August 30, 2014
WATAKIWA KUZAA WATOTO KWA MPANGO NA SIYO BAHATI.
Watanzania
wametakiwa kuzaa watoto kwa kwa kupanga na siyo kwa bahati mbaya kama
wenge wao wanavyosema ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana kwamba
kila mtoto anazaliwa na Bahati yake.
Wito huo
umetolewa leo na Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr Valentino Bangi wakati
wa ufunguzi wa Zahanati wa Marie Stopes uliofanyika katika katika
wilaya ya Nyamagana.
Dr Bangi amesema
kuwa watanzania wengi wamekuwa na mazoea ya Kuzaa watoto wengi licha ya
kwamba hawana uwezo wa kuwatunza hali inayopelekea ongezeko la watoto
waishio katika mazingira Magumu.
Katika hatua
nyingine Dr Bangi ametoa wito kwa makampuni ya Bima ya Afya kutumia
uwepo wa zahanati hiyo kuwekeza katika afya na kuwataka vijana jijini
Mwanza kutumia Zahanati hiyo kupata Elimu ya Mapambano ya virusi vya
ukimwi.
Awali akisoma
Hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Rasilimari watu wa Marie Stopes
iliyosomwa na Bi Elly Reweta,amesema kuwa Zahanati hiyo itatoa huduma
zote za matibabu ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi kwa vijana iliyopewa
jina la CHAGUA MAISHA THE GOOD LIFE.
Uzinduzi wa
Zahanati hiyo jijini Mwanza una kamilisha idadi ya Zahanati kumi katika
mikoa mbalimbali nchini zinazomilikiwa na Marie Stopes ikiwa ni pamoja
na Hospitali kubwa moja iliyopo jijini Dar es Salaam.
na fredy mgunda
No comments:
Post a Comment