Monday, 1 September 2014

MJUE KAMANDA ROSE J.MAYEMBA::MPIGANAJI MPYA

ROSE JOHN MAYEMBA NI MPIGANAJI MWENYE NDOTO KUPELEKA NGUVU ZAKE BAVICHA TAIFA

 Rose John Mayemba
..........................................
 JINA la Rose John Mayemba  ( 25) si  jina  geni katika harakati  za  chama  cha  Demokrasia  (CHADEMA)  mkoa  wa  Iringa na mikoa ya  nyanda za  juu  kusini 


Kwani  kila  unapotaja  vijana  waliopelekea  Chadema  kutambulika katika  mikoa  ya nyanda za  juu  kusini  hasa  Iringa na  Njombe  basi  ni  vigumu kulisahau  jina na Rose John Mayemba ambae kwa  muda  mwingi  wa  masomo  yake  katika  manachuo  wa  chuo  kikuu  cha Ruaha  Iringa  alipata  kutumia nafasi hiyo  kuhamasisha uhai  wa  chama .

"Mimi mteknologia dawa( pharmaceutical technician) elimu niliyoipata katika chuo kikuu cha RUCO....nimekuwa mwanachama mtiifu wa chadema tangu mwaka 2005."

Rose  anasema  kuwa lengo  lake la  kuwania  nafasi  ya  umakamu mwenyekiti  BAVICHA  Taifa ni  kutaka   kuunganisha  nguvu  na  safu  nzima ya  uongozi  itakayochaguliwa  katika  uchaguzi  utakaofanyika  hivi karibuni  ili  kuongeza  mapambano ya  CHADEMA  kwenda  Ikulu.
Kwani  alisema  kuwa   uwezo  wa kuunganisha  nguvu na  viongozi  wenzake anao hasa  ukizingatia  nguvu  alizo nazo  kwa  sasa katika  kukipigania  chama  hicho.


"Nimekuwa kiongozi wa chadema katika nyanja mbalimbali.
-nilikuwa mwenyekiti wa chadema  katika tawi la RUCO 2012/2013.
Ndiye mtunza takwimu wa jimbo la Njombe kusini kwa sasa"
Nimeshiriki harakati mbalimbali za kukujenga Chama, nimeshiriki chaguzi ndogo mbalimbali za kuwapata madiwani na wabunge mfano kilolo, mbalamaziwa, Njombe mjini  na kalenga.

Nimeshiriki operesheni za kukijenga Chama kama M4C na Chadema ni msingi  hivyo  ni matumaini  yangu  uzoefu  wa kuendelea  kukitumikia  chama ninao  tena mkubwa na iwapo  vijana  wenzangu  watanichagua  kuongoza  BAVICHA kama makamu  mwenyekiti  naamini kabisa  nafasi  hiyo  itakuwa  imempata mpiganaji  wa  kweli mwenye nia ya  dhati  kuleta mapinduzi makubwa katika serikali  ya  CCM.

No comments:

Post a Comment