Leo naomba tufanye uchambuzi wa timu ya kampeni ya bwana Edward Lowassa..... kwa hakika mpaka sasa yeye ndiye anaongoza kwa kuwa na nguvu ndani ya CCM, anaongoza kwa kujipanga zaidi na vizuri, anaongoza katika mikakati mizuri sana, anaongoza kwa kushika media zote kasoro Uhuru na magazeti ya serikali na hata katika kura za maoni Lowassa ndio kinara (REDET august 2014 report, ITV survey july data).

Katika timu ya kampeni ya huyu jamaa naweza kuilinganisha na timu kama David Plouffe & Co., kama Chriss Hunges, Digital Wizards (Rejea Obama 2008 kampeni)...naomba tuwalete kwa uchache tu

1. Mzee Apson
Huyu kila mtu anafahamu umahiri wake, amekuwa mkurugenzi wa usalama na ndicho kipindi usalama wa taifa wa Tanzania ulikuwa imara sio tu Tanzania ila na nchi za Africa kote...ni kipindi hichi usalama wa taifa uliweza kulisaidia dunia katika vita ya ugaidi katika kanda hii yote ya Africa na Latin America, na ukisoma kitabu cha Ogot (2012), katika kitabu chake cha current African story to the World anasema pamoja na Tanzania kupata hizo sifa lakini Mzee Apson Mwangonda alistahili pongezi zaidi na zaidi kwa kazi aliyofanya ya kuimarisha amani katika maziwa makuu na kujenga imani kwa nchi za magharibi kwamba africa mashariki kwa ujumla imekomaa katika usalama hasa wa ushushushu; sasa huyo ndio leo ni mwenyekiti wa kampeni ya Lowassa ebu jaribu kupata picha ninayopata sasa hivi...

2. Bashe
huyu ni kijana mdogo kwa umri ila sikufichi ni mkubwa kwa matendo.. wachambuzi wa siasa wanakuambia ukimtoa mzee lowassa na kikwete katika hii karne hakuna mtu mwingine mbaya wa siasa za chini kwa chini kama Hussen Bashe.. Ni kijana ambaye akitaka kitu chake lazima akifanikishe iwe kwa kutumia fedha kiasi gani, kwa kutumia njia yoyote ile isipokuwa kuuwa tu... Umuhimu wake katika kambi hii ni kwamba huyu jamaa amekamata media zote yaani kwa maana nyingine magazeti yote kayakamata pamoja na vituo vya habari kasoro uhuru redio, na clouds... Kwa upande wa magazeti ndio usisema anatumia fedha nyingi sana kuweza kuwa maintain ukienda mwananchi yuko Bakari pale, ukienda mtanzania kawajaza watu wenye weledi mkubwa kama Kibanda, na Msaki, ukienda Nipashe yuko Jesse, yaani kwa kifupi jamaa ndio nguzo ya media katika nchi hii......(niwape mfano kidogo juzi pinda alivyotangaza kisiri kesho yake magazeti manane makubwa yote yalikuja na hiyo story).

Huyu jamaa
wanakuambia wajumbe wengi wanampenda kwa sababu ya roho yake ya huruma, akiwa na elfu ishirini atakupa elfu kumi na saba na yeye kubaki na elf tatu tu kitu ambacho wengine hawawezi hata kidogo.

3. Serukamba
huyu ni kijana mwenye msimamo zaidi na zaidi, na hasa kwa kuwa anatoka kigoma wanasema msimamo wake sio wa kuyumba (kumbuka watu wa kigoma hawabadiliki na ni viburi sana)... mchango wake mkubwa ni kuwa na msimamo dhabiti usiyo yumba hata kidogo, ni Serukamba aliweza kumwambia January Makamba ukweli kuwa January ni mnafiki hiivyo hastahili kuwepo kwenye hiyo kambi atoke mara moja..... Ni huyu jamaa ndio alimwambia january kuwa nafasi anayotaka kwa Lowassa wa uwaziri mkuu 2015 haumtoshi kwani hana uwezo na bado anaitaji kufanya kitu cha ziada ili watanzania wamuamini, ila sio kupata cheo cha unaibu then unaibuka nafaa kuwa PM.

4. Mzee Chizi
kama umekulia ndani ya ccm uwezi kutofahamu uwezo na umahiri wa mzee chizi..amekuwa mkufunzi wa chama katika miaka mingi sana hivyo ni mtaaluma wa chama anayejua chama vizuri, anayejua misingi ya chama, anayejua conceptual za chama, anayejua theories za chama, anawajua wanachama na misimamo yao... kwa kifupi ni mwanachama wa muda mrefu anayeheshimika katika chama.

5. Karamagi
huyu jamaa kwa kifupi kazi yake ni moja tu, ambayo ndio ilikuwa ni kazi yake 2005 kipindi cha JK, ni kukusanya wanasema mapene, wengine wanaita fedha, dungula, money, pesa na vitu kama hivyo. kipindi cha JK ndio alikuwa mbongo (not Asian origin or colour) aliyetoa fedha nyingi katika kampeni hizo.

6. Rostam Aziz
kila mtu anamfahamu huyu jamaa.. ni tajiri namba moja Tanzania.. kati ya matajiri watatu kutoka Africa waliotengeneza ela zao na sio za kurithi ni huyu bwana, Kirubi kutoka Kenya, na Ndegwa kutoka Kenya pia...katika hizi kampeni kazi yake sio kutafuta au kukusanya pesa kama karamagi bali ni kutoa fedha yeye mwenyewe kama rostam....ni mmiliki wa voda kwa asilimia kubwa, crdb yupo kwa asilimia kubwa pamoja na Caspian hivyo umfanya awe na ela nyingi sana, na ela zake upitisha kwa bwana Bashe kwa kuwa saizi amepata tender nyingi sana za kujenga huko Asia, latim America na Sudan kusini. sylogan yake kubwa ni Money Talks

7. Asian Group
Hili group lilijitoa kwa hali na mali kufanikisha kampeni za JK 2005 kwa kutoa fedha nyingi sana sana kama wakina Patel et all....... ila baadaye jamaa waliwageuka na kuwapa mashataka ya EPA wakati dhumuni la fedha hizo zilikuwa za kampeni, kwa hiyo majamaa wamekasirika sana na sasa wamehamisha majeshi kwa Lweiganan... hawa watu kama tunavyojua ni wazuri sana wa kutoa fedha hasa kwa ajili za kampeni Moja wao nilimsikia ofisini kwake akiwaeleza wenzake "huyu mtu sio mtu iko nafiki sana, tumesaidia sana sana ila saizi aacha sisi, iko hakuna shida sisi 2015 iko shinda tena bila problem".

8. Sophia Simba
huyu ni komandoo wa NEC anaitwa hivyo.. kazi yake kubwa ni kuongoza majeshi NEC ili jina la mzee linarudi na kisha kupata ushindi.... aliwai kusema ndani ya NEC kuwa hakuna mwanamume katika ndani ya ccm zaidi ya Lowassa huku mkulu alikuwa ndani ya hicho kikao.....ni jembe la jembe na zaidi ya yote ni mtoto wa ilala....

9. Wanndishi wa habari
hili ni group muhimu sana wakiongozwa na Kibanda, Msaki, Pasco, Bakari na kwa sasa bbc iliyoanzishwa hapa nchini.


NB: Kipindi ccm wanawapiga ban viongozi wake wakijua watammaliza Lowassa, walisahau kuwa jamaa kaanza kazi hii tokea 2008 ya kujipanga.

- Membe sasa kanyosha mikono hawezi gemu na sasa kumsapoti Pinda, hii ni baada ya familia ya JK kuacha kumsapoti kwa kuwa jamaa hauziki hata kidogo, hana mvuto wa kisiasa, na zaidi kusapotiwa na familia ya salma imemfanya aonekane ni mtu wa kubebwa bebwa tu wakati wanaume wanapigana wenyewe...Hatuwezi kumpa nchi mtu dhaifu tena na tena...........