UTETEZI WA WA MUUNDO WA SERIKALI MBILI KATIKA MUUNGANO
Watanzania wengi hasa vijana na hata ambao ni watu wazima hawajui na hawajapata nafasi ya
kujiuliza kwanini Muungano wetu una serikali mbili na siyo tatu na kwanini serikali hizo ziko jinsi
zilivyo. Kutokana na kutojua hili wengi hufanya haraka na kusema “tuwe na serikali tatu” bila
kujiuliza kama kufanya hivyo kutatua tatizo au la au kutaongeza tu tatizo. Nyerere anawajibu wale
wenye kuhoji haya kwa kuwapa historia kidogo ya mfumo wa Muungano. Kwa kutumia hoja za
kimantiki na kiufundi wa maneno kuonesha kuwa Muungano wa Tanzania ndio nchi pekee katika
Afrika iliyoundwa na Wananchi wenyewe. Tanzania siyo zao la mipaka ya ukoloni au matokeo ya
Mkutano wa Berlin wa 1884-1885 kama zilivyo nchi karibu zote za kiafrika. Nyerere anajenga hoja
kuwa Watanzania wasiwe dhaifu kukumbatia kilichoundwa na mkoloni kuwa ni chao halafu
walichounda wao wenyewe kukibeza na kujaribu kukivunja. Siyo hivyo tu, anashangaa kwanini watu
waone kilichoundwa na mkoloni bila kura ya maoni ya waliotawaliwa au kwa hiari ya wananchi kuwa
ni halali lakini kilichoundwa na wananchi wenyewe kwa makubaliano ya wananchi bila ya kura ya
maoni kuwa ni haramu? Hapa tunaweza kuona tofauti ya ujengaji hoja wa Mwalimu na wale wenye
kutaka kukubaliwa tu bila ya kuwa na hoja zenye nguvu. – M. M.
BUNGENI: 14/8/1993
Kesho yake tarehe 14/8/1993 tulikwenda bungeni.
(i) Nadhani jana yake Waziri Mkuu alikuwa amekwisha kutangaza uamuzi wa Zanzibar kutoka katika
OIC, na wakubali mapendekezo ya Kamati ya Bomani kuhusu utaratibu wa kuchagua Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano. Na kwa upande wa Zanzibar Rais wa Zanzibar alikuwa amekwisha kufanya
hivyo. Bungeni Waziri Mkuu alieleza sababu za kutuomba tuseme na wabunge.
(ii) Rais alieleza historia ya kisa cha OIC na uamuzi wa Zanzibar kujitoa. Akapinga hoja ya Serikali
tatu.
(iii) Mimi nilieleza kwa kirefu sana ile migogoro miwili ya awali. Pia kupinga hoja ya Serikali Tatu.
Katika kufanya hivyo nilieleza historia ya Muungano wa Serikali Mbili, badala ya serikali moja au
shirikisho la serilali tatu.
MFUMO WA SERIKALI MBILI: Kisanduku 1
Nchi mbili zinapoungana na kuwa Nchi moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili:
Muungano wa Serikali Moja, au Shirikisho la serikali Tatu. Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafuta
serikali yake na nchi mpya inayolizaliwa itakuwa ni nchi moja yenye Serikali moja. Katika mfumo wa
pili kila nchi itajivua madaraka ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho na itakuwa na serikali
ambayo ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki.
Mambo yatakayoshikwa na serikali ya Shirikisho ni yale ambayo yakibaki katika nchi zilizungana basi
kwa kweli nchi hizo zitakuwa hazikuungana kuwa nchi kuwa nchi moja bali zinaendelea kuwa nchi
mbili zenye ushirikiano mkubwa katika mambo fulani fulani.
Nchi za Afrika Mashariki zilikuwa katika hali kama hiyo kabla ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Zilikuwa ni Nchi Tatu zenye ushirikiano mkubwa, lakini hazikuwa Nchi Tatu zilizoungana
kuwa Nchi Moja yenye muundo wa Shirikisho. Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni Nchi Moja
yenye Serikali tatu, Serikali ya Shirikisho, na Serikali mbili za nchi mbili za awali zilizoungana kuzaa
nchi mpya moja.
Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa
mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zanzibar na
ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi
na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza
Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tutuhumiwe hata kwa makosa,
kwamba tunaanzisha ubeberu mpya!
Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama
kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha
Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa
Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali
yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la
watu 12,300,000.
Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo
ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tanganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na
wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya
Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tanganyika.
Kwa hivyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa
kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? Hivi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila kuwa na
SerikaIi yake, itaonekana kuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja
Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute mfumo ambao utaiondolea
Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili
zenye uzito unaolingana.
Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya muundo wa Muungano wa serikali mbili. Badala ya
kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazamia hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo
uliotufaa zaidi.
Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa ni kuunganisha nchi za Afrika
Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na
Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungumzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo,
lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni
Shirikisho; au la Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne au Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali
Tano.
Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki,
naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya
Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao
Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki
iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.
Siku ya pili yake tarehe 15/8/1993, Wabunge wenye hoja yao na wengine zaidi, waliomba tena kuja
'Tunywe chai'. Na baada ya mazungumzo nao ilikuwa ni dhahiri kabisa kwangu kwamba hata kama
hawakuondoa hoja yao (wala mimi sikuwaomba waiondoe), wataitumia kutoa dukuduku zao tu;
hawataitumia kung'ang'ania kudai Serikali ya Tanganyika. Kwa hiyo sikushangaa baadaye niliposikia
kuwa waliiondoa hoja yao ya awali, na badala yake wakaleta hoja ya kutafuta maoni ya wananchi.
Mimi kwa upande wangu nilihisi kuwa hoja mpya hii ilikuwa na shabaha ileile ya "kunawa uso",kama
Zanzibar kusema kuwa wanatoka katika OIC, 1akini utafanywa uchunguzi wa kuona kama Tanzania
inaweza kuingia katika OIC.
