Sunday, 7 September 2014

HABARI NJEMA KUTOKA HESLB:::FEDHA ZA VITENDO ZA PELEKWA VYUONI.

VYUO VYOTE SASA VYAPELEKEWA FEDHA ZA MASOMO KWA VITENDO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
Vyuo vyote nane ambavyo vilichelewa kupatiwa fedha za mafunzo kwa vitendo vimepatiwa fedha hizo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania, (Tahliso), Musa Mdede, vyuo vinne vilivyopatiwa fedha hizo wiki iliyopita na kumaliza mgogoro kati ya Tahliso na Bodi ni Tumaini Makumira- Iringa, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMUCCO), Chuo Kikuu cha Jordani (Morogoro), Saut (Mwanza) na Saut Tabora.

Alisema vyuo ambavyo vilipatiwa fedha hizo Agosti 23, mwaka huu ni Chuo Kikuu Teophilo Kisanji (Teku), Chuo Kikuu cha Katoliki cha Sayansi , Afya na Tiba-Bugando (CUHAS-Bugando) kwa wanafunzi wa fani ya udaktari wa mwaka wanne.

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya HESLB, tayari fedha hizo zilipelekwa kwa vyuo hivyo vitatu Jumanne iliyopita na kwamba iwapo hazijafika itakuwa ni tatizo katika benki walikopeleka.

Mapema wiki iliyopita, HESLB ilisema bado inaendelea na utaratibu wa kukamilisha malipo ya fedha kwa vyuo vilivyobaki, baada ya kukamilisha kwa vyuo vitatu.

Kabla ya kutolewa kwa fedha hizo, Tahliso walikuwa wametangaza mgogoro na  HESLB kutokana na kucheleweshewa fedha hizo wanazodai kuwa ni Sh. bilioni 6.6.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment