompeleka hosptali mtoto wetu au kuna jambo lingine.
 “Nahisi kuna mtu anamtia kiburi kwa sababu mke wangu hakuwa na tabia hizi za kujibu kijeuri na moyo wa kikatili, watu wengine walidhani huyu mtoto yupo kwa mama wa kambo,” alisema Mushi.
Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mtoto amelazwa katika kitengo cha watoto walioungua.
AFISA WA POLISI ANENA
Mama wa mtoto huyo anashikiliwa  katika Kituo cha Polisi Urafiki, jijini Dar es Salaam ambapo afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwa kuwa siyo msemaji alisema upelelezi ukikamilika ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
MUUGUZI ANASEMAJE?
Muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Cristene Chilambo, alishangazwa na kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo na kuongeza kuwa hali ya mtoto inaendelea vizuri.
“Mtoto huyu hana kosa lolote, mama yake amekosea sana na naomba taasisi za haki za binadamu zifanyie kazi ukatili huu maana huu ni unyama na ukatili wa aina yake,” alisema Chilambo.

HIZI NDO PICHA ZA SHOW YA DIAMOND ILIYOHARIBIKA UJERUMANI..JIONEE

Picha za Kilichotokea Baada ya Diamond Kupelekwa Kwenye Show Saa Kumi Alfajiri Ujerumani.

Mmiliki wa hit single ya ‘mdogo mdogo’ Diamond Platnumz anahusika tena kwenye zile habari zinazoongelewa sana ambapo time hii imetokea Stuttgart Ujerumani.
Alitakiwa kufanya show weekend iliyoisha sehemu inaitwa Stuttgart lakini ikashindikana baada ya kudai kucheleweshwa na Promota na badala yake akampeleka kwenye ukumbi saa kumi alfajiri.
Inasemekana mashabiki wenye hasira waliosubiri kuanzia saa nne usiku walianza kufanya fujo kwa kurusha chupa na kuvunja vyombo vya muziki vilivyokua vimefungwa hapo kwa madai pia kwamba vilikua vibovu ambapo inataarifiwa kwamba Ma Dj wawili walijeruhiwa kwa kiasi kikubwa pamoja na vyombo vyao kuharibiwa.




Diamond alipowasili saa kumi alfajiri tayari mashabiki walikua wametoka nje kama hivi ambapo mmoja wa mashabiki waliokuwemo kwenye tukio hilo amesema Polisi walilazimika kuingilia kati na Diamond hakudhurika.

JIFARIJI NA HII:::HARUSI YA KIPEKEE NDANI YA MAJI...WAPI?Soma chini


Harusi ya kipekee ndani ya maji


Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''
Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Hawa ni wateja wake, Lin Enxiao na He Huan.
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote.
''Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,'' asema YY. "sisi tulitaka kitu tofauti. ''
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, '' asema Lamea.
"sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.''
Sio mara ya kwanza kuona watu wakipigwa picha wakiwa ndani ya maji wala China sio nchi ya kwanza kuanzisha mtindo huu, ila China imeanza kuitumia kwa njia ambayo imewapendeza wengi.
'Vipodozi visivyoharibiwa na maji'
Kuna studio nyingi za picha zinazotoa huduma hii nchini China, soko lina ushindani mkali lakini baadhi ya wafanyabiashara hawana maadili ya kazi.
''Baadhi ya wafanyabiashara wana uelewa wa kazi na ni wabunifu lakini huwa hawadumu kwa sababu wanakosa maadili ya kazi. ''
Duka hili la Mr Wedding lina wabunifu wengi ambao huwa wanawapendekezea maharusi namna ya kupigia picha , wakitumia muda mwingi kuwapodoa na kuwapamba nywele maharusi.
"tunapendekeza bibi harusi akiwa ndani ya maji avalie gauni nyeupe na ndefu. Na sisi hutumia vipodozi ambavyo haviwezi kuharibiwa na maji. ''
Kisha maharusi hawa wanatembezwa na kuingizwa ndani ya tenki ya maji ambako wanapigiwa picha.
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.
Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.
bbc swahili...

MAMBO YA MTANI HAYO...WENGINE MIPANGO YA HELA WENGINE NA OKWI...YANGA NA CRDB

Mkataba mpya walioingia Yanga na benki ya CRDB

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dr Charles Kimei (kulia), akimkabidhi kadi mpya ya uanachama wa klabu ya Yanga SC mjumbe wa bodi ya Wadhamini Bi Fatma Karume (katikaki), kushoto ni makamu mwenyekiti wa Yanga Bw Clement Sanga
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umewekeana sahihi ya makubaliano na Benki ya CRDB nchini juu ya uboreshaji na utengenezaji wa kadi za uanachama, hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Benki hiyo eneo la Posta mpya jijni Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dr Charles Kimei amesema anaushukuru uongozi wa Yanga kwa kuwaamini benki yao kuwa wanaweza kufanya kazi hiyo, na sisi tunaamini tutafanya kazi vizuri na kuweza kufikia malengo yao waliyotuwekea katika kipindi muafaka.
Kwetu sie kupata nafasi ya kufanya kazi na klabu ya Yanga ni jambo jema, tunatambua wana wana wapenzi zaidi ya milioni 20 nchi nzima, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunawifikia kila sehemu walipo na wanajiunga na uanachama wa kalbu yao pendwa alisema “Dr Kimei”.
Aidha Kimei amesema kwa utaratibu huo wa mfumo wa kisasa, wataanza kwa kutoa bure kadi za uanchama wa Yanga ambazo zitakua na nembo ya VISA itakayomfanya mtumiaji aweze kuitumia sehem yoyote alipo na kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa ada za uanachama.
Gharama ya kadi itakua ni Tshs 8,000 tu kwa watakaoanza upya (bure kwa waliokua tayari wanachama) na mteja/mwanachama ataendelea kuichangia klabu yake ya Yanga kiasi cha Tsh 250/= tu kwa wiki ambapo kwa mwezi ni sawa Tsh 1,000/= na kufanya kwa mwaka ada kuwa ile ile Tshs 12,000/=.
Kwa upande wa mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Young Africans Bi Fatma Karume amesema anaishukuru benki ya CRDB kwa kubali kufanya kazi hiyo, na kwa uwezo wao wa utendaji kazi anaamini wataifanya kazi hiyo kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kikubwa nilichofurahi ni kuwa hawa CRDB Bank wapo mpaka kwetu Unguja, hivyo naona zoezi hilo litafanikiwa vizuri na kurahisisha upatikanaji wa kadi za wanachama kwa uharaka zaidi alisema ” Bi Fatma.
Kadi mpya za uanachama wa Yanga zitakazotolewa na CRBD Bank zitakua za aina mbili, Premieum Visa Card kwa ajili ya viongozii mashuhuri wa klabu ya Young Africans tangu kuanzishwa kwake na nyingine ni Normal Visa Card kwa ajili ya wanachama wa kawaida.
Awali klabu ya Young Africans ilikuwa na mkataba wa aina hiyo na Benki ya Posta, Uongozi wa Yanga umeshawasilisha Notice kwa benki ya Posta juu ya kusitisha mkataba nao na sasa huduma hiyo itaanza kutolea kupitia benk ya CRDB.
Source: http://www.youngafricans.co.tz

KWANINI FAKE WANAKUA WENGI??AFISA USALAMA FEKI,SILAHA ZA KAMATWA NA POLISI.

AFISA USALAMA FEKI, SILAHA ZAKAMATWA NA POLISI

Posted by GLOBAL on September 2, 2014
Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.
Kamanda Suleiman Kova akionyesha  silaha zilizokamatwa kwa wanahabari (hawapo pichani).
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kova.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam,  kwa tuhuma za kujifanya  mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa .
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa.
Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata  bastola nne na shot-gun moja wiki hii.

NANI ALIPANGA???..Babu Tale: Fujo Kwenye Show ya Diamond Ujerumani ilipangwa Itokee

BONGO MOVIEZZ::HII NDO MUVI MPYA YA MR. CLOUD NA WENZAKE...COMING SOON

CLOUD NA WENZAKE KUZINDUA ‘MATESO YA UGHAIBUNI’ ILIYOREKODIWA UINGEREZA


Issa Mussa 'Cloud 112' akipozi ndani ya studio za Global TV Online.
Mkongwe wa filamu za Kibongo, Yvonney Cherry ‘Monalisa’.
Mastaa wa filamu za Kibongo, Riyama Ali na Wastara Juma.
FILAMU ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo imerekodiwa Uingereza  na wasanii  Issa Musa ‘Cloud 112’,  Riyama Ally, Wastara Juma  na Monalisa itazinduliwa Alhamisi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza  na mtandao huu, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif,  ambaye kampuni yake ndiyo iliwapeleka wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi filamu hiyo, alisema licha ya  kampuni yake kujihusisha na mambo ya mavazi na vitu vingine ameona kuna kila sababu ya kuwasaidia Watanzania wanaofanya  sanaa  ya uigizaji.

KIDAKUZZZ...ONA BIBIE ALIVOJALIWA UCHUMI HUKO NYUMA..ZAWADI TOSHA.....

Hii ndio sababu aliyotoa Di Maria kwanini hakuhama Madrid msimu uliopita

Hii ndio sababu aliyotoa Di Maria kwanini hakuhama Madrid msimu uliopita

1409586928356_wps_8_MANCHESTER_ENGLAND_AUGUSTMchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria amezungumzia juu ya uhamisho wake kutoka Madrid na huku akisema kwamba isingekuwa mmoja wa marafiki zake kwenye klabu ya Snatiago Bernabeu basi angeweza kuihama timu hiyo msimu uliopita.
Di Maria amejiunga na Manchester United mapema wiki iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £59m ambayo imeweka rekodi mpya nchini Uingereza
Winga huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye tayari alishaanza kuhususishwa na uhamisho wa kutoka Real wakati wa dirisha la usajili la msimu uliopita, lakini baadae aliendelea kubaki Santiago Bernabeu kwa sababu ya mchezaji Cristiano Ronaldo, abaye kwa mujibu wa Di Maria ni marafiki sana. 

“Ukweli ni kwamba nina mahusiano mazuri mno na Cristiano Ronaldo na nilibaki Madrid msimu uliopita shukrani kwa Ronaldo,” Muargentina huyo aliiambia ESPN Radio

Di Maria ameshaanza kuitumikia Manchester United ambapo alianza kwenye mechi ya ligi kuu ya England dhidi ya Burnley.