Idara ya Uhamiaji imewataka wananchi wenye taarifa za uhakika juu ya watumishi wa idara hiyo waliohusika na upokeaji wa rushwa katika zoezi la utoaji wa ajira 200 zilizofutwa na serikali kufikisha ushahidi huo katika vyombo husika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watumishi hao.
Kauli hiyo imekuja baada ya watumishi wa idara hiyo kuingia katika kashfa ya kuchukua rushwa ya Sh. bilioni 2.5 kwa nyakati tofauti kupitia waombaji wa nafasi hizo katika idara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna wa Idara hiyo, Abbas Irovya, aliwataka wananchi hao kujitokeza mapema iwezekanavyo kwa sababu sheria ya idara hiyo inakataza kutoa au kupokea rushwa.
“Kutokana na taarifa hiyo idara inamtaka kumfikisha katika vyombo au mamlaka husika ili taarifa hiyo ifanyiwe kazi ipasavyo kwani hakuna mtumishi yeyote aliye juu ya sheria ndani ya idara na anayeweza kukiuka maadili ya kazi kwa baraka za idara,” alisema Irovya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, alisitisha zoezi la ajira za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji zilizotangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari na Idara ya Uhamiaji.
Sababu za kusitisha ajira hizo zilitokana na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya Kijamii kuwa kulikuwa na upendeleo kwa ndugu na jamaa za watumishi wa Idara hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, Abdulwakil aliunda Kamati Ndogo ya Uchunguzi itakayochunguza kuhusu tuhuma hizo.
CHANZO: NIPASHE
Thursday, 11 September 2014
Uhamiaji: Mwenye ushahidi wa rushwa ya ajira 200 aulete
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment