OHOOOOH! Siku chache baada ya mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Sitti kujinyakulia U-Miss Tanzania 2014, tayari joto la ushindi huo limetikisa taji hilo na kuibua maswali ‘chungu mbovu’ kuhoji uhalali wa ushindi huo, Risasi Mchanganyiko linashuka na mchongo kamili.
“Tatizo lilianzia kwa watu wengi kuingia na vibendera vyenye picha ya Sitti vikionyesha dhahiri kwamba walijua kabla kwamba ni mshindi hivyo kuja wakiwa wamejipanga kabisa,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema hata katika suala zima la mshindi kuandaliwa gari maalum la Hammer ambalo baadaye lilimchukua na kumrudisha kivyake tofauti na washiriki wengine ambao waliondoka ukumbini hapo na basi waliloandaliwa.
Aidha, vuguvugu hilo lilijiongeza zaidi baada ya watu kudai huenda ushindi huo ulitokana na mgongo wa baba yake (mbunge wa Temeke) madai ambayo kwa pamoja yalikanushwa na muandaji wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga.
“Hakuna kitu kama hicho, malalamiko kila siku hayakosekani, vipeperushi havikatazwi, majaji sita kati ya tisa waliwekwa na wadhamini (TBL kupitia kinywaji chao cha Red’s), haiwezekani akawahonga majaji wote hao.
Kwenye shindano hilo, Sitti aliwagaragaza washiriki wenzake 29 na kuondoka na kitita cha shilingi milioni 18. Mrembo huyo ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia (Miss World) hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment