Monday, 25 August 2014

SIASA SI HASA:::USICHEZE VIBAYA NA SIASA....MAKONDA ROHO JUU JUU

Hali Ndani ya CCM ni Mbaya, Roho ya Makonda Inatafutwa Usiku na Mchana

Udaku Specially on Monday, August 25, 2014
Kwa mujibu wa nzi wetu anayecheza viunga vya Lumumba akitutiririshia habari zote mpaka mapigo ya mioyo ya akina Kinana, Nape na wana CCM wote walio juu ya maharamia wote, anatujuza kuwa huko CCM moto wake sio wa kitoto,

Makonda anatuhumiwa kumtusi Lowassa hadharani tena akivaa mwavuli wa UVCCM ilihali hana cheo chochote ndani ya Chama,

Baada ya matusi yale ya nguoni ambayo aliyaporomosha huyu dogo nikuwa mashitaka rasmi yalifikishwa kwenye kamati ya maadili na Lowassa,

Sheria ya CCM inasema kama mtu hayupo kwenye kikao husika cha mashitaka ni mwiko kujadiliwa,

Sasa siku ambayo tayari kamati kuu ilijipanga kumwajibisha (kumvua uanachama) kwenye kikao chake cha mwezi jana, Makonda alikimbilia Ufaransa akitoroshwa na Ridhiwan Kikwete na Bernard Membe kwa madai kuwa anakwenda kwenye semina ya masuala ya katiba,

Baada ya kutokuwepo kwenye kikao husika huvyo iliamuliwa suala hilo lisogezwe kwenye kikao kitakachofuata hasa hiki cha dharula juzi,

Kikao cha juzi tena wakati akiwa tayari kajulishwa kwa barua toka kwa katibu mkuu, Makonda tena alisafiri kwenda Ujerumani kwa madai ya kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake, safari hii Membe akihusika kuratibu na taarifa za kuaminika nikuwa hakwenda Ujerumani bali aliongozana na Membe kwenye ziara yake huko Mashariki ya Mbali ambako aliendelea kubaki huko hata baada ya Membe kurudi mpaka cc ilipomaliza kikao chake juzi,


Upande wa Lowasa wanaoonekana ndio wenye nguvu wameapa kuwa ni lazima waikate "roho" ya kisiasa ya Makonda kwa kuhakikisha anafukuzwa uanachama.

TATHIMINI YAKO:KUOLEWA NA MZUNGU NI SIFA KUBWA.

 
Lucy Komba akiwa na mpenzi wake wa mamtoni.

ONA PICHA ZA NDOA YA JAGUAR.....(KIGEUGEU)

Kama uliona hizi picha zilizosambaa ukaamini ni ndoa ya Jaguar. @RealJaguarKenya

Screen Shot 2014-08-25 at 5.33.37 AM
Jaguar aliandikwa na vyombo kadhaa vya habari Kenya kwamba amekwenda kufunga ndoa ya Mwanamke wa maisha yake nchini Afrika Kusini ambapo picha zilianza kusambaa toka wiki iliyopita.
kwenye exclusive na millardayo.com Jaguar amesema ni kweli wengi walidhani ni ndoa amekwenda kufunga ila ukweli ni kwamba hiyo ni video yake mpya ambayo inatoka Jumatatu ya leo August 25 2014.
Screen Shot 2014-08-25 at 5.32.04 AM

Screen Shot 2014-08-25 at 5.33.31 AM
Screen Shot 2014-08-25 at 5.33.19 AMScreen Shot 2014-08-25 at 5.33.12 AM

HISTORIA NZURI MPAKA UFANIKIWE:FROM ZERO TO HERO...Huyu ndo MBWIGA WETU.

HII NDIO HISTORIA YA MAISHA MBWIGA WA MBWIGUKE


Kikwete na mtangazaji wa Cloud FM Mbwiga MbwigukeRais Dkt. Jakaya Kikwete akipozi katika picha na Mbwiga wa Mbwiguke wa Clouds fm (kulia)



Na Maregesi Paul



SIKU moja nilikuwa katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri ambao mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginard Mengi.



Katika mazungumzo yake, Mengi aligusia historia ya maisha yake ambapo alisema alikulia katika familia masikini.



Kwa mujibu wa Mengi, nyumba aliyokulia ilikuwa na panya wengi pamoja na mende na kwamba kila walipokuwa wakilala usiku, wapita njia walikuwa wakiwaona kwa sababu nyumba ilikuwa imejaa matobo.



Pamoja na mazingira hayo, Mengi kwa sasa ni kati ya matajiri wakubwa wanaoheshimika ndani na nje ya nchi na suala la umasikini aliokulia, limebaki kuwa historia.




Hivyo hivyo, hata mimi niliyeandika makala haya, niliwahi kuvua dagaa na sangara kwa kutumia nyavu haramu ziitwazo makokoro. Lakini sasa mimi ni mhariri wa gazeti hili na suala la uvuvi, limebaki katika historia.



Wakati hayo yakitokea, katika Radio Clouds kuna watangazaji wengi wanaovuta masikio na hisia za wasikilizaji kutokana na lugha na vichekesho wanavyovitumia pindi wanapokuwa studio.

Miongoni mwao ni Said Seleman maarufu kwa jina la Mbwiga wa Mbwiguke.

EX6Mbwiga wa Mbwiguke (kuli) akipozi na Shaffih Dauda kwenye moja ya mechi iliyoihusisha timu ya mpira ya Clouds Media Group maarufu kama ‘The Dream Team’



Kama ilivyo kawaida kwa watu kuwa na historia tofauti tofauti kama nilivyoeleza hapo awali, wakati wa mahojiano maalum na MTANZANIA Jumatatu, Mbwiga anaeleza kwa kirefu ni wapi alikotokea hadi akawa mmoja wa watangazaji maarufu katika radio hiyo maarufu nchini.



“Kwanza nianze na maana ya jina Mbwiga. Mbwiga ni neno la kizaramo ambalo maana yake ni rafiki. Kwa hiyo mimi ni rafiki wa kila mmoja kwa sababu huwa napenda sana kuwachekesha watu.

“Lakini pia, maisha ni mzunguko na kamwe hakuna binadamu anayezaliwa na kujua maisha yake yatakuwaje kwa siku zijazo.



“Kwa maana hiyo, hiki nitakachokieleza ndivyo kilivyo kwa sababu hapa nilipo sikutarajia kama itatokea siku nikawa mmoja wa watu wanaoungwa mkono na mamilioni ya Watanzania.



“Kwanza kabisa niseme tu kwamba, mtu aliyenifikisha hapa ni mtangazaji mwenzangu aitwaye Shafii Dauda. Huyu ndiye aliyenileta Clouds baada ya kuniona naweza kuwa na mchango fulani fulani katika redio yetu hii.


“Sikumbuki ni mwaka gani, lakini nakumbuka ni kama miaka mitatu iliyopita, siku moja usiku nilikuwa pale Muhimbili Shule ya Msingi kwenye mazoezi ya mpira unaowahusisha wachezaji wakongwe kama akina Akida Makunda, Mohamed Binda, Idd Moshi, Ally Mayai, Crement Kahabuka, Dua Said na wengineo wengi .



“Siku hiyo nilikuwa sichezi bali nilikuwa shabiki tu nikiwashangilia wenzagu, kwa hiyo, mazoezi yalipomalizika, Shafii Dauda alikuja mahali nilipokuwa na akina Ally Mayai na alitukuta tunacheka,” anasema Mbwiga na kuongeza.



“Alipoona tunacheka, akauliza tunacheka nini, Ally Mayai akamwambia huyu jamaa anatuchekesha, hebu mchukue umtumie kwenye kipindi chako kile cha michezo cha saa tatu usiku atakusaidia sana,” anasema Mbwiga.



Kwa mujibu wa Mbwiga, Shafii alikubali na hapo ndipo ukawa mwanzo wa safari yake kujiunga na Radio Clouds.



Anasimulia kwamba, baada ya kukubaliwa, Shafii akawa anampigia simu ili aripoti matukio mbalimbali ya michezo na kwamba taarifa hizo alikuwa akiziripoti katika mazingira magumu.

“Wakati mwingine nilipokuwa nikiripoti, kuna wakati Shafii alikuwa akinipigia simu nikiwa kwenye daladala, kwa hiyo, nilikuwa nikilazimika kushuka ili nitafute sehemu nzuri iliyotulia ili nirekodi kipindi.

Mtangaaji wa Clouds Fm, Mbwiga wa Mbwiguke (kushoto) akipozi na shabiki wake Imani Ntila.

“Jambo la kuwaeleza wapenzi wa Radio Clouds ni kwamba, wakati ule nilipokuwa nikirekodi kipindi na Shafii, nilikuwa nikifanya kazi pale Uwanja wa Azamu kule Chamazi. Kule Azam nilikuwa nikisafisha uwanja kwa kuokota vyuma na chupa za maji zilizokuwa zikitupwa wakati wa ujenzi na zilizokuwa zikitupwa na wachezaji walipokuwa wakifanya mazoezi.


“Lakini kumbuka kwamba, pale Azam nilikwenda kuomba kazi za uselemala, nilipokosa hiyo kazi, nikaangukia katika kusafisha uwanja kama nilivyokwambia.


“Kwa maana hiyo, kuna wakati nilipokuwa nikitakiwa kurekodi kipindi na Shafii, nilikuwa nikijificha kwenye majukwaa chini kabisa kwa sababu kule pametulia kweli kweli.


“Nilipokuwa nikifanya hivyo, wenzagu niliokuwa nikifanya nao usafi walikuwa wakilalamika kweli kwa sababu waliamini nategea kazi, kumbe mwenzao nilikuwa naandaa maisha,” anafafanua Mbwiga.


Mbwiga Mbwiguke akiwatuliza wanachama wa Yanga waliojitokeza kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo mwaka huu.


Baada ya kufanya kazi hiyo kwa miezi kama mitatu hivi, anasema baadaye Shafii aliamua kumpeleka ofisini kwao Mikocheni Dar es Salaam ambako alianza kutangaza akiwa studio.

Alipofika ofisini hapo, anasema alikutana na mmiliki wa radio hiyo, Joseph Kusaga ambaye alisoma naye Shule ya Msingi Forodhani (zamani St Joseph).


“Siku moja baada ya kuanza kutangaza, ilifanyika sherehe ya wafanyakazi wote ambapo MC alinipa fursa ya kuzungumza. Hapo nilimshukuru bosi Kusaga kwa kumwambia amenipa nyavu badala ya samaki, hivyo ni wajibu wangu kuendelea kuvua,” anasema Mbwiga.


MAISHA YAKE KAZINI

Mbwiga anasema baada ya kuanza kazi rasmi, anasema alikutana na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na kutakiwa kujua mambo mengi yanayotokea duniani.


Pia anasema kwa kiasi fulani amefanikiwa kufikia malengo kwa kuwa pamoja na kutangaza katika kipindi cha michezo cha saa tatu usiku, hivi sasa anashiriki katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa kila siku asubuhi.


“Nashukuru kwa sababu sasa niko katika vipindi viwili, yaani kile cha usiku na cha asubuhi na nadhani wakubwa wangu wameniongezea majukumu baada ya kuona nina msaada fulani kiofisi.

“Jambo la kushangaza ni kwamba, wakati naanza kutangaza Power Breakfast, moyo uliuma sana, yaani niliogopa kwa sababu sikujua kama ningeweza kufanikiwa.


“Lakini Jerad Hando alinitoa hofu, akaniambia usiogope, hakuna kitu kipya, nikamuelewa na mwishowe nikawa nimefanikiwa,” anasema.


Mbwiga Mbwiguke (kulia) akiwa na mdau wa michezo


MAISHA YAKE KWA SASA

Mbwiga anasema kwa sasa anaonekana mtu wa maana mtaani kwake anaokoishi Magomeni Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla tofauti na alivyokuwa mwanzo.


“Maisha yangu yamebadilika sana mtaani kwetu na jambo jingine ninaloshukuru ni kwamba, nina marafiki wengi na nafahamika kila mahali.


“Yaani hata Rais Kikwete ananifahamu kwa jina kwa sababu mwaka jana nilifuturu naye Ikulu tukiwa naye meza moja.


“Hata hivi karibuni tulikutana naye kwenye tamasha la wasanii kule Dodoma na aliponiona, aliniita kwa jina akaniambia, Mbwiga hujambo, nilimjibu, sijambo mheshimiwa, msimu wa embe nyani hakondi, halafu akacheka,” anaeleza.


HISTORIA KIFAMILIA

Anasema yeye ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao akitanguliwa na kaka yake aitwaye Nassor Fadhir anayeishi jijini Cologne, nchini Ujerumani.


MALENGO YAKE

Mbwiga ambaye anapenda kujitambulisha kuwa ni mzaramo, anasema ana mpango wa kujiendeleza kielimu ili aweze kuitumikia vizuri kazi yake.


“Elimu yangu siyo kubwa sana ila nimesoma pale VETA Chang’ombe kwa miaka miwili na kutunukiwa cheti cha ujenzi wa barabara.


“Baadaye nilijiingiza katika masuala ya ufundi selemala, kwa hiyo, naweza kusema mimi ni fundi selemala mzuri wa fenicha zote za ndani.


“Ili niweze kwenda na wakati, niko katika mikakati ya kujiendeleza kielimu kwa sababu hata wafanyakazi wenzangu wamekuwa wakinihimiza juu ya hilo,” anasema.


Katika mazungumzo yake, anawashukuru wafanyakazi wenzake wote na kuwataja baadhi kwa majina kuwa ni Joseph Kusaga, Ruge Mutahaba, Joyce Shebe, Shafii Dauda, Gerad Hando, Maestro, Alex Luambano, Bonge, PJ na Simalenga.


“Nimewataja hao, lakini lazima umuweke Babra Hassan, yaani usipomtaja huyo, ataninunia mpaka basi,” anatania Mbwiga.

LUCY KOMBA: HARUSI BONGO, SHEREHE MAMTONI

LUCY KOMBA: HARUSI BONGO, SHEREHE MAMTONI

HISTORIA
Dada Lucy hongera kwa kuwa na kipaji, kiukweli unaweza, kubwa napenda kuijua historia yako kwa ufupi. Thabiti Kiula, Igunga, 0786947474
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lucy Komba akipozi.
LUCY: Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Nimezaliwa Dar katika Hospitali ya Lugalo. Nina elimu ya kidato cha nne baada ya hapo nikasomea mambo ya usekretari. Mimi ni mwajiriwa wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Sanaa nimeanza mwaka 2010 kwenye Kundi la Fukuto Art Professional.
USHAURI
Hongera dada Lucy, nakushauri ukaze buti, naikumbuka sana muvi uliyocheza na Dk. Cheni na Mzee Magali. Jofu Mwaik, Dar, 0782780264
LUCY: Sijawahi kucheza muvi na Cheni ila ni tamthiliya tu. Mzee Magali ni kweli nilishawahi kucheza naye filamu.
NDOA
Dada Lucy ndoa yako itafanyika mwaka gani? Lee Cantana, Mwanza, 0753369500
LUCY: Mwaka huu.
WABONGO
Hivi dada kwa nini umeamua kuwatosa Wabongo wenzako na kuamua kuwa na Mzungu? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
LUCY: Ni mapenzi tu kwani hayaangalii sura, kabila wala dini.
MATARAJIO
Lucy kiukweli mimi nakuzimia sana uigizaji wako mzuri kunako tasnia ya filamu Bongo, je, nini matarajio yako ya baadaye kuhusiana na usanii? Salim Liundi, Dar, 0659601205
LUCY: Siwezi kusema matarajio yangu ni nini maana natarajia kuhama nchi.
Lucy Komba akiwa na mpenzi wake wa mamtoni.
YEYE NA KEPTENI KOMBA WAKOJE?
Lucy eti una undugu na Kepteni Komba na je, wewe ni Mngoni? Muddy Madiley, 0652672805
LUCY: Ni ukoo tu vilevile ni Mngoni mwenzangu.
HARUSI
Napenda kujua kama harusi yako itafanyika hapa Bongo au mamtoni kwa jamaa? Brosco, Mwanza, 0685244622
LUCY: Harusi ni hapahapa, mamtoni tutaenda kumalizia sherehe.
SWALI
Hivi Lucy ulishawahi kuandika filamu yako mwenyewe na kama umewahi inaitwaje? Muddy, Dar, 0755462633
LUCY: Asilimia kubwa ya filamu zangu huwa naandika mwenyewe kama Fedheha, Kipenzi Changu, Cleopatra na nyingine nyingi.
TASNIA INAKUFA?
Sekta ya filamu Tanzania inaonekana inaelekea kufa, unafikiri nini tatizo? Elia, Iringa, 0762431001
LUCY: Tatizo ni wasambazaji kwani ni wabaguzi hawaangalii nani anafanya filamu nzuri bali wanaangalia kujuana tu.
KAFUATA PESA KWA MZUNGU?
Dada Lucy upo vizuri kwenye fani, hongera kwa kumpata Mzungu ila mbona kama watu wanaponda eti hakuna ‘real love’ hapo bali umefuata mkwanja, je, wewe unalichukuliaje hili au ndiyo wale vijiba vya roho? Rocky, Moshi, 0715289337
LUCY: Ni majungu tu na maneno ya watu hata kwenye khanga yapo.
URAFIKI
Wewe ni msanii mzuri, naomba uwe rafiki wa kubadilishana mawazo, kama upo tayari naomba unitafute. Irene, Tanga, 0657146670
LUCY: Nashukuru, nitakutafuta.
AKIOLEWA ATAHAMA?
Je, huyo Mzungu akikuoa utakwenda kuishi kwao au mtabaki hapa Tanzania? Loth, Moro, 0788133987
LUCY: Nitaenda kwao.
ALIMUIBUA WOLPER?
Wewe ni mwigizaji mkongwe, je, ni kweli wewe ndiye ulimuibua (Jacqueline) Wolper kwenye fani ya uigizaji? Ebeshente, Dar, 0757174278
LUCY: Ndiyo, asante.

