Wajumbe wa Bunge la Katiba waaswa kurejea Bungeni :
August 16, 2014
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi
wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema
akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba
wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa
kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Jaji
Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi
kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo
kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza
bunge hilo.
“Sheria
inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba
kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na
kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji
Werema.
Pia
Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi
kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza
kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha,
Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili
muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji
wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza
kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
Mwisho.