Huko nyuma baadhi ya viongozi wa Zanzibar wapinzani wa Muungano wamewahi kudai tufanye
referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano. Tukakataa kwa sababu safi kabisa. Maoni haya ya
Wabunge wa Bara ambao mimi naamini kabisa si wapinzani wa Muungano, nayo yangeweza
kukataliwa na Chama na Serikali kwa sababu zile zile na mambo yakesha.II
SURA YA TANO
SERIKALI ILIPOSALIMU AMRINyerere aliamua kuvunja mzizi wa fitina kwa kuchambua jambo moja muhimu sana ambalo hata
baadaye lingetusaidia kama tungeona umuhimu wake kuanzia wakati huo. Kwamba, uongozi mara
zote ni kuongoza siyo kufuata. Nyerere alisikitishwa sana na kitendo cha viongozi wetu kushindwa
kuonesha uongozi na badala yake kulazimika kufuata. Ulikuwa ni udhaifu ambao kama ungekubaliwa
basi ungesababisha kusambaratika kwa Tanzania kama tuijuavyo. Analolisema hapa lina ukweli hata
leo hii tunapoendelea kuhangaika na uongozi wetu kwani mara kadhaa tumeona jinsi ambavyo
viongozi wetu wanafuata matukio na hali badala ya kuonesha uongozi kukubali matatizo kabla
hatujafika mbali. Kile ambacho Nyerere anakiita “kusarenda” kimejirudia tena na tena katika taifa
letu tangu wakati wa kijitabu hiki kutolewa. Tumeona haya kwenye masuala ya EPA, Meremeta,
Richmond/Dowans n.k Nyerere anasema “kuongoza ni kuonesha njia”, hii ni kauli yenye ukweli
mkubwa sana kwani endapo mtu anayeitwa kiongozi anashindwa kuonesha njia basi kiongozi huyo
yampasa aachie ngazi ili waje watu wanaoweza kuonesha njia siyo kufuata. – M.M
Baadaye, nadhani siku iIiyofuatia niliitisha kikao cha Watangazaji wa Habari nikapinga kwa kirefu
hoja ya Utanganyika. Wakati naondoka Dar es Salaam ili kurudi Butiama nilitumaini kabisa kwamba
Serikali ingeendeleza Bungeni na kama hapana budi nchini kazi tuliyoanza pamoja ya kupinga hoja ya
Tanganyika. Sikuwa na sababu yoyote ya kuhofia kuwa siku chache tu baadaye Serikali itageuza
msimamo wake na kufanya "abautani".
Sijui lililotokea, maana kila nilipouliza sikupata maelezo. Kama nilivyokwisha kusema hapo nyuma
baadaye wabunge wahusika waliiondoa hoja yao ya awali ya kutaka Bunge lipitishe azimio la kudai
Serikali Tatu, wakaleta hoja mpya ya kutaka Serikali ifanye referendamu ya kutafuta maoni ya
wananchi kuhusu suala hili. Nasema, Serikali ingeweza kuikataa hoja hii kwa maelezo safi kabisa na
mambo yakesha.
Au kama wangeona kuwa si siasa nzuri kuipinga hoja hii nayo wangeweza kuikubali; na mimi nina
hakika wananchi wangeikataa na mambo yakesha. Lakini Serikali ya Muungano bila maelezo ilikataa
hoja mpya ya wabunge ya kutaka maoni ya wananchi na yenyewe ndiyo ikafufua hoja ya Utanganyika,
na kupendekeza kwamba badala ya hoja ya Serikali Tatu kujadiliwa Bungeni na kupigiwa kura Bunge
zima pamoja na Serikali yenyewe likubali hoja hiyo, bila mjadala!
Kumbe jambo ambalo viongozi wetu walikuwa wanahofu kabisa kabisa ni mjadala, maana huo
ungewalazimisha kujitambulisha kama si katika mjadala wenyewe basi wakati wa kupiga kura hasa
ikiwa ni kura ya kuita mbunge mmoja mmoja kwa jina pamoja na mawaziri wetu! Badala ya kupita
katika adha hiyo wakaona afadhali wakubali Serikali Tatu bila ya mjadala. Basi SerikaIi yetu ikanywea
ghafIa kama mpira uliotoboka au puto lililopasuka. Nadhani hata wabunge wenye hoja ya awali
walishangaa!
Kuongoza ni kuonesha njia. Viongozi wetu walikuwa wametumwa na chama chao waende bungeni,
Bunge la wanachama watupu wa CCM wakawaoneshe njia. Wakawaambie wabunge wahusika
kwamba hoja yao ya kutaka Serikali Tatu ni kinyume cha sera ya chama chao na ina hatari ya kuigawa
na kuiangamiza Nchi yetu.
Waliagizwa wazi wazi wakaipinge hoja hiyo. Wakapata mtihani mdogo sana bungeni.
Wakasarenda. Wakatupa silaha chini; wakasalimu amri. Viongozi hawa hawawezi kusimama mbele ya
Kamati Kuu au mbeIe ya Halmashauri Kuu ya Taifa kusema kwa fahari kama wao ni hodari: Kazi
mliyotutuma tumeikamilisha! Wala hawataki kukubali matokeo ya kusarenda kwao.
Kwa sababu uamuzi wa kutaka Serikali ya Tanganyika ‘ndani ya muungano’ ulifanywa na viongozi
wetu kwa hila na kupitishwa bungeni bila mjadala sisi wengine hatukujua lililotokea. Baadaye
tulifahamishwa kuwa huo ndiyo ulikuwa uamuzi wa ‘bunge zima” kutokana na kauli ya Pius Msekwa
aliyekuwa msimamizi wa kikao cha Bunge kilichofikia uamuzi huo. Nadhani viongozi wetu walitaka
kuendelea kuficha na kuuvuga vuga, lakini yeye akatoboa. Nasikia baadaye aliitwa akakemewa. Sijui
kwa nini.
