MSANII mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba amefunguka kwamba baada ya kufunga ndoa hivi karibuni ameishi na mumewe Janus kwa wiki mbili tu.
“Mume wangu alikaa kwa wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa nikamwambia aniache ili nimalizie kufanya maandalizi ya kumfuata huko kwao Denmark ambapo mpaka sasa sijajua nitaenda lini maana bado sijamaliza mambo yangu ila tunaaminiana na tumeshazoea kwani tangu wakati wa uchumba tulikuwa tuko mbalimbali lakini nitaenda.
“Nikienda huko nitakaa kwa miezi mitatu nitarudi hapa Bongo kusalimia na kukaa kama wiki kadhaa, nampenda sana mume wangu na ninammis kwa kweli,” alisema Lucy Komba.
No comments:
Post a Comment