KAMA HAMJUI VILE:::ONA PICHA ZA MKAUSHO WA RIHANNA KWA CHRISS

Rihanna ampigia mikausho Chris Brown kwenye mechi ya basketball

0
Chris Brown na Rihanna wamejikuta wapo karibu kwa umbali mdogo sana walipokua kwenye mechi ya basketball kwa ajili ya kuchangia taasisi ya CC Sabathia na Robinson Cano. Mechi hiyo ilikuwa ya mafanikio kwa kuingiza zaidi ya dola milioni 1 lakini story kubwa sio hiyo.
Kitu kilichotengeneza headline ni pale Rihanna alivyoonyesha mikausho mikali hasa wakati Chris Brown anapokuwa karibu yake wakati wa mechi hiyo. Kuna wakati Chris Brown alikuwa anawasalimia mashabiki waliokuwa wamekaa karibu na kiti cha Rihanna na picha zilipigwa Rihanna anaonekana ameweka mikausho na kuangalia pembeni.
Mechi iliisha vizuri na picha ya hapo juu imekuwa maarufu sana kwenye instagram hivi sasa.
1
2
3
4
5

Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana

Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana

 25 Agosti, 2014

Wapiganaji wa Renamo nchini Msumbiji
Habari kutoka Msumbiji zinasema serikali ya nchi hiyo imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo ili kumaliza uhasama kuelekea uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya chini kwa chini kati ya wafuasi wa Renamo wenye silaha na majeshi ya serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo walijitoa katika mkataba wa amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, mkataba ambao ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Wiki iliyopita ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza kuwaachilia wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi karibuni.
Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani.

KESI KIFO CHA KANUMBA, SURA MPYA!

KESI KIFO CHA KANUMBA, SURA MPYA!

 
Stori: Shakoor Jongo
Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea.
 
Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi (open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.
 
Wakili maarufu Bongo anayemtetea 'Lulu', Peter Kibatala.
YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.
ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa mahakamani.
 
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.
 
Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.
“Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

BURUDANI NA PICHA:Picha 8 mpya za P Square

Picha 8 mpya za P Square zinazoangaliwa sana kwenye internet hivi sasa.

ddd
Peter na Paul mapacha wa P Square wanakaribia kutoa album yao ya sita na hivi sasa wametoa picha zao mpya ikiwa ni moja ya promotion kuelekea uzinduzi wa album hiyo.
Kama wewe ni shabiki wa P Square enjoy kucheki hizi picha.
0
1
2
3

5
6
7

DIMPOZ AWACHANGANYA JOKATE, VENESSA MDEE!

DIMPOZ AWACHANGANYA JOKATE, VENESSA MDEE!


 Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money, Ijumaa Wikienda limeinyaka.
 
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akipozi kimahaba na Vanessa Mdee, 'V-Money'.
Kikizungumza na gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa Bongo, chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani.
“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema:
 
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akishow love na Jokate Mwengelo ‘Kidoti’.
“Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa mshikaji tu.”
Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.

Sunday, 24 August 2014

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JESHI

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JESHI
  August 24, 2014

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais…
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Oficer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli jana.
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.

AJALI:AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA COASTER MOROGORO

AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA COASTER MOROGORO

Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali.
Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa ndani ya gari.
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mgogo, ambaye ni dereva  wa bodaboda amegongwa gari na kufariki papo hapo, jioni hii mkoani Morogoro.Gari iliyomgonga dereva huyo ni aina ya Coaster  inayofanya safari ya Kihonda Mjini mkoani humo.