Sunday, 24 August 2014

MPASUKO CCM IRINGA

MPASUKO CCM IRINGA

Mwenyekiti wa CCM Iringa, Jesca MsambatavanguJOTO la kuwania ubunge Iringa Mjini, katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani limeanza kuwagawa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa.
Mgawanyiko huo umekua zaidi baada ya kutangazwa kuwa sherehe za kumsimika kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa huo, zitafanyika Agosti 23 na Wilaya ya Iringa Mjini Agosti 29 mwaka huu.
Awali ilipangwa sherehe hizo zifanyike kwa siku moja lakini inadaiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa, Jesca Msambatavangu, ameingilia mchakato huo.
Inadaiwa anafanya hivyo kupunguza nguvu ya kujizolea umaarufu kamanda wa vijana wilaya ya Iringa Mjini atakayesimikwa Fredrick Mwakalebela anayetajwa kutaka kuwania ubunge kama inavyotajwa kwake.
Inaelezwa tishio la Msambatavangu ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ameshaanza maandalizi hayo na tishio kwake ni Mwakalebela.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Mwenyekiti huyo juu ya kuingilia mchakato wa sherehe hizo lakini hakuwa tayari kupokea wala kujibu ujumbe mfupi aliotumiwa.
Katibu wa CCM Iringa, Hassan Mtenga, alikana mkoa kuingiza mkono wake kwenye sherehe hizo kwakuwa kila kitu hufanywa na UVCCM.
Tanzania Daima Jumapili, iliwasiliana na Katibu wa UVCCM, mkoa Iringa Al Haidary Fumu, alisema wameamua kutenganisha sherehe hizo ili kutoa fursa ya kuzifanya kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa Kamanda wa UVCCM, Salim Abri Asas, akishaapishwa yeye ndiye atakuwa na jukumu la kumuapisha wa wilaya ambaye naye atawapisha wa kata.
“Mimi sijui kama kuna sarakasi za kuwania ubunge katika jambo letu, najua kufanya hivyo tutaongeza gharama lakini ni lazima tufunge mkaja,” alisema.
Naye Mwakalebela alisema kutenganishwa kwa sherehe hizo kutaongeza gharama kwakuwa maandalizi ya pamoja yalishafanyika.
“Haya mambo ya siasa yana vitu vingi, mimi naona wana CCM tuna kila sababu ya kuepuka kushughulikiana katika kuwania ubunge,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

MAMBO YA KATUNI HAYO:CHANGAMSHA AKILI KIDOGO

PICHA YA WIKI:VIPI KAJALA ALIPENDEZA?

Msanii wa Bongo Muvi Kajala akifuatilia shoo kwa karibu zaidi

HAYO NDO MAMBO YA SERENGETI FIESTA WAJA LEO(TANGA)

SERENGETI FIESTA YAFUNIKA MKOANI TANGA

Mshindi wa Serengeti Super nyota 2013, Edo Boy akifungua burudani.Young killer akikonga nyoyo za mashabiki katika Tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
Mr. Blue akiwapagawisha washabiki jukwaani katika tamasha hilo.Recho akitumbuiza katika Tamasha la Fiesta mkoani Tanga.Tunda Man naye akifanya yake.Khadija Maumivu akifanya maajabu jukwaani.Shabiki akimkubali jux kwa shoo aliyoionyesha....Linnah naye akilishambulia jukwaa.
...Ni MO Music ndani ya usiku wa Tamasha la Fiesta mjini Tanga.Msanii wa Bongo Muvi Kajala akifuatilia shoo kwa karibu zaidi.Linnah akiwa na wanenguaji wake.Ommy Dimpoz akiwajibika mbele ya mashabiki zake.Madee akifanya makamuzi jukwaani.Vannesa Mdee akiliteka jukwaa usiku wa Fiesta mjini Tanga.

HUYO NDO MKUU WA WILAYA TANGA......HAPO VIP?

Ruge akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwenye Tamasha la Serengeti FiestaRuge akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya, Halima Omar Dendegu (kulia).

MSIBA:MASHABIKI WAMUUA MCHEZAJI ALGERIA..

MASHABIKI WAMUUA MCHEZAJI ALGERIA

MCHEZAJI kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya Ligi ya Algeria.
Albert Ebosse enzi za uhai wake.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyefunga mabao mengi katika Ligi ya Algeria msimu uliopita.
Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.

Marehemu ndiye aliyefunga bao hilo pekee kwa timu yake.
Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe kuhusiana na kifo hicho.

JE,HAO NI WALEVI AU ?MPAKA WAKAPOST HIYO PICHA

Sunday, August 24, 2014
 Picha ya Familia On Facebook;Vipi walilewa au ?

HABARI NA PICHA:VIPI MBUNGE WAKO YUPO KAMA HUYU???

Wananchi wa Kijiji cha Luvuyo Kata ya Madope wakimpokea Mbunge wao, Deo Filikunjombe kwa maandamano.
Wanachama wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wa Kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wakishirikiana jana na Deo Filikunjombe (kushoto) kuchimba mifereji ya maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe yenye urefu wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 50.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luvuyo mara baada ya  kuzindua ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe.
Deo Filikunjombe akisafirishwa katika mkokoteni wa kukokotwa na ng'ombe baada ya wananchi wa  Luvuyo ambao awali walitishia  kuhama  wilaya ya Ludewa kuhamia Njombe kusikilizwa kilio chao  cha ubovu wa  miundombinu kwa  kuanza kujengewa barabara na mbunge huyo

PICHA YA LEO:ALIKUWA ANAWAZA NINI HAPO FETTY?

SALIM ASAS SASA ANAFAA KUWA MBUNGE WA IRINGA MJINI,hutaki chechemea...

August 24, 2014

MWIGULU AMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA, MH. MWIGULU NCHEMBA AKIMSIMIKA KAMANDA WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM), MKOANI IRINGA SALIM ASAS, KATIKA VIWANJA VYA MWEMBETOGWA..
MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI IRINGA, TUMAINI MSOWOYA NA MWENYEKITI MWENZAKE WA MKOA WA KATAVI, WILLIAM MBOGO WAKIJADILI JAMBO WAKAZI WA ZOEZI LA KUMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM IRINGA SALIM ABRI
VIONGOZI WA UVCCM KUTOKA MIKOA MBALI MBALI WALIKUWEPO..ILIKUWA BURUDAAANI1...
MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI IRINGA TUMAINI MSOWOYA KIBIKI, MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI KATAVI, WILLIAM MBONGO NA KATIBU WA UVCCM WILAYANI MUFINDI KANTALA, MAMBO YALIKUWA YAKIENDA SAWIA WAKATI KAMANDA ASAS AKIAPISHWA
KATIBU WA UWT MANISPAA YA IRINGA CHIKU MASANJA NA MNEC WA MBEYA JIJI WAKILI, SAMBWE SHITAMBALA NDANI YA VIWANJA VYA MWEMBETOGWA KUSHUHUDIA SALIM ASAS, KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA AKISIMIKWA RASMI 
MH MWIGULU NCHEMBA, NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA, AKISAINI KITABU CHA WAGENI KWENYE OFISI YA CCM MKOA WA IRINGA....KABLA YA KUANZA SHUGHULI RASMI...
KAMANDA ASAS AKIWA MAKINI KUSIKILIZA KINACHOJILI MKUTANONI
SAFARI NI SAFARI...TUNAENDA ENEO LA MKUTANO..WA KWANZA KUSHOTO; TULA TWEVE MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM MKOA WA IRINGA

PICHA ZOTE NA FRANK KIBIKI
KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA, SALIM ABRI  AMEAPISHWA RASMI KUANZA KAZI YAKE YA UKAMANDA IKIWA NI KIPINDI CHA TATU KUANZA KUTUMIKIA NAFASI HIYO.
 
VIJANA WANAMPENDA SALIM ASA KUTOKANA NA UTU WAKE, MAPENZI YAKE YA DHATI KWA CCM, UPENDO WAKE, USHAURI, UALIMU NA ULEZI WAKE USIOJALI ITIKADI, RANGI, DINI, KABILI, MASKINI WALA MATAJIRI..
UDUMU SALIMU ASASI.

UJASIRIAMALI UNAOLIPA AFRIKA NI SIASA:TUNDAMAN NAE ANATAKA UBUNGE

Tundaman: Iddi Azan Ananiandaa kuwa Mbunge, 'Napata Ushauri kwa Mheshimiwa Lowasa..'

Sunday, August 24, 2014
Tundaman ameweka wazi mpango wa kuingia rasmi katika siasa na kukitafuta kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu baada ya 2015.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Tundaman ameeleza kuwa alipata moyo na wazo la kugombea kiti cha ubunge kutoka kwa mbunge wa Kinondoni, mheshimiwa Iddi Azan.

“Rafiki yangu sana Iddi Azan, sometimes nikikaa nae sehemu wananchi wananishangilia mimi anasema ‘Tunda unapendwa hivi, basi na wewe uje kugombania mambo haya’. Nikasema basi sawa na hilo suala nalifanyia kazi, kwa hiyo mimi ntachukua details nyingi kutoka kwake na yeye ndiye anaeniandaa mimi kuwa mbunge baadae (sio 2015).” Amesema Tunda Man.

Ameeleza pia kuhusu jinsi anavyopata ushauri wa siasa kutoka kwa wanasiasa wakubwa akiwemo waziri mkuu wa zamani Mheshimiwa Edward Lowasa.

“Kwa sababu niko karibu sana na waheshimiwa wananishauri, kwa hiyo najua nini cha kufanya na nini nisifanye. Sometimes nakaa na Lowasa ananiambia vitu vingi mheshimiwa kwamba siasa iko hivi… kwa hiyo kuna vitu fulani mimi ninapata bila wao kujua napata kutoka kwao. Lengo baadae nitakapovifanya nisiwe nakosea, niwe straight katika kuvifanya ili nifanikiwe.”

CHRIS BROWN ANUSURIKA KIFO

CHRIS BROWN ANUSURIKA KIFO, SUGE KNIGHT AKIJERUHIWA KWA RISASI

Cris Brown akiwa Klabu 1OAK kabla ya vurugu kutokea.
 
Prodyuza mkongwe, Suge Knight amejeruhiwa tumboni na mkononi katika shambulio hilo.
MWIMBAJI Cris Brown amenusurika kuuawa katika shambulio la risasi ndani ya klabu ya usiku jijini Los Angeles ambapo prodyuza Suge Knight amejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika klabu ya usiku iitwayo 1OAK iliyopo magharibi mwa Hollywood wakati wa shoo iliyokuwa ikiongozwa na Cris Brown kabla ya zoezi la utoaji Tuzo za VMA ambapo watu watatu wamejeruhiwa mmoja akiwa mahututi.
Suge Knight alipigwa risasi mara mbili tumboni na mkononi na kukimbizwa hospitali ambapo anaendelea na matibabu.
Mastaa wengine waliokuwepo kwenye klabu hiyo wakati tukio hilo likitokea ni pamoja na Justin Bieber, rappa The Game, Pia Mia, Tyson Beckford, Robert Ri'chard  na wengineo.
Indaiwa mlengwa mkuu katika shambulio hilo alikuwa Cris Brown.

Saturday, 23 August 2014

DJ FETTY NDANI YA MAHABA NIUEEEE NA MUL B'

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’ na DJ Muli B, wamenaswa wakiwa kwenye pozi la mahaba huku tena wakiwa wamejisahau utadhani mume na mkewe.
 
Mtangazaji wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty' akiwa na 'DJ Muli B’.
Ishu hiyo ilitokea Agosti 17, Mwaka huu ndani ya Uwanja wa Kahama, ambapo walienda kwa ajili ya kutazama burudani za Serengeti Fiesta 2014 zilizokuwa zikifanyika siku hiyo.
Wakiwa nyuma ya jukwaa, wawili hao walionekana kubebana wakati wamekaa jambo lililowafanya baadhi ya wasanii waliokuwa nyuma yao kukonyezana na wengine kuulizana maswali ambayo hayakuwa na majibu kama ni wapenzi au laa.
 
‘DJ Fetty' na 'DJ Muli B’ wakila ujana.
Paparazi wetu apowauliza kama wana uhusiano wowote, wawili hao walikanusha na kusema wamepozi kama mtu na mfanyakazi mwenzake Clouds FM.