Stori: mwandishi wetu, songea
MY God! Hali huenda ikigeuka, wakati jamii inaamini akina baba ndiyo
wenye tabia ya kutokuwa na uchungu kwa watoto, imekuwa tofauti kwa mama
huyu!Ni mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwanamonga, Kata ya Lilambo, Manispaa
ya Songea, Kasiana Komba (60) anadaiwa kuuawa na mumewe, Allan Menas
Lwambano (76) kisa kikidaiwa mambo ya kumtoa kafara mtoto.
Bwana Allan Menas Lwambano anayedaiwa kumuua mkewe.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri usiku wa Agosti 25, mwaka huu
ambapo maelezo ya mume huyo yanasema ni baada ya marehemu kumtaka
akubali kumuua mtoto wao mmoja (jina tunalo) kati ya saba ili walipe
madeni kwa imani ya kishirikina na kufanikiwa katika kipato (utajiri).
RPC wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msekela.
ILIVYOKUWA Ilielezwa kuwa, mwanaume huyo
alikataa ombi hilo na mkewe akamwekea mgomo wa kumnyima unyumba hadi
pale atakapokubali ombi lake hilo.
MAISHA YA NDOA Ilidaiwa kuwa, maisha ya wawili
hao yakawa ya ‘sitaki nataka’, mume akitaka unyumba mke hataki kwa vile
amemkatalia kumtoa mtoto wao kafara wakati yeye mke alishawaambia
wenzake (kwenye ushirikina) kuwa, ameamua kumtoa mtoto huyo lakini baba
yake hakutaka kufanya hivyo.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya
tukio usiku, Lwambano alirudi nyumbani na kumkuta mkewe amelala,
alianza kumshikashika mwilini kuashiria alimhitaji faragha, ndipo mke
huyo alipotoka nje na kuchukuwa mchi wa kutwangia mahindi kwa lengo la
kumpiga mumewe.
Kasiana Komba aliyedaiwa kumtoa kafara mtoto wake ili apate utajili.
“Mumewe aliuzuia, akamnyang’anya na kumpiga mkewe kichwani, alianguka palepale na kufariki dunia,” kilisema chanzo.
MUME AHANGAIKA KUUZIKA MWILI Habari za ndani
zinasema kuwa, mume alipobaini ameua aliuchukuwa mwili wa mkewe na
kuupeleka nyuma ya nyumba ambako kuna choo na kuuzika huku akipanda
migomba juu ili kuzubaisha watu.
WATOTO: “BABA, MAMA YUKO WAPI?” Agosti 26, mwaka
huu, siku moja tu baada ya tukio hilo la kutisha, watoto ambao wanaishi
mbali na nyumba hiyo walifika na walipoona hawamuoni mama yao,
walimwuliza baba yao: “Baba, mama yuko wapi?” akawajibu: “Mama yenu
ameenda mjini Songea, atarudi.”
WATOTO WAENDA KWA MGANGA
Ikazidi kudaiwa kuwa, Agosti 27, mwaka huu, watoto hao hawakukubaliana
na majibu ya baba yao, wakaenda kwa mganga wa kienyeji (jina
halikupatikana mara moja) kwa lengo la kupiga ramli ili kujua alipo mama
yao.
Waombolezaji wakiwa msibani.
“Mganga baada ya kuangalia ‘king’amuzi’ chake aliwaambia kama
wanataka kujua mama yao alipo, warudi wakamchukue baba yao na kumfikisha
kwa mganga huyo kwani yeye (baba) ndiye ana siri nzito.
“Watoto hao
wakiongozwa na kaka yao mkubwa (Mathias) walimpa baba yao maagizo ya
mganga. Ndipo baba huyo naye akawaambia kama wanataka kujua ukweli wa
mama yao alipo, waongozane hadi kwa mtendaji wa kijiji akasimulie mbele
yake.
MBELE YA MTENDAJI Septemba 4, mwaka huu, familia
hiyo ikiongozwa na baba mtu walifika kwa Mtendaji wa Kijiji cha
Mwanamonga, Said Mango na Mwenyekiti wa Kijiji, Maria Kahimba ambapo
katika maelezo yake , mzee huyo alikiri kumuua mkewe kwa kumpiga na mchi
kichwani.
NUKUU YA MUME
Mzee huyo ananukuliwa hivi: “Nimemuua mke wangu nikamfukia nyuma ya nyumba yangu kwenye choo (watu wakapigwa butwaa).
Polisi wakiwa eneo la tukio.
“Sababu kubwa ya chanzo cha tukio ni mke wangu nilimkatalia ombi lake
la kutaka tumuue mtoto wetu mmoja ili alipe madeni ya uchawi na
kufanikiwa kimapato.
“Nilimkatalia, akawa ananinyima unyumba. Siku
ya tukio nilimlazimisha kunipa unyumba, akakataa akataka kunipiga na
mchi, nikamuwahi yeye na kumpiga, akakata roho.”
NANI ANAYEJUA? Mwanamke mmoja aliyekataa kutaja
jina lake, aliliambia Uwazi kwamba, marehemu aliwahi kumlalamikia kuhusu
mumewe kugoma kumtoa mtoto wao mmoja kafara ili waweze kupata mali.
Alisema mumewe haoneshi kutaka mabadiliko.
“Alisema namwambia mume wangu tumtoe mtoto mmoja kafara tupate
utajiri lakini alisema sitaki kusikia habari hizo, kwani yeye ameridhika
na ufukara,” alisema mwanamke huyo akimkariri marehemu.
POLISI WAFUKUA MWILI, WAKUTA UMEHARIBIKA Baada
ya maelezo ya mzee huyo, vilio vilitawala, hakuna aliyeamini kisha
familia kwa kushirikiana na wananchi na jeshi la polisi,
walifika nyumbani kwa mzee huyo akaonyesha sehemu aliyomfukia mkewe,
polisi wakaamuru mwili huo ufukuliwe ukakutwa umeharibika vibaya, hasa
sehemu ambazo mchi ulipiga.
Baada ya polisi na madaktari kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, waliwaruhusu wanandugu wauzike.
MTUHUMIWA YUKO POLISI Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma, ACP Mihayo Msikela (pichani), amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya
taratibu za kisheria.