Wednesday, 22 October 2014

BIASHARA::NMB YAWAPA SOMO WATEJA WAKE MBEYA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wateja wa Nmb, Jeremia Mahenge akifungua mkutano wa umoja wa wateja wa NMB katika ukumbi wa RC Mwanelwa

Meneja Mahusiano wa NMB Makao makuu, Dickson Pangamawe, akiwapa somo wateja wake 

Mtaalamu wa Biashara ya kimataifa wa NMB makao makuu Alatunoze Sanga akitoa somo kwa wateja wa Nmb katika mkutano huo

Wateja wa NMB Mkoa wa Mbeya wakiwa makini kusikiliza somo

Afisa mikopo NMB Mbalizi Road HANCESON Kyambi akieleze sasa wanatoa mikopo ya bajaji na pikipiki kwa vijana

Wateja wa NMB makini kuwasikiliza wawezeshaji

Alex Masawe mwezeshaji toka NMB

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule akiongea na mwandishi wa habari

Picha yapamoja

BENKI ya NMB imefanya mkutano wake wa mwaka na umoja wa wateja wao(NMB BUSINESS CLUB) na kuwafundisha ujasiliamali na fursa za biashara.
Katika mkutano huo Wateja hao pia walitoa maoni mbali mbali ya uboreshaji wa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na maofisa wa benki hiyo kutambulisha bidhaa na huduma mpya kwa wateja.
Mwezeshaji katika Mkutano huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule, ambaye pia ni Mtaalamu wa Biashara na Ujasiliamali ambaye aliwafundisha wateja hao upatikanaji wa fursa na namna ya kutafuta masoko kwa wakati huu.
Senyamule  pia alitoa wito kwa Wafanyabiashara na Wajasiliamali  kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya kimataifa.
Alisema wafanyabiashara wa sasa hawapaswi kubweteka kwenye maduka yao kusubiri wateja bali wanapaswa kuzunguka kutafuta fursa zingine na kuzitumia ili kujiongezea vipato zaidi na sio kulizika na aina moja ya shughuli anazofanya.
Alisema mitandao ya kijamii ikitumika vizuri kwa wafanyabiashara itasaidia kumtafutia masoko kimataifa na kuitangaza biashara yake kwa gharama ndogo na sio kuwaachia vijana kwamba ndio wanaostahili kutumia mitandao hiyo.
Aliongeza kuwa Tanzania na Mkoa wa Mbeya kuna fursa nyingi ambazo wafanyabiashara wanaweza kuzitumia na hatimaye wakaongeza vipato vyao ikiwa ni pamoja na sekta ya Uwekezaji ambapo aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo na sio kuwaachia wawekezaji kutoka nje.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wateja wa Nmb, Jeremia Mahenge,alisema tangu umoja huo uanzishwe changamoto nyingi zimetatuliwa kutokana na Benki hiyo kupokea maoni kutoka kwa wateja wao kupitia umoja huo.
Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo zimeboreshwa kuwa ni pamoja na ongezeko la mikopo na kupungua kwa makato kwa wafanyabiashara, kupungua kwa foleni wakati wa kupata huduma pamoja na uboreshaji wa huduma ambapo hadi sasa Benki hiyo imeongeza siku za kufanya kazi.
Naye Meneja Mahusiano wa NMB Makao makuu, Dickson Pangamawe, alisema lengo la kuanzisha umoja huo ni baada ya kuona Benki inashindwa kupata maoni kutoka kwa wateja wao kirahisi pamoja na kutambulisha bidhaa zinazoanzishwa na benki hiyo kwa wateja.
Mwisho.

Na Mbeya yetu

MBEYA::KANDORO AYASHUKIA MAKAMPUNI YANAYONYANYASA WAKULIMA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,  alipokuwa akizindua umoja wa Wakulima wa Mpunga (MTAYArF) unaoziunganisha Kampuni za Mtenda rice , Tanseed na Yara katika sherehe zilizoenda sambamba na mafunzo kwa Wakulima wa Mpunga Mkoa wa Mbeya zilizofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sun Set uliopo Soweto jijini hapa.
Mkurugenzi wa Mtenda Kyela Rice Company ltd, George Mtenda, alisema lengo la kuungana ni kuwapunguzia gharama wakulima za upatikanaji wa pembejeo bila kupitia kwa madalali jambo ambalo litamsaidia Mkulima kutengeneza faida moja kwa moja.
 Mwenyekiti wa Bodi ya MTAYArF, Stella Mutagwaba, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
Wakulima wa Mpunga Mkoa wa Mbeya na wadau wa kilimo wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya
Picha ya pamoja

MAKAMPUNI  yanayofanya shughuli sambamba na wakulima nchini  yametakiwa kuwa na mikataba ambayo itawanufaisha moja kwa moja wazalishaji ili waondokane na kilimo kisichokuwa na tija kwao.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,alitoa wito huo  alipokuwa akizindua umoja wa Wakulima wa Mpunga (MTAYArF) unaoziunganisha Kampuni za Mtenda rice , Tanseed na Yara katika sherehe zilizoenda sambamba na mafunzo kwa Wakulima wa Mpunga Mkoa wa Mbeya zilizofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sun Set uliopo Soweto jijini hapa.
Kandoro alisema mara nyingi makampuni yanaingia ubia wa kushirikiana na Wakulima kwa lengo la kutengeneza faida kwa kuwanyonya na kutengeneza mikataba ambayo ni kandamizi kwa Mkulima na kuishia kuwa mtumwa dhidi ya kampuni husika kupitia mikopo ya pembejeo.
Alisema Makampuni huingia makubaliano na wakulima kwa lengo la kuwakopesha pembejeo lakini huwalazimisha kununua mazao wao wenyewe tena kwa kujipangia bei ambayo haimletei mafanikio Mkulima hivyo kushindwa kuendelea licha ya kuzalisha mazao mengi.
Alisema tabia hiyo haipaswi kuvumiliwa jambo ambalo Serikali inasisitiza wakulima kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kukopeshwa pembejeo kupitia vikundi vyao ambapo alitoa rai kwa umoja wa Mtayarf kufanya kazi na vikundi na sio mkulima mmoja mmoja ili kuepuka hujuma.
Aidha mbali na kutoa wito huo pia aliwapongeza wamiliki wa Makampuni hayo kwa kuanzisha umoja ambapo alisema kama utafanya  vema utasaidia kutoa mafunzo kwa wakulima jambo litakalochangia kuongeza uwezo wa uzalishaji na kuwatafutia masoko ya mazao yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtenda Kyela Rice Company ltd, George Mtenda, alisema lengo la kuungana ni kuwapunguzia gharama wakulima za upatikanaji wa pembejeo bila kupitia kwa madalali jambo ambalo litamsaidia Mkulima kutengeneza faida moja kwa moja.
Awali katika risala iliyosomwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Bodi ya MTAYArF, Stella Mutagwaba, alisema muungano huo ni wa kampuni tatu zinazotoa huduma katika mnyororo wa thamani wa zao la mpunga na wakulima wa Mpunga wilaya za Kyela, Mbarali na Momba.
Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Kampuni ya ununuzi wa Mpunga, usindikaji wa Mpunga na uuzaji wa mchele(Mtenda Kyela Rice supply companyltd),Kampuni ya mbegu(Tanseed international ltd) na Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania ltd.

TUNDUMA-SUMBAWANGA::UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.

Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma  –Sumbawanga.  

Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC).
Mhandisi Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma  akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa barabara ya Tunduma – Sumbawanga. 
Mhandisi Mgalula anaongoza timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo  kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Hapa anamsikiliza Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya  Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.  
Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC).

PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA

Monday, 20 October 2014

PEOPLE'S POWER:::CHADEMA YAFUNIKA IRINGA MJINI

Dk Slaa mbele ya wafuasi wa Chadema wa Iringa Mjini katika mkutano uliofanyika Mlendege mjini Iringa
Sehemu ya vijana waliohudhuria
Akisisitiza jambo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanya mkutano katika uwanja mpana wa stendi ya mabasi ya Mlandege, mjini Iringa; mkutano uliolezwa na wapekuzi wa mambo ya siasa wa mjini hapa kwamba umevunja rekodi ya mikutano yote iliyowahi kufanywa na chama hicho mjini Iringa.
Kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda wapenzi na wasio wapenzi wa chama hicho waliendelea kumiminika katika stendi hiyo na kusikiliza kile kilichohotubiwa na baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.
Mbali na  Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, mkutano huo ulihutubiwa na Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa, Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.
Wakati Mchungaji Msigwa alizungumzia mambo mbalimbali aliyofanya tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini mwaka  2010, wengine wote walizungumzia uchaguzi wa mwaka huu wa serikali za mitaa na vijiji, uchaguzi mkuu wa mwakani na dhamira ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja mmoja katika chaguzi zote zajazo.
Katika mkutano huo, Dk Slaa aliwataka wafuasi wa chama hicho kwenda kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa lengo la kuandikishwa katika daftari la kuandikisha wakazi wa kila kaya ndani ya kata.
Daftari hilo kwa mujibu wa Dk Slaa ndilo litakalotumika kwajili ya uchaguzi wa Desemba mwaka huu wa serikali za mitaa na vijiji.
“Ni haki ya kila mtanzania kuandikishwa katika daftari hilo. Daftari hilo sio la CCM wala la chama chochote, ni kwa ajili ya watanzania wote, kwahiyo akikisheni mnaandikishwa ili muwez kushiriki katika uchaguzi huo,” alisema.
Aliwasihi wafuasi wa chama hicho kutopuuza suala hilo kwani wakianya hivyo nafasi yao ya kushinda katika uchaguzi huo itakuwa ndogo.
“Kwahiyo msije mkajitokeza kuilalamikia CCM baada ya kuangushwa katika uchaguzi huo,” alisema.
Kuhusu Katiba
Dk Slaa alisema Ukawa watapita mtaa kwa mtaa na kijiji kwa kijiji pindi Katiba inayopendekezwa itakapopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
“Hata ikiletwa kesho, hatuna shida, lakini CCM ni lazima wajue kwamba tutapita kila mahali kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuikataa,” alisema na kuongeza kwamba wanaikataa kwa kuwa haitokani na mapendekezo ya wananchi.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwakani
Dk Slaa alisema Ukawa wako katika hatua za mwisho za makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja mmoja katika chaguzi zote.
Hata hivyo alisema pamoja na makubaliano hayo kutakuwa na vigezo vitakavyotumiwa ili kuwapata wagombea safi .
“halitakuwa suala la kupeana tu, eti kwasababu tumekubaliana hivyo, ni lazima tupate wagombea wenye sifaili tuweze kukabiliana vizuri na CCM,” alisema.
Ili kufanikisha chaguzi hizo, chama hicho kilisema kinahitaji rasilimali fedha na ndipo ulipotolewa wito kwa wafuasi wake kuchangia kupitia mfumo wa simu za mkononi.
“Hatuhitaji fedha nyingi kutoka kwenu, tuchangieni Sh200, 300 au 500 ili zisaidia katika harakati za mabadiliko,” Dk Slaa alisema wakati Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu aliyewahi kufanya kazi na VODACOM akitoa maelezo ya namna ya kukichangia chama hicho kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.
Itaendelea……………………………………………………………….

MBEYA::WALIMU MBEYA WAMUUNGA MKONO LOWASSA

NA GORDON KALULUNGA, MBEYA
WALIMU wa wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbeya Vijijini, wameunga mkono sera isiyo rasmi ambayo imewahi kutolewa hivi karibuni na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuwa kipaumbele cha Serikali kiwe Elimu kwanza badala ya kilimo kwanza.
Hayo yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Mbeya, Anthony Mwaselela, alipokuwa akisoma risala ya walimu katika maadhimisho ya siku ya walimu duniani-Wilaya ya Mbeya yaliyofanyika katika tarafa ya Isangati, kata ya Ilembo, mbele ya mgeni rasmi Prof. Norman Sigalla.
Mwaselela alisema kuwa, kutokana na serikali kutoweza kuwekeza kikamilifu katika elimu, walimu kwa sasa wanachopata na kukifurahia kwa taaluma yao ni neno Shikamoo.
“Nchi zilizowekeza kwenye elimu kwanza, ndizo zinazotisha kimaendeleo duniani mfamo China, hata sisi tunaweza kutoa tamko maana hatujachelewa, twaweza kimbia, elimu kwanza badala ya kilimo kwanza” alisema Mwalimu Mwaselela.
Alisema katika wilaya ya Mbeya inakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na kutowekeza katika elimu, ikiwemo suala la nyumba za walimu, madawati, ofisi za walimu, vyoo, madai ya fedha za likizo, kuchelewa kupanda madaraja hasa kwa walimu wanaojiendeleza na malimbikizo
Kuhusu nyumba za walimu alisema mahitaji ni nyumba 1906, zilizopo ni nyumba 477 nazo zina hali mbaya, mahitaji ya vyoo vya walimu ni matundu 373, yaliyopo ni matundu 267 yenye hali mbaya na madawati mahitaji ni 21931, yaliyopo ni 17328 lakini nayo yana viraka.
“Hali hii inatokana na kutowekeza katika elimu. Kutojipanga vizuri kwa serikali upande wa elimu kiuwekezaji, kumesababisha walimu wengi kuwa na kero nyingi zinazowavunja moyo kiutendaji na hata kuwafanya vijana wengi kutopenda kazi ya ualimu pamoja na kuwa na heshima nyingi za Shikamoo”alisema Mwaselela.
Akijibu risala ya walimu hao, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Prof. Norman Sigalla, alisema kitaalamu mwalimu bora zaidi ni yule wa shule ya Msingi akifuatiwa na mwalimu wa Sekondari.
Alisema changamoto za walimu walizosema mbele yake ni halali lakini tatizo ni uwoga wa walimu kueleza kero zao kwa viongozi wanaohusika, ambapo kwa wilaya hiyo, asilimia 90 ya walimu hawajawahi kufikisha malalamiko yao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ambaye ni mwajiri wao na kiongozi wa serikali ambaye ni yeye Mkuu wa wilaya.
Akielezea tatizo la walimu kutopandishwa madaraja kwa wakati alisema kuwa, tatizo siyo la kimfumo kama walimu wanavyotafsiri, bali ni kutotimiza wajibu wa baadhi ya watumishi wanaohusika katika suala hilo na bahati mbaya walimu wananungunika badala ya kufikisha malalamiko yao kwa viongozi wa serikali hasa ofisi za wakuu wa wilaya.
“Nisisitize kwenu walimu wenzangu kuwa, serikali yenu ya CCM, ina lengo zuri, bali wakosaji wengi wa utumishi wa umma wanapokosea wanasingizia wegine. Wakiwazungusha na kuwajibu kwa dharau, njoo ofisini kwangu, maana Mkuu wa wilaya ndiye mwenye serikali”alisema mkuu huyo wa wilaya.
Alisema katika ofisi yake anapokea walevi, wavuta bangi na watu kadha wa kadha kwa ajili ya kusikiliza hoja wala siyo ulevi au uchafu wa mwonekano wa mtu, na akahoji sembuse Mwalimu?

baada ya hotuba yake, aliendesha harambee ya kuchangia madawati ya shule za msingi za tarafa hiyo ambapo zilipatikana Milioni Shilingi sita.

UCHAMBUZI WA KISIASA>>SAUTI YA NYIKANI..... MWAITELEKE, KIJANA MSOMI ANAYETAJWA MBIO ZA UBUNGE MBEYA MJINI

NA GORDON KALULUNGA
WIKI hii ni wiki ya Vijana, Rais Jakaya Kikwete, wakati anazima mwenge wa uhuru mkoani Tabora mwanzoni mwa wiki na kumbukumbu ya miaka 15 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, alisema vijana ndiyo wanufaika wakubwa na Tanzania ijayo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, akiwa mjini Dodoma wakati wa semina za makatibu wa CCM nchi nzima katikati ya wiki hii, amewaambia kuwa katika ngazi zao za uteuzi wawe makini kupendekeza majina ya watu wanaokubalika na jamii badala ya fedha.
Ukitaka kuwaudhi baadhi ya viongozi wa CCM, ambao wamezoea kufikiri kidogo badala ya kufikiri sana, waulize swali la kwanini majimbo ya upinzani yanaongezeka.
Wanaishia kusema kuwa ni kutokana na makundi ndani ya chama, badala ya uhalisia kuwa rushwa katika ngazi za uteuzi imetawala, hivyo watu wanaokubalika katika jamii wasio na fedha huachwa.
Leo sauti ya nyikani inatokea mkoni Mbeya na kuangaza upepo wa kisiasa uliopo jimbo la Mbeya mjini.
Kwa sasa Jimbo la Mbeya Mjini lipo chini ya Chama cha demokrasia na Maendeleo(Chadema), na Mbunge wake ni Joseph Mbilinyi.
Mbunge huyu amekuwa akipongezwa na baadhi ya wananchi kuwaletea maendeleo katika kata zao kwa kile wachambuzi wa masuala ya siasa mkoani hapa wakisema anatumia vema hasa usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo.
CCM, inahaha kulirejesha jimbo hilo katika himaya yake, lakini kitendawili kinabaki miongozi mwao kuwa ni nani mwenye kuwaunganisha wote, ukizingatia kuwa asilimia sabini ya wajumbe wa kamati ya siasa ambayo ni kikao cha maamuzi kwa watakaohitaji kugombea nafasi hiyo nao wanatajwa kuwemo kwenye mstari wa safari hiyo ya matumaini.
Baadhi ya watu wanaotajwa kuwemo katika kinyanganyilo hicho cha ubunge nje ya kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Mbeya mjini ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la nyumba Tanzania(NHC), Nehemiah Mchechu, Mwenyekiti wa saccos kubwa Jijini Mbeya, (UWAMU SACCOS), Rodrick Y. Nyaluke na mjasiliamali kijana, Nwaka Mwakisu.
Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Newala, Christopher Magala na Mtaalamu wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathimini, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM – TAMISEMI), Eliurd Leonard Mwaiteleke.
Leo nikianza na kijana Eliurd Mwaiteleke, anatajwa katika mbio hizo za kuweza kupeperusha bendera za CCM katika jimbo hilo la Mbeya Mjini kwa nia ya kukomboa jimbo, huku baadhi ya vijana wakimpa ‘‘dole’’, ukizingatia kuwa ni kamanda wa UVCCM kata ya Sinde Jijini Mbeya na alipendekezwa kuwa kamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya, akuweza kufanikiwa kutokana na umri wake.
Kabla sijaandika makala haya, nilijaribu kumtafuta na kutaka kujua wasifu wake, mbali na kukataa kuwa ni mmoja wa waliotangaza nia katika jimbo hilo, alisema kuwa yeye ni mtoto wa masikini lakini jitihada zake zimemfikisha hapo alipo.
Mwaiteleke alizaliwa May 28, 1977,  eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya, mwaka 1986 alipelekwa kujiunga na shule ya Msingi Salemu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuhitimu mwaka 1992, kisha akajiunga na shule ya sekondari Ivumwe Jijini Mbeya kati ya mwaka 1993-1996 na mwaka 1997 na 1999 akajiunga na kidato cha tano na sita shule ya Sekondari Malangali
 Kijana huyu, anasema kwa sasa ana elimu ya Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Maendeleo ya Sera (Master Degree of Science in Development Policy (MSc.DP), aliyotunukiwa katika Chuo Kikuu Mzumbe, baada ya kusoma tangu mwaka 2009 – 2011, akitokea Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (Institute of Rural Development Planning - Dodoma (IRDP) baada ya kuwa na cheti na stashahada ya juu katika masuala ya mipango na mazingira.
Kijana huyu pia ni mtaalam wa masuala ya Ukusanyaji Takwimu Muhimu za usafi wa Mazingira, mtambuzi wa walengwa wa njaa  na ugawaji wa chakula na mwibuaji na msimamizi wa miradi ya kijamii kwa jamii iliyoathirika na UKIMWI.
Mwaiteleke anaonesha hulka na akipendacho kuhusu mipango na masuala mengine muhimu ya  mwelekeo wake kuwa ni kuungana na vijana wenzake kusaidiana mambo ya maendeleo kwa kutumia ujuzi na elimu aliyonayo hasa kuelezana kuhusu fursa zilizopo, changamoto na namna ya kuzifikia pamoja na kuzitatua ili wapate maendeleo yanayotarajiwa.
Kuhusu heshima ya Mbeya anasema, ni vema vijana wa mkoa wa Mbeya, wakatambua namna wazee wao jinsi walivyojenga heshima ya Mkoa wa Mbeya na namna wao wanavyoweza kusaidia kurudisha heshima na hadhi ya Mbeya inayopotea siku hadi siku.
Anaamini katika juhudi kwa kila jambo ili kuweza kuleta tofauti katika maisha ya jamii nzima ya wana Mbeya, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mijadala ya wazi kwa vijana katika Nyanja mbalimbali.
Nyanja ambazo anazipa kipaumbele katika mijadala ni pamoja na masuala ya maendeleo ya elimu (tathimini ya elimu katika mkoa), afya, Mazingira na usafi wa Jiji la Mbeya, ukuzaji kipato cha jiji na kuwafikia wananchi, Miradi ya maendeleo, fursa za mikopo kwa vijana na wanawake na namna ya kuzikifikia.
“Tulikuwa na viwanda Jijini Mbeya, leo hii vimepungua, ni suala ambalo pia linahitaji mijadala kwa ajili ya kujua namna vinavyoweza kutengeneza ajira kwa vijana, kuanisha mapungufu yanayokwamisha maendeleo ya Mkoa na Kuanisha mapungufu na changamoto zinazowakabili vijana” anasema Mwaiteleke.
Anasema angependa vijana wawe na mwanga wa kutambua masuala ya jiji , uwajibikaji wake pamoja na ubunifu wa kiutendaji, kujua kufanya mapitio ya mipango inayopangwa kila mwaka kama inaleta tija kwa kundi kubwa la vijana ama la.
Kwa upande wa mtazamo wake kuhusu wazee anasema ni muhimu kutambua mahitaji halisi ya wazee na vipaumbele vyao na jinsi ya kuwatekelezea mahitaji yao bila kusahau masuala ya akina mama na vipaumbele vyao.
Hasiti kueleza kuhusu masuala mtambuka ya VVU, kilimo na fursa ya kilimo cha maua kwa vijana hasa ukizingatia fursa ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe na fursa za wasomi waliopo na wajasiliamali.
Huyu ndiye kijana Eliurd Mwaiteleke, ambaye anatajwa kuwa na nia ya kuipeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Mbeya Mjini kwa lengo la kulikomboa Jimbo kutoka mikononi mwa Chadema.
Wiki ijayo tutamwangalia kijana mjasiliamali na mpenda michezo kwa vijana wenzake Nwaka Mwakisu.

