September 7, 2014
Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw.
Emmanuel Boaz(wa kwanza kulia) akiwaeleza waandishi wa habari(Hawapo
Pichani) sababu zilizopelekea kutoa toleo jipya la sarafu ya shilingi
500, ambapo alisema noti ya shilingi 500 inatumika zaidi kwenye
manunuzi ya kawaida ya kila siku hivyo hupita kwenye mikono ya watu
wengi na kuchakaa haraka,noti hizi hukaa katika mzunguko kwa muda
mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki na sarafu hukaa kwenye mzunguko
kwa muda mrefu kuliko noti. Katikati ni Mshauri wa Fedha kutoka ofisi
hiyo Bw. Hassan Jarufu na Mwisho ni Meneja Msaidizi, Sarafu Bw. Abdul
Dola.
Mkurugenzi
Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel
Boaz (kulia) na Mshauri wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu
wakiwaonesha waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Toleo jipya la
sarafu ya Shilingi 500 inayotarajiwa kuingizwa kwenye mzunguko
kuanzia mwezi Oktoba 2014.
Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO
Na
Frank Mvungi MAELEZO
Benki
Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500 itakayoanza
kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi 500
inayoonekana kuchakaa
haraka.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki wa benki hiyo Bw. Emmanuel
Boaz
wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Noti
ya shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi zidi na ndiyo
inayotumika
zaidi kwenye manunuzi ya kawaida hivyo kuchakaa haraka ndio maana
tumeamua
kutoa toleo la sarafu itakayoanza kutumika mapema mwezi wa 10 mwaka
huu.”alisema
Boaz.
Akifafanua
zaidi Boaz amesema Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi zaidi
kuliko
noti na pia noti zimekuwa zilikaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila
kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe.
Akitaja
sifa za sarafu hiyo mpya Boaz amesema kwanza umbo lake ni la duara lenye
michirizi pembezoni na kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5.
Sifa
nyingineni kuwa ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini aina ya
chuma na
Nickel na kwa upande wa mbele ina sura ya Rais wa kwanza wa Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar sheikh Abeid Aman Karume na kwa nyuma ina taswira
ya
mnyama nyati akiwa mbugani.
Pia
Boaz alibainisha kuwa sarafu hiyo kwa upande wa
nyuma ina kivuli kilichojificha ambacho huonesha thamani ya
sarafu ya
500 au neno BOT inapogeuzwa geuzwa.
Kwa
upande wa matumizi Boaz amesema sarafu hiyo itakapoanza kutumika
itatumika
sambamba na noti za shilingi 500 hadi zitakapokwisha kwenye mzunguko.
Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye
jukumu la
kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini
ambapo katika kutimiza jukumu hili
Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani
(denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza
kugawika katika zile zenye thamani ndogo.
No comments:
Post a Comment