Friday, 22 August 2014

POLE KAMA ULIPATA KAZI UHAMIAJI.... ISOME KWA MAKINI

POLE KAMA ULIPATA KAZI UHAMIAJI....
Week Kama tatu zilizopita Udaku Special tuliweka Habari kuhusu Majina ya Waliofauli Usaili wa Nafasi ya Ukonstebo na Koplo Pale Uhamiaji ambayo ilisemekana yalikuwa yamechakachuliwa kwani wengi waliopata kazi hiyo walikuwa na undugu na wafanyakazi wa Idara hiyo, Baada ya Habari hiyo Serekali ilisimamisha mchakato huo kupisha uchunguzi , Leo taarifa zimepatikana kuwa ni ukweli majibu ya usaili huo yalichakachuliwa na kuwaacha waliofaulu na wahusika kuweka ndugu ama jamaa zao hivyo basi matokeo ya usaili huo yamefutwa rasmi Mpaka hapo Utakapofanyika Usaili Mwingine 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kamati maalumu ya kuchunguza ajira hizo kubaini wazi kwamba waliopewa nafasi hizo hawakukidhi vigezo.

Abdulwakil alisema wizara imesikitishwa na udhaifu huo baada ya kubainika wazi kwamba malalamiko yaliyotolewa na wananchi na kusababisha wizara kuingilia kati na kufuta usaili wa kuitwa kwenye ajira kwa watu 200 ulikuwa sahihi.


Alisema baada ya kubainika kwamba kweli kulikuwa na upendeleo wa dhahiri kwani watahiniwa wenye sifa na waliopata alama za juu wakati wa usaili hawakuitwa na kukiukwa kwa vigezo vya wazi, ajira hizo zitatangazwa upya na kusimamiwa moja kwa moja na wizara na siyo idara hiyo kama ilivyokuwa awali.

LULU AHONGWA HELA ILI ANUNUE GARI wakati akina nani WANAHONGWA GARI...NANI MJANJA?

Lulu Michael Aonyesha Kadi ya Gari yake Mpya, Aseme yeye si Kama Wakina Nanii Wanaohongwa

Friday, August 22, 2014
Kwa Kuonyesha kuwa yeye ni Tofauti na Mastaa Wengine wa Kike Walioingia katika Mkumbo wa Kuhongwa Magari wakati kadi ya Gari lina jina la muhongaji ambayo upelekea kunyang'anywa Penzi likiisha Mrembo Lulu Michael Ameonyesha Kadi ya Gari Lake Jipya aina ya Rav 4 New Model ,
Lulu Amesema yeye si Mswahili ndo maana ameamua kuonyesha kadi ya gari yenye jina lake ili kutowapa nafasi watu kusema amehongwa , Ameongeza kuwa yeye si kama wakina nanii ambao waliohongwa na kunyang'anywa magari... Hongera sana Lulu Michael Kwa Gari Jipya.

BOKO HARAM:KAMA CHUO CHA POLISI KINATEKWA,VIPI USALAMA WA RAIA NA MALI ZAKE?

Boko Haram Wateka Chuo Cha Polisi

 
Boko Haram wazidi kumlaza macho Raisi Jonathan Moyo
Kundi la wapiganaji la kiislam la Boko Haram,wamevamia shule moja ya mafunzo ya kipolisi.kituo hicho cha mafunzo kilichoko kwenye kitongoji cha Gwoza kiko karibu na mpaka wa nchi ya Cameroon ambacho hufundisha maofisa wa Polisi nchini Nigeria.
Kikundi hicha Boko Haram pia kinasemekana kuudhibiti mji wa jirani na Gwoza uitwao Buni Yadi.
Nalo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wametoa takwimu ya vifo vilivyosababishwa na kundi hilo kua watu zaidi ya elfu kumi mpaka sasa tangu walipoanzisha harakati za kutaka upande wa kaskazini mwa Nigeria uwe chini ya utawala wa Kiislam.

Kwanini kila baada ya kombe la dunia tu?Shakira Atuhumiwa Kuiba Wimbo

Shakira Atuhumiwa Kuiba Wimbo

 22 Agosti, 2014

Mwimbaji nguli wa pop Shakira atuhumiwa:
Wimbo uliovuma wa mwimbaji wa Pop Shakira ulinakiliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa kazi ya mtungaji mwingine wa nyimbo, jaji mmoja mjini New York amegundua.
Jaji Alvin Hellerstein alisema toleo la wimbo “Loca” la lugha ya kihispania 2010 lilikiuka haki za umiliki za wimbo wa mwimbaji Ramon Arias Vazquez.
Toleo la Ramon la “Loca” kwa lugha ya kiingereza- lililotumika katika Dizzee Rascal – “halikutolewa kama ushahidi,” katika kusikizwa kwa kesi hiyo.
Hakuna toleo lolote kati ya matoleo hayo mawili lililotolewa Uingereza.
Hata hivyo, toleo la kihispania – linalomshirikisha Eduard Edwin Bello Pou, anayefahamika kama El Cata – lilitolewa na kuvuma kote ulimwenguni na kuuza zaidi ya kanda milioni tano na kuongoza kwenye chati za kilatino kwenye Billboard Magazine.
Aidha, wimbo huo ulikuwemo kwenye albamu yake ya 2010 ‘Sale el Sol’ iliyouzwa kwa wasikilizaji wa Kiingereza na mada ya “The Sun Comes Out,” na matoleo yote mawili ya wimbo huo yalikuwemo.
Katika uamuzi uliotolewa Jumanne, jaji Hellerstein alisema kuwa, japo wimbo huo ulikuwa umetungwa ukifuata wimbo uliokuwa umerekodiwa hapo awali na Bello [El Cata], pia ulikuwa umenakiliwa kutoka kwa wimbo mwingine wa Arias Vasquez.
"Hakuna shaka kuwa toleo la Shakira la wimbo huo lilitungwa likifuata toleo la hapo awali la Bello,” jaji huyo aliandika kwenye uamuzi wake.
"Kwa hiyo, nimepata kuwa, kwa kuwa Bello alinakili Arias, yeyote aliyeandika toleo la Shakira pia alinaliki kwa njia isiyo ya moja kwa moja Arias,” alikata kauli.
Ramon Arias Vazquez alitunga wimbo Loca con su Tiguere miaka ya 1990, lakini Bello amekana kuunakili wimbo huo.
Uamuzi unatarajiwa kuelekeza fidia atakayolipwa mlalamikaji Mayimba Music, mmiliki wa haki miliki za hati ya Aria.
Sony ilisambaza matoleo yote mawili ya wimbo wa Shakira, toleo la Kiingereza, na la Kihispania, lakini tuhuma zilizotolewa ziliangazia toleo la kihispania.
Tarehe 13 Julai, Shakira, mwimbaji wa Colombia, alitumbuiza umati na wimbo huo katika sherehe ya kuhitimisha kombe la Dunia huko Rio de Janeiro.

DIVA KWA KING CRAZY GK AMEOZA MPAKA BASI!!!!

Diva:Sijampenda Gk Sababu ya Pesa Au Umaarufu Nampenda Yeye Kama Yeye

Udaku Specially on Friday, August 22, 2014
Ile hatua ya U boifriend na U girlfriend ikiwa imepita na kuingia katika hatua ya uchumba wa mahaba kedekede, dada yetu Diva alijikuta anamwaga chozi baada ya watu mbalimbali kumtupia maneno kwamba amempendea King Crazy Gk umaarufu wake ili abaki kupata KIKI Mjini.
Diva alijikuta anatoa maneno makali ya hasira na kuangua kilio na kudai kuwa hajampendea Gk umaarufu wake sababu yeye ni Diva ni maarufu pia hapa Tanzania, hakuishia hapo alizidi kudai ya kuwa amechoshwa na watu wengi kusema ana mahusiano na Gk ambae hana Pesa na ameachana na mwanaume ambae anapesa na cheo kikubwa Tanzania.
Diva:Nimechoshwa kuulizwa maswali ya Prezzo au mwanasiasa sababu huko siko tena na sina mahusiano nao zaidi ya urafiki wa kawaida wa kuongea nao kama watanzania wenzangu na pili amedai kuwa hana hisia zozote za kimapenzi na watu hao sababu yeye yuko na Mpenzi wake na anafurahia mapenzi hayo na mume wake ambae ni Mungu wa Muziki Tanzania.
Diva Binti mwenye mvuto na umbo la kuvutia na mvuto wa sura ya babyface na macho ya duara alidai kuwa King Crazy Gk ni Mtu mwenye kipato kizuri tu ila sio mtu wa kujionyesha au kuishi maisha ya kujionyesha na ni mtu mtaratibu anaeishi maisha yake alioridhika nayo na anatumia pesa zake kulipia elimu na kufanya mambo yake na biashara zake binafsi tofauti na watu wanavyomfikiria. Diva la Diva alisema kuwa Hakumpendea Gk Pesa au Umaarufu wake amempenda yeye kama yeye na anachukia baadhi ya watu kumuingilia kimawazo maisha yake ya mapenzi ambayo mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa nayo kupitia mtandao wa instagram.

PESA ZA DIAMOND ZAITISHA SERIKALI....MPAKA WAKAHISI NI PUSHA KUMBE ZA SHOW TU..

Fahamu Kiwango Kipya Anacholipwa Diamond Kwa Show Moja ya Mziki Hapa Tanzania

Udaku Specially on Friday, August 22, 2014
Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.

Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo.

Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania).

“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.”  Babu Tale aliiambia Bongo5.

Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani).

“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.

Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na  $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500).

Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania.

Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava.

Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.


Thursday, 21 August 2014

KATUNI:MECHI ZA UGENINI HIZO(MICHEPUKO)

HUU NDO USHAURI ALIOPEWA CHID BENZZZZ......

Chid Benz Zingatia Haya ili Usirudi Ulipotoka La Sivyo Tutakupoteza Kama Wengine

Udaku Specially on Thursday, August 21, 2014
Kati ya watu ambao hawakufiri kama msaanii Chid benz angeweza kurudi vyema kwenye ulingo wa muziki Mimi ni mmoja wapo maana nilihisi kama huyu mtu amesha changanyikiwa na amepoteza uwezo wa kufikiri au kukaa chini akatunga wimbo mzuri tena.

Pengine mwenendo wake na tabia zake zilimponza na sasa amejua pakurekebisha. Chid Benz ni kati ya wasanii waliopendwa na wengi na alipata mafanikio makubwa kupitia mziki wake na akabweteka na kujisahau!

Ujio wake mpya umenifurahisha sana na hakika tunaanza kumuona Chid Benz yule wa wimbo kama" Dares-salaam stand up" na nimefarijika sana kumsikia karudi rasmi na huyu ndio Chid benz ambaye tumekuwa tukimfahamu.

Wanajamvi hasa wale wapenzi wa burudani kama mmepata nafasi ya kuusikiliza wimbo wake unaoitwa "Mpaka kuchee" ambao amewashirikisha Diamond na Ay mtakubaliana nami kuwa huyu ndio Chid Benz mwenyewe maana mule ka rapu vyema naona sasa yuko serious!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ...Diamond anajua kutumia nafasi anazopewa hasa kwenye kuimba, kwakweli kwenye wimbo huu kaimba vizuri sana na kautendea haki wimbo huu!Hata Ay mzee wa biashara ametenda haki nusu afunike.... kwakweli walijipanga big up sana kwa zawadi hii.

USHAURI KWA CHID BENZ

Kuna mambo ambayo amekuwa akifanya Chid benz na huwa kera wengi hasa sisi mashabiki wake mfano ...Kupigana hovyo,Kupiga hovyo,Matumizi ya madawa na bangi
hayo inabidi aachane nayo maana yanamchango mkubwa kuharibu muziki na kipaji chake.

Hawa alio imba nao ndio wanaweza kuwa muongozo wake hasa Ay anaweza akamsaidia sana kama akiamua kuwa sambamba nae.
Nivyema akaangalia aina ya marafiki ambao amekuwa nao siku zote ambao wamempelekea kuzama kwenye madawa inabidi awapunguze na afanye muziki sasa.

Namtakia kila la kheri kwenye safari alio ianza upya.

TAFAKAFARI YA KATUNI:WAKUSOMA JIBEBE

DIAMOND KUFANYA KOLABO NA ALIKIBA ANYTIME....Wanafiki wamefyata mikia

HII NDO KOLABO YA DIAMOND NA ALIKIBA FOR REAL>>>Coming soon.

Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia.

Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko.

“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho kitu kipo.

 "Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! 

"Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” alisema AliKiba.

Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”
Udaku Specially

HABARI NA PICHA:NANI MZURI HAPO.......mie mgeni tu ndo nafika



PICHA YA LEO:UMEGUNDUA NINI HAPO KINAENDELEA.....

FLAVIANA MATATA:NA UTATA WA KUCHUMBIWA......soma pole pole...

Posted by GLOBAL on August 21, 2014
Stori:  ERICK EVARIST

MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha katika tukio la kuchumbiwa kunaswa na mwenyewe kudai si yeye aliyechumbiwa.
Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo limedaiwa kufanyika kwa siri hivi karibuni nyumbani kwa miss huyo, Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu wa karibu.
“Inaonesha hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu…
Stori:  ERICK EVARIST
MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha katika tukio la kuchumbiwa kunaswa na mwenyewe kudai si yeye aliyechumbiwa.
Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo limedaiwa kufanyika kwa siri hivi karibuni nyumbani kwa miss huyo, Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu wa karibu.
“Inaonesha hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu wengi siku hiyo, hata hao ndugu wenyewe hawakuwa wengi kiivyo lakini picha zinaonesha Flaviana akichumbiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data chanzo hicho kilidai kwamba, mwanaume anayetaka kumuoa mrembo huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ni Mchaga mwenye fedha zake aishiye Marekani.
“Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.
Flaviana Matata akiwasalimia wazee kwa kupiga magoti.
Amani lilifanikiwa kuzinasa picha hizo ambazo zinamuonesha mrembo huyo akiwa amepiga magoti huku amemshika mkono mmoja wa wazazi wake aliyeshiriki katika hafla hiyo ya kupokea mahari.
Baada ya kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Flaviana kwa njia ya simu ya mkononi ndipo alipokataa katakata kuwa si yeye aliyekuwa akichumbiwa bali ni dada yake.
“Hamna kitu kama hicho,  unayesema alikuwa anachumbiwa si mimi ni dada yangu, mila za kwetu Shinyanga nalazimika mimi kumsindikiza hivyo kama umeona picha hizo uelewe hivyo,” alisema Flaviana.
Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ni la Flaviana na si dada yake hivyo kuzidi kuzua utata juu ya ukweli halisi, Amani linaendelea kufatilia kwa karibu.

HUYU NDO MREMBO WA BONGO MOVIE ANAYEBADILI SANA NAMBA ZA SIMU

WOLPER NDO BINGWA WA KUBADILI NAMBA ZA SIMU

Posted by GLOBAL on August 21, 2014
Na Mwandishi Wetu

KUNA nini kwani? Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper anatajwa kuongoza wasanii wenzake kwa kubadili namba za simu za mkononi huku baadhi ya mashoga zake wakijiuliza kulikoni?
Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu na Wolper (jina lipo), anamshangaa sana shoga yake huyo kwani amekuwa akibadili namba za simu kwa mwaka mmoja hata mara saba.
“Unajua kwa maisha ya sasa, simu ikipotea mtu unairinyuu laini yako ileile, maana ndiyo…
Na Mwandishi Wetu
KUNA nini kwani? Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper anatajwa kuongoza wasanii wenzake kwa kubadili namba za simu za mkononi huku baadhi ya mashoga zake wakijiuliza kulikoni?
Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu na Wolper (jina lipo), anamshangaa sana shoga yake huyo kwani amekuwa akibadili namba za simu kwa mwaka mmoja hata mara saba.
“Unajua kwa maisha ya sasa, simu ikipotea mtu unairinyuu laini yako ileile, maana ndiyo inayojulikana na wadau. Lakini yule mwenzetu siyo. Nimeshamsevu kwenye simu yangu kwa majina ya Wolper, Wolper Tena, Wolper Nyingine, Wolper Nyingine Kabisa na Wolper Hakuna Tena, lakini zote kwa sasa hazipo hewani,” alisema shoga yake huyo huku akicheka.
Wolper alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi iliyozoeleka, hakupatikana. Jitihadi zilifanyika akaja kupatikana kwenye namba mpya ambapo alisema:
“Mimi nikishapoteza laini naona uvivu kwenda kuirinyuu, ndiyo maana nanunua nyingine.”

UKATILI WA AINA YAKE....dah DUNIA YA VICHAA SASA

UKATILI WA AINA YAKE:WATOTO WATATU WABAKWA KWA ZAMU

Posted by GLOBAL on August 21, 2014
Stori:Chande Abdallah na Deogratius Mongela

Inaumiza kusikia! Watoto watatu ambao ni majirani wamejikuta wakiingia kwenye kadhia ya kubakwa kwa zamu na watoto wenzao ambapo mmoja anadaiwa kuwa na umri wa miaka 17 huku mwingine akiwa na umri wa miaka 14 ambaye pia ni denti wa darasa la nne.
Watoto watatu wadogo waliobakwa kwa zamu na watoto wenzao.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Mbagala-Mianzini jijini Dar ambapo awali ilidaiwa kuwa wazazi wa watoto hao walishtushwa walipogundua…
Stori:Chande Abdallah na Deogratius Mongela
Inaumiza kusikia! Watoto watatu ambao ni majirani wamejikuta wakiingia kwenye kadhia ya kubakwa kwa zamu na watoto wenzao ambapo mmoja anadaiwa kuwa na umri wa miaka 17 huku mwingine akiwa na umri wa miaka 14 ambaye pia ni denti wa darasa la nne.
Watoto watatu wadogo waliobakwa kwa zamu na watoto wenzao.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Mbagala-Mianzini jijini Dar ambapo awali ilidaiwa kuwa wazazi wa watoto hao walishtushwa walipogundua watoto wao wameingiliwa na kuharibika vibaya baada ya kuwakagua kila mmoja kwa wakati wake walipokuwa wakiwaogesha.
Wazazi wa kiume wa watoto hao.
Wakizungumza na gazeti hili kwa masikitiko kwa nyakati tofauti, wazazi wa watoto hao walidai kwamba walipowabana waliwataja kwa majina waliowafanyia vitendo hivyo, jambo lililowafanya ‘kuwataiti’ watuhumiwa kwani walikuwa wakiwafahamu.
Wazazi hao walidai kwamba walipowauliza watoto hao walikiri kuwaingilia wenzao kwa zamu kwenye jumba bovu (pagala) ambapo walienda mbali zaidi na kusema kuwa walikuwa wamewafanyia vitendo hivyo kwa muda mrefu sasa kwa zamu, nyakati ambazo watoto hao walirejea kutoka shuleni chekechea (jina kapuni kimaadili).
Wazazi wa kike wa watoto hao.
“Nilishtuka na kuumia sana baada ya kugundua mwanangu ameingiliwa, tena kwa kipindi kirefu kiasi kwamba ameharibika kabisa.
“Huwezi kuamini mke wangu alipopata taarifa alipandwa na presha kiasi cha maisha yake kuwa hatarini,” alisema mmoja wa wazazi hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Hussein.
Waraka(RB) wa polisi wa kukamatwa kwa watuhumiwa.
Kwa pamoja wazazi hao waliripoti ishu hiyo kwenye Kituo cha Polisi cha Charambe na baadaye Mbagala-Kizuiani ambapo majalada ya kesi hizo yalisomeka MBL/RB/9608/14-KUBAKA, CHAR/RB/1292/2014-KUBAKA CHAR/RB/2192/2014-KUBAKA ambapo watuhumiwa wanasubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

KAJALA KAACHA UTOTO:Hivi utoto mwisho miaka mingapi????

Kajala:Nimeweka Vitu Vyote vya Kitoto Pembini Ikiwemo Ugomvi na Wema Sepetu

Udaku Specially on Thursday, August 21, 2014
STAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja, ameibuka na kudai kuwa ameweka vitu vyote vya kitoto pembeni likiwemo suala la malumbano na kujikita katika suala la ujasiriamali.

Akizungumza na paparazi wetu, Kajala alisema amefanya tathmini na kugundua mastaa wengi wamekuwa wakiambulia umaskini baada ya umaarufu kupotea hivyo ameona ashtuke mapema kwa kufanya biashara mbalimbali ambazo zitamjengea msingi mzuri maishani.

“Nimeshtuka, sihitaji bifu na mtu, biashara tu na hata safari za nchini China kwa sasa ni kwa ajili ya biashara pekee na si vinginevyo, ukitaka pochi, viatu na vitu vingine vingi utapata,” alisema Kajala aliyekuwa akiogelea katika bifu kali na aliyekuwa shosti wake, Wema Sepetu.

