UTAFITI WAIBUA MAKUBWA NGONO ZA UTOTONI DAR
Posted September 1, 2014
Mratibu
wa mradi wa PREPARE ambaye pia ni Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili, Kitengo cha magonjwa na afya
ya akili, Lusajo Kajula (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) baada ya kukamilisha SAMPULI tathmini ya matokeo ya
mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana
kupunguza ngono mwishoni mwa wiki kwenye kituo cha maelezo ya afya
Muhimbili katika idara ya magonjwa ya akili. Kulia ni Mtathmini kiongozi
wa mradi huo, Mrema Kilonzo.
Mtathmini
kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni mwandishi
wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro akiuliza swali kwenye
mkutano huo.
SAMPULI
tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia
uwezekano wa vijana kupunguza ngono, imebainisha haja ya elimu ya afya
ya uzazi kukabili hali ya sasa ya tabia hatarishi zinazowakabili vijana
wadogo.
Matokeo ya
awali ya mradi yalionesha kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa miaka
12 mpaka 14 ambao ni darasa la tano na sita waliofanyiwa utafiti
walikuwa wameshawahi kufanya ngono na asilimia kubwa ikiwa ni kwa
kutumia njia ya haja kubwa.
Kauli hiyo
imetolewa na mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
shirikishi cha Muhimbili,Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo
Kajula.
“Vijana wengi
walionekana wakifanya ngono ya uke na ya mdomo ikifuatiwa na ngono ya
njia ya haja kubwa Kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia
6.3 wamefanya ngono ya njia ya haja kubwa wakati asilimia 93.7
hawajawahi.”
Aidha alisema
utumiaji wa kondomu ulionekana kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao
wameanza kufanya ngono.“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono
hawajawai kutumia kondomu kabisa wakati asilimia 32 wamewahi kutumia
kondomu.”
Alisema
utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Vyuo
Vikuu vya Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini,
Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha nchini
Uingereza.
Alisema
utafiti umeonesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana
wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa
mfumo wa kisaikolojia ili waweze kujitambua na kuacha kufuata nadharia
za kisayansi pekee ambazo ndizo zinazotumika katika shule mbalimbali
kuwaeleza mabadiliko ya miili yao.
Katika
utekelezaji wa utafiti huo idadi ya wanafunzi 5,099 walichaguliwa
mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo ambapo wanafunzi 4783 (asilimia
93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4370 (asilimia 85.8)
walifuatiliwa kwa miezi 12.
Utafiti
ulionesha elimu inayojishughulisha na masuala ya ujinsia na afya ya
uzazi kwa vijana wadogo itumie mtazamo mpana utakaoleta mabadiliko ya
msingi kwenye misingi ya virekebisho vya mabadiliko ya tabia.
Mradi huo wa
PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka manispaa ya Kinondoni
zilizochaguliwa kwa kutumia taratibu sampuli mtawanyiko zilizopangwa
katika makundi mawili ya shule za mwingilio yaani ilikotolewa elimu hiyo
zilizokuwa 19 na za kulinganisha zilizokuwa 19.
Ili kuweza
kupata matokeo yaliyokusudiwa mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano
wakufunzi wa wakufunzi; ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na
waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya
katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza muingiliano.
Tathmini
iliyotoa majibu ya jinsi utendaji unavyoendelea na ya matokeo ilihusisha
shule zote na wanafunzi zaidi ya 6,000 waliowekwa kwenye muingiliano,
huku uchambuzi wa tathmini ukihusisha wanafunzi wenye umri wa miaka
12-14, wenye kujua kusoma na kuandika.
Matokeo
yaliyotathminiwa ni Mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono) na
Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwisha anza
ngono.Kwa wastani mradi uliona kwamba mwingilio wa PREPARE ulipunguza
uwezekano wa vijana wadogo (wavulana na wasichana) kuanza ngono na
kuongeza uwezekanao wa kutumia kondomu kwa wale walioanza.
Hata hivyo,
katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua
yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio
ukilinganisha na wale ambao hawakupata mwingilio.
Uchukuaji wa
hatua ulisababisha tabia ya kutumia kondomu miongoni mwa wanafunzi wa
kiume lakini siyo miongoni mwa wanafunzi wa kike.“Kimsingi tunataka
kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya mradi wa
PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa kiume na
wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika mkoa wa Dar es Salaam,
Tanzania;
“Kuongeza
uchukuaji wa hatua ulio chanya katika kutumia kondomu kwa jinsia zote na
taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa
kiume. “Mradi huu uliofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, Programu ya
utafiti wa afya umelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya
utamaduni na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya
uzazi miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 12-14 kwa kutumia
shule kama njia ya kufundishia.
No comments:
Post a Comment