Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.
WAKATI
wajumbe maalum wa katiba wakiwa wamependekeza suala la haki za binadamu na
mgawanyo sawa wa madaraka kati ya mwanamke na mwanaume, vitendo vya ukatili na
mauaji kwa wanawake vimezidi kushika kasi mkoani Mbeya.
Katika
tukio la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa kwa jina la Rutina Ng’ekele(75),
mkazi wa kijiji cha Mabondeni, kata ya Bulyaga, tarafa ya Tukuyu mjini wilayani
Rungwe, amefariki dunia katika hospitali ya Makandana wilayani Rungwe, akiwa
anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa mateke na ngumi.
Taarifa
zinasema kuwa, Bibi huyo alishambuliwa vikali sehemu mbalimbali za mwili wake
na mtu aliyefahamika kwa jina la Nicolous Afyasisye.
Tukio
hilo limeelezwa kutokea Octoba 4, mwaka huu, majira ya saa moja usiku na
kupelekea marehemu kulazwa hospitalini hapo mpka mauti yalipomfika jana Octoba
14, mwaka huu, saa sita mchana.
Chanzo
cha tukio hilo, kimeelezwa kuwa ni marehemu kumlipa mtuhumiwa Tsh.7,000/=
badala ya Tsh.10,000/= aliyokuwa akidaiwa na mtuhumiwa, jambo ambalo
lilisababisha mtuhumiwa aanze kumshambulia marehemu.
Baada
ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana na Jeshi la polisi
limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.
Kamanda
wa polisimkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema kuwa anatoa wito kwa yeyote mwenye
taarifa za mahala alipo mtuhumiwa wa tukio hilo, azitoe katika mamlaka husika
ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
CHANZO.
www.marymwanjelwa.blogspot.com
No comments:
Post a Comment