KUTAFUTA UFAFANUZI WA KUSALIMU AMRI KWA SERIKALI
DODOMA II 14/10/1993
Nilipokwisha kuhakikishiwa kuwa sasa sera ya Serikali Tatu ndiyo sera rasmi ya Bunge la Muungano
na Serikali ya Muungano nilijaribu kupata maelezo kutoka kwa viongozi wetu lakini sikufanikiwa.
Waziri mkuu nilipomuuliza kama kweli wamebadili sera alicheka tu! Nilikuwa na safari ya
kutembelea nchi za Asia kwa ajili ya shughuli zinazotokana na uenyekiti wangu wa Tume Nchi za kusini.
Niliporudi kutoka safari nilijaribu tena kuonana na viongozi wetu ili nipate maelezo lakini sikufanikiwa
kumpata kiongozi yeyote mhusika. Nilipopata habari kwamba halmashauri Kuu ya Taifa itakutana
Dodoma nilihisi kuwa bila shaka viongozi wetu wataeleza kwa nini wameacha msimamo wa Chama na
maagizo ya Kamati Kuu ya kupinga hoja ya Utanganyika, wakaamua kukubali hoja hiyo. Basi
nikaomba angalau nipatiwe nafasi nihudhurie kikao hicho cha Halmashauri kuu ya Taifa ili nami
nisikie maelezo watakayotoa. Baada ya maajabu ambayo haina maana kuyaeleza nilikubaliwa nikaenda
Dodoma.
KIKAO CHA FARAGHA
Safari hii tulikuwa na vikao viwili. Kwanza kikao cha faragha wakiwapo viongozi wakuu wote wa
Chama na Serikali, na wengine wa nyongeza. Kilikuwa kikao kirefu na kigumu. Sina kawaida ya
kulizwa na mambo ya siasa lakini katika kikao hiki nilishindwa kujizuia kulia. Sikupata maelezo
ya maana ya kuwafanya watu wafanye walivyofanya. Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya
Serikali tatu kama tulivyokuwa tumekubaliana majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ya ajabu
kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa
wakali kama mbogo! Tena walikuwa wakiwatukana wenzao (yaani wabunge wa Zanzibar) kwa
kuwataja majina.
Hizi ni sababu za ajabu sana za kuwafanya viongozi watu wazima watelekeze msimamo mzima wa
Chama chao na makubaliano ya watu makini kuutetea msimamo huo na waamue kuikumbatia hoja ya
mbogo wakali! Huu ni uongozi wa ajabu kabisa!
Nilipowabana zaidi niliahidiwa kuwa maelezo mazuri yatatolewa kesho yake na waziri wa Sheria na
mambo ya katiba katika kikao cha Halmashauri Kuu ya taifa.
KIKAO CHA HALMASHAURI KUU:
Hakika siku ya pili yake waligawiwa ‘TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE
KUHUSU HAJA YA KUUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA
MUUNGANO’.
Taarifa yenyewe ni ndefu ina maelezo mengine ya mapambo tu, au ya kiini macho.
Lakini vipengele vinavyohusika na suala lenyewe vilikuwa vichache na nimevinukuu kwa ukamilifu
(tazama kisanduku 2)
“9: Tarehe 30 Julai, 1993 wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ukiendelea, zaidi ya wabunge 50 kwa
pamoja walitoa taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja Bungeni ambayo inadai miongoni mwa mambo
mengine;
Kwa kuwa kuendelea mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja ni
kuhatarisha kuendelea na kudumu kwa Muungano na pia kuathiri uelewano kati ya watu pande zote
mbili; na
Kwa kuwa uwezekano wa kuunda serikali moja ya Jamhuri ya Muungano kwa nchi nzima kwa mambo
yote haujajionesha;
Hivyo basi wabunge hawa wanaliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano katika mkutano wake wa kumi
na mbili unaofanyika Dar Es salaam liazimie kwamba;
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilete Muswada Bungeni kabla ya Februari 1994, kurekebisha katiba
ya Jamhuri ya Muungano ili kuwezesha uundaji wa “Serikali ya Tanganyika” ndani ya Muungano.
Tarehe 12 Agosti, 1993 hotuba ya kuwasilisha Makadirio ya Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba
ilisomwa Bungeni. Katika hotuba hiyo Serikali ilieleza kusudio la kuandaa waraka wa Serikali (White
Paper) kutafuta maoni ya wananchi kuhusu muundo wa Muungano. Tarehe 20 Agosti, 1993 wabunge
wahusika waliwasilisha taarifa nyingine inayobadilisha ile hoja ya awali iliyosambazwa kwa wabunge
wote. Hoja mpya ilikuwa inalitaka Bunge zima liazimie kwamba:
Serikali ya Jamhuri ya Muungano iandae kura ya maoni ambayo itafanyika kabla ya 31 Desemba,
1994 ili kupata maoni ya wananchi wa Tanzania juu ya kuundwa kwa “Serikali ya Tanganyika” ndani
ya Muundo wa Muungano utakaozingatia mabadiliko hayo. Kutokana na taarifa hizi, Baraza la
Mawaziri lilifanya kikao cha dharura ili kutafakari taarifa hizi na athari zake kama zingewasilishwa
Bungeni na kupigiwa kura.
Kwanza kabisa, inaonekana kwamba hoja ya awali ingekuwa vigumu kutekelezeka kutokana na muda
mfupi uliowekwa kufikia Februari 1994, na pia haikutoa fursa kupata maelekezo ya Chama wala
serikali zetu mbili kushauriana. Kwa kutambua kwamba Bunge linafanya maamuzi yake kwa njia ya
kura baada ya mijadala ya wazi, Serikali iliona kwamba hoja yote kati ya hizi ingewasilishwa
Bungeni, ingeweza kuligawa Bunge, kukigawa chama chetu na kuwagawa wananchi katika suala zito
kama hili la Muundo wa muungano.
Kuhusu suala la kura ya maoni serikali iliona kwamba utekelezaji wake ni sawa na kufanya uchaguzi
mkuu, jambo ambalo ni la gharama kubwa. Aidha, kwa kuzingatia kwamba kura ya maoni kupigiwa
suala linalohitaji jibu la ‘NDIYO’ au ‘HAPANA’ , ni vigumu kupata swali lililo wazi kwa wananchi
ambao hawana uzoefu wa utaratibu huo wa kura ya maoni.
Pamoja na hayo, kwa kuzingatia kwamba uamuzi wa kura ya maoni ni lazima ukubalike katika sehemu
zote mbili za Muungano, itakuwa vigumu kupata uwiano wa kura utakaokubalika pande zote mbili
kuwa ndio kiwango cha uamuzi.
10. Pamoja na juhudi za Serikali zote mbili kupitia Kamati ya Pamoja, Serikali zetu pia zilifikia
makubaliano na kufanya maamuzi kuhusu baadhi ya matatizo mazito yaliyokuwapo katika Muungano
wetu. Maamuzi hayo ni:
(a) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukubali Zanzibar kujitoa katika uanachama wa 'OIC';
(b) Utaratibu wa kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano uwe ni kwa njia ya kupigiwa
kura kwa pamoja na mgombea urais (running mate).
11. Kwa msingi huu na kwa kuzingatia maamuzi ya awali ya Serikali ya kutaka kupata maelekezo ya
chama na maoni ya wananchi kuhusu muundo utakaotatua matatizo ya Muungano, Serikali iliona kuna
umuhimu wa kushauriana na wabunge waliohusika ili kupata muafaka wa maudhui ya hoja yenyewe.
Muafaka huo ulifikiwa katika Kikao cha Kamati ya Wabunge wakikaa kama Kamati ya Chama tarehe
12/8/93. Kutokana na muafaka huo hoja ya wabunge ilirekebishwa na azimio la Bunge kupitishwa kwa
kauli moja kwamba:
"Serikali iandae na kusimamia utaratibu utakaoshirikisha wananchi na taasisi mbali mbali ili
kufikisha Bungeni kabla ya Aprili, 1995, mapendekezo ya muundo muafaka wa Muungano ambao
utazingatia haja ya kuwapo Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano pamoja na mambo mengine.
12. Azimio hili linaagiza mambo mawili yaliyo wazi:
(a) kupatikana kwa muundo muafaka wa Muungano ambao unazingatia haja ya kuwapo Serikali ya
Tanganyika.
(b) Kuwapo na utaratibu wa kushirikisha wananchi na taasisi mbalimbali utakaosimamiwa na Serikali
kabla ya mapendekezo ya mwisho kufikishwa Bungeni.
13. Kwa kuwa suala la muundo wa nchi ni zito na ni la kikatiba, ushirikishwaji wa wananchi ni jambo
lisiloweza kuepukwa. Aidha kwa uzoefu wetu na hali halisi ya nchi yetu, ni lazima utaratibu wo wote
utakaokubalika, uwezeshe Serikali yaJamhuri ya Muungano kushauriana na Chama na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Hatua za Serikali baada ya azimio na mapendekezo
14. Kutokana na Azimio la Bunge, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeona kwamba suala la muundo
wa Muungano sasa linahitaji kufanyiwa kazi na kupatiwa uamuzi haraka zaidi na hivyo ni muhimu
kuwasilishwa kwenye Chama mapema kwa maelekezo, bila kusubiri mapendekezo ya Kamati ya
pamoja i1i kuondoa hisia kwamba Serikali inajaribu kulikwepa suala hili.
15. Katika hali hii, Serikali inapendekeza kwamba Halmashauri Kuu ya Chama iafiki pendekezo la
Serikali la kuandaa Waraka wa Serikali wa kutafuta maoni ya wananchi (White Paper) kuhusu
muundo muafaka wa Muungano kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
(a) Dhana ya kuwa na Serikali tatu ndani ya Muungano, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika ikubalike. Muungano wa aina hii kwa Sheria za Katiba
na za Kimataifa ni wa Shirikisho (Federation).
(b) Kwamba muundo uwe ni Muungano wenye Serikali tatu, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya
Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. lkumbukwe kwamba neno Muungano linavyofahamika
kwenye Sheria za Katiba na za Kimataifa linamaanisha kwamba majukumu yale ya msingi ya dola
yanahamishiwa kwenye Serikali ya Muungano."
Haya ni maelezo ya ajabu sana kutoka kwa watu wazima kwenda kwa watu wazima wengine.
"Kwanza kabisa", Serikali yetu inaiambia Halmashauri Kuu ya Taifa, "inaonekana kuwa hoja ya awali
ingekuwa vigumu kuitekeleza kutokana na muda uliowekwa kufikia Februari, 1994, na pia haikutoa
fursa ya kupata maelekezo ya Chama wala Serikali zetu mbili kushauriana.
Aidha, "Kwa kutambua kwamba Bunge linafanya maamuzi yake kwa njia ya kura baada ya mijadala ya
wazi wazi, Serikali iliona kwamba hoja yo yote kati ya hizi ingewasilishwa bungeni ingeweza kuligawa
Bunge, kukigawa chama chetu na kuwagawa wananchi katika suala zito kama hili la Muundo wa
Muungano."
Kwanza, hii "hoja ya awali" ambayo waheshimiwa hawa wanasema hawakuwa na muda wa kutosha
kuitekeleza ni ile ya kutaka Serikali Tatu ambayo kwanza, ni kinyume na sera ya Chama; pili,
walikuwa wameagizwa na Kamati Kuu ya CCM siku chache zilizopita wakaipinge Bungeni; Tatu,
tarehe 12 Agosti, 1993, Serikali yenyewe ilikuwa imeliambia Bunge kwamba ilikuwa inaandaa waraka
wa kutafuta maoni ya wananchi kuhusu suala hili; na nne, (na pengine kutokana na kauli hii ya
Serikali) tarehe 20 Agosti, 1993, wabunge wahusika walikuwa wamekwisha kuondoa hoja yao ya awali
nao wakaleta hoja mpya: ya kuitaka Serikali ifanye referendamu ya kutafuta maoni ya wananchi.
Labda waheshimiwa wabunge nao waliona kuwa hoja hii ya kudai Serikali tatu "ikiwasilishwa
Bungeni, ingeweza kuligawa Bunge, kukigawa Chama chetu; na kuwagawa wananchi katika suala zito
kama hili la Muundo wa Muungano." Mimi siamini hivyo; naamini kuwa kama ingewasilishwa
bungeni ili ijadiliwe, ingejadiliwa ikakataliwa na mambo yangeisha Maamuzi yoyote ya
kidemokrasia hayana budi yatokane na mjadala. Bila ya mjadala, maamuzi, hata yaliyo muhimu
kabisa yatafanywa kwa nguvu ya hila. Lakini kwa vyo vyote vile, hoja hii Wabunge wahusika
walikwisha kuiondoa.
Kama viongozi wetu waliamini kuwa kujadiliwa kwake kutaleta mgawanyiko huo waliouhofu, kwa
nini basi wakati CCM ilipotaka kubadili sera yake haikutafuta kwanza maoni ya wananchi?
Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni
ya wananchi. Na walikuwa na haki kufanya hivyo, maana sera ni yao. Ubaya wao ni kwamba jambo
lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi
kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea.
Ndivyo viongozi wetu waheshimiwa wanavyojaribu kufanya hata katika suala hili la Muungano.
Wanataka kuvunja Tanzania maana "wamechoka na Wazanzibari"; lakini hawataki kusema hivyo wazi
wazi. Wanachosema ni kwamba wanataka Serikali ya Tanganyika "ndani ya Muungano", ingawa
wanafahamu, maana si watu wapumbavu, kwamba ukifufua Tanganyika utaua Tanzania.
Saturday, 16 August 2014
MAMBO YA BABY J' HAYO....ALIMANUSURA ABAKWE...kisa
Baby Madaha Anusurika Kubakwa Baada ya Kupanda Jukwaani Akiwa na Kivazi Cha Nusu Uchi
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.
“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.
JE,TANZANIA ITAPATA KATIBA MPYA 2014?
Tanzania na katiba kulikoni?
14.08.2014 13:35
Umoja wa katiba ya wananchi – UKAWA umegoma kuingia na kushiriki katika bunge la katiba hadi pale watakapofikia maridhiano ya nini cha kujadiliwa ndani ya bunge hilo.
Viongozi wa ukawa wamefanya mkutano na waandishi wa habari jumanne na kutishia kuitisha maandamano ya nchi nzima kama rais Jakaya Kikwete asipoingilia na kusitisha vikao hivyo.
serikali ya Tanzania Alhamisi imesema rais hana mamlaka ya kuingilia mchakato wa katiba kwa sasa. Lakini baadhi ya wapinzani waliogoma kuingia kwenye bunge hilo wameanza kugawanyika baada ya mbunge wa maswa magharibi John Shibuda , na Saidi Arfi mbunge wa mpanda kushiriki kwenye vikao hivyo wakidai kuwa wanatetea wananchi wao.
Wachambuzi wanaona hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, huenda katiba hiyo haitatumika kama malumbano hayatamalizika haraka iwezekanavyo.
HAMSIN ZA SHILOLE NA MZIWANDA ZAWA MIA TENA....100/=
Shilole Afunguka Sababu za Kurudiana na Mziwanda Baada ya Kuachana kwa Siku Moja
Udaku Specially on Saturday, August 16, 2014
Shilole alisema mpenzi wake huyo
aligundua kwamba aliteswa na wivu na kusababisha wagombane hivyo
alipotambua kosa lake, aliomba msamaha wakarudiana na mambo yakawa
swari.
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema Shilole.Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake.
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema Shilole.Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake.
HATARI HATARI.....ONA MAJERUHI WALIOLIPUKIWA NA JIKO LA KUYEYUSHIA VYUMA KIWANDANI
HAWA NDIYO MOJA WA MAJERUHI WA KIWANDA CHA SAYONA JIJINI MWANZA WAKIHANGAIKA NA VIDONDA
BAADA YA KULIPUKIWA NA JIKO LA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA HICHO.

Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO

Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona Lucas Nkalango akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO


Kwa upande wa nyuma anavyoonekana Lubinza akiwa ameungua vibaya
Posted by
tamra tanzania
BAADA YA KULIPUKIWA NA JIKO LA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA HICHO.
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona Lucas Nkalango akiwa ameumia vibaya baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Majeruhi wa Kiwanda cha Sayona LUCAS LUBINZA akiwa ameumia vibaya sehemu ya nyuma baada ya kulipukiwa na jiko la kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha Sayona kilichopo Nyang'homango Jijini Mwanza Picha na ANTONY SOLLO
Kwa upande wa nyuma anavyoonekana Lubinza akiwa ameungua vibaya
HUYU NDO Irene UWOYA MWENYEWE...Hataki KUVAA............
Irene Uwoya Chizi , Asema Apendi Vazi Linaloitwa Chupi aka Kufuli
Alipoulizwa na mwandishi wa jarida hilo kuwa ni nguo gani ni vigumu kuikuta kwenye kabati lake, “Chupi – sipendi kabisa hilo vazi” Alisema Irene uwoya. Hatari sana hii....
SERIKALI YAWAAMURU ukawa KURUDI BUNGENI WAKARIDHIANE
Wajumbe wa Bunge la Katiba waaswa kurejea Bungeni :
August 16, 2014
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi
wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema
akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba
wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi
wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa
kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Jaji
Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi
kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo
kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza
bunge hilo.
“Sheria
inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba
kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na
kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji
Werema.
Pia
Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi
kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza
kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha,
Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili
muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji
wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza
kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
Mwisho.
TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI - 2014/2015
TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI - 2014/2015
Katika mwaka wa fedha
2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya
Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza
kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya
Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo:
Inspekta Jenerali wa
Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM
WAOMBAJI WAWE NA
TAALUMA ZIFUATAZO:
Shahada: Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala
katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa
Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa
Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio
Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya
Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt],
Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in Fine
Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical Doctor] na
Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].
Stashahada: Utunzaji Kumbukumbu, Katibu
Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta,
Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari,
Ugavi[Procurement & Supplies], TV na Video Production, Manahodha,
Tabibu[Clinical Officer], Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza
Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu
Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].
Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi
Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse].
MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake “Ppt Size” kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania.
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania.
Fomu:- Fomu ya Ajira Elimu ya Juu 2013/2014 zinapatikana kwenye tovuti www.policeforce.go.tz au kwa wakazi wa Mbeya wafike ofisi ya
kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI
WA MBEYA.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,
BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya
majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014
na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye
tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya
kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.
Muhimu:
·
Mwombaji anaruhusiwa
kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana
na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe
amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi
halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili
hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
·
Mwombaji aliyeitwa
kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic
Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya
cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa
haitakubalika.
·
Mwombaji awe na
namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
·
Kila mwombaji
aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote
wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa
kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia
muda wa kuanza usaili.
TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI 01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.
TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI 01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.
HII NDO STUDIO YA BBC JIJIN DAR...Linganisha na YAKO
Taswira za Studio za BBC jijini Dar.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar.
Wadau Salim Kikeke na Nicolas wakipitia habari kabla ya kuipeleka hewani.
CAPT. SHITAMBALA APANDISHWA KIZIMBANI
CAPT. SHITAMBALA APANDISHWA KIZIMBANI
![]() |
Wakili Capt. Sambwee Shitambala(kushoto) akijadiliana na wakili anayemtetea Luambano nje ya mahakama leo asubuhi. |
Wakili na
mwanasiasa machachari Mkoani Mbeya, Capt. Sambwee Shitambala,
amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Mbeya
leo, baada ya mfanyabiashara raia wa Kiasia Jaswinder
Palsingh mkazi wa Jijini Mbeya kumtuhumu.
Wakili wa serikali Ahmed Stambuli, mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, alisema kuwa mshitakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuingia kwa
jinai kinyume cha sheria namba 79 ya mwaka 2014 kinyume cha kanuni namba
16 za
sheria ya adhabu. Alisema
Shitambala anadaiwa kumfanyia maudhi Singasinga huyo kwa kuingia kwa
jinai na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 Kitalu BB vilivyopo eneo
la Gombe Uyole jijini Mbeya ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali halali ya
Kalasinga huyo.
Shitambala
ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM(mnec) kupitia wilaya ya Mbeya mjini, amedaiwa kufanya
kosa hilo kati ya Juni, 18 2012 na Novemba 28,2013.
Mara baada
ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa ambaye alikuwa akitetewa na wakili wa
kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo hakimu Ndeuruo alisema
kuwa dhamana ya mshitakiwa iko wazi na anaweza kuwa nje kwa dhamana iwapo atatimiza masharti ya kuwa
na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha sh. milioni 1.
Mshitakiwa
ambaye hakuwa na mdhamini aliruhusiwa kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya fedha
sh. milioni 1.
Hakimu
Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa
rasmi.
Akizungumza
nje ya mahakama wakili anayemtetea Shitambala, Luambano alisema kuwa mteja anawakilisha
wakazi wengine 400 ambao wamejenga pamoja naye katika eneo hilo na kuwa hata
hivyo ameshitakiwa yeye peke yake.
Aidha
washitakiwa wengine wanne ambao walikamatwa pamoja na Shitambala na kufika
mahakamani hapo hawakuhusishwa na kesi hiyo na kutakiwa kukaa pembeni kwa kuwa
kesi hiyo haikuwahusu wao.
Waliokuwa pamoja na
Shitambala mahakamani hapo ambao waliwekwa pembeni kwa madai kesi hiyo
haiwahusu ingawa walikamatwa na polisi na kufikishwa kituo cha polisi
cha Kati Jijini Mbeya, hapo ni pamoja na Jane Kamage, Hilda
Ngowi,Clavery Mayangu na Said Mpunga.
Friday, 15 August 2014
CHADEMA IRINGA YAMCHOKA MSIGWA ,KAMATI YA UCHAGUZI YAFYEKA JINA LAKE KUWANIA UENYEKITI
August 15, 2014
> mbunge mchungaji
Msigwa kushoto akiwa na mbunge Chiku Abwao katika moja kati ya vikao
vya baraza la madiwani Manispaa ya Iringa
CHADEMA IRINGA YAMCHOKA MSIGWA ,KAMATI YA UCHAGUZI YAFYEKA JINA LAKE KUWANIA UENYEKITI .........
![]() |
mh Msigwa |
Mbunge Msigwa kulia akiwa na mbunge Chiku |
KAMATI
ya uchaguzi wa mkuu wa wilaya ya Iringa mjini kupitia chama cha
Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemuengua katika kinyang'anyiro cha
uenyekiti wa wilaya hiyo mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji
Peter Msigwa ambae ndie alikuwa wenyekiti anayemaliza muda wake kwa
kukosa sifa ya kutetea tena nafasi hiyo.
Hatua
hiyo ya kuenguliwa kwa Msigwa imekuja baada ya wajumbe kulalamikia
hatua ya chama kushindwa kulipa kodi ya ofisi ya kata na ile ya wilaya
pia ugomvi mkubwa uliopo kati ya mbunge Msigwa na mbunge mwenzake wa
viti maalum mkoa Chiku Abwao aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti mkoa wa
Iringa nafasi ambayo msigwa pia alitangaza kugombea .
Hivyo
kutokana na mvutano huo kamati hiyo iliyoketi usiku wa leo ukumbi
wa Sambala mjini hapa ililazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kufyeka
majina ya wabunge hao kugombea nafasi hizo ili kunusuru chama.
Mmoja
kati ya makada wa ambae alishiriki kikao hicho cha kumuengua Msigwa na
Chiku alisema kuwa chanzo cha msigwa kuenguliwa ni kutokana na
kuendekeza kukuza makundi ndani ya chama na kuwa mbali na chama zaidi ya
kufanya chama kuendelea kukosa heshima.
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Pamoja
na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa
wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote
ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
Hivikaribuni
Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa
chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.
Kuenguliwa
kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili
wanaomenyana katika nafasi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo
yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea ubunge jimbo la
Iringa Mjini mwaka 2015.
Wagombea
hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa
Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la
wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
Kundi
linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa
mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka
katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.
Mchungaji
Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi,
mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka
ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku
akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru
jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Wakati
Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika
zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa
kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa
kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo
la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
Wanachama
wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza
ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh
540,000 walizokuwa wakidaiwa.
Kwa
upande wake mbunge Msigwa alinukuliwa na mwandishi wa habari hizi
akimrushia maneno mmoja kati ya viongozi wa chama hicho kuwa watu
wanamchafua kwa suala la ofisi na kuwa ni ruksa kwa wanachama ambao
wanapenda vyama vyenye ofisi kuhama chadema na kujiunga na vyama
hivyo .
Huku
mbunge Chiku Abwao amethibitisha kuenguliwa kwao katika nafasi hizo
japo amedai kwa upande wake kaonewa na ataendelea kutumia vikao
kuomba kurejeshwa kwa jina lake.
JE,ALI KIBA NI BORA KULIKO DIAMOND PLATNUMZZ?BABU TALE
Babu Tale Azungumzia Inayoitwa beef ya Diamond na Ali Kiba, Aifananisha na ya Davido na Wizkid
Akizungumza kupitia kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Babu Tale amejibu swali la msikilizaji aliyetaka kufahamu mtazamo wake kuhusu uwepo wa beef kati ya wasanii hao wawili.
“Mimi sidhani kama Diamond na Ali Kiba wana beef, ni biashara…challenging. Sijawahi kuona wanagombana katika maisha yangu. Watu wanaoandika nyuma wanaandika kwa sababu wanaamua kuandika lakini mwisho wa siku Diamond na Ali Kiba wote ni wanamuziki. Without challenge Diamond hawezi kuendelea au Ali Kiba hawezi kuendelea.” Amesema Babu Tale.
Ameeleza kuwa hiyo kwake anaona challenge hiyo ni nzuri kibiashara na sio tatizo na kwamba likionekana ni tatizo watalitatua.
“Kama unamfollow Davido na Wizkid. Kila anapopost Wizkid kwamba hapa nafanya show hivi, Davido nae anamjibu kuwa angalia watu wamejaa huku hivi. Ni biashara. Ugomvi wanagombania nini? Ali Kiba anakula kwaKe ana maisha yake, Diamond anakula kwake na ana maisha yake.” Ameongeza Babu Tale.
Alipoulizwa kuhusu ujio wa Ali Kiba kuchukuliwa kama ndio sehemu ya mapinduzi dhidi ya utawala wa Diamond, Babu Tale aliipinga kauli hiyo.
“Huwezi kusema Ali Kiba anakuja, Ali Kiba yupo na alikuwepo. Huwezi kumuambia anakuja unamdhalilisha, Ali Kiba yupo alikuwepo na ana uwezo wake. Anafahamu base yake. Huwezi kumwambia anakuja, anakuja ni msanii mpya…Raymond wa Tip Top anakuja sio Ali Kiba. Usiwe na mind kuwa Ali Kiba hayupo kwenye Game, yupo.”
Ameongeza kuwa hajafirikia kuhusu suala la Ali Kiba kumpindua Diamond.
KISA HIV:WAPIGWA STOP KUKWEA PIPA
Wakatazwa Kuingia Kwenye Ndege, Kisa HIV
Abiria wawili wa china waliokuwa
wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la China (China Airline),
wameamua kulipeleka shirika hilo mahakamani kwa kile walichokieleza
kuwazuia kusafiri na shirika hilo eti tu kwasababu walikua wanaishi na
virusi vya ukimwi HIV.
Hata hivyo inaelezwa kwamba abiria hao si mara ya kwanza kusafiri na China Airline kutoka kaskazini mwa mji wa Shenyang katika kipindi cha machipuko ,wakati huu sasa shirika hilo la ndege lilipoamua kughairisha safari za abiria hao.
Masharti ambayo abiria hao wameyatoa Kufuatia kughairishwa kwa safari hiyo,shirika hilo la ndege litalazimika kuomba radhi na kulipa fidia ya dola za kimarekani elfu nane .Mahakama katika mji wa Shenyang imeipokea na kukubali kesi hiyo ya kwanza na ya kipekee nchini China.
Viongozi wa serikali kutoka China wamesema kua wamejitahidi kujaribu kupunguza historia ya muda mrefu ya unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya HIV na ukimwi.
Hata hivyo inaelezwa kwamba abiria hao si mara ya kwanza kusafiri na China Airline kutoka kaskazini mwa mji wa Shenyang katika kipindi cha machipuko ,wakati huu sasa shirika hilo la ndege lilipoamua kughairisha safari za abiria hao.
Masharti ambayo abiria hao wameyatoa Kufuatia kughairishwa kwa safari hiyo,shirika hilo la ndege litalazimika kuomba radhi na kulipa fidia ya dola za kimarekani elfu nane .Mahakama katika mji wa Shenyang imeipokea na kukubali kesi hiyo ya kwanza na ya kipekee nchini China.
Viongozi wa serikali kutoka China wamesema kua wamejitahidi kujaribu kupunguza historia ya muda mrefu ya unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya HIV na ukimwi.
UMEPANIC DIAMOND PLATINUMZZZZ!!!!!!!!!!!
Diamond Amepanic Kuwajibu Mashabiki wa Wema, Majibu Yake Yanaweza Tia Doa Mapenzi Yao
Leo Diamond Aliamua Kuwajibu Mashabiki wa Wema Sepetu walio mshutumu anamtumia Wema Kwa Faida yake
Bahati mbaya, majibu ya Diamond kupitia Instagram yamekuwa makali kiasi cha kuwashtua wengi na kuona kama kamkosea heshima mpenzi wake. Kwakuwa sitaki kuonekana kama namhukumu Diamond kwa kile alichoandika, ningependa kuongea kwa lugha ya busara kadri iwezekanavyo, na isitoshe nimegusia suala la ‘udhaifu’ na ‘ubinadamu’ katika aya zangu za mwanzo.
Diamond ametumia kauli nzito na ya hasira kidogo katika kuwajibu vinara wa kampeni hiyo. Si jambo la busara kumuita mtu umpendaye kwa kuandika ‘msanii wenu’ baada ya jina lake, pale alipoanza kwa kuandika: Nafikiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa ‘Msanii wenu’. Ingekuwa vyema kama angeandika; Nafikiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa ‘Wema Sepetu’. Again, hizo ni hasira tu na ndio maana aliamua kuifuta post hiyo.
Kwa maelezo aliyoyatoa staa huyo, imebainika wazi kuwa ni Wema ndiye aliyeamua kuishi hivyo na pengine ameridhika na hatua aliyofikia. Inavyoonekana Diamond hapendwezi na muenendo na maisha ya mpenzi wake hasa kwa kudai anaendekeza urafiki na watu wanaopenda anasa na kula bata.
“Mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, wenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe,” yanaendelea kusomeka majibu ya Diamond. Maelezo hayo yanaeleweka wazi kuwa Wema amekuwa ni mtu wa starehe na kula raha na marafiki zake (Aunty Ezekiel haikwepi hii sentensi, inamhusu). Kwa kauli ya Diamond, Wema anaonekana kuendekeza ulevi kwa kutumia fedha anayopewa na mchumba wake.
“Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumwezesha mtaji wa kufanyia kazi.”
Sentesi hiyo inamaanisha kuwa, Diamond anatimiza wajibu wake na tayari amempa mtaji mpenzi wake. Kuna taarifa pia kuwa hata filamu yake ya Family aliyoigiza na Aunty Ezekiel ilidhaminiwa na Diamond.
“Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi, ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji,” anaendelea Diamond. “Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie mie? Ni juhudi zako kwanza.”
Maneno ya Diamond yanajielezea yenyewe kuwa Wema amejisahau. Maswali ya wengi ni kuwa wao kama wapenzi hawajawahi kuzungumza haya na kushauriana? Diamond hajawahi kumkanya mpenzi wake kuwa mwenendo wake sio? Au ameshamuambia hadi amechoka na ndio maana ameamua kuuambia umma kile kinachoendelea?
Kwa lawama na matusi ambayo Diamond ameyapata kutokana na kampeni hiyo, ilikuwa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu kukaa kimya. Nahisi uvumilivu ulimshinda na ndio maana aliamua kuandika alichokiandika ambacho bahati mbaya kinaweza kutia tena doa uhusiano wao. Sijui Wema atasemaje!!
Bahati mbaya, majibu ya Diamond kupitia Instagram yamekuwa makali kiasi cha kuwashtua wengi na kuona kama kamkosea heshima mpenzi wake. Kwakuwa sitaki kuonekana kama namhukumu Diamond kwa kile alichoandika, ningependa kuongea kwa lugha ya busara kadri iwezekanavyo, na isitoshe nimegusia suala la ‘udhaifu’ na ‘ubinadamu’ katika aya zangu za mwanzo.
Diamond ametumia kauli nzito na ya hasira kidogo katika kuwajibu vinara wa kampeni hiyo. Si jambo la busara kumuita mtu umpendaye kwa kuandika ‘msanii wenu’ baada ya jina lake, pale alipoanza kwa kuandika: Nafikiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa ‘Msanii wenu’. Ingekuwa vyema kama angeandika; Nafikiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa ‘Wema Sepetu’. Again, hizo ni hasira tu na ndio maana aliamua kuifuta post hiyo.
Kwa maelezo aliyoyatoa staa huyo, imebainika wazi kuwa ni Wema ndiye aliyeamua kuishi hivyo na pengine ameridhika na hatua aliyofikia. Inavyoonekana Diamond hapendwezi na muenendo na maisha ya mpenzi wake hasa kwa kudai anaendekeza urafiki na watu wanaopenda anasa na kula bata.
“Mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, wenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe,” yanaendelea kusomeka majibu ya Diamond. Maelezo hayo yanaeleweka wazi kuwa Wema amekuwa ni mtu wa starehe na kula raha na marafiki zake (Aunty Ezekiel haikwepi hii sentensi, inamhusu). Kwa kauli ya Diamond, Wema anaonekana kuendekeza ulevi kwa kutumia fedha anayopewa na mchumba wake.
“Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumwezesha mtaji wa kufanyia kazi.”
Sentesi hiyo inamaanisha kuwa, Diamond anatimiza wajibu wake na tayari amempa mtaji mpenzi wake. Kuna taarifa pia kuwa hata filamu yake ya Family aliyoigiza na Aunty Ezekiel ilidhaminiwa na Diamond.
“Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi, ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji,” anaendelea Diamond. “Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie mie? Ni juhudi zako kwanza.”
Maneno ya Diamond yanajielezea yenyewe kuwa Wema amejisahau. Maswali ya wengi ni kuwa wao kama wapenzi hawajawahi kuzungumza haya na kushauriana? Diamond hajawahi kumkanya mpenzi wake kuwa mwenendo wake sio? Au ameshamuambia hadi amechoka na ndio maana ameamua kuuambia umma kile kinachoendelea?
Kwa lawama na matusi ambayo Diamond ameyapata kutokana na kampeni hiyo, ilikuwa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu kukaa kimya. Nahisi uvumilivu ulimshinda na ndio maana aliamua kuandika alichokiandika ambacho bahati mbaya kinaweza kutia tena doa uhusiano wao. Sijui Wema atasemaje!!
Subscribe to:
Posts (Atom)