Sunday, 19 October 2014

HABARI::JK ahitimisha Mafunzo ya Wakongo...Atunuku kamisheni kwa watanzania 23

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Kitanzania 23 miongoni mwa maafisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo liliwajumuisha maafisa wa kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka Kongo.

Jumla ya wanajeshi 414 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  leo (18/10/2014 wamehitimu mafunzo ya Uafisa katika chuo cha maafisa  (TMA) Monduli baada ya kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja.
Maafisa hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa watanzania 23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu baada ya kula kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Tofauti na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 23 .
Aidha, leo hii kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi kutunukiwa kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa  wa kongo wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na wakiwa katika ardhi yao, hivyo wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.
Akitoa shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye alishuhudia maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru kwa kukubali kutoa mafunzo kwa maafisa hao.
Pia alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia kuimarisha usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha amani nchini Kongo.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mlongo, majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond Tshibanda N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma Alfani, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa Mafunzo, ya Kijeshi,  brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.

IRINGA>>MSIGWA: KINANA AMETUSAIDIA KUPONDA MAWE MAGUMU

 Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt.Yahaya Msigwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Iringa kuhusu ziara ya siku sita ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya mkoani hivi karibuni. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
NA FRIDAY SIMBAYA
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt. Yahaya Msigwa amesema kuwa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya mkoani hapa imesaidia kuponda mawe magumu na kutuachia mawe madogo madogo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mawe magumu hayo ndani ya chama katibu mwenezi huyo wa mkoa alisema kuwa ziara ya siku sita ya kinana kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zinakikabili chama hicho.
Alisema kuwa kiongozi huyo wa kitaifa aliwapa fursa wananchi kuuliza maswali ambayo yamesadia kuibua changamoto mbalimbali na wao kama chama mkoa kero hizo wanaendelea kuzifanyia kazi.
“Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye walikuwa katika ziara ya siku sita mkoani Iringa kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi,” aliongeza katibu mwenezi wa mkoa huyo.
Aidha, katibu mwenezi huyo wa mkoa alisisitiza viongozi kuwa karibu na wananchi ili kuweza kusikiliza matatizo yao kuliko kukaa ofisini kuhusu kuletewa kero hizo ofisini.
Alisema kuwa katibu mkuu kinana alisisitiza umuhimu wa kuweka viongozi wanaokubalika na wananchi pamoja kuheshimu moani ya wananchi ili kusimamisha viongozi  wanaokubalika  kwa kufuata katiba, kanuni na taratibu za chama.
Wakati huohuo, Katibu Mwenezi CCM Mkoa, Dkt. Msigwa aliwaasa wananchi kujiandikisha katika daftari ya mpigakura ili wawezekushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema kuwa ni lazima wananchi wa hakikishe wanachagua viongozi wazuri wanaotokana na chama cha CCM ili kuweza kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu  kama tunu aliyetuachia Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.