Friday, 17 October 2014

MAFANIKIO::ORIJINO KOMEDI WANUNUA NYUMBA 7 ZA NSSF ZENYE THAMANI YA MILIONI 840

Kundi la vichekesho la orijino Komedi limenunua na kuwakabidhi nyumba 7 wasanii wa kundi hilo zwnye thamani ya shilingi milioni 840 ambapo kila nyumba moja imenunuliwa kwa shilingi milioni 120

MIKUMI::Breaking news basi la kwa wapendwa lapata ajali laua


Ajali mbaya ya basi la kampuni ya Kwa Wapendwa lenye namba za usajili T 951 BBK kutoka mkoni Njombe kwenda Dar es Salaam yaua mmoja huku abiria zaidi ya 50 wakinusurika.


Ajali hiyo imetokea Leo Majira ya saa 6 mchana katika barabara kuu ya Iringa -Dar es Salam kwenye kijiji  cha Msimba  mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Mmoja Kati ya abiria wa basi hilo John Sanga ameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kuendesha kwa Mwendo kasi katika eneo hilo lenye kona kali kabla ya kuligonga lori lililokuwa limesimama mbele yake.

Sanga alisema kuwa dereva huyo alilazimika kuingia katika lori hilo kukwepa kugongana uso kwa uso na lori  lililokuwa mbele yake kutoka Morogoro.

"Dereva wetu alikuwa katika Mwendo Mkali sana kwani iwapo angekuwa katika Mwendo wa kawaida baada ya kuliona lori hilo mbele na hakuna uwezekano wa kupita angeweza kusimama"

Hata hivyo alisema kutokana na ajali hiyo mmoja Kati ya abiria aliyekuwa amekaa siti ya mbele kushoto kwa dereva ndie aliyepoteza maisha eneo la tukio na baadhi ya abiria kupata majeraha ya kawaida na kukimbizwa hospitali .

Mmoja Kati ya askari waliokuwepo eneo la tukio ambae hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro alidai kuwa ni mtu mmoja pekee ambae ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka Kati ya 50 na 55 ndie aliyefariki na jina lake halijaweza fahamika.

Aidha alisema chanzo ni dereva wa basi hilo la abiria kulazimisha kupita pasipo na njia huku akijua wazi lori la mbele yake lilikuwa limesimama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro hakuweza kupatikana kuelezea zaidi tukio hilo.

TETESI::GARI JIPYA LA KIFAHARI LINALODAIWA KUWA LA DIAMOND PLATNUMZ


 

Gari aina ya Mercedes 350 Cdi inyosemekana inamilikiwa na msanii Diamond.

Hiyo ni Mercedes Ml 350 Cdi ya mwaka 2014 Radio Mbao moja ya mjini imevumisha kwamba ni kitu kipya cha Diamond Platnumz bado hata namba hakijabatizwa nazo na ni kipya kabisa kama Waswahili wasemavyo zero kilomita.
Hivi wote mwajua hakuna siri dunia hii, na kama halipo lajongea, ukweli utajulikana tu…
Gari ya kifahari.
Gari ya kifahari.
Kwa sasa Diamond anatamba na kibao cha 'Mdogo mdogo'.  
Kwa sasa Diamond anatamba na kibao cha ‘Mdogo mdogo’. Picha na Taarifa News

MAJERUHI WA MOTO WA PETROLI MBAGALA WALIOLAZWA MUHIMBILI



 



Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa wodini.



MAJERUHI 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.

Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.

Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).

Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.

(Picha/Habari na Haruni Sanchawa/GPL)

Thursday, 16 October 2014

UDAKUZZ::SIRI NZITO ZAFICHUKA TRAFIKI WA MAHABA

Na Ojuku Abraham
BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Askari aliyefukuzwa kazi kutokana na kosa la ukiukaji wa maadili, Veronica Mdeme.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazoleta umeme nchini kutoka Uganda.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.
Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.
Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia  na kuwa nipe nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai chanzo hicho.
Veronica Mdeme akiwa kwenye pozi.
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.
Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
“Wakiwa katika vituo hivyo tofauti, Linga alitulia kwa muda mchache tu kabla ya kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa Veronica ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya pili, akina Mpaji wakaamua kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile suala lao lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vilivyoamua kuripoti.
Veronica Mdeme alipokuwa akidendeka na askari mwenzie.
“Picha hiyo ilipoonekana mtandaoni, moja kwa moja polisi walijua imewekwa na Linga kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine aliyefahamu kuhusu picha hiyo. Ndiyo maana wote watatu walifukuzwa kazi siku moja, hawakuwa na sababu ya kuhangaika kujua nani kaweka,” kilisema chanzo hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha ukurasa wa mbele).
Kwa mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
“Ni kama walivyoimba wale watoto wa Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye kidonda siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto mashalaah,” ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi, Amani lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu Mwaibambe.

MAAJABU::Miss Tz 2014 ni ajuza?

MISS TZ AVULIWE TAJI
Haya wamempa taji kwa kujuana na baba yake. Sasa tunaomjua na ambao tumesoma nae sekondari  tumewaletea proof kuwa ni mkubwa.



na hakuruhusiwa kushiriki miss tz. Ana Miaka 25 kuelekea 26. Records zake zote za marekani zinaonyesha ana miaka 25 sasa imekuwaje kurudi Tanznaia kawa na miaka 18.

Huyu miss anatakiwa kuvuliwa taji mara moja na mshindi wa pili apewe hilo taji. wajue kuwa huu ushahidi tunautuma mpaka kwa kamati ya MISS WORLD wasitufanye wajinga. Huyu dada tumemaliza nae  form 6 2007 hivi anakuwaje na miaka 18 leo hii? okay hata angesema ana miaka 22 ambayo ni limit ya kushiriki miss TZ still ni uongo na ushuzi mtupu. Na uzuri huku marekani kila kitu kinabaki online na ndio vinamuumbua.Na records zake za chuo kikuu hapa marekani pia zinasema she is turning 26. vichwa wa jamii forums wamempigia hesabu ya age yake na elimu yake na matokeo ndo haya18yrs of ageMinus 2yrs masters 3yrs bachelor = 13yrs of ageMinus 6yrs secondary education = 7yrs of ageMinus 7yrs primary education = 0yrs of ageMinus 2yrs nursery school = -2yrs of ageMinus 3yrs ya kugrow at hom kabla ya nursery xcul = -5 yrs of ageSo ur friend jus conjured a new miracle,, alianza kusoma 5yrs kabla hajazaliwaHuyo ni Miss Tz wetuuu…Bado tu wanamwandama miss tzkwa maana hiyo huyu mwenzetu yeye alianza shule 5 yrs kabla hajazaliwa.Lundenga miss wako kakiuka masharti ushahidi huo hapo juu. Lakini kwa vile umeshakula pesa za Mtemvu utajidai sio kweli. Basi tunaomba uonyeshe kuwa sio kweli kwa kutoa passport ya huyu binti hadharani. Hapana hatutaki passport mpya iliyotengenzwa mwaka huu.Tunaomba passport yake aliyoingia nayo marekani iwekwe hadharani. Hapo hapo tutaomba na records zake za DMV huku marekani ziwekwe hadharani.Huko miss world mnaenda kujiaibisha tu mwaka tu mwaka huu, tumeshawastua.All in all Lundenga tunaomba utoe tamko rasmi kuhusu hili na utuonyeshe Passport ya siti aliokuwa anaitumia marekani. Hatutaki kuona passport mpya all peoples knows in Tanzania you can make passport in any age you need.MEDIA HOUSE TUNAOMBA MTOE SUPPORT KWA HILI. MKIMBIZENI LUNDENGA HADI TOILET MPAKA AONYESHE OLD PASSPORT YA SITTI WASITUFANYE WATANZANIA WAJINGA NAMNA HIYO. WANASIASA WATUTAPELI ,LUNDENGA NAE ATUTAPELI HAIWEZEKANI.YEYE SI ALIDAI SITI HAKUPENDELEWA HAYA SASA AMEKIUKA MASHARTI AMVUE TAJI. HAPO ATASEMA NINI TENA?MWEEEEEH, HILI BALAA SASA. HUKO INSTA SASA WASHARUSHA HII. JAMII FORUMS NDO WAMETOA NA CALCULATOR ZAO KABISA WANAPIGA HESABU….HAHAHAHAH
Source: www.u-turn.co.tz

MAREKANI::Facebook kuwahifadhia wanawake mayai ya uzazi

Je ni sawa kwa kampuni hizi za kitekonoljia kuwa na sera kama hii?
Wanawake wanaofanya kazi na kampuni za Facebook na Apple wanapewa nafasi ya kipekee katika kazi yao:Wanapewa fursa ya kugandisha Mayai yao ya uzazi hadi watakapokuwa tayari kushika mimba.
Facebook imekuwa ikitoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wanawake nchini Marekani tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Sera hii inalenga kuwavutia wanawake kufanya kazi na Facebook na pia kwa Facebook kupata wafanyakazi wazuri wenye kipaji na kuwasaidia kuchagua kati ya kazi na uzazi.
Nayo kampuni ya Apple inajiandaa kuanzisha sera hii ifikapo Januari mwaka 2015.
"tunaendelea kuwapa faida nyingi wanawake , kwa kuwaongeza muda wa kupumzika baada ya kujifungua, pamoja na kuhifadhi mayai yao kama sehemu ya mpango wa kuwasaidia baadaye ikiwa watakosa kushika mimba, '' ilisema taarifa ya kampuni ya Apple.
Kampuni hizo mbili, zinatoa hadi dola elfu 20 kwa wafanyakazi wanawake kuhifadhi mayai yao na kuyangadisha wakitarajia kuyatumia wakati watakapokuwa tayari kuzaa au ikiwa watapwa na tatizo la kushika mimba basi wataweza kuyatumia.
Kuna ushindani mkubwa sana katika kuwaajiri wafanyakazi wenye talanta na kipawa pamoja na tajriba ya kazi na kampuni hizi pia zinataka kupata wafanyakazi bora wenye uzoefu wa kazi na watakaofanya kazi na kampuni hizo kwa mda mrefu.
Baadhi ya wadadisi wanasema jambo la kuhifadhi Mayai ya wanawake, linawapa uwezo zaidi wa kudhibiti kizazi hata hivyo kampuni hizi zinapaswa kuwa tayari kuwasaidia wanawake wanaoamua kupata watoto wakiwa wanafanya kazi badala ya kufanya jambo hili.
Tayari sera hii imekosolewa baadhi ya wanwake wakisema kampuni hizi zinajali zaidi faida badala ya kuabdilisha mazingira ya kazi na kufanya mambo kuwa mepesi kwa wanawake wanaofanya kazi nao.
Kwa kuwa wanawake wengine huwa hawako tayari kushika mimba, kwa sababu labda ya maujukumu ya kikazi na kazi nyingi, wao hauamua kuhifadhi mayao ya o kwa mnjia ya kisayansi na kuyatumia baadaye watakapokuwa tayari.

DAWA YA NGUVU ZA KIUME::Kahawa ya kipekee kwa ngono


Kahawa ni kinywaji kinachoenziwa na watu wengi
Ama kwa hakika duniani kuna mambo! wachuuzi wa kahawa yenye vijimambo ndani yake,ambayo ukiinywa tu basi inakupa mzuka wa kufanya ngono kwa kiwango cha hali ya juu na biashara inawaendea vyema katika mitaa ya Harare nchini Zimbabwe.
Kahawa hiyo huuzwa kati ya dola za kimarekani 3 hadi 5 kwa kifuko kidogo kinachotosha kikombe kimoja cha chai, na bei hiyo itategemea jinsi wewe ulivyo mtaalamu wa kuomba punguzo la bei inaweza kushuka.
Wachuuzi hao wa mitaa ya Harare wamezungumza na kudai kuwa kahawa hiyo huwasaidia wanaume kupata hamu ya kufanya ngono kwa muda mrefu Zaidi,lakini pia humchelewesha mwanaume kupata mshindo kwa muujibu wa utafiti wao.
Pindi tu uinunuapo kahawa hiyo,wachuuzi hao hukupa maelekezo kuwa uinywe dakika 15 kabla ya tukio lenyewe na humpa nguvu mtumiaji ya kufanya ngono kwa saa sabini na mbili,ingawa madai hayo hayajathibitishwa kitabibu.
 
Wanaume wengi inaarifiwa wamechangamkia sana kahawa hio yenye vijimambo
Wachuuzi hao wameamua kufanya biashara yao katika mtindo wa aina yake,kwa kuiuza kahawa hiyo katika maeneo maarufu nchini Zimbabwe yenye mikusanyiko ya watu kama eneo la KwaMereki kwenye viunga vya bustani ya kitongoji cha Warren, Zindoga eneo lililoko kwenye maporomoko ya maji (Waterfalls) na eneo la vilima la KuHuku .
Kitu cha kuvutia biashara hiyo hufanywa na wachuuzi wa kike wafanyao kazi katika duka kubwa la Fife Avenue Shopping centre wenye kutoa ushuhuda na kukubali kuwa waume zao waliitumia kahawa hiyo na wakayaona matokeo yake nao wakafaidi kwani uwezo wao uliongezeka maradufu.
Ingawa wanawake hao pamoja na kukubali na kutoa ushuhuda huo, bado hawako tayari kuelezea wapi wanakozinunua kahawa hizo za majamboz na kwa sasa mjini Harare mahitaji ya kahawa hiyo ni makubwa mno na ni rahisi kuitumia kwani unaweza kuitumia kwa maji moto ama baridi anaeleza muuzaji aliyejitaja kwa jina moja la Anna.
Anna anasema wateja wake wakubwa ni waume kwa wake ingawa wanawake wana aibu kuinunua kahawa hiyo hadharani kuliko wanaume wao hawana aibu pindi wanapotaka kahawa hiyo kwa matokeo mazuri ya kulinda heshima shughulini.
Kwa muujibu wa daktari mmoja nchini Zimbabwe aliyekataa kutajwa jina lake amesema kwamba tatizo la nguvu za kiume nchini Zimbabwe ni kubwa mno kwa wanaume walio wengi na linakua siku hadi siku na kusema ni tatizo kubwa.

DODOMA::NEC:HATUNA TIME KUJADILI UKAWA



Na Joyce Kasiki,Dodoma

CHAMA cha Mapinduzi kimesema hakina muda wa kujadili watu waliokataa ama kukubali mchakato wa Katiba mpya katika Bunge Maalum la Katiba.

Kauli hiyo imetolewa  leo  na Katibu w itikadi na Uenezi wