Thursday, 11 September 2014

RAHA ZA DUNIA::PICHA ZA NDEGE MAALUM YA WANAMICHEZO

Muonekano wa ndani wa ndege maalum kwa ajili ya wanamichezo ili kuwasaidia kupunguza uchovu.
Muonekano wa viti (kushoto) vya ndege hiyo.
Sehemu ya kupumzikia wachezaji wakati wa safari.
Vitanda vya kupumzikia wachezaji ndani ya ndege hiyo.
Kampuni moja ya ndege imeamua kutengeneza ndege maalum kwa ajili ya wanamichezo ili kuwasaidia kupunguza uchovu.
Inaaminika wanamichezo wamekuwa katika uchovu mkubwa kutokana na safari nyingi za ndege kwenye klabu ikijumuishwa na timu zao za taifa.
Kutokana na hali hiyo kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imeamua kushirikiana na kampuni hiyo ya ndege ambayo haijatajwa kupata ndege ambayo itakuwa na sehemu maalum kwa ajili ya wanamichezo ambayo itawapunguzia uchovu licha ya safari ndefu.
PICHA NA MTANDAO.

No comments:

Post a Comment