Monday 10 November 2014

HABARI::WAZIRI MKUU ATAKA VITA DHIDI YA UJANGILI IWE YA PAMOJA

IMG_5158
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga Mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu na wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

* Ataka iundwe timu kufuatilia utekelezaji wa Azimio la Arusha 2014

Na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii kama kweli tunataka tuitokomeze.”

“Kwenye hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,” alisema.

Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20 ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi na kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

IMG_5160
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akielekea kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.

“Nimepata faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau wa maendeleo,” alifafanua.

Ili kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake. Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji huo,” alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili katika ukanda huu.

IMG_5167
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

“Tumeanzisha vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.

“Nakubaliana nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.

Alisema Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa Azimio hilo unakuwa wa ufanisi.
Jumla ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

IMG_5170
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, huku Waziri wa Mali asili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifurahi jambo ndani ya chumba cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mikutano.

IMG_5169
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli (wa pili kulia) kwenye chumba cha mapumziko baada ya kuwasili ukumbi hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.

IMG_5182
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye chumba maalum cha mapumziko.

IMG_5253
Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kushoto) kufunga rasmi mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magese Mulongo, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli wakiwa meza kuu.

IMG_5264
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014 wakati akifunga rasmi mkutano huo wa siku mbili.

IMG_5198
Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania akichukua taswira za baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea mkutanoni hapo.

IMG_5197
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo.

IMG_5236
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi tisa wakitia saini Azimio la Arusha la kukabili ujangili mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

IMG_5205
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwenye ufungaji wa mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

IMG_5224
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, akizungumza kwa niaba ya serikali ya Ujerumani.

IMG_5212
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu wakati wa ufungaji rasmi wa mkutano huo uliodumu siku mbili jijini Arusha.
IMG_5268
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka ukumbini hapo mara baada ya kuufunga rasmi mkutano huo.

VIPI TENA::KUNA MTU KAIBIWA???

VIPI TENA::KUNA MTU KAIBIWA???

TUNZA MAZINGIRA:::PANDA MITI

WACHA MUVI IENDELEE::MISS TANZANIA EPISODE 2.

Baada ya kuvuliwa taji aliyekuwa miss Tanzania Sitti mtemvu kwa kughushi umri...nafasi ya mimi Tanzania imenyakuliwa na Mshindi wa pili Lilian Kamaziama

Lakini  mshindi huyu wa pili naye inasemekana sio raia wa Tanzania ni mnyarwanda. LILIAN nini mtoto wa generali wa jeshi KAMAZIAMA ambaye inasemekana sio mtanzania ni mnyarwanda na mmoja wa makamanda na jasusi wa jeshi la kinyarwanda aliyepenyezwa na raisi Kagame.

MICHEZO::Ushahidi wa Azam FC kukipokea kifaa kipya kutoka Ivory Coast.

k1
Unaambiwa Azam FC wameshamshusha bongo huyu mkali wa soka kama inavyoonekana kwenye picha na wanatarajia kumsajili  beki huyu wa Ivory Coast aitwae Serges Pascal Wawa Sfondo akitokea klabu ya El Mereikh ya nchini Sudan.
Ameingia na ndege ya saa nane usiku wa kuamkia November 10 2014 ambapo millardayo.com na AyoTV ilikua kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam kuhakikisha stori haipiti bilabila.
Imeshindikana kumpata sana Pascal akizungumza kwenye interview kwa sababu hajui kuzungumza lugha nyingine tofauti na za Kiarabu na Kifaransa alizozizoea.
k2
Club alizozichezea ni ASEC Mimomas kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 alipojiunga na Al-Merrikh ya Sudan ambapo kwa mujibu wa mtandao, hajawahi kuzifungia timu hizi goli lolote.
k3
Umri wake ni miaka 28, alizaliwa January 1 1986.
k4
Kwa leo utanisaheme manake picha hazikua kwenye ubora unaotakiwa.
Screen Shot 2014-11-10 at 4.29.23 AM

Saturday 8 November 2014

MAISHA NI NYUMBA::NSSF YAKABIDHI NYUMBA KWA WASANII WA ORIJINO KOMEDI

Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery 'Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Mac Reagan 'Kipara' na Mjuni Silvery 'Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki wakiangalia nyumba zao walizokabidhiwa na NSSF.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akimkabidhi funguo ya nyumba msanii wa Orijino Komedi.  

Msanii Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga' akipokea funguo ya nyumba yake.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akipokea funguo ya nyumba yake kutoka kwa Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia)
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa wasanii kikundi cha Orijino Komedi.
Msanii Mac Reagan akizungumza baada ya makabidhiano ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba.