Thursday, 21 August 2014

VITA INAENDELEA:Israeli yaua makamanda 3 wa Hamas.

Israeli yaua makamanda 3 wa Hamas.

 21 Agosti, 2014
Pengo lililowachwa na jengo la orofa nne lililoharibiwa kabisa katika shambulizi hilo
Shambulizi la Israeli kwenye nyumba moja mjini Rafa limewauwa makamanda watatu wakuu katika jeshi la Hamas.
Huduma za uokoaji za Palestina zinasema kwamba watatu hao Mohammed Abu Shamala, Mohammed Barhoum and Raed al-Attar waliuawa karibu na mji wa kusini wa Rafah miongoni mwa watu sita waliouawa.
Mashambulizi yalianza upya siku ya jumanne kila upande ukilaumu mwengine kwa kutofaulu kwa mazungumzo ya amani mjini Cairo huku Israeli ikiapa kuendelea na kampeni hadi usalama wake uimarike.
Mwandishi wa BBC Yolande Knell anaripoti kwamba makamanda hao watatu walikuwa nguzo kuu ya kwa operesheni zinazohusisha kupenyeza, ujenzi wa handaki na kumteka mwanajeshi wa Israeli, Gilad Shalit.
Babu ya watoto watatu waliouawa Gaza akiomboleza Gaza
Bwana Attar alikuwa kamanda mkuu zaidi katika eneo la kusini na alionekana akimpeleka Bwana Shalit kutoka kwa gari na kumpatiana kwa Wamisri wakati wa mabadilisho ya mfungwa mwaka wa 2011.
Bwana Shamala alikuwa kamanda wa Rafah aliyesemekana kuwa na jukumu la kupanga kutekwa kwa Shalit.
Bwana Barhoum naye ambaye ni jamaa wa karibu wa Fawzi Barhoum msemaji wa Hamas alikuwa kamanda mkuu wa mitaa.
Katika maendeleo mengine, Hamas imeonya kampuni za ndege za nchi za kigeni kusimamisha safari zake za ndege kwenda na kutoka katika uwanja wa ndege wa Gurion mjini Tel Aviv kuanza Alhamisi.
Usalama umeimarishwa katika uwanja wa Ndege wa Ben Gurion
Kundi hilo pia limehakikisha kwamba litaacha kutia juhudi za mazungumzo ya kusitisha mapigano kabisa nchini Israeli.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeeleza wasiwasi wake kutokana na kurejea kwa uadui na likaitaka pande hizo mbili kurejelea meza ya mazungumzo.
UN inahimiza kupatikana suluhisho la kudumu haraka iwezekanavyo ili kusitisha mapigano hayo.
Misri pia imeeleza masikitiko makubwa baada ya siku kumi za mazungumzo ya amani na ikasema kwamba itaendelea kutafuta suluhisho la kudumu.

HAYA NDO MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMTI KUU MJINI DODOMA

August 21, 2014

MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMTI KUU MJINI DODOMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alisema,
Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa na kufanya tathimini juu ya maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini, ndani na nje ya Bunge.

Kamati Kuu vilele imepokea na kujadili taarifa kuhusu mazungumzo na mashauriano kati ya vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI  na CCM. Mazungumzo ambayo yalisimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Aidha Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya kikao cha Baraza la Vyama vya siasa na pia taarifa ya kikao cha Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD). Vikao hivyo vyote vilihusu maendeleo ya mchakato wa Katiba nchini.


Kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba, Kamati Kuu imearifiwa maendeleo ya majadiliano na upigaji kura katika kamati za Bunge hilo. Kwa ujumla Kamati Kuu imeridhishwa na namna wajumbe wa Bunge Maalum wanavyoshiriki katika kujadili na kujenga hoja na wanavyoshughulikia tofauti za kimtazamo na kimawazi katika vikao vyao na hatimaye uhutimishaji wa majadiliano kwa kura.

Kamati Kuu inawahimiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kuhudhuria vikao vya kamati na vile vya Bunge na kushiriki katika mijadala kwa kutanguliza masilahi mapana ya taifa na hatimae kuipatia nchi katiba inayotarajiwa na watanzania wote. Chama Cha Mapinduzi kinautakia kila lakheri mchakato huu.


Aidha Kamati Kuu imeridhishwa na juhudi za vyama na wadau mbalimbali katika kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano kwa lengo la kupata muafaka. Hata hivyo Kamati Kuu imesikitishwa na kuvunjika kwa mazungumzo kati ya CCM, CUF,CHADEMA na NCCR-MAGEUZI yaliyokuwa yanasimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kengo la kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano ili kupata muafaka.


Kamati Kuu imepokea na kuridhishwa na taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD) pamoja na vyama vinavyounda TCD katika kutafuta muafaka wa kisiasa kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na kuaminiana kati ya wadau mbalimbali na hasa kati ya vyama vya siasa.

Kamati Kuu inaunga mkono juhudi za TCD za kuendeleza mashauriano kati ya vyama na ndani ya vyama kwa lengo la kupunguza mivutano, kujenga uaminifu na ustahimilivu na umoja kati yao.

Hivyo Kamati Kuu imempongeza Katibu Mkuu wa CCM kwa namna alivyoshiriki na kukiwakilisha Chama kwenye vikao hivyo.

Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu aendelee kukutana na vyama na wadau wengine katika kufanikisha lengo la maridhiano hayo.

Mwisho Kamati Kuu inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuendelea kushikamana na kuvumiliana pale wanapopishana kimtazamo juu ya hoja mbalimbali za katiba kwani Amani,  Utulivu na Utanzania wetu ni muhimu kuliko tofauti zetu za kimitazamo. Mchakato wa Katiba nchini uendelee kuwa fursa ya kuijenga nchi yetu badala ya kutumika kutugawa na kututenganisha.

na fredy mgunda

KIDOTI NDANI YA PENZI ZITO NA POZI KWA POZI(OMMY D)

Inasemekana Ommy Dimpoz Amehamishia Mapenzi Kwa Jokate Baada ya Kumtema Demu Wake

August 21, 2014
Kupitia Gazeti la Makorokocho leo mezani tumepata story ya muda mrefu ya Penzi la siri kati ya Ommy Dimpoz na Jokate aka Kidoti.
stori hii ilivuja baada ya beef la chini kwa chini kati ya Jokate na mwimbaji mmoja wa kike ambae hawana maelewano mazuri na chanzo kikidaiwa kuwa ni mwanamuziki huyu wa kike (jina lake linaanzia na herufi V)
kukuta meseji za Mapenzi kati ya Mpenzi wake huyo na dada yetu kidoti.
Chanzo kinasema kidoti na Ommy Dimpoz walianza mapenzi ya siri kwa siri baada ya dada huyo kuachana na diamond.
Mapenzi hayo yalianzia huko mikocheni A ambapo Ommy Dimpoz alikwa akiishi nyumba ya kushare na kila bibie kidoti alipokuwa akienda hapo watu walimuona na kuna kipindi dada yetu kidoti alikuwa akiminya ndani ya gari bila kushuka mahaba yakiwa tele kwenye gari hilo.
sasa wataalamu wa mambo wanasema dada yetu huyu anaonekana sana maeneo ya kinondoni katika mjengo wa kupanga wa star huyu wa ndagushima chande na mapenzi yao bado inasemekana yanaendelea chini kwa chini lakini nje nje.
ommy dimpoz ameingizwa kwenye list ya wanaume walio na mapenzi ya siri na dada yetu kidoti.
patamu hapoooo.
kama namiona vile
by  makorokocho: SOUDY BROWN

Wednesday, 20 August 2014

PICHA ZA BABA LA BABA NDANI TANGA:NI SHEEEDAAAH

Maandalizi ya Serengeti Fiesta 2014 Tanga.

13tng
Huu utakua mkoa wa 4 kwenye list ya miji 18 ambayo watapata nafasi ya kuonja utamu wa Serengeti Fiesta 2014,ilianzia Mwanza ikafuata Bukoba ikasogea hadi Kahama na sasa ni zamu yao Tanga.
Tanga itakua ni Jumamosi hii August 23 kwenye viwanja vya Mkwakwani,hizi ni shamra shamra za Serengeti Fiesta ambapo Clouds Fm iko live kutokea hapa wakiongozwa na Adam Mchomvu,Gea Habib na Bonge.

3tng
17tng

18tng
24tng

27tng
31tng
36tng
1tng

KATUNI YAKO:AFRIKA NI SHIDA TU


KINDOA ZAIDI:Je, Talaka ni Suluhisho la matatizo ya Ndoa?


Je, Talaka ni Suluhisho la matatizo ya Ndoa?


Tanzania huwezi kudai talaka bila sababu za msingi kisheria. Wapo wanandoa ambao kabla ya kudai talaka  hujaribu  kutafuta  njia mbalimbali za kupata suluhu kwa mfano, kutafuta ushauri nasaha (marriage counseling), wengine huamua kujitenga kwa maana ya kuhama nyumbani.
===========================================
Utangulizi
Ndoa ni taasisi muhimu sana katika jamii. Sheria, imani za kidini na hata mila na desturi nyingi duniani huthamini sana taasisi hii na kuilinda kwa gharama yoyote. Hata hivyo polepole tunashuhudia taasisi hii kama zilivyo taasisi nyingine, ikikumbwa na misukosuko ya kila aina. Maendeleo na uhuru vinapoongezeka, ndivyo taasisi hii inavyozidi kutishiwa kuendelea kuwepo. Kuna hata watu wanadiriki kusema kwamba itafikia wakati  taasisi hi itaonekana haina maana wala nafasi tena ( irrelevant) na kufutiliwa mbali.
Mawazo haya japo yanaogofya, hatuwezi kuyapuuza; yatupasa kujaribu kuyafanyia kazi kadiri tunavyoweza. Jamii zote zinakabiliwa na kuongezeka kwa talaka baina ya wanandoa. Haijalishi kiwango cha maendeleo makubwa waliyofikia au umaskini uliokithiri unaozitafuna.
Mfululizo wa makala zangu kuhusu talaka, utajikita katika zile “ndoa za mwanamke na mwanaume” iwe ndoa ya “mke” mmoja au wengi, na siyo vinginevyo! Hapa ninamaanisha kwamba zile “ndoa za watu wa jinsia moja”, au “ndoa ya mwanamke mmoja na wanaume wengi”  hazihusiki katika tafsiri yangu ya ndoa na hivyo haziangukii katika wigo wa makala zangu! Aidha mjadala utajikita zaidi kwenye “talaka zinazotolewa kimahakama” na siyo zile za kupeana kienyeji kwa kufukuzana, au zinazotolewa kwa utaratibu tofauti bila kufuata Sheria ya Ndoa ya 1971 inayotumika Tanzania.
Nimeanza na angalizo hili ili tuwe na uelewa wa pamoja tunaposoma kilichoandikwa hapa. Pia ninafahamu kuna mambo yanayoweza kuzua mjadala au kuingiza mambo mengine yahusuyo “haki za binadamu” na hata “imani za kidini” na hivyo kupoteza mwelekeo wa makala na mtizamo wangu. Ninawaomba wasomaji wangu tuepuke kutoa tafsiri tofauti nje ya kile kilichoandikwa na kukusudiwa hapa.
Kusudio la makala hii ni kuanzisha fikra akilini mwa wasomaji, ili nao waweze kutoa maoni yao kwenye hili suala nyeti.
 
Talaka katika takwimu

Pamoja na kujua kwamba kadiri miaka inavyoenda, talaka zinaongezeka kwa kasi hapa Tanzania kama ilivyo sehemu nyingi duniani kama nchi za Ulaya na Marekani, ni vigumu kuwa na takwimu sahihi kwa vile watu wanapotalikiana hawaendi kuandikisha talaka kwa wakala wa  RITA (Registration, Insolvency and Trusteeship Agency) kama wafanyavyo pale kifo kinapotokea au pale mtoto anapozaliwa. Kutokuandikishwa huku kunatokana na sababu nyingi, moja ikiwa ni pamoja na unyanyapaa kuhusu talaka, na kutokujua kwamba talaka nazo ni lazima ziandikishwe kisheria ili pamoja na mambo mengine kuwezesha kukusanya takwimu zitakazosaidia kupanga  mipango ya maendeleo na kutunga sera.
Takwimu zilizopo japo hazionyeshi hali halisi, bado zinaashiria kuongezeka kwa idadi ya talaka. Kati ya 2007 na 2008, kesi za talaka zilizoandikishwa RITA ziliongezeka na kufikia 43 ukilinganisha na hali ilivyokuwa kati ya 2005 na 2006 ambao kesi zilizoandikishwa zilikuwa 37 tu! Kwa kiwango chochote kile, idadi hii ni ndogo ukilinganisha na hali halisi.Yatosha tukisema kwamba talaka bado imebakia kuwa kitu cha binafsi baina ya wanandoa wenyewe, japo watu wanapooana mara nyingi haifanywi siri.
Mwelekeo na mtizamo kuhusu Talaka
Suala la talaka haliwezi kuongelewa bila kuangalia  mila na desturi na hata imani za kidini. Tafiti zilizokwisha fanyika kuhusu  mwelekeo wa kupeana talaka (divorce trends) miongoni mwa jamii za Kitanzania, zinaonyesha kwamba “jamii zinazoishi mijini na kufuata utamaduni wa Kiswahili” (Swahili culture) ziko na mwelekeo zaidi wa kupeana talaka kuliko “jamii za bara zenye mila na desturi au hata mwelekeo wa kiimani hasa ya kikristo” unaopinga talaka. Mara nyingi kuna dhana potofu kwamba wanaume tu ndio huweza kutoa talaka na wanawake wao ni wapokeaji wa talaka ilhali siyo hivyo.
Mtizamo huu unatokana na mila na desturi ambapo mwanamke aliyeolewa kwa kulipiwa mahari, hakuwa tofauti na bidhaa au mali ya muoaji! Hata hivyo, kisheria mwanaume au mwanamke anaweza kuomba mahakama itoe talaka na kusitisha mahusiano yale ya kindoa.Mtizamo wa kudhani kuwa mwanaume tu ndio ana haki au “uwezo wa kumkataa mwanamke” ndio hupelekea watu kuwanyanyapaa wanawake “walioachika” kwamba hawafai, na kuwaogopesha wanawake walioolewa kusita kwenda kuomba talaka mahakamani, hata pale ndoa inapogeuka kuwa kihatarishi cha maisha.
Unyanyapaa kwa wanaume huchukua sura tofauti na mara nyingi huhusishwa na uwezo wa kuongoza. Mwanaume aliyeshindwa “kutawala au kuongoza kaserikali kadogo ka nyumbani” atawezaje kutawala serikali au taasisi kubwa? Hapa tunapata dhana nyingine tofauti kwa nini baadhi ya wanaume nao husita kuachana na wake zao hata pale wanapotamani kusitisha  mahusiano ya ndoa.
Tukirudi tena upande wa mila na desturi, katika “utamaduni wa Kiswahili”, mara nyingi ndoa na talaka zilishikamana na imani ya dini na kwa wale wenye kuishika dini ya Kiislam, talaka ni kitu kinachoruhusiwa. Wanawake wengi walisubiri kupewa talaka na kuendelea na maisha yao ambapo kuolewa tena ilikuwa ni uwezekano. Kwa watu wa bara na hasa wenye kufuata imani ya kikristo ile inayosema ndoa ni pingu za maisha, basi ilikuwa vigumu sana kutaka ama kupewa talaka. Pia mwanamke aliyeachika huweza kujikuta haolewi tena kwa vile kikanisa ndoa ya mwanzo bado inatambuliwa na inamzuia kutokufingishwa ndoa nyingine. Tafiti zimefanyika kuonyesha kwamba, wakati wanawake wa kiislam hawakuogopa talaka, wanawake wa kikristo walionyesha kuogopa kupewa talaka kwa sababu imani ya dini inakataza.
Pamoja na unyanyapaa na woga, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba mambo yamebadilika sana siku hizi ambapo kutokana na kuongezeka kwa uelewa wa jamii na hasa wanawake wenyewe katika kuzijua haki za kisheria, na hususan  Sheria ya Ndoa ya 1971, wanawake wanaoishi maisha wasiyoyafurahia, yenye manyanyaso, hutafuta suluhu kwa kuomba talaka mahakamani lakini kwa gharama na kwa kupitia mchakato wenye changamoto.
Talaka kama  mchakato wenye  changamoto lukuki
Mchakato wowote ule una gharama zake. Talaka  siyo tukio la mara moja bali ni hitimisho la mchakato na kwa kiasi kikubwa humgharibu mtu kwa namna moja ama nyingine kwa maana ya muda, fedha, ustaarabu, heshima, staha nakadhalika. Gharama hizi kwa kiasi fulani huweza kumfanya mtu afikirie mara mbili kabla hajaanzisha huu mchakato wa  kufungua minyororo ya pingu za maisha. Mchakato huu unaweza kumfanya mtu aumbuke na kujikuta siri zake nyeti zikianikwa waziwazi bila staha wala heshima mahakamani, kwenye magazeti na hata kwenye machapisho mengine ya kudumu kama taarifa za kisheria ( Law Reports) na kadhalika.
Kabla uamuzi wa talaka haujachukuliwa, aghalabu mambo mengi yanaweza kuwa yametokea baina ya wenza wa ndoa yenye kuleta machungu.Katika jamii nyingine hasa Ulaya na Marekani, ikitokea wanandoa hawaifurahii tena ndoa kwa maana ya kupungua mapenzi baina yao, si ajabu hili pekee likamsukumu mmoja wapo au wote  kuona hakuna jinsi isipokuwa kudai  talaka na siyo ajabu ukasikia mtu anasema mahakamani “anadai talaka bila sababu”.
Tanzania huwezi kudai talaka bila sababu za msingi kisheria. Wapo wanandoa ambao kabla ya kudai talaka  hujaribu  kutafuta  njia mbalimbali za kupata suluhu kwa mfano, kutafuta ushauri nasaha (marriage counseling), wengine huamua kujitenga kwa maana ya kuhama nyumbani. Mara nyingi Ulaya au Marekani mwanaume huwa ndio mwenye kuhama! Uzoefu unatuonyesha kwamba jamii za kiafrika  hususan Tanzania  mwanamke “huhamishwa” kwa kufukuzwa au kufanyiwa visa na vitimbi. Wako wanandoa ambao badala ya kuhama, wao hutafuta mtu mwingine kwa siri wa kufarijiana naye na kusogeza siku huku wakitafuta kufikia malengo yao ya maisha kama kulea na kusomesha watoto na mengine. Vyovyote iwavyo, njia hizi siyo suluhisho la kudumu kwa maana ndoa bado ipo na inazidi kujenga ufa zaidi badala ya kujenga ukuta ulioanza kubomoka!
Tukiangalia Tanzania, kama zilivyo nchi nyingine za kiafrika zilizo maskini, tunaweza kusema kwamba hakuna nyenzo au “miundombinu” ya kuwafanya wanandoa waliochoka ndoa kupata   msaada wa kurekebisha ndoa zisivunjike. Ndoa zinapoanza kupitia magumu, msaada wa kwanza huwa ni familia au marafiki wa karibu na siyo taasisi za ushauri nasaha kwa maswala ya ndoa kwa vile taasisi hizi ni ngeni katika tamaduni zetu. Msaada mwingine ni taasisi za kidini na kwa baadhi, huweza kuwa hazina “uzoefu” kwa maana baadhi ya hao viongozi wa kidini wanaofuata kutoa ushauri, hawajawahi kuishi maisha ya ndoa na kujua kinachoweza kutokea humo kwa vitendo. Nadharia ya kusoma kwenye vitabu au kusikia simulizi wakati mwingine inaweza kuwa tofauti na uzoefu wa vitendo. Kutokana na maendeleo na utandawazi, polepole tunaanza kujua umuhimu wa kutumia taasisi zaidi ya familia na zile za dini ili kupata tiba au suluhu kwa matatizo ya ndoa.
Talaka, japo yaweza kuwa suluhu ya matatizo ya ndoa, suluhu hii inaweza kuzaa matatizo makubwa zaidi tena kwa watu wasio na hatia yeyote mathalani watoto wadogo wasioweza kujitegemea bado, wazazi wazee, ndugu wenye kuhitaji msaada na kadhalika. Inawezekana kuzuia talaka kama tutajaribu kuzuia visababishi vinavyomsukumu mwanandoa kutaka talaka.
Kufuatana na Sheria ya Ndoa ya 1971 mahakama haiwezi kutoa talaka kwa vile wanandoa wamekubaliana kuachana (divorce by consent)  au kusema kwamba wanadai talaka kwa vile wanatofauti zisizoweza kusuluhishika (irreconcilable differences). Hizi ni dhana ngeni kwetu watanzania. Sheria yetu bado ni ile ya mwaka 1971, kabla ya utandawazi, kipindi ambacho hata hao wanaotumia sababu hizi walikuwa bado hawajapiga hatua na kuwa wabunifu kiasi cha kuwa na jeuri ya kusema wamechokana na wamekubaliana kuachana pasina sababu za msingi.
Sheria yetu hii kongwe (iliyopitwa na mambo mengi katika ulimwengu wa utandawazi)  ya 1971 imeweka bayana sababu kuu inayoweza kuruhusu mahakama itoe talaka kuwa ni “uthibitisho kwamba ndoa imeshavunjika pasina shaka yoyote”.Kwamba liwake jua, inyeshe mvua wanandoa hao hawawezi kuishi tena pamoja  kama mke na mume na endapo watalazimishwa kuishi pamoja inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi. Hii ina maana kwamba lazima uthibitisho utolewe kulionyesha kuthibitisha  jambo. Kuna matendo ambayo kisheria yanaweza kuvunja ndoa kwa mfano ukatili (Cruelty), Uzinzi (adultery), kutelekezwa (dissertation/abandonment) na hata kubadili dini. Matendo yote haya huweza kuingiliana kwa namna moja au nyingine na ndio maana mahakama inataka uthibitisho wa zaidi ya kosa moja kati ya hayo.
Kwa Tanzania, kisababishi kikubwa zaidi kufuatana na uzoefu wa kusikiliza kesi za ndoa ni  ukatili kwa mapana yake yote. Ukatili ni mwendelezo wa vitendo vinavyovuka mpaka wa udhalilishaji na kusababisha madhara ya kimwili na kihisia. Kutokana na habari zinazotolewa katika vyombo vya habari, mara nyingi taswira inayotolewa ni kama vile ukatili na unyanyasaji katika ndoa hufanywa zaidi na wanaume. Vipigo, kunyimwa mahitaji ikiwemo unyumba, na mateso mengine huonekana kufanywa na wanaume zaidi, japo ni jambo lisilofichika tena kuwa hata wanawake nao hufanya vitendo hivyo.
Kutelekezwa (abandonment/desertion) nako huweza kuhesabika kama ni ukatili kwa maana ya kwamba mwanandoa hukoseshwa ile haki ya kuwa na mwenziwe. Wanandoa wanapoasiana na kuishi mbalimbali kuna hali fulani ya mateso hujitokeza hasa kisaikolojia kwa sababu Yule aliyetelekezwa huwekwa kifungoni. Hawezi kuchukua uamuzi wa kuishi maisha yake apendavyo nje ya wigo wa ndoa.
Ndoa nyingi zimeendelea kukosa upendo na kumfanya mwanandoa kutafuta upendo sehemu nyingine kupitia namna mbalimbali. Wengine hujikuta wakiwa walevi wa vileo aina mbalimbali, wengine hujikita kwenye kusali zaidi na hata kutokutimiza wajibu muhimu katika ndoa.Wakati haya yote yanatendeka, wanaoumia zaidi ni wale wanaowategemea wanandoa hususan watoto.
Tukija kwenye uzinzi tunapata kwamba kosa moja la uzinzi kimahakama linaweza lisitoshe kuivunja ndoa. Pia nitahadharishe kwamba mwanamke hawezi kudai talaka mahakamani kwa vile kamfuma mumewe ana mwanamke mwingine siku moja tu! Hata hivyo, wakati mwingine uzinzi huambatana na matendo mengine kama ukatili wa kisaikolojia na pia kuondoa upendo  pale mhusika anapozama kwenye mahusiano ya nje na kusahau kuwa kuna mwenza anayehitaji upendo. Kwa miaka ya sasa kuna tishio la UKIMWI pale mwanandoa anapoanza mahusiano nje ya ndoa nah ii inaweza kabisa kuhesabika kama ukatili kwa maana mtendwa hupata mateso kisaikolojia.
Katika suala la kutelekeza, kuna mengi yanaweza kutokea na kusababisha wanandoa wawe mbalimbali na huenda ikawa vigumu kuthibitisha kwamba mtu katelekezwa. Kwa mfano mke au mume anapofungwa kwa muda mrefu, je hii itahesabiwa kuwa ni kumwacha mwenziwe?Katika nchi nyingine huwa tunasoma mara nyingi kwamba mke/mume anaomba talaka kwa vile mwenza wake kafungwa.Je kwetu hili linachukuliwa vipi? Nadhani huu ni mjadala mpana ndugu msomaji na pengine tunahitaji kulijadili hili kwa mapana yake bila kuangalia zaidi mambo ya mila na desturi. Hebu tujiulize, ikiwa mke kafungwa miaka 5 jela, je mume atakaa muda wote huo akimsubiri? Je ni sawa kwa mke kuomba talaka kwa sababu mume kafungwa miaka 10? Ikiwa siyo sawa, je mwanandoa anaweza kukaa miaka yote hiyo akiwa mpweke bila kuwa na haja ya kuliwazwa?

KATUNI HAIFICHI KITU....


LAST SPEECH OF MUAMMAR GADDAF before his death


GADDAFFI'S LAST SPEECH:(ENGLISH N SWAHILI)


In the name of Allah, the beneficent, the merciful...

For 40 years, or was it longer, I can't remember, I did all I could to give people houses, hospitals, schools, and when they were hungry, I gave them food. I even made Benghazi into farmland from the desert, I stood up to attacks from that cowboy Ronald Reagan, when he killed my adopted orphaned daughter, he was trying to kill me, instead he killed that poor innocent child. Then I helped my brothers and sisters from Africa with money for the African Union.

I did all I could to help people Understand the concept of real democracy, where people's committees ran our country. But that was never enough, as some told me, even people who had 10 room homes, new suits and furniture, were never satisfied, as selfish as they were they wanted more. They told Americans and other visitors, that they needed "democracy" and "freedom" never realizing it was a cut throat system, where the biggest dog eats the rest, but they were enchanted with those words, never realizing that in America, there was no free medicine, no free hospitals, no free housing, no free education and no free food, except when people had to beg or go to long lines to get soup.

No, no matter what I did, it was never enough for some, but for others, they knew I was the son of Gamal Abdel Nasser, the only true Arab and Muslim leader we've had since Salah-al-Deen, when he claimed the Suez Canal for his people, as I claimed Libya, for my people, it was his footsteps I tried to follow, to keep my people free from colonial domination - from thieves who would steal from us.

Now, I am under attack by the biggest force in military history, my little African son, Obama wants to kill me, to take away the freedom of our country, to take away our free housing, our free medicine, our free education, our free food, and replace it with American style thievery, called "capitalism" ,but all of us in the Third World know what that means, it means corporations run the countries, run the world, and the people suffer.

So, there is no alternative for me, I must make my stand, and if Allah wishes, I shall die by following His path, the path that has made our country rich with farmland, with food and health, and even allowed us to help our African and Arab brothers and sisters.

I do not wish to die, but if it comes to that, to save this land, my people, all the thousands who are all my children, then so be it.

Let this testament be my voice to the world, that I stood up to crusader attacks of NATO, stood up to cruelty, stoop up to betrayal, stood up to the West and its colonialist ambitions, and that I stood with my African brothers, my true Arab and Muslim brothers, as a beacon of light.

When others were building castles, I lived in a modest house, and in a tent. I never forgot my youth in Sirte, I did not spend our national treasury foolishly, and like Salah-al-Deen, our great Muslim leader, who rescued Jerusalem for Islam, I took little for myself...

In the West, some have called me "mad", "crazy", but they know the truth yet continue to lie, they know that our land is independent and free, not in the colonial grip, that my vision, my path, is, and has been clear and for my people and that I will fight to my last breath to keep us free, may Allah Almighty help us to remain faithful and free.

-- Mu'ummar Qaddafi.

-QADAFFI ANAANZA HIVI:(KISWAHILI)

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.

-- Mu'uammar Qaddafi.

EBOLA:AFRICANS ARE NOT ACCEPTED IN KOREANS BAR(PUBS)

PICHA YA SIKU:ANGALIA PICHA KWA MAKINI...UKIGUNDUA KAA KIMYA..SHIII!!!!!!

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Nchemba.

SOMA SHUTUMA JUU MWANDISHI ALIYECHINJWA

Shutuma kufuatia mauaji ya mwandishi

 20 Agosti, 2014

Picha kutoka kwa kanda hiyo ya video ya James kabla ya kuuawa
Kumekuwa na shutuma za kimataIfa kufuatia kuuawa ukatili kwa mwandishi wa habari raia wa Marekani na kundi la islamic state nchini Syria.
Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond amesema kuwa mashirika ya kijasusi yanajaribu kumtambua yule aliyemuua Foley ambaye anaoneka kuwa na lafudhi ya Uingereza.
Rais wa Marekani Barack anatarajiwa kutoa taarifa yake baadaye leo.
Kikosi cha wapiganaji wa kiislam wenye msimamo mkali Islamic State kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani aliyetekwa nyara nchini Syria 2012.
Naye waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesitisha mapuziko yake na anarejea mji London .
James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.
Mamake mwandishi huyo ambaye aliuawa na wapiganaji wa jimbo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kiislamu nchini Syria, ametoa risala za rambirambi kwa kijana wake na kusema kuwa alipoteza maisha yake akijaribu kufichua dhuluma walizokuwa wakipitia watu wa Syria.
Katika video hiyo mwandishi huyo wa kujitegemea anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
James Foley enzi za uhai wake akiwa na vitendea kazi vyake.
Foley ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa ''Ninawaomba ndugu jamaa na marafiki wangu wasimame na kuzuia adui wangu Serikali ya Marekani kwa ukatili wanaoendelea kutekeleza ndani ya Iraq.''
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''
anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake bwana huyo anaanza kumchinja Foley lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde chache baadaye mwaandishi mwengine pia raiya wa Marekani Steven Sotloff, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa Obama na hatua atakayochukua .
Scotloff alitekwa mwaka wa 2013 nchini Syria karibu na mpaka wa Uturuki.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.
James akiwa kazini.
Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa ’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya mabomu yanayowalenga wa Iraq

SAMAHANI KWA PICHA HIZO:ILA TANZANIA BILA AJALI HAIWEZEKAN???

TUKIO KATIKA PICHA AJALI MBAYA: LORI LA MIZIGO LAGONGA KILABU CHA POMBE NA KUUA WATU WATANO PAPO HAPO

 Lori la Mizigo likiwa limepaki katikati ya kilabu hicho cha pombe ambacho kilisambalatishwa chote na chini ni mabaki ya kilabu hicho.
Tunaomba Radhi kwa Picha
 Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ajali hiyo baada ya kutokea
  Miili minne ya Marehemu ambao walifariki papo hapo baada ya Lori hilo kugonga kilabu hicho ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya Iringa.
 Baadhi ya wananchi wa Eneo la Isimila wakiwa wameongezeka kushuhudia ajali hiyo mbaya iliyo uwa wata watano papo hapo.
 Hivi ndivyo Lori hilo la Mizigo lilivyo umia vibaya baada ya kugonga kirabu hicho na kukisambalatisha usiku wa kuamkia jana na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.
 Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakipata taarifa za Ajali hiyo katika eneo la tukio isimila
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa ajili ya kuwaona Marehem hao.

Picha zote na Iringa Yetu Blog

ONA BASI LA ABOOD LILIVOPATA AJALI MAFINGA

BASI LA ABOOD LAPINDUKA MAFINGA NA KUSABABISHA MAJERUHI 30










.

Ajali hii imetokea saa kumi jioni Jana hakuna aliyepoteza maisha majeruhi zaidi ya 30 wamekimbizwa katika hospitali ya Mafinga kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao huu.

KWA WADADA:JIHADHARI NA SIFA ZA UONGO

Wadada Jihadharini na Kusifiwa Sifa Ambazo Kiukweli Hamna, Zitawagharimu Sana

Udaku Specially on Wednesday, August 20, 2014
Wanaume kwa kawaida hutumia mbinu nyingi pale wanaposaka papuch. 

Mdada utasifiwa hadi sifa ambazo hata malaika hana! Mara romantic eyes... sijui nini nini mouth (mnajua wenyewe mnavyoita) nk nk. 

Wakati huohuo hata anayesifiwa anajua kabisa hizo sifa hana. Lakin anadhani pengne anayemsifia anaziona maana kuna vimisemo vya kudanganyana kama Yako machoni mwa mtu, mapenz hayana formula nk. nk.

Lakini niwaeleze tu hasa wadada ukiona umesifiwa sifa hadi ambazo huna ujue lengo la msifiaji ni kukugegeda tu na akishafanya hivyo lazima akupige chini labda kama ameona kingine cha ziada huko faraghani. 

Jihadharini na sifa zisizo za kweli

TUKIO NA PICHA:5,000/= YAPOTEZA UHAI WA MTU IRINGA MJIN.

TUKIO KATIKA PICHA: MTU MMOJA AUAWA PAPO HAPO KWA KUCHOMWA NA KISU KISA WALIKUWA WANADAIANA TSH 5,000, KITUO CHA MABASI IRINGA

 Tunaomba Radhi kwa picha.
 Tukio tulilopokea muda mchache uliopita mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika amemuua mwenzake kisa walikuwa wanaiana Shilingi Elfu tano... Tunaendelea kufuatilia tukio zaidi .. endekea kufuatilia hapa hapa.
 Kijana huyo ambaye jina halijafahamika akiwa amefariki baada ya Kuchomwa kisu na mwenzake kisa madai ya Tsh 5000 tuu
Mamia ya watu wakiwa wanashuhudia tukio hilo.
Picha na Iringa yetu Blog

Agness Masogange Aingizwa Mkenge na Mnigeria na Kuikana Nchi Yake

Agness Masogange Aingizwa Mkenge na Mnigeria na Kuikana Nchi Yake

Udaku Specially on Wednesday, August 20, 2014
Stori: Sifael Paul na Imelda Mtema

Habari ya mjini kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ni taarifa kuwa video queen maarufu, Agness Gerald ‘Masogange’ amepatiwa passport (pasipoti) ya kuishi nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara raia wa Nigeria.

MWANAUME KAMWINGIZA MKENGE?
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, ishu hiyo ambayo imekuja miezi kadhaa baada ya ule msala wa Masogange wa madawa ya kulevya ‘unga’ inadaiwa ‘imeinjiniwa’ na mwanaume huyo ambaye haijajulikana kama naye amechukua uraia wa Sauzi au la.

KWA NINI MKENGE?
Ilisemekana kwamba ni mkenge kwa sababu ili Masogange apate pasipoti hiyo, ilibidi aikane nchi yake ya kuzaliwa ya Tanzania. Sheria za uraia wa Bongo kwa sasa zinakataza mtu kuwa na uraia wa nchi mbili.

KIKAZI ZAIDI!
Awali, miezi kadhaa iliyopita ilielezwa kuwa Masogange alitimka Sauzi kwa mwanaume huyo ambaye anadaiwa kufanya naye ‘kazi’ (haikutajwa aina ya kazi) nchini humo.
Miezi kadhaa iliyopita Masogange alionyesha kuukataa kabisa Utanzania, baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa kuanzia sasa hataitwa tena Agness, bali umma umtambue kama Thando, jina lenye asili ya watu wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika.

Pia Masogange alitupia mtandaoni picha ya hati yake ya kusafiria ya Sauzi akidai kwamba maskani yake kwa sasa ni kwenye Jiji la Johannesburg nchini humo.Kitendo hicho kinamfanya Masogange ambaye ana asili ya Mkoa wa Mbeya, kuingia nchini kwa viza kama wageni wa mataifa mengine wanavyofanya, wakipewa muda walioomba wa kukaa au kufanya shughuli nyingine yoyote.

Kana kwamba haitoshi, endapo msichana huyo atakumbwa na kosa lolote la kisheria akiwa nchini, anaweza kufukuzwa na kutakiwa kutokuja tena, kama inavyotokea kwa wageni wengine na hivyo kumnyima fursa ya kuwaona wajomba na mashangazi zake walio Mahenge, Kondoa, Mkuranga na maeneo mengine Tanzania.

SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria za Kibongo, Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili (duo citizenship) hivyo Masogange au Thando siyo Mtanzania tena.

MBALI NA MNIGERIA KUNA MSAUZI
Habari ziliendelea kuyeya kwamba mbali na Mnigeria huku, Masogange anadaiwa kuwa na mwanaume mwingine, raia wa Sauzi aitwaye Louis Dolnard ‘anayeminya’ naye nchini humo.
Kwenye Mtandao wa Instagram, mwanadada huyo amekuwa akitupia picha za mahaba niue na mwanaume huyo huku akidaiwa kumsifia jamaa huyo na kumpotezea aliyekuwa mchumba’ke, Evance Komu.

MASOGANGE ANASEMA?
Akizungumza na gazeti hili, Masogange anayeishi Mbezi-Beach jijini Dar, mara baada ya kukamilisha taratibu za pasipoti hiyo kwenye ubalozi wa Afrika Kusini nchini, mrembo huyo alikiri kukamilisha kila kitu hivyo kukwaa uraia wa nchi hiyo.

Kuhusu mwanaume huyo Mnigeria, Masogange hakuwa tayari kuzungumzia lakini alipoulizwa juu ya yule Msauzi, video queen huyo alikiri kumfahamu huku akigoma kufunguka zaidi.

TUMEFIKAJE HAPA?
Miezi kadhaa iliyopita, Masogange na mwenzake Melissa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na matirio ya kutengenezea madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8 ambapo katika hukumu ya kesi hiyo, staa huyo alitakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela. Yeye alilipa faini hiyo akaachiwa huru. 


MENINAH: NAOGOPA MAPENZI YATAVURUGA MUZIKI WANGU

MENINAH: NAOGOPA MAPENZI YATAVURUGA MUZIKI WANGU

Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah Ladivah akifanya mahojiano katika kipindi cha Hatua Tatu leo.
Meninah akiwa studio na mtangazaji anayeongoza kipindi cha Hatua Tatu, Times Fm, Maryam Kitosi.
Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah  amesema anaogopa kuwa katika uhusiano wa mapenzi kwa sasa anaamini mapenzi yatavuruga muziki wake.

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Meninah ameeleza kuwa hivi sasa yuko single na hajawa na mpango wa kuingia katika uhusiano kutokana na sababu hizo.

“Kwa sasa niko Single naangalia kazi yangu kwanza... Nikiingia kwenye mahusiano kazi yangu itakuwa shaghala bagala.” Amesema Meninah.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa mwimbaji huyo ana ukaribu na Diamond lakini alikanusha na kueleza kuwa hajawahi hata kuwa na ukaribu na mkali huyo.

Unaweza kuwa umeshasikia na unaamini Meninah yuko kwenye uhusiano na….. Lakini msikilize pia yeye. “Unajua watu wanaamini ukiwa msichana mzuri basi ni lazima uwe katika uhusiano!”

Meninah ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Pipi ya Kijiti’.

KILA SIKU MAPENZI YA DIAMOND NA WEMA TUUUUUU!!!!!!DUH,JISOMEE

Maneno ya Diamond Kwa Wema Kuwa na Marefiki Wapenda Starehe Yamchoma Vikali Aunt Ezekiel

Udaku Specially 
Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema…

Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza Udaku Special jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.

“Urafiki wa Wema  na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty anataka kumuacha Wema na bwana’ke yeye achukue hamsini zake” kilisenma chanzo hicho.

BEYONCE NA JAY-Z:MAHAKAMAN KISA BLUE IVY WALIIBA

Beyonce na Jay Z Washitakiwa Kwa Kuiba Mtoto (Blue Ivy) na Kujifanya ni Wao

Udaku Specially on Wednesday, August 20, 2014
Tina Seals, a New York woman has allegedly moved to court seeking custody of Pop singer Beyonce and Rapper JayZ's daughter Blue Ivy as the legal mother.

According to sources, the woman's move to court  is aimed at determining if she is indeed the biological mother to Blue.

NewsOne reports that the legal documents indicate that Seals is the woman who actually gave birth to Blue and further associates her with the celebrity couple.

Prior to Blue's birth, there were rumours that Beyonce was only sporting a prosthetic pregnancy and they were planning on getting a surrogate to carry the baby. We all witnessed the bump grow and eventually she went into delivery and shared baby photos of their newborn from the hospital.

A majority of her fans have chosen to trash the rumour, saying that Seals is just delusional but a section of those who believe that the power couple is linked to the Illuminati claim that it could be possible that Seal 'has been used and was used' to breed as a surrogate for the stars.

Other sources reveal that Beyonce is not the first star she has pulled this kind of move on alleging that she previously filled against Kim Kardashian, Mariah Carey and even Kate Middleton.

Do you believe that Tina Seals could be the biological mother to Blue Ivy or is it just another obsessed fan trying to get 15 seconds in the spotlight?

VANESSA vs KIDOTI:NAN KAMZIDI MWENZIE?

Vanessa Mdee vs Jokate Mwegelo

Wednesday, August 20, 2014
They are both smart, classic, intelligent, talented, educated and they both have natural beauty.