CHICHARITO ATUA RASMI REAL MADRID
Posted September 1, 2014
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Mexico, Javier Hernandez 'Chicharito' (kushoto) na Florentino Perez (kulia) wakisaini mkataba baada ya uhamisho wa mkopo kutoka Manchester United kwenda Real Madrid leo.
Florentino Perez (kulia) akimkabidhi Chicharito (kushoto) jezi namba 14.
Javier Hernandez akiwa katika vipimo vya afya leo mjini Madrid.
Hernandez akisaini jezi za mashabiki wa Real Madrid.
MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa mkopo
kwenda Real Madrid pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa moja
kutoka Manchester United baadaye.
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza moja kwa moja mchezaji
huyo, lakini kwa mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa msimu, Louis
van Gaal anachukua Pauni Milioni 1.5.
United imethibitisha katika ukurasa wake wa Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwenda Real Madrid.
No comments:
Post a Comment