Thursday, 14 August 2014

KITUKO CHA MWEZI:AMEZA SIMU KISA MESEJI ya mchepuko.

Kwenye vile visa vya mapenzi na simu… hii nayo ilivunja rekodi

Screen Shot 2014-08-01 at 8.50.06 AM
Kuna zile habari ambazo hata ziwe zimetokea miezi au miaka mingapi nyuma, huwezi tu kuzisahau kwa sababu sio za kawaida kuzisikia au kuzishuhudia kabisa.
Screen Shot 2014-08-01 at 8.33.09 AM
Tumekua tukisikia visa vingi sana vinavyotokana na mapenzi, yani pale Mwanamke au Mwanaume anakuta msg za ajabu baada ya kuchukua simu ya mpenzi wake ila hii ya Brazil ilivunja rekodi.

Ilitokea kwa binti mmoja kumeza simu muda mfupi tu baada ya boyfriend (Renato) wake kutaka kusoma msg ambapo msichana alikimbia na simu kutoka kwenye mikono ya boyfriend na kuimeza kwa kuhofia angeikamata simu.
Ilibidi akimbizwe hospitali na kufanikiwa kutolewa hiyo simu tumboni ambapo haikujulikana ni nini ambacho mrembo huyu alikua anakificha kwa boyfriend wake ila iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani kwamba tayari mrembo huyu alikua na mwanaume mwingine nje ya uhusiano.