Wednesday, 10 September 2014
RAIS YOWERI MUSEVENI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MOJA
Uamuzi mgumu: Rais hataongeza muda Bunge la Katiba.....Sitta Aitisha Vikao vya Dharura kamati ya Uongozi
Kutwa
nzima ya jana, viongozi wa Bunge Maalumu walishinda kwenye vikao vya
mashauriano huku wabunge wa CCM wakitarajiwa kukutana jana usiku kwenye
makao makuu ya chama hicho kupewa taarifa rasmi za uamuzi huo.
Katika
makubaliano baina ya TCD na Rais Kikwete, imeamuliwa kuwa uamuzi wa
Rais kupitia Tangazo la Serikali (GN) 254 la kuongeza siku 60 hadi
Oktoba 4 uheshimiwe na baada ya tarehe hiyo Bunge liahirishwe.
Uamuzi
huo ni kinyume cha azimio la Bunge Maalumu la Agosti 5, 2014 ambalo
lilirekebisha Kanuni ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku
zilizotajwa kuwa za kazi, pia sikukuu na siku za Jumapili.
Mwenyekiti
wa Bunge, Samuel Sitta alikaririwa akiwaambia wajumbe wa Bunge hilo
kwamba Rais alikuwa ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazingejumuisha
Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.
Ni
kwa msingi huo, Bunge hilo likapanga kwamba lingeendelea na shughuli
zake hadi Oktoba 31, wakati Mwenyekiti wa Bunge atakapokabidhi Katiba
inayopendekezwa kwa Rais Kikwete.
Hata
hivyo, makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa TCD na Rais
yanaonekana kuvuruga kabisa ratiba ya Bunge hilo ambalo jana na juzi,
Kamati ya Uongozi ilikutana mara kadhaa kuona jinsi ya kunusuru mchakato
huo.
Ingawa
haikufahamika mara moja kama vikao hivyo vya kamati ya uongozi
inayoongozwa na Sitta mwenyewe vinajadili nini, lakini taarifa zimedai
huenda kukawa na mabadiliko makubwa ya ratiba.
Habari
nyingine zinadai kwamba mabadiliko hayo huenda yakapunguza muda wa
baadhi ya shughuli za kazi za Bunge hilo ili liweze kukamilisha kazi
yake ikiwamo wajumbe kupiga kura ya uamuzi.
Katika
kikao cha jana asubuhi, kamati hiyo ilishindwa kurekebisha ratiba yake
ili iendane na siku zilizosalia, hivyo kuahirishwa kwa kuwapa kazi
wataalamu wake kuleta mapendekezo ambayo yangejadiliwa jana mchana.
Katibu
wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha jana kwamba ratiba
ya Bunge imebadilika kutokana na hoja nyingi kukubalika ndani ya kamati.
“Kamati
ya uongozi itakutana baadaye (jana) kuangalia vipengele ambavyo
hawakukubaliana kwenye kamati ndivyo wavipangie muda na ratiba
itajulikana baada ya kikao hicho,” alisema Hamad.
Hofu ya akidi
Hata
hivyo, habari zaidi zinadai kwamba uongozi wa Bunge Maalumu
ulichanganywa na kuwapo kwa hoja za baadhi ya wajumbe wake kutaka kwenda
Makka kwa ajili ya kushiriki Ibada ya Hijja, hali inayotishia akidi kwa
ajili ya kuendesha vikao.
Kanuni
za Bunge Maalumu zinataka kuwapo kwa nusu ya wajumbe kutoka pande zote
za Muungano wakati wa kuendesha vikao vyake na theluthi mbili ya wajumbe
hao kila upande wakati wa kufanya uamuzi au kupiga kura.
“Tumetoka
kwenye kikao mchana huu na pengine tutaitana tena maana hatujafikia
mwafaka, kuna mambo mengi yamejitokeza lakini kubwa ni hili la wenzetu
ambao wanataka kwenda Hijja, kuondoka kwao kunaweza kuathiri akidi kwa
kiasi kikubwa,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo.
Kutokana
na matakwa hayo, hivi sasa Ofisi ya Katibu wa Bunge inafanya tathmini
ili kufahamu idadi ya wajumbe ambao watakwenda Hijja Septemba 22, mwaka
huu, ambao wengi wanatoka Zanzibar.
Hamad alikiri kwamba kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inayafanyia kazi na kwamba hilo la Hijja ni mojawapo... “Kwa
sasa siko katika nafasi ya kuzungumza kwa kirefu, kikao cha Kamati ya
Uongozi kimeisha na bado kuna kazi nyingi za kuona jinsi
tunavyoendelea.”
