Saturday, 11 October 2014

DAR ES SALAAM::WAZIRI MKUU AKAGUA CHUO KIKUU DAR NA CHUO KIKUU HURIA

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema uamuzi wa Serikali wa kukopa fedha ili kuboresha miundombinu kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ulichukuliwa kwa lengo la kujibu tatizo la sasa la wingi wa vijana wanaohitimu kidato cha sita.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Oktoba 10, 2014) wakati akizungumza na wahadhiri, wakufunzi, wanafunzi na wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria (OUT) mara baada ya kuzindua jengo la ghorofa 10 linalojulikana kama Ghorofa la Elimu ya Masafa ya Huria (Open Distance Learning Tower – ODL Tower) lililogharimu sh. bilioni 3.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili jijini Dar es Salaam jana mchana akitokea Morogoro, alitembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ili kukagua utekelezaji wa mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Elimu ya Juu (Science and Technology Higher Education Project - STHEP) unaoendeshwa chini ya uhisani wa Benki ya Dunia.
“Mradi huu ni wa miaka mitano ambao ulianza mwaka 2009 na unakamilika mwaka huu. Lengo hasa lilikuwa ni kujenga uwezo wa wataalamu wetu ambao watakuja kufundisha watoto wa kidato cha sita ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila mwaka.”
Alisema Serikali iliridhia pia fedha hizo zitumike kujenga miundombinu mipya ya kufundishia pamoja na kukarabati baadhi ya zamani kwani kama miundombinu haipo, kazi ya kufundisha haitakuwepo.
“Tulikubaliana pia fedha hizo zinunue vifaa kwa maana ya kompyuta, vifaa vya maabara pamoja na samani za maktaba na baadhi ya madarasa. Ni fedha za mkopo lakini zimetumika kusaidia Watanzania wote.”
Chini ya uhisani wa mradi huo, Chuo Kikuu Huria kimesomesha wahadhiri 29 kati 12 ni masomo ya Uzamifu na 17 ni masomo ya uzamili. Pia kimejenga Maabara za kompyuta tatu, maktaba ya kuweka watu 224 kwa wakati mmoja, vyumba vya mihadhara (seminar rooms) maabara ya lugha (language lab), ununuzi wa kompyuta na samani.
Mapema akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Mkuu alikagua majengo mapya ya ghorofa la shule kuu ya elimu, sayansi ya majini (Aquatic Sciences and Technologies), Multi Complex Building ambalo litakuwa na kituo cha wanafunzi, pamoja kuzindua jengo jipya la Uhandisi Migodi na Usindikaji Madini (Mining and Mineral Processing Building) lililopo kwenye Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering Technology).
Akitoa taarifa ya miradi yote hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala alisema katika awamu hii ya kwanza ya mradi wa STHEP, Chuo hicho kilifanikiwa kupata ufadhili wa Dola za Marekani milioni 40.79 (sawa na sh. bilioni 67).
Chini ya mradi huo, Prof. Mukandala alisema chuo kimefanikiwa kuendeleza kimasomo wafanyakazi wake zaidi ya 150, kujenga majengo mapya manane, kusomesha wahadhiri tarajiwa 163 ambapo 63 wamesoma shahada za umahiri (masters) na 67wamepata shahada za uzamivu (Ph.D).
“Tumeweza kununua vifaa mbalimbali vikiwemo vya maabara, kompyuta 864, vitabu zaidi ya 960, na vifaa vya teknolojia, uhandisi na sayansi. Pia tumeweza kupanua madarasa, maabara na ofisi .”
“Tumepata maabara mpya 49 zitakazokuwa zikitumiwa na wanafunzi 3,630 kwa wakati mmoja; madarasa 53 yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 4,200 kwa wakati mmoja; ofisi 322 zitakatumiwa na wafanyakazi wasiopungua 600,” aliongeza.
(mwisho)

NENO LA SIKU::Siasa madhabahuni zitatufikisha pabaya-Padre Nkwera


Padre Felician Nkwera

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kiongozi wa Kikundi cha Sala cha Wanamaombi, Padre Felician Nkwera amesema nafasi ya Kanisa katika kuhakikisha mchakato wa kupata Katiba mpya unafanikiwa, ni kufunga na kumwomba Mwenyezi Mungu ili awapatie Watanzania Katiba wanayoitaka.

Alisema ushauri ambao Kanisa linatakiwa kuutoa kwa viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa ni kufunga na kusali.

Padre Nkwera alikuwa akijibu maswali kuhusu nafasi ya Kanisa katika kuhakikisha Tanzania inapata Katiba itakayojibu kero za wananchi.

Alisema ni kosa kwa viongozi wa dini kutumia madhabahu yao kuisema serikali pamoja na vyama wa siasa, kinachotakiwa kufanyika ni kuwaita viongozi wa pande zote mbili zinazosigana ili kuzishauri namna ya kufikia mwafaka.

“Kanisa siyo wanasiasa, zamani kazi kubwa ya manabii ilikuwa kumuomba Mungu miongozo yake kwenye masuala mbali mbali.
 
 Manabii walifunga na kumuomba Mungu awape majibu katika masuala ya vita, njaa au shida yoyote iliyolihusu taifa, walimuomba Mungu awasaidie kuwatatulia,” alifafanua.

Kwa sasa Tanzania iko katika mchakato wa kutunga Katiba mpya yenye lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi wengi. Katika mchakato huo kumekuwa na mvutano ambao umesababisha mgawanyo wa makundi mawili ya Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) na Tanzania Kwanza.

Padre Nkwera alisema nchi itapata Katiba lakini siyo kwa kasi tunayoihitaji sisi kama binadamu. Tanzania ina wenyewe na wao ndio watakaoamua lini Tanzania iwe na Katiba mpya.

“Katiba itapatikana lakini siyo kwa spidi tunayoitaka, itapatikana hata katika kipindi cha awamu inayofuata,”
alisema.
 
Aliwataka Wanamaombi waombe ili Taifa lipate Katiba mpya inayofaa, kwani ni jukumu walilokabidhiwa kuombea mchakato huo ili nchi ipate Katiba mpya katika hali ya utulivu.

Alisema malumbano ya kwenye vyombo vya habari hayatatoa mshindi na badala yake malumbano hayo yataendelea kuivuruga Serikali na kusababisha kutokuelewana kuendelea.

“Jukumu la viongozi wa dini ni kuwashauri viongozi wa Serikali na wale wa vyama vya siasa ili wafikie mwafaka ambao utasaidia kupatikana kwa Katiba ambayo wananchi wanaitamani,” alisema.

Alipoulizwa iwapo Katiba haitapatikana Watanzania wafanye nini, Padre Nkwera alijibu kuwa zamani Waisraeli waling’ang’ania kuwa na mfalme wao kama yalivyo mataifa mengine, Mwenyezi Mungu akawaambia “Nikiwapatia mfalme atawafanya watumwa na atawalipisha kodi, hamtakuwa na amani”.

Waisraeli hawakumsikiliza na badala yake wakaendelea kung’ang’ania mfalme wao, Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Waisraeli hawakupingi wewe bali wananipinga mimi, wapatie mfalme wao”. Mungu aliwapatia Saulo kuwa mfalme wao na toka siku hiyo walikumbuka maagizo ya Mungu.

Akizungumzia suala la upande upi Wanamaombi wasimamie kati ya kikundi kinachojiita UKAWA au Tanzania Kwanza, Padre Nkwera alisema Wanamaombi hawatakiwi kuwa na upande wowote kati ya hizo mbili, wanatakiwa kuwa neutral ndio maana wamepewa jukumu la kuombea mchakato.

Aidha alisema serikali tatu zitabomoa Muungano kwa sababu, serikali ya tatu haitakuwa na sehemu ya kupata mapato yake zaidi ya kutegemea nchi wahisani. 
 
Alisema hatari ya kutegemea mapato kutoka kwa nchi wahisani ni pale nchi moja itakapogoma kutoa fedha kwa nchi ya tatu.

Alisema Tanzania ni nchi ya serikali mbili lakini uroho wa madaraka ndio unaosababisha watake serikali tatu.

Padre Nkwera alisema ili serikali mbili zifanye kazi, Zanzibar haina budi kufunga balozi zote ambazo imeingia nazo uhusiano, iondoe Katiba yake, iondoe bendera na hata wimbo wa Taifa, nchi iwe na bendera moja, wimbo mmoja wa Kaifa na Katiba moja.

Kwa kufanya hivyo Muungano utaendelea kudumishwa vizazi kwa vizazi. 
 
Alitahadharisha kuwa serikali tatu siyo suluhisho la matatizo yaliyopo nchini bali ni kuongeza matatizo na hatimaye kuubomoa Muungano ambapo mwisho wake hautakuwa mzuri.

Source:Jarida kwa wanamaombi:Safina ya Malkia.

Friday, 10 October 2014

MAUAJI IRINGA::JESHI MKOANI IRINGA LINAMSHIKILIA NGAGA KWA KUMPIGA RISASI RAFIKI YAKE



NA FRIDAY SIMBAYA, IRINGA
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Gwerino Ngaga (70) mkazi wa Mbigili kwa kosa la kumpiga risasi  kifuani Thadei Mbugu(40) mkazi wa Mbigili  na kusababishia kifo chake papo hapo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi akielezea tukio hilo la kinyama kwa waandishi wa habari ofisini kwakw leo alisema kuwa limetokea Oktoba 9 majira ya saa moja za jioni  katika kijiji chaMbigili kata ya Lugalo tarafa ya mazombe wilaya ya kilolo mkoani hapa.


Kamanda Mungi alisema kuwa awali kabla ya tukio marehemu pamoja na mtuhumiwa wakiwa na wakezao walikuwa wakinywa pombe  za kienyeji katika kilabu kinachoendeshwa na mke wa Gwerino.


Mungi alisema kuwa sababu kubwa ya  mtuhimiwa kumpiga risasi marehemu Thadei lilitokea mara baada ya mke wa mtuhumiwa kumuomba pesa marehemu mbele ya mkwewe na mumewe kitendo kile kilimuudhi mtushtakiwa  na  kuamua kuenda nyumbani kuchukua bunduki aina ya shortgun na kumpiga  kifuani hali iliyopelekea kupoteza maisha. 

‘’Hawa jamaa walikuwa wote na wake zao wakipata kinywaji sasa wakati wanakunywa huyu mke wa mtuhumiwa alimuomba marehemu ampe hela ya  kutumia na mke wa  wa marehemu aliposikia mumewe akiombwa hela alifoka kwa nguvu kwa kulaani kitendo cha mumewe kumhonga mke wa mtu hela tena kilabuni huku angali akiwa na mumewe’’
“Sasa mume wa yule mke aliposikia mkewe anapewa hela na marehemu alimuuliza kisa cha kumdhalilisha kwa kumpa mkewe hela mbele yake ndipo marehemu akamjibu kwa dharau kuwa amezeeka na hivyo hana hela hivyo anamsaadia kumlea kitendo kilichomuudhi mstakiwa na kumlipua kwa bunduki yake,”  alisema Mungi.




Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi wa karibu ili kubaini nini chanzo hasa kilichosababisha mtuhumiwa kuchukua bunduki na kumpiga mwenzie kwani hapo awali kulikuwa hakuna ugomvi wowote na wote walikuwa ni majirani wanaokaa mtaa moja .


Mungi alieleza kuwa  baada ya kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa bunduki hiyo  aina ya shotgun iliyotumika katika mauaji hayo  inamilikiwa kihalali na Gwarino Ngaga mkazi wa Mbigili.

SIASA::PROFESA BAREGU AFICHUA SIRI NZITO TUME YA KATIBA


Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu

Aliyekuwa  mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ametoboa siri kuwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Warioba alikuwa na msimamo wa serikali mbili, kabla ya tume kuja na rasimu yenye muundo wa muungano wa serikali tatu uliotokana na maoni ya wananchi walio wengi.


Baregu alitoboa siri hiyo wakati akizungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki hii. Alikuwa akijibu moja ya maswali aliyoulizwa kuhusiana na namna wao (tume) walivyoondosha tofauti za kimtazamo miongoni mwa wajumbe na kuandaa rasimu iliyokubaliwa na wajumbe wote; tofauti na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambayo walitofautiana sana kuhusiana na suala la muundo wa muungano na mwishowe, wajumbe wengi wa upinzani wakasusia vikao kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuwaachia wenzao wanaoundwa na wafuasi wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea na kazi hiyo.

Wajumbe wanaounda Ukawa ambao wengi ni kutoka vyama vikuu vya upinzani nchini vya NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) walisusia vikao vya Bunge la Katiba kutokana na madai yao kuwa rasimu iliyoandaliwa na tume iliyoongozwa na Warioba kwa kuzingatia maoni ya wananchi ilibadilishwa kwa maslahi ya CCM. Ukawa walikuwa wakitetea rasimu ya Warioba iliyopendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu huku wajumbe wengi wa CCM wakisisitiza kuwa na muundo wa muungano wa serikali mbili lakini ulioboreshwa. 

Akieleza zaidi, Baregu alisema kuwa kwa ujumla, tume ilijigawa kwenye kamati ndogo tatu wakati wa kuanza kujadili mapendekezo, ambazo ni kamati ya mihimili ya utawala (bunge, serikali na mahakama), kamati ya iliyokuwa ikishughulikia misingi na maadili ya taifa na kamati ya tatu ndiyo iliyokuwa ikishughulikia masuala ya muungano.

“Labda niwaeleze tu, hiyo kamati ya muungano tuliipa jina kama kundi la kifo... na ninalitaja kundi hili kwa masikitiko kwa sababu mmoja wetu, Dk. Mvungi alifariki kweli,” alisema.

Prof. Baregu alisema kundi la kifo lilikuwa la  watu wenye misimamo kuanzia wa serikali moja, mbili, tatu  na wengine waliokuwa na mawazo ya kuwa na muungano wa mkataba.

“Akina nanihii hawa... akina Warioba, akina Butiku, Jaji August... walianza na msimamo wa serikali mbili. Mimi siku nyingi ni mtu wa serikali moja. Wakawapo watu wa serikali tatu, including (akiwamo) Dk. Mvungi. Na kundi la nne la watu wenye msimamo wa serikali ya mkataba,” alisema.

Alisema pamoja na minyukano iliyojitokeza kutokana na misimamo hiyo binafsi ya wajumbe, bado waliweza kusimama imara na kuzishinda nafsi zao kutokana na mawazo ya wananchi waliyoyapata wakati wakikusanya maoni katika maeneo mbalimbali nchini, chini ya uongozi wa mwenyekiti wao (Warioba).

Alisema kuwa awali, mwenyekiti wao (Warioba) alitoa nafasi kwa kila mjumbe kwenye suala la muungano kuzungumza na kutoa mchango wake.

“Ninakumbuka kwenye issue hii ya muungano, kila mjumbe ilibidi azungumze. Na mwenyekiti ali-insist kwamba kila mmoja wetu ni lazima achangie, na tukalizungumza kwa karibu wiki nzima,” alisema.

Prof. Baregu alisema pamoja na kila mjumbe kuzungumza, pia waliangalia maoni  waliyokusanya kutoka kwa wananchi na mwisho wa siku wakaja na maamuzi ya pamoja,  ambayo yaliwafanya kuchukua msimamo wa pamoja pia.

Alisema hawakumuacha mjumbe yeyote nyuma akiwa bado hajaridhika kwa hoja na maoni waliyokusanya na kwamba, pale ilipotokea hivyo, walianza naye kwenye kikao kilichofuata hadi kuhakikisha kwamba mhusiaka ameridhika.

“Na ndiyo maana sasa hivi ukizungumza na wajumbe wote, sijasikia hata mmoja ambaye amebadilisha mawazo, ama... au amesema kwamba alirubuniwa kwenye tume au labda kwamba Jaji Warioba alifanya maamuzi ya ubabe,” alisema.

Alisema kutokana na namna walivyoendesha mambo yao kwa uwazi na kufikia maamuzi ambayo wote waliyaafiki kikamilifu kuwa yamezingatia kwa usahihi matakwa ya wananchi, ndiyo maana bado wana mshikamano mzuri hadi sasa na wameamua kwenda kuitetea rasimu ya tume kwa wananchi.    

Amesisitiza kuwa wajumbe wa tume hiyo wamejipanga kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyokuwa kwenye rasimu hiyo.

Alisema walipokuwa kwenye Tume walifanyakazi kwa bidii, weledi, nidhamu na kujenga maridhiano ndani ya jamii na ndani ya tume.

"Tuliwasikiliza wananchi wanataka nini na kuzingatia maoni ya Watanzania, na lengo la tume lilikuwa ni kupata katiba yenye maoni ya wananchi,” alisema.

KATIBA ILIYOPENDEKEZWAAlisema sasa hivi, kwenye Katiba iliyopendekezwa, kuna mambo mengi ya msingi yamenyofolewa; kama mambo ya maadili, uwajibikaji, kumwajibisha mbunge, ukomo wa ubunge, madaraka ya rais na  mawaziri kutokuwa wabunge; mambo ambayo yalipendekezwa na wananchi wengi.

Prof. Baregu alisema njia pekee ya kunusuru mchakato mzima wa katiba ni kukubali kwamba tumekwama na kukubali kusahihisha makosa badala ya kuburuza mchakato huo bila maridhiano.

Katiba iliyopendekezwa ilikabidhiwa juzi mjini Dodoma kwa marais, Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk. Ali Mohamed Shein wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

“Sisi ndani ya Tume tulijenga kwanza maridhiano ndiyo maana tuliweza kutoa rasimu ambayo sote tulikubaliana,” alisema
Prof. Baregu alisema: "Kwa hali hii, ilipaswa tuwe na ujasiri wa kupumua kwanza, tukaulizana na tukakubali kwamba tumekwama kwa malengo tuliyokuwa tumejiwekea... sasa hivi ni kama mtu umepotea njia lakini unasema twende tu."

Aliongeza kuwa: "Tulikuwa na lengo, tulikuwa na ramani kwa hiyo kama tungekuwa na ujasiri kama taifa tukasema ngoja tujiulize hapa tufanye nini ili tuweze kutoka hapa, mengi tungeweza kubadilisha." Alisema mchakato umekwama baada ya kutawaliwa na wanasiasa ambao hawawezi kupitisha mapendekezo ambayo yanapingana na maslahi yao.

"Ni vyema kama tungekubali kusema hapa tumekosea, tuunde upya Bunge la Katiba, na kukubali kwamba tumekosea sana... na siyo serikali tu, lakini sote kama taifa."

Alisema. "Nimekuwa nafikiri hivi... ni kama mama mwenye mimba anayepata abortion (mimba kuharibika). Anajisikiaje?” alisema Baregu.

Alisema kwa hali ilivyopelekwa, anahisi kuwa na hali kama hiyo ya mama aliyeharibikiwa na mimba yake, kwamba amekuwa kwenye timu iliyofuatilia watu karibu mwaka mmoja na nusu kutunga katiba, lakini inaishia kusakamwa.

Alisema tume imefanya kazi kwa uadilifu, weledi

MTOTO ALBINO::Huyu ndio mtoto ambae Polisi wa Kenya wamemuokoa akija kuuzwa Tanzania.



K1


Kenya Polisi
Ni pale ambapo unaweza kuvuta picha baba anajaribu kufanya mbinu za kumsafirisha mtoto wake kwenda nchi ya pili ili akamuuze kwa watu ambao ameshazungumza nao kabisa na wako tayari wanasubiria biashara ifanyike.
Yani hiki kisa kilichotokea Kenya kina uzito wake mpana tu sababu Baba mzazi na Baba wa kambo wote wamehusika kwa nyakati tofauti kufanya mbinu za kutaka kumsafirisha mtoto huyu ambae ni Albino ili aje Tanzania kuuzwa na viungo vyake vitumike kwa imani za kishirikina.
K3 
NTV wameripoti kwamba Polisi wa Kenya ndio walimuokoa huyu mtoto akiwa tayari ameshaingizwa Tarime Tanzania akiwa anasafirishwa kwa siri na baba yake wa kufikia (wa kambo) ambapo mama mzazi amesema baada ya kuolewa na mume wa pili baada ya kuachana na yule wa kwanza ambae ndio baba wa mtoto, amekutana na kitu kilekile kama alichotaka kufanya mume wa kwanza, mume wa pili pia anataka kumuuza huyu mtoto.
Mama wa mtoto anasema ‘ninachoshangaa ni kwamba baba yake mzazi alipotaka kumuuza huyu mtoto alikamatwa, tena baba yake wa pili amejaribu kuja kutaka kuiba tena huyu mtoto, ni giza ambalo nimeliona kwangu na kuhofia maisha ya mtoto na mpaka sasa tunamfungia ndani hawezi kutoka hata kwenda shule’
Kwenye sentensi nyingine mama wa mtoto huyu anasema ‘Wakati mwingine najiuliza kwa sababu baba yake mzazi wa kwanza alishikwa na Polisi lakini sijui hiyo kesi iliendeleaje na akaachiliwa, sasa ni kama wameona ni  kawaida hata kama wanakwenda kuripotiwa hakuna hatua yoyote inachukuliwa kuhusu huyu mtoto’

UDAKUZ>>MAPENZI: WEMA NA BABA, DIAMOND NA MAMA

Stori: Hamida Hassan
Tofauti na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye miili yao kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu wamekuwa tofauti, Ijumaa limegundua.
Tattoo ya Diamond Platinum ikionekana kwenye mkono wake wa kushoto.
Mastaa hawa wameonyesha kuwa na mapenzi na wazazi wao ambapo mwandishi wetu amebaini Diamond ameandika jina la mama yake mkononi huku Wema akiandika jina la baba yake mkononi pia.
Wote wamefanya hivyo kwenye mikono yao ya kushoto sambamba na uwepo wa tatoo nyingine ambapo Wema ameandika ‘Daddy Sepetu’ na Diamond akaandika Sandra…’
Tattoo ya Wema Sepetu ikionekana kwenye mkono wake wa kushoto.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wao wamedai huenda penzi la mastaa hao si la kudumu ndiyo maana wamekwepa kuandikana ili isije ikawa shida pale watakapomwagana

HONG KONG>>Wanafunzi: Maandaamano bado Hong kong


Waandamanaji Hong Kong
Serikali ya eneo la Hong Kong imeitisha mazungumzo maalumu na viongozi wa wanafunzi ambao wamekuwa wakiratibu maandamano yaliyodumu kwa wiki mbili hadi sasa.
Mkutano huo wa serikali ya eneo hilo na wanafunzi unatarajiwa kufanyika leo.waandamanaji hao wanapinga utawala wa Beijing kuwachagulia mgombea katika uchaguzi mkuu wa eneo hilo 2017.
Hata hivyo wanafunzi hao wamesisitiza kuwa wataendelea na mgomo huo pamoja na serikali hiyo kuhitaji mazungumzo na viongozi wao.
Waandamanaji hao kwa sasa wamekuwa wakiendelea na maandamano huku baadhi ya huduma mhimu na kazi zikidorola.BBC

UREMBO::LORRAINE ATUA NCHINI APONGEZA WATANZANIA

Lorraine Clement akishukuru
Lorraine Clement akimshukuru Mungu, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Lorraine akiwasili muda
Lorraine Clement akipungia watu waliofika kumlaki alipowasili jijini Dar.
Lorraine na meneja wake Abubar Faraj
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia)
Lorraine kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
Na Andrerw Chale
MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Katika mapokezi hayo, Lorraine alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na mtendaji Mkuu wa Redline Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau wengine walijitokeza uwanjani hapo.
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu, Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu, ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na thamani za ndani.

KIGOMA::MASIJALA ARDHI KIGOMA YACHOMWA MOTO

WATU wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuchoma moto jengo la masijala ya Idara ya Ardhi Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketeza nyaraka mbalimbali.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Japhari Muhamed, alisema jengo hilo liliungua juzi majira ya saa 4 usiku baada ya kuchomwa na watu ambao hawakujulikana.
Alisema kuwa mbinu iliyotumika ni kuchoma ofisi kwa kutumia mafuta ya petroli ambako moto huo uliteketeza ofisi yote na kusababisha hasara kubwa.
“Hakuna kitu kilichosalia baada ya moto kuteketeza ofisi, vyote viliungua zikiwemo hati na nyaraka mbalimbali,” alisema Kamanda Muhamed.
Alisema wanawashikilia watu wanne kuhusiana na tukio hilo ambao ni Anna Fanuel (46), mhudumu wa ofisi, Makrina Paulo (49), karani, Saimon Pius (37), mkazi wa Burega na Tumaini Esau (44), mkazi wa Mwasenga.
Kamanda Muhamed, aliongeza kuwa uchunguzi wa kina dhidi ya tukio hilo unaendelea

MOROGORO::WAZIRI MKUU AVUTIWA NA KASI YA MABADILIKO SOKOINE

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema amevutiwa na kasi ya mabadiliko katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na hasa uanzishwaji wa kozi mpya zinazolenga uongezaji thamani wa mazao ya kilimo (Agri-processing).
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Oktoba 9, 2014) wakati akizungumza na wahadhiri, wakufunzi, wanafunzi na wanajumuiya ya SUA mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua utekelezaji wa mradi wa Sayansi na Teknolojia ya Elimu ya Juu (Science and Technology Higher Education Project - STHEP).

“Nimefurahia sana hili suala la Agri-processing kwa sababu hivi tuna mzigo mkubwa unaoisumbua Serikali nao ni namna ya kununua mazao ya wakulima. Tuna ziada ya tani milioni 1.5 za mahindi na tani laki nane za mpunga wakati uwezo wa NFRA ni kununua tani 240,000 tu. Haya ni matokeo ya wahitimu waliotoka SUA na kupelekwa wilayani na vijijini wakahimiza kilimo bora kwa wananchi,” alifafanua.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili Morogoro jana mchana akitokea Dodoma, alifanya ziara ya siku kwa kutembelea Chuo Kikuu hicho pamoja na kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21stCentury.
Akiwa chuoni hapo, Waziri Mkuu alikagua majengo matatu yaliyojengwa chini ya mradi wa STHEP na kuzindua mawili kati ya hayo, alitembelea maabara za upimaji ubora wa vyakula na kisha kuzungumza na wanaSUA.
Akizungumza na wanajumuiya hao, Waziri Mkuu aliwataka wawe ni viongozi wa mfano kwa kumiliki walau ekari moja ya shamba, walime au kuweka mifugo ili yale wanayofundisha darasani yaonekane kwa vitendo katika mashamba hayo.
“Tatizo la sasa hivi miongoni mwa wasomi wengi ni kudhani kwamba kazi ya kilimo ni ya watu wa hali ya chini lakini wakifika mezani wao ndiyo wa kwanza kudai ubwabwa na kuku. Sisi wenye upeo ndiyo tunapaswa tuonyeshe njia na mashamba au mifugo yetu yawe ni ya mfano kwa wengine,” alisema.
Mapema,akiwasilisha taarifa ya mradi wa STHEP, Profesa Gerald Monella alisema mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.48 (sawa na sh. milioni 12.5/-) umekisaidia chuo hicho kupata majengo manne yenye kati ya ghorofa moja na mbili, ambayo yameongeza nafasi za kufundishia wanafunzi, vyumba vya maabara na vifaa vyake, kuanzisha mitaala miwili pamoja na kusomesha walimu 21.
Kwa kutumia majengo hayo, Chuo kinaweza kufundisha wanafunzi 807 kwa wakati mmoja ambayo ni sawa na wanafunzi 10,565 kwa wiki moja. Chuo hicho pia kimeweza kupata vifaa vya maabara vyenye thamani ya dola za marekani milioni 1.71 ambavyo vimenunuliwa na kufungwa kwenye maabara hizo.
“Kwa upande wa elimu ya juu, mradi umeweza kusomesha walimu 21, miongoni mwao 11 wakiwa ni wa shahada ya uzamivu (PhD) na 10 ni wa shahada za uzamili (Masters’).
Aliiomba Serikali iongeze muda wa kustaafu kwa wahadhiri wa vyuo vikuu kwani wanapozeeka ndiyo wanapata muda wa kufanya tafiti zaidi. “Fani nyingie watumishi wanastaafu wakiwa na miaka 60 au zaidi, nasi tunaomba tuongezewe muda badala ya kutumia mfumo wa sasa wa kuongezewa miaka miwili miwili halafu mmoja,” alisema.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Mama Kate Kamba wakati akitoa salamu za shukrani kwa Waziri Mkuu, alisema Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza bajeti ya Chuo kwani kinahitaji fedha zaidi kwa ajili ya kufanya tafiti na kuboresha miundombinu.
“Tunahitaji fedha za kufanya tafiti zaidi, fedha za kuboresha miundombinu ya kufundishia ili tuweze kwenda sambamba na azma ya Serikali ya kuimarisha viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo,” alisema.

MAPENZI NA SHULE::MWANAFUNZI WA SEKONDARI AMPACHIKA MIMBA MWALIMU WAKE


WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.


Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.


Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.

Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.

Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.

“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni sawa tu…

“Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu masomo yake…” alisema.

  
 Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.

“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.”

Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.

Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba baada ya watu wao wa karibu kumweleza  mwandishi  kuwa hawako tayari kuuzungumzia mkasa huo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutoandikwa majina yao  kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao.

Walisema pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.

“Huyu mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa mwalimu mwenzake,“ alisema mmoja wao.

Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi, bali kukubaliana na matokeo.

“Usiniandike jina, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.

“Isitoshe tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?”Alihoji.

Baadhi ya wazazi mkoani hapo waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati tofauti wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake.

ELIMU BORA::MAZINGIRA MABOVU YA UTOAJI ELIMU

Mwalimu wa shule ya msingi Nyiboko wilaya ya Serengeti akifundisha wanafunzi wa darsa la tano wakiwa wamekaa chini,juu hakuna paa
pamoja na mazingira haya mnanielewa?
Wanafunzi wa darasa la nne na sita shule ya msingi wa Nyiboko wilaya ya Serengeti wakiwa wamekaa darasa moja kwa ajili ya kusoma ,pamoja kutokana na kukosa vyumba vya madarasa.
wanashindwa kumfuatilia mwalimu

KIGOMA>>MWANAFUNZI AFARIKI AKISAKA MAEMBE

MWANAFUNZI Hamimu Mussa (11), wa Shule ya Msingi Uhuru  Manispaa ya Kigoma Ujiji, amefariki dunia baada ya kuanguka kwenye mti wa mwembe na mwingine kuvunjika mguu na mkono.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi (ACP), Japhari Muhamed, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni wakati wanafunzi wakiwa mapumziko, ambako wawili hao walipanda juu ya mwembe kwa lengo la kutafuta maembe.
Alisema kuwa wakati wanafunzi hao wakiwa juu ya mwembe, ghafla walianguka wote na Hamimu kupasuka kichwa na kufariki papo hapo, huku Baraka Ramadhani akivunjika mkono na mguu.
“Mti waliokuwa wameupanda ni mkubwa na mrefu, hivyo walikuwa mbali sana na ndio maana walipoanguka mmoja akafariki na mwingine kuvunjika,” alisema Kamanda Muhamed.
Alisema kuwa mwili wa marehemu tayari umeshakabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi, wakati majeruhi amelazwa hospitali ya Mkoa Maweni kwa matibabu.
Kamanda Muhamed, amewataka walimu na wazazi kwa ujumla kuwa waangalifu kwa wanafunzi ili kuwaepusha na michezo ambayo ni hatarishi kwa maisha yao.

UDAKU>>HII NDIO BARUA NZITO: WOLPER JIHESHIMU BWANA


 
Kwako
mtoto mzuri unayekimbiza kwenye anga la filamu Bongo, Jacqueline Massawe Wolper. Bila shaka ni mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.

Binafsi mimi naendelea vizuri mambo yanakwenda kwenye mstari na leo nimekukumbuka kupitia barua nzito.
Nataka kusema na wewe mawili matatu ambayo mimi nimeona si sawa kufanywa na wewe!
Nisichelewe sana wala nini, madhumuni ya barua hii kwanza kabisa ni kutaka kukukumbusha kwamba unapaswa kujiheshimu katika kila sekta kwa kuwa wewe ni kioo cha jamii.
Jamii inakuheshimu, inakufuatilia kila hatua unayopiga maishani.

Wanaokufuatilia ujue wanakupenda ingawa pia hata wale wasiokupenda nao pia wanakufuatilia.
Wanakufuatilia kwenye vyombo vya habari, katika mitandao ya kijamii na hata live mitaani. Kauli yako lazima iwe na staha.

Sababu ya kukwambia jiheshimu ni kauli zako kwenye mitandao ya kijamii. Mara kadhaa nimekuwa nikiona ukiposti lugha ya matusi kwa waliokuudhi.Kwa nini utukane? Kwa mtu anayejiheshimu kama wewe si busara hata kidogo kutukana hata kama umechokozwa.
Akili yako inapaswa kutafakari kwa kina kabla ya kuposti kitu chochote katika mitandao ya kijamii. Unapoposti kitu pia ujue kuna watu ambao watakipenda na ambao hawatakipenda, sasa kwanza kuwajibu wale wasiokipenda unajishushia heshima!
Mfano mzuri ni siku ile ulipoweka aina mpya ya simu katika mtandao wa kijamii. Niliufuatilia mjadala ule, kuna watu walikuponda kwamba aina ya simu hiyo mpya haipo na kwamba ulifanya hivyo ili kujipa sifa.
Mtoto wa kike ukaona bora umtukane, ukaandika tusi zito kabisa kumjibu shabiki huyo. Ukimjibu mjinga unategemea nini? Najua kabisa dhamira yako kuweka simu hiyo ilikuwa ni utani lakini walivyoipokea baadhi ya mashabiki wakakusababisha utukane.
Wewe unaheshimika, kutukana si jambo la busara. Siku hizi teknolojia inakua, ni rahisi mtu kukufuatilia na kukupata na hata kukuchukulia hatua za kisheria.
Kwa nini utukane? Kwanza hata ukiamua kutukana, utatukana wangapi katika mitandao ya kijamii? Si sawa!
Siku hizi mitandao inatumika kama chombo cha biashara, ni vyema ukawa makini na unavyoposti ili ikiwezekana hata ukatumia mitandao hiyo kujiingizia mkwanja kuliko kutukana na watu wanaokuheshimu wakakuona hauna maana.
Usipoteze muda wako kuwajibu watu ambao hawakosi cha kuongea. Utajisumbua tu, fuata mifano ya mastaa wengi ulimwenguni, wanapoweka kitu katika mitandao ya kijamii huwa hawageuki kutazama watu wamekomenti nini baadaye.
Weka kitu chako kisha fumba macho kama huoni vile, si wote watakaokichukulia kitu chako chanya. Kuna wengine wataponda au watakutukana, ukiwajibu watu watakuona wewe mpuuzi kuliko hao waliokuanza!
Kwa leo acha niishie hapo, kuwa makini sana na mitandao ya kijamii.

UDAKU>>BAADA YAKUACHIKA: ROSE NDAUKA AANGUSHA SHEREHE!

SIKU chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.
Msanii nyota wa filamu nchini, Jack wa Chuz (kushoto) akimtunza msanii mwenzake, Rose Ndauka (kulia)
Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.
Msanii wa filamu nchini, Mayasa (kushoto) akitoa sapoti ya kufungua shampeni katika sherehe hiyo ya bethidei ya Rose Ndauka.
Katika pati hiyo kulikuwa na vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi, huku pia vyakula vya aina mbalimbali vikipatikana, kiasi kwamba hadi gazeti hili linaondoka, pombe na vyakula bado vilikuwepo.
Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Shamsa Ford naye pia alikuwepo.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.
Baadhi ya wasanii  wa filamu nchini na wageni waalikwa wakila na kunywa.
Kwa upande wake, Rose alisema: “Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo yote yako vyema kabisa.”

habari::STEVE NYERERE AMPA JK ZAWADI YA BETHIDEI YAKE


WAKATI Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumanne wiki hii alisherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 64,  Mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jumatano iliyopita alimpa zawadi baada ya kumvunja mbavu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Katiba Mpya Inayopendekezwa iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete.
Steve, aliyepanda jukwaani kuwakilisha wasanii, alitumia dakika zisizozidi tano kumsifu Rais Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii, akidai ndiye amewafungulia milango ya mafanikio na kwamba watamkumbuka kwa kitendo cha kutambuliwa kwao kikatiba.
Baada ya hapo, mchekeshaji huyo maarufu wa kuiga sauti za watu mbalimbali, alianza kwa kuigiza sauti ya Rais Barack Obama wa Marekani, akimuigiza kumsifu Rais Kikwete kwa kutengeneza katiba mpya na kisha kuwasifu Watanzania na nchi yao kisha akawashukuru kwa kuwaambia asante.
“Mbona hamuitikii jamani Watanzania, au Kiingereza not reachable, naona mna-vibrate tu,” maneno hayo licha ya kuwachekesha mamia ya waliomsikiliza, pia walimfanya Rais Kikwete na Dk. Shein, kuvunjika mbavu hadi kulazimika kulalia meza zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein, kwa pamoja wakionyesha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Alipomaliza kuiga sauti ya Obama, akaendelea kwa kumuiga Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akimnukuu akielezea jinsi Rais Kikwete alivyokwenda kwake na kumuambia kuhusu nia yake ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania.
Baada ya kumaliza kumuiga Mwalimu, Steve Nyerere alimgeukia JK na kuiga sauti yake na jinsi anavyofanya baadhi ya mambo katika hotuba. Aliiga staili ya Rais anapowasalimia watu walio mbali, anavyojishika kichwani na maneno yake, hali ambayo kwa muda wote ilimchekesha Rais na viongozi wengine wengi waliokuwepo meza kuu, akiwemo Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Rais Mohamed Bilal na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta.
Mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Kabla ya Rais kukabidhiwa Katiba hiyo inayopendekezwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalum la Katiba, Andrew Chenge, alitoa muhtasari wa kilichomo ndani ya Katiba hiyo mpya, ambayo hatua itakayofuata ni kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni kabla ya kuthibitishwa na kuanza kutumika rasmi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, ndiye aliyekabidhi katiba hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeasisi mchakato huo, akizima ajenda ya muda mrefu ya vyama vya upinzani.

Thursday, 9 October 2014

MAAHABU::MTOTO MIAKA 9 AKUTWA AMEJINYONGA

Stori: Gabriel Ng’osha
MY God! Katika hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda, Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa sebule yao.
Baba mzazi wa marehemu Focus Saimon (9).
Focus aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa siku ya tukio,  Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo wake, Irene Steve (5).
Mama mzazi wa Focus Saimoni (kushoto) akihuzunika kumpoteza mwanaye.
“Alipofika alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia ndani,  akanywa chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na kumkuta tayari ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
Mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria (kushoto) akiwa na mama mzazi wa Focus Saimoni.
“Nilimwambia Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi, nilipomwangalia vizuri ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa mama mdogo anayeishi jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.
Mdogo wa marehemu Focus Saimoni, Irene.
Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi  aliukuta mwili umeshushwa chini.

“Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Marehemu Focus Saimoni (9) enzi za uhai wake.
’’Tukio hili lina shaka ndani yake, mtoto wa miaka 9 anawezaje kujinyonga, kwa stress zipi? Kwa kweli inasikitisha sana, jeshi la polisi lina wajibu wa kuchunguza ukweli wa kifo cha mtoto huyo,” alisema mama huyo.Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.

MBEYA>>AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI KUGONGANA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, UMRI ATI YA MIAKA 25 – 30 AMEFARIKI DUNIA WAKATI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.397 AQT AINA YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE NOEL MAHENGE KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.505 BYG/T.843 CUG AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GODFREY PHILIMON (37) MKAZI WA TUKUYU WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI HUKO CHAPWA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
 AIDHA, KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI TUNDUMA AMBAO NI 1. SHABANI KIPANDE (22) MKAZI WA UYOLE NA 2. MUDDY MSELEMU (25). CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.397 AQT AINA YA ISUZU. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA – MBOZI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
 TAARIFA ZA MISAKO:
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AITWAYE SEYIM LATABO (45) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
 MHAMIAJI HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO KATIKA STENDI YA MABASI – TUKUYU, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMESHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MATATIZO NA MADHARA YANAYOWEZA TOKEA.

KONGO>>UN:M23 walibaka mamia ya wanawake

Waasi wa M23 waliweka chini silaha baada ya kushindwa vita
Kikosi cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, kimetuhumu kundi la waasi wa zamani M23 kwa kufanya uovu mkubwa ikiwemo kuwabaka mamia ya wanawake.
Waasi hao pia wanadaiwa kufanya uhalifu dhidi ya binadamu.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa, inasema kuwa miezi 18 kabla ya kundi hilo la waasi kujisalimisha liliwaua zaidi ya watu 110 na kuwabaka wanawake zaidi ya 160 pamoja na wasichana wadogo.
Inaarifiwa wengi wa wanawake waliobakwa walikuwa wake wa wanajeshi au maafisa wa jeshi.
Waasi wa M23 waliwalenga zaidi maafisa wa eneo hilo waliokataa kushirikiana nao pamoja na vijana waliokata kujiingiza katika harakati za kundi hilo.
Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua wote waliotenda uhalifu huo.