HAKUNA NDOA AMBAYO HAINA DOA HAPA DUNIANI

Tetesi za Kuvunjika Kwa Ndoa Yake JAY DEE Ahamia Hotelini

Udaku Specially on Thursday, August 21, 2014
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.

Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.

Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani  hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.

Hata hivyo, gazeti dada ya hili, Ijumaa toleo la Ijumaa  iliyopita lilizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.

Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani.

Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao!
Juzi, mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka nayo.

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide (jina tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki.“Ni kweli Anaconda (Jide) anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo,” alisema mtu huyo.

Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi.

HICHO NDO ALICHOPOST chriss brown:" My WCW"

CHRISSBROWN ATAKA MTOTO KWA KARRUECHE

 
Baada ya kipindi kirefu cha mapenzi ya kuwaka na kuzima, sasa Chris Brown anahitaji kuwa baba mtoto wa Karrueche Tran.

Mkali huyo wa R&B ameandika mpango wake huo katika Instagram ikiwa ni siku moja baada ya Karrueche kutoa tamko rasmi kuhusu kurudiana kwao na kueleza kuwa katika mapenzi yao kuna vitu vya ndani ambavyo havijulikani na havipaswi kujulikana kwa watu ambavyo vinawafanya waendelee kuwa pamoja.

"@karrueche damn near 5 years and this woman still putting up with my s---. Need to have this baby and stop playing! Lol! My WCW" Ameandika Chris Brown na kupost Karrueche

KWANI DIAMOND NAE NI PUSHA WA SEMBE???? hatari sana

Skendo ya Madawa ya Kulevya Yamweka Pabaya Diamond

Udaku Specially on Thursday, August 21, 2014

Stori:  Shakoor Jongo na  Makongoro Oging’
NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.

Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.

Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.

MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.

“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.

Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar
GPL

HUYU NDO MSANII ANAEMKUBALI KASSIM MGANGA, Diamond aangalie mbelee

Kassim Mganga Amwagia Sifa Ali Kiba, 'My Favorite Artist'

Thursday, August 21, 2014
Mwimbaji kutoka Tanga, ‘Tajiri wa Mahaba’ Kassim Mganga amemtaja Ali Kiba kuwa ndiye msanii  wa bongo flava anaemkubali zaidi Tanzania.

Ali Kiba amefunguka katika mahojiano maalum aliyofanya na tovuti ya Times Fm na kueleza kuwa mbali na kuwa ni mwimbaji mwenye uwezo mkubwa, hata kitabia yuko vizuri.

“Ali Kiba (ndiye my favorite artist in TZ), mimi binafsi nampokea vizuri sana. Nafikiri anachokifanya mimi kinanivutia sana. Napenda uandishi wake, napenda melodies zake na napenda utulivu wake. Ana hekima kama zangu, yuko kimyaa (anacheka).” Kassim ameiambia tovuti ya Times Fm.

Kassim Mganga ameeleza kuwa mwaka jana kabla hajatoa wimbo wake ‘I Love You’ uliokuwa hit, alikuwa na mpango wa kufanya wimbo na Ali Kiba na walikuwa tayari wamekubaliana lakini mambo yaliingiliana na kazi haikukamilika.

Katika hatua nyingine, Kassim Mganga ameeleza kuwa watanzania hatupaswi kuendekeza majigambo na uadui kati ya wasanii badala yake kufanya kazi na kuwasapoti wale ambao wanaiwakilisha nchi yetu katika mataifa mbalimbali kama vile Diamond badala ya kuwajengea uadui.

“Diamond ni mtu ambaye ameweza kutufungulia sana soko letu kiukweli, tunashukuru. Tunatakiwa kuwa nyuma yake tumsapoti tuendelee kumsukuma na sisi huku tunaendelea kujongea. Kwa hivyo, vinapokuwa vinajengwa vitu kama hivyo (uadui/majigambo) sio jambo zuri kwa sababu vinajenga uadui na mwisho wa siku muziki tunakuwa tunaufanya kimajigambo tu lakini sio kwa ajili ya kuutangaza muziki wetu…”