Mshambuliaji
mpya wa kilabu ya Arsenal Danny Welbeck anaweza kufunga mabao 25 kwa
msimu mmoja ,hayo ni matamshi ya aliyekuwa mshambuliaji wa England Allan
Shearer.
Wellbeck mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na kikosi cha
The Gunners kutoka kilabu ya Manchester United kwa kitita cha pauni
millioni 16 katika siku ya mwisho ya dirisha la kuwasajili wachezaji wa
soka barani ulaya na anaweza kuanzishwa kwa mara ya kwanza dhidi ya
watetezi wa ligi hiyo Manchester City siku ya jumamosi.Nimesikia watu wakisema kwamba Wellbeck hawezi kufunga mabao 20 ama 25 kwa msimu mmoja ,sikubaliani na hilo Shearer aliiambia Radio 5 live ya BBC'',.
''Sasa ana uwezo wa kuonyesha umahiri wake katika ligi hiyo.''.
Siku ya Alhamisi Meneja wa kilabu ya Manchester United Van Gaal alisema kuwa Wellbeck hakuweza kufunga mabao ya kutosha wakati alipkuwa katika kilabu hiyo ya Old Trafford.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Manchester ambaye aliifunga mabao yote mawili timu ya Uingereza dhidi ya Switzerland siku ya jumatatu ,hajawahi kufunga zaidi ya mabao tisa katika ligi ya Uingereza tangu alipoanza kuchezea mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment