Friday, 29 August 2014

HUU NDO UNAFIKI WA MBOWE....BAADA YA KUMTOA ZITTO KAMA MSALITI.

MBOWE: ANAYETAKA KUPIMA KIFUA NA MIMI AJE CHADEMA
Friday, August 29, 2014

Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe akisoma fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho baada ya kukabidhiwa na mwakilishi wa wazee wa Mkoa wa Kigoma, Athumani Mzigo
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.
“Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.
“Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:
“Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.
Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).
Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:
“Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.
Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.
“Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.
Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo
Mbowe akubali
Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”
Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.
“Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.
Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000... “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu.
Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.
“Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.
Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”
Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji... “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.
Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.
Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”
Chanzo;Mwananchi

MANJI ACHARUKA....SUALA LA OKWI KWENDA SIMBA

SUALA LA OKWI KUSAINI SIMBA, MANJI ACHARUKA..

August 29, 2014
Manji akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakisikiliza kwa makini.
Kikao kikiendelea.
Mwenyekiti wa Yanga (Manji) akisisitiza jambo, kushoto ni Makamu wake, Clement Sanga.
Msistizo ukiendelea.
... Akionesha kidole kutoa mfano.
Kocha Marcio Maximo (kushoto) akizungumzia kuimarika kwa timu yake Visiwani, Zanzibar.
BAADA ya jana uongozi wa timu ya Simba chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope, kutangaza kumsainisha mshambuliaji, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda, uongozi wa Yanga kupitia mwenyekiti wake, Yusuph Manji, mchana huu nao umetoa tamko rasmi la kumshitaki mchezaji huyo kwa shirikisho la soka nchini (TFF) pamoja na viongozi wa Simba na Klabu hiyo.
Katika mashitaka hayo Yanga imemshitaki Okwi, Simba na viongozi wake kwa kuvunja mkataba wakati mgogoro wa mchezaji huyo na Yanga ukiwa haujapatiwa ufumbuzi. Manji amesema katika madai hayo wanadai fidia ya dola milioni mia tano za Kimarekani.
Wakati huohuo, kocha wa kikosi hicho Mbrazil Marcio Maximo ameelezea kuimarika kwa kikosi chake kwenye kambi ya wiki mbili waliyofanya Visiwani Unguja na Pemba.

NANI MKWELI HAPO:::DIVA AMLIPUA ZITTO KABWE


BAADA YA ZITTO KUMKANA DIVA....DIVA NAE ALIPUA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZVbLymMwdNr3s-SRZYtC404LXg8tCLnpw4NpqRfAoHUB_YBDkl1EwL_eH1OrKoi70v4a9S_gwLdzHgegDjN4GHmM7azp09x6w_RM-snTx-WLibDCWpz5unz30L2iMkN5UcVzLwjmBaZj4/s1600/dz1.jpg

MOTO! MOTO! MOTO!!!JAMAN MBEYA LEO KUNANI???HOTELI INAUNGUA

BREAKING NEWS LIVE MUDA HUU: ILIYOKUWA HOTEL YA STOCKHOLM UYOLE MBEYA YATEKETEA KWA MOTO MUDA HUU

29TH AUGUST 2014




AJALI!! AJALI!!AJALI::::WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA MBEYA

August 29, 2014

WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 

Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni Ajali mbaya 

Mashuhuda 
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 

WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
na fredy mgunda

Cristiano Ronaldo

http://api.ning.com/files/bsmQVYBkFPjGkbKe25gfBpNlUOO*VS1eMzVsRaiTSjDyWBY7qoCthQpG14tEziCudirpbOouHdg0f5A*UryIdadoM8FKgW8m/1409261957864_wps_1_epaselect_epa04372610_Por.jpg

Thursday, 28 August 2014

JB: JIONEE ALINICHONIFANYA Q-CHILLAH!

JB: JIONEE ALINICHONIFANYA Q-CHILLAH!

 August 28, 2014
Stori: Mwandishi Wetu
Sura ya mauzo kwenye Bongo Movies, Jacob Steven ‘JB’ ameweka plain kwamba alichomfanyia staa wa Bongo Fleva, Aboubakar Shaban Katwila ‘Q-Chillah’ kwa mara ya kwanza kwenye filamu yake ya Hukumu ya Ndoa Yangu (part III), kimemshtua.
Akistorisha na safu hii, JB alifunguka kwamba staa huyo ambaye amerudi upya aliitendea haki sinema hiyo kwani alionesha kipaji cha aina yake.
“Kama ulikuwa hujui kwamba Q-Chillah ana kipaji cha kipekee, pata nakala yako ya sinema yangu mpya ya Hukumu ya Ndoa Yangu sehemu ya tatu, ipo madukani tangu alhamisi wiki hii. Kama unavyojua, Jerusalem Film Productions huwa hatufanyi kosa. Ndani ya Hukumu ya Ndoa Yangu utakuwana na mimi mwenyewe, Q-Chillah, Shamsa Ford, Mayasa Mrisho, Wellu Sengo na wengine kibao,” alifunguka JB

MESSEJI YA LEO....

Screen Shot 2014-08-19 at 8.45.55 AM

HAWA NDO MADAKTARI BINGWA WA KUTOA MIMBA MADENTI

KIMBEMBE CHA MADAKTARI

August 28, 2014
Stori: Chande Abdallah, Mayasa Mariwata na Deogratius Mongela
IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya  kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.
Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu  ‘OFM’ ya Global Publishers  ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani humo, Dokta Chacha alidai kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi hivyo alikuwa akitaka kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa na denti huyo aliyedai kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba ili akaendelee na masomo chuoni.
Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.
Zahanati iliyotumiwa na madaktari hao katika jaribio la utoaji mimba.
Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.
Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.

KUDADADEKIII::JESHI UGANDA KUANDAA "MISS UGANDA"

Jeshi la Uganda lime-take over! sasa ndio litaandaa shindano la Miss Uganda.

Screen Shot 2014-08-28 at 8.27.35 AM 
Toka nimeanza kuandika na kufatilia habari sijawahi kusikia jeshi la nchi limechukua hatamu kuendesha mashindano ya urembo tena mashindano yanayokutanisha warembo kutoka sehemu mbalimbali za taifa ili kumtafuta mshindi.
Stori hii ya kipekee inatokea Uganda ambapo jeshi la nchi hiyo limeamua hivyo baada ya kuona ubabaishaji unaofanywa na Waandaaji wa Miss Uganda shindano ambalo halikufanyika kwa miaka kadhaa kutokana na ubabaishaji.
Ripota wa TZA Kampala Bill the African, ameripoti kwamba mmoja kati ya wenye vyeo vyao jeshini ambae pia ni mdogo wake Rais Museven amesema jeshi limeamua kuchukua usimamizi wa mashindano haya kwa madai kwamba ni njia ya kuwavutia vijana wapende kilimo kitakachotangazwa kupitia haya mashindano ikiwa tayari pia jeshi hilo limechukua Wizara ya kilimo kwa ajili ya kuiongoza.
Screen Shot 2014-08-28 at 8.11.06 AM 
Bill alipozunguka mtaani kuwauliza watu maoni yao imekua 30 kwa 70 yani kuna ambao wanaona hakuna shida Wagumu hawa kuongoza mashindano hayo lakini wengine wengi wanapinga wakisema Jeshi hili linajulikana kabisa huwa halicheki na mtu wala halina urafiki na Raia sasa ndio wataweza kuendesha mashindano ya Urembo? ni vitu viwili tofauti kabisa.

KUMBE ZITTO ANA MTOTO....AMKANA DIVA

Zitto Kabwe Kwa Mara ya Kwanza Aongelea Uhusiano Wake na Diva Loveness, Amkana Diva

August 28, 2014
KWA mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.

Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.

Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.

Alisema anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.

“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.

Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.
GPL

MAMBO YA WAPENDANAO HAYO:MARIAH CAREY NA NICK ,NDOANA

MARIAH CAREY, NICK CANON WABWAGANA BAADA YA MIAKA SITA

  August 28, 2014

Mariah Carey alipokuwa mjamzito
ILE ndoa ya kijana mdogo, msanii Nick Canon (33) na mwanadada (shuga-mami) mwimbaji Mariah Carey (44)  imefikia ukingoni baada ya kuweko kwa miaka sita.…

Mariah Carey alipokuwa mjamzito
ILE ndoa ya kijana mdogo, msanii Nick Canon (33) na mwanadada (shuga-mami) mwimbaji Mariah Carey (44)  imefikia ukingoni baada ya kuweko kwa miaka sita.
Wanandoa hao wakiwa na watoto wao Moroccan and Monroe.
Hata hivyo, mtengano huo umezusha mgogoro wasiwasi mkubwa, hususani kwa Canon, kuhusu hatima ya watoto wao mapacha waliobahatika kuwapata – mmoja wa kiume na mwingine wa kike.

Carey na Canon enzi za upendo wao.
Sababu za kutengana kwa wasanii hao wanaoishi California, Marekani, bado hazijawekwa wazi.

Namna ya Kuondokana na Tatizo la Kutojiamini

Namna ya Kuondokana na Tatizo la Kutojiamini

Kila kitu ambacho ni halisi kinawezekana. Bila shaka unakumbuka vizuri kuhusu namna kutojiamini kwetu kunavyojengwa. Kwa kuwa tunajua chanzo, ni rahisi kupata tiba.

Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia katika kujenga kujiamini. Kuna njia nyingi zinazopendekezwa, lakini kuna zile ambazo zimetumika sana katika kufanya kazi hiyo. Hizi zifuatazo ni baadhi yake.

1. Yachunguze mawazo yako na vitendo vyako kwa uangalifu ili kujua ni kitu gani hukufanya usisimke. Anza kufanya mambo ambayo unaona kwamba una uwezo kuyafanya bila wasiwasi na kuchukua uamuzi unaojitegemea kufuatana na utashi wako. Ikibidi unaweza kuomba msaada wa wengine, lakini jaribu kila mara kufanya mambo kufuatana na unavyoyaona.

2. Jifunze kujithamini. inawezekana kwa miaka na miaka umekuwa unajiona kama mtu usiye na thamani. Pia unaweza ukaona kwamba, hadhi uliyokuwa nayo mbele ya ndugu, jumuiya na jamii imepungua. Jali ujuzi na vipaji vyako; hata kama kuna ndugu wametajirika pamoja na kuwa ni mbumbumbu hiyo isiwe chanzo cha kukuvunja nguvu. Iko siku utafanikiwa kama utaanza kujiamini.
3. Jisamehe bila masharti yoyote. Kama maisha yako ya awali yalikuwa si ya kiungwana, jisamehe na anza maisha yako upya. Njia bora ya kujisamehe ni kujipenda bila masharti yoyote.

4. Pambana na hofu. Hofu ni kitu kibaya sana kwa sababu inaingilia kwenye uwezo wako wa kufikiri. Ili ufanikishe malengo yako ya maisha huna budi kuhakikisha kuwa huna hofu tena.

5. Fanya vitu unavyoviogopa. Orodhesha idadi ya vitu ambavyo ulikuwa unaviogopa. Kisha anza na vitu ambavyo unaviogopa zaidi na jiulize kwa nini usiweze kuvifanya.

6. Jifunze kupambana na kushindwa. Kubali kwamba kushindwa ni kama chombo cha kujifunzia na si kitu cha kukukatisha tamaa. Jua, na amini kwamba, bila kushindwa hakuna kukua. Pia elewa kwamba, kushindwa siyo dalili ya udhaifu, bali uimara.
7. Kubali kupingwa kwa moyo mkunjufu. Watu wa nje wanaweza kukusaidia kwa mambo yako mengi ambayo huyaoni. Watu wakikusoa, hata kama ni kifedhuli, chukua yaliyo mema na yafanyie kazi.

8. Fanya mazoezi ya kujiamini. Jifunze kusimama kwa miguu yako mwenyewe kimawazo, kiimani na kimatendo. Bila kuonyesha ujeuri unaweza kulinda haki zako, matarajio yako na maadili yako. Anza kujifunza kujenga taswira ya kujiona uko mwenyewe na unamudu kila kitu. Bila msaada na utegemezi kwa wengine.

9. Jipongeze kwa maneno mazuri. Jiamini na daima jipe moyo kwa maneno ambayo yatakutia moyo ili kwenda vyema katika shughuli zako. Usitumia maneno ya kejeli, kashfa na chuki dhidi yako mwenyewe, ‘mimi ni mjinga kweli yaani jambo dogo kama hili limenishinda….’ Unaweza kujisemea baada ya kukosea. Kama umekosea, jiambie maneno mazuri ya kujipa moyo na siyo maneno ya kero na fadhaa.

10. Usijilinganishe na wengine, bali iga. Kama wengine wanakuzidi isikukatishe tamaa ila iwe ni chachu ya maendeleo . jiambie, ‘kama wanaweza, maana yake ni kwamba, inawezekana, nami nitaweza tu.’

11. Fikiria mambo ambayo yanakufanya usiwe na furaha na jaribu kupambana nayo na kuondokana nayo. Kila wakati jiulize, ni kwa nini uko kwenye hali ya kihisia uliyo nayo. Usikubali kufuga huzuni kwa muda mrefu ndani mwako.
12. Fanya mambo uyapendayo zaidi. Kujiamini kutaongezeka kama utafanya mambo unayoyafahamu zaidi kwa sababu ni rahisi kuyafanikisha na kukuletea furaha.

13. Jifunze namna ya kushughulikia hasira zako. Mtu asiyejiamini ana kawaida ya kutaka kupendwa na watu, na katika kufanya hivyo, hapendi kuonekana kuwa ni mtu mwenye hasira na hivyo kuendelea kubakia na hasira zake moyoni hata kama ameudhiwa.

14. Kuzuia hasira hakusaidii, zaidi ya kukuongezea kuchanganyikiwa na kukufanya kuwa mtu usiye na furaha au kisirani. Ukiudhiwa, mwambie aliyekuudhi kinaganaga, lakini katika mazingira ya kistaarabu ambayo hayawezi kukuumiza wewe wala mtu ambaye amekuudhi.