Sunday, 7 September 2014

MAMBO YA SIASA:::ZUBAA UCHEKWEE...WANNE WA CHADEMA WAENDA CCM IRINGA...

September 7, 2014


 KATIBU WA CCM MKOANI IRINGA HASSAN MTENGA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA MIGOLI
MMOJA YA VIJANA WAOJIUNGA NA CCM NA KUACHANA NA CHADEMA ANAITWA  BENI HOYA AKIWA NA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA HASSANI MTENGA
 MTENGA AKIIPOKEA KADI YA WAPINZANI KUTOKA KWA BENI HOYA WA KATA YA MIGOLI
               BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA MIGOL 

Akiwahutubia wananchi wa kata ya migoli katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa iringa HASSANI MTENGA amewataka wananchi wa kata ya migoli wilaya ya iringa vijijini kuwa makini katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni na kuongeza kuwataka kuungana katika kazi za kimaendeleo ili kuleta maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katibu huyo amesema kuwa wananchi wa migoli wanahitaji maendeleo na kuongeza kuwa hawatakuwa na maendeleo ikiwa na migogoro baina yao itaendelea na kuwataka wananchi kukaa pamoja na kuijenga kata hiyo.

Hata hivyo baadhi ya vijana wapatao wanne wa kata hiyo waliamua kurudisha kadi zao za chama upinzani cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kutokana na maneno makali yenye ukweli wa maisha ya mtanzania yaliyotolewa na katibu chama cha mapinduzi mkoani iringa.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo HESSEINI KISWILI amesema kuwa toka ameingia madarakani amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu na kuwafanya wanafunzi wa kata hiyo kusoma kwa utulivu na mazingira yaliyo salama.

Aidha KISWILI ameongeza kuwa upande wa afya nako wameboresha na kuokoa maisha ya wananchi wa kata hiyo kwa kuwapa gari la kubebea wagonjwa na kupunguza vifo vya akina mama ambavyo vilikuwa vikitokea hapo awali na kuongeza kuwa wafamenya kazi kwa kujenga nyumba za waganga sehemu zote zenye huduma ya afya.
Wakizungumza baada ya kujiunga na chama cha mapinduzi vijana hao walisema kuwa vijina wengi wamekuwa wakiiga mikumbo na kuingia kwenye vyama vya upinzani bila kujua faida na hasara za kuingia huko 
 
vijana hao wameongeza kuwa wamekuwa wakijiingiza kwenye maandamano yasiyo na faida kwao na kusababisha kurudisha maendeleo nyumba hivyo wamewaomba vijana wengine kufanya maendeleo na kuacha kuandamana basipo sababu za kuleta maendeleo
MWISHO.
NA FREDY MGUNDA

No comments:

Post a Comment