Tayari
Bunge hilo limetikiswa na kutokuwapo kwa wajumbe waliosusia vikao tangu
Aprili 16, mwaka huu ambao ni wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR
Mageuzi na baadhi kutoka Kundi la 201.
Taarifa ya TCD
Jana
saa 7:00 mchana, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alikutana na wanahabari
na kueleza kuwa katika mazungumzo yao na Rais wamekubaliana mambo matano
ya msingi kwa mustakabali wa nchi.
Alisema
pamoja na kazi ya msingi iliyofanywa na Bunge Maalumu, mchakato
unaoendelea hauwezi kutoa Katiba Mpya ambayo itatumika katika Uchaguzi
Mkuu wa 2015.
“Muda
hautoshi kukamilisha mchakato na kufanya mabadiliko yatakayohitajika ya
sheria, kanuni na taasisi mbalimbali zinazohitajika,”alisema Cheyo ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP).
Alisema
kura ya maoni ilipangwa kufanyika Aprili 2015 na kama itabidi irudiwe,
basi itabidi irudiwe itakuwa Juni au Julai 2015, muda ambao Bunge la
Jamhuri linatakiwa livunjwe.
“Ili
Katiba Mpya itumike katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, itabidi uhai wa Bunge
na Serikali uongezwe zaidi ya 2015, jambo ambalo sisi viongozi wote
hatuliungi mkono,” alisema Cheyo.
Alisema
kwa kutambua kuwa kama kura ya maoni ikifanyika, italazimisha Uchaguzi
Mkuu wa 2015 kuahirishwa, wamekubaliana kura hiyo iahirishwe hadi baada
ya uchaguzi huo.
Bunge Maalumu
Cheyo
alisema Bunge Maalumu kwa sasa linafanya kazi kwa mujibu wa Tangazo la
Serikali (GN), namba 254 lililotolewa na Rais Kikwete ambalo uhai wake
utakoma Oktoba 4.
“Inategemewa
kuwa Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana. Tulikubaliana hatua
hii iachwe ifikiwe na baada ya hapo Bunge liahirishwe hadi baada ya
Uchaguzi Mkuu 2015.
“Tarehe
4 Oktoba ndiyo mwisho. Hiyo ndiyo sheria iliyopo, sisi hatuna mamlaka
ya kuandika GN mpya, GN imetolewa na Bunge hili liko kihalali.
Tulichokuwa tunabishana lisife kesho,” alisema.
Akijibu maswali ya wanahabari kama ana uhakika Bunge hilo litaweza kukamilisha kazi yake ndani ya siku zilizobaki, Cheyo alisema“Tumeheshimu
sheria iliyopo tarehe nne Watanzania wanategemea Katiba Mpya itakuwa
imepatikana, sasa kama haitapatikana hilo msiniulize kwa sababu hilo si
jukumu langu.”
Alipoulizwa kama rais ajaye baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 ataendeleza mchakato pale ulipoishia alisema:
“Naomba
Mungu rais ajaye awe anayejali maoni ya wananchi hilo naomba kabisa.
Sasa tukipata rais ambaye hatutambui sisi wote na mawazo yetu, basi
tutakuwa tumekosea katika kupiga kura.”
Mabadiliko ya 15 ya Katiba
Cheyo
alisema kwa vile Uchaguzi Mkuu wa 2015 utafanyika kwa kutumia Katiba ya
1977, ni vyema yakafanyika mabadiliko madogo ili kuruhusu uchaguzi huru
na wa haki.
Mabadiliko
hayo yatalenga kuwezesha uwapo wa tume huru ya uchaguzi, mshindi wa
urais ashinde kwa zaidi ya asilimia 50, kuruhusu mgombea binafsi na
kuingiza ibara itakayoruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani.
“Vyama
vya siasa ambavyo vinapenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha
katika Katiba ya 1977 vinaombwa kufanya hivyo kwa vile muda tulionao ni
mdogo,” alisema Cheyo.
Alisema
walikubaliana kuwa marekebisho hayo yafanyike katika Bunge la Jamhuri
litakaloanza Novemba 5 na ikishindikana yafanywe Februari 2015.
Ukawa kurudi bungeni
Cheyo
alisema suala la kurudi au kutorudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba
kwa wajumbe wa Ukawa halikuwa sehemu ya mkutano kati ya Rais na TCD.
Uliipata ile ya Nabii Tito?leo wamezungumza Dr.Isack Maro na Anti Sadaka.
chanzo millard.

Kama uliiskiliza Hekaheka ya jana ambayo ilikua ikimhusu Nabii mmoja aliyejipa jina la Nabii Tito anayepatikana maeneo ya sinza,ambapo mahubiri yake yako tofauti na maagizo anayofundisha Mungu kwenye vitabu vyake.
Miongoni mwa mambo ambayo aliyazungumza na kuwashangaza watu ni pale alipodai kunywa pombe sio dhambi na hata kuzaa na msichana wako wa kazi yaani House Girl ni ruksa.
Kingine alichosema ni kuhusu matumizi ya mipira ya kujamiiana(CONDOM) ni dhambi na waumini wake ni WALEVI TU,Leo utamskia Ant Sadaka ambaye ni mwanasaikolojia pamoja na Dr Isack ambao watamwelezea kwakina huyu nabii Tito matatizo gani aliyonayo ya kiakili.
Tuesday, 9 September 2014
BEN MKAPA::VIJANA WEKENI MSISITIZO MASOMO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI MUWE WAJUZI NA KULETA MAENDELEO NCHINI
Kiukweli sayansi na teknolojia inasadikiwa kuwa mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi yenye kuhitaji haraka hutegemea sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa.
Licha ya kuwepo kwa changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi nyingi za Afrika katika kupata maendeleo ikiwa ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia, hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa Wataalam wa kutosha katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo nchi za Afrika zinahitaji kujikwamua na changamoto hiyo kwa kuhakikisha kuwa zinawekeza katika sayansi ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
Sayansi na teknolojia hapa duniani huleta maendeleo makubwa hivyo Vijana wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili kuweza kuleta uchumi endelevu.
Sambamba na hilo, katika Kongamano liloandaliwa hivi karibuni na Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania ambao ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.
Dkt Mohammed Gharib Bilal ambao ulikuwa ni mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani wenye lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki vyema katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa uchumi thabiti, Wakala wa Jiolojia nchini, Profesa Mruma alisema kuwa Mkutano huo una lengo la kurithisha taaluma ya jiolojia inayohusisha madini, rasilimali, gesi na mafuta kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Kongamano hilo la Vijana liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya 42 zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika Tanzania ikiwemo na ambaye ndiyo alikuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.
Katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na madini, Mhe. Masele alisema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake kwa katika kuendeleza sayansi ya mambo ya gesi na mafuta pamoja na afya kwa kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwapeleka baadhi ya Watanzania kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi, mafuta na afya kwa lengo la kuja kuisaidia nchi.
Aidha, Mhe. Masele alisisitiza kuwa wajibu wa Serikali kuamua kwa makusudi kusomesha vijana katika nchi mbalimbali ni kuwawezesha vijana waweze kupata elimu juu ya sayansi na teknolojia hasa katika masuala ya gesi ili kupata wataalam na wakaguzi wa kutosha nchini ambao watalisaidia taifa kuinua uchumi wake.
“Hivi sasa Serikali imeanzisha vyuo mbalimbali nchini, programu mbalimbali za mafunzo kwa watanzania, imetoa ufadhili wa masomo kwa watanzania na imedhamini makongamano ya vijana ili wapate fursa ya kujiendeleza’, alisema Masele.
Mhe. Masele pia aliyataka Makampuni ambayo ndiyo yalikuwa Wadhamini wa kongamano hilo kuendelea kuwekeza nchini pamoja na kuendelea kulipa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato na wananchi wapate kunufaika na mapato hayo.
Halikadharika, katika mkutano mwingine uliohusiana na mambo ya Jiolojia uliowakutanisha Wataalam mbalimbali wa mambo ya jiolojia ulimwenguni jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi wa mkutano huo aliziasa jamii hizo za Kiafrika kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo ya sayansi na teknolojia ili ziweze kujikwamua kimaendeleo.
Mhe. Mkapa alisema kuwa jamii nyingi za kiafrika hazijaelewa mchango mkubwa wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo licha ya ukweli wa kwamba maendeleo daima yanatokana na rasilimaliwatu iliyopo juu ya ardhi na chini ya ardhi, mchango wake huo hauthaminiwi na wengi lakini wanaoweza kufanya hivyo ni Wanasayansi.
“Serikali licha ya kudhamini mafunzo mbalimbali na masomo kwa vijana nje na ndani ya nchi, fedha za kutosha bado zinahitajika katika kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakuwa endelevu”, alisema Mhe. Mkapa.
Bila shaka kuna haja ya kizazi kilichopo na kijacho kurithishwa uelewa mzuri kuhusiana na mambo ya jiolojia ya jamii, jiolojia ya madini, mazingira na mabadiliko ya tabianchi, vyanzo vya nishati, matatizo yanayotokana na milipuko kama jiolojia na kuunganisha elimu ya Tehama na jiolojia kwani hii itawasaidia vijana wengi kuelimika vya kutosha kuhusiana na mambo ya jiolojia na pamoja na maendeleo kwa manufaa yao wenyewe.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao huo kwa upande wa Tanzania Bw. Stephen Joseph Nyagonde alitaja kauli mbiu ya mkutano huo kuwa ni ”Kuhakikisha ushiriki wa vijana katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi imara”.
Katika mikutano hii yote, wadau mbalimbali wakiwemo Wanasayansi Vijana walipata fursa ya kujadiliana kwa kina na kutoa mapendekezo ya kisayansi ya namna ya dunia inavyotakiwa kupiga hatua za kimaendeleo na kuboresha maisha ya wakazi.
Jamii nyingi za Kiafrika kiuhalisia hazina uelewa wa kutosha kuhusiana na mchango wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo nchini hali inayopelekea kuzorota kwa maendeleo ya nchi nyingi za Kiafrika.
Hivyo Wanasayansi ulimwenguni wanatakiwa kujenga utamaduni wa kukutana mara kwa mara na kujadili mambo yanayohusu Sayansi na teknolojia ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii hizo.
Endapo vijana nao wakichangamkia fursa mbalimbali za masomo yanayohusiana na mambo ya rasilimali zipatikanazo nchini mwao kama vile gesi asilia, mafuta na madini mengine wataweza kutatua kitendawili cha umasikini Barani Afrika na nchini mwao, hasa vijana wa kike kujenga utamaduni wa kujikita katika masomo ya sayansi ili waweze kuwa wabunifu na kujikwamua na maisha yao.
Spika Sitta Kumpa Nafasi Hamad Rashid ili Amtukane Maalim seif ni Sawa ?
ampa dakika za kutosha kumshambulia na kumtukana na kujitangaza kua yeye ni msafi na kutangaza kuwa atagombea wa urais wa Zanzibar.
Ninajiuliza ni sawa kwa mheshimiwa spika kufanya haya?
Kwa nini asiache hayo masuali ya Hamad Rashid wamalizane kwenye vyombo vya habari kama Maalim alivyofanya?
Mtanzania Wameandika Hivi Kuhusu Hilo:
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amemshambulia kwa maneno Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, huku akimfananisha na popo.
Mbunge huyo alisema hayo baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, akisema lengo ni kujibu mashambulizi yaliyoelezwa kwake na Maalim Seif kupitia kituo kimoja cha televisheni.
Baada ya kupewa fursa hiyo, Hamad alisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kwa kuwa hana msimamo kisiasa jambo ambalo linamfanya awe kama popo ambaye hajulikani kama ni ndege au mnyama.
Breaking news:KATIBA YA ZAMANI KUTUMIKA 2015..
Posted by: Millard Ayo

Ni taarifa kutoka bungeni ambayo itasaidia kukata kiu ya waliokua wanaisubiria au wanasubiri kufahamu kuhusu katiba mpya ambayo imekua ikiundwa, kama itatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Ripoti kutoka Dodoma zinaamplfy kwamba katiba ya zamani ndio itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho 2015 lakini itafanyiwa marekebisho ambayo ni
1. kumpa ruhusa mgombea binafsi kugombea,
2. kuwa na tume huru ya uchaguzi ya kusimamia uchaguzi,
3. mshindi wa Urais ashinde kwa zaidi ya asilimi 50,
4. matokeo ya uchaguzi wa Urais yaweze kupingwa Mahakamani,
5. kuwe na tume huru ya kusimamia uchaguzi.
‘Vyama vya siasa vinavyopenda kupendekeza mambo mengine ya kurekebisha katika katiba ya Jamuhuri ya muungano ya mwaka 1977 vinaombwa kufanya hivyo mapema’ – John Cheyo
Haya yametokana na kikao kilichofanyika kati ya Rais Kikwete na kituo cha demokrasia Tanzania ambapo Mwenyekiti wa kituo hicho John Cheyo.
Kisirani Champonza Lulu Michael…Tajiri Wa Madini Ammwaga
Star wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto
wa kipekee, Lulu Elizabeth Michael anadaiwa kutodumu na mwanaume
sababu ya kuendekeza ubabe na kutaka kum-control mwanaume anayekuwa
naye.
Inadaiwa Lulu hataki mchezo, mwanaume
akishakuwa nae basi lazima ahakikishe hafurukuti. Taarifa zinadai kuwa
miezi ya hivi karibuni alikuwa na jamaa mmoja mdogo kimapenzi
akammwaga na baada ya muda akawa anatoka na tajiri mmoja wa madin toka
Arusha lakini tajiri huyo alinyoosha mikono juu baada ya Lulu kama
kawaida kuruhusu majeshi yake yam-control jamaa huyo.
Chanzo kimoja kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kimesema:
TAMKO LA KUDHALILISHWA KWA MASHEIKH WANAOTUHUMIWA KWA UGAIDI
Listi ya waigizaji matajiri duniani, Shahrukh Khan wa India katisha kwenye listi
Wapenzi wengi wa filamu duniani watakuwa wanalitambua jina lake ambapo kwa Tanzania ni maarufu zaidi uswahilini lakini duniani ndio anatajwa kuwa muigizaji anayejulikana zaidi.
Jina lake ni Shahrukh Khan ambae ni mwigizaji wa filamu kutoka India ambapo jana ametengeneza headlines baada ya kutajwa na jarida la maswala ya fedha la Wealth-X la Singapore ndio mwigizaji tajiri zaidi Asia pia anashika nafasi ya pili duniani nyuma ya comedian Jerry Seinfeld ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani milioni 820.Khan ambaye ni maarufu kwa jina la Kingh Khan ana utajiri wa $600m akiwa kawazidi waigizaji wakubwa Hollywood kama Tom Cruise mwenye $480 million, akiwafuatia na Johny Depp na Tyler Perry ambao wote wana $450 million.
Listi hiyo imechanganya waigizaji washindi wa tuzo za Academy kama Jack Nicholson ($400 million), Tom Hanks ($390 million) na Clint Eastwood ($370 million) Nicholson ni namba 6 akifuatiwa na Hanks, Bill Cosby, Eastwood na Adam Sandler
BADO ULAYA...Mwigizaji Mkongwe Nchini Lucy Komba Afunga Ndoa. Tazama Picha za Harusi
Hatimaye yule mwigizaji mkongwe nchini Lucy komba amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi aishie nchini Denmark aliyefahamika kwa jina la Stanley,. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii nchini lucy ameandika
"..Asante Mungu kwa siku hii nzuri na muhimu sana katika maisha yangu, wengi hawakutaka nifikie siku hii, kunawengine walinuna, kunawengine waliniombea mabaya, kuna wengine walichukia na wengine waliambiana wanichunie walifikiri bila wao Mungu hawezi kuifanikisha siku hii, nasema asante Mungu kwa sababu aliifanikisha siku hii kwa nguvu zake wqtu wanaonipenda walisheherekea siku hii vizuri walikunywa na kula na kusaza watu zaidi ya miasita walikuwa ukumbini wakishangilia pamoja nami haleluyaaaaaaaaaaaaaaa anachokiunganisha Mungu binadamu hawezi kukitenganisha hata ieeje.."
Hongera sana lucy.
KATI YA UKIMWI NA AJALI BORA NINI?::AJALI YA LORI YAUA DEREVA SEKENKE, SINGIDA

Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
MMHH::UNAMPENDA YUPI...HAWA NDO MADEMU WAZURI KULIKO WOTE DUNIANI...








Fathima Kulsum Zohar Godabari who was once a royal Princess is now an official Queen in Saudi Arabia.
She was recently photographed without niqab covering her face and the
pictures were published on the internet, exposing her beautiful facial
features to the world for the first time.
TANZANIA BILA AJALI HAIWEZEKANI:::MWANAMKE AGONGWA NA LORI HADI KUFA..SAMAHANI KWA PICHA.
AJALI

Mwili wa mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake baada ya kukanyagwa na lori na kupoteza maisha.
Msamalia mwema akiufunika mwili wa mwanamke huyo.

Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la ajali.
MWANAMKE
mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepoteza maisha baada
ya kukanyagwa na lori lenye namba za usajili T277 CLY JANA katika maeneo
ya Mbezi Tanki Bovu, jijini Dar es Salaam.
MWAKA WA DIAMOND HUU:::ACHUKUA TUZO YA KOLABO HUKO AUSTRALIA.
Tuzo waliyopata Dezert Eagle na Diamond Platnumz.
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametwaa tuzo
nyingine ya Afro-Australia Music and Movie Awards (AAMMA) 2014 kutoka
Australia ya Collabo Bora ya Mwaka kupitia nyimbo aliyoshirikishwa na
Desert Eagle iitwayo Everyday. Kupitia akaunti yake ya Instagram,
Diamond aliyeko nchini Nairobi amewajulisha mashabiki wake kuhusu tuzo
hiyo kwa kuandika hivi:
Views: 54
Subscribe to:
Comments (Atom)






.jpg?width=650)
.jpg?width=650)
.jpg?width=650)
.jpg?width=650)
.jpg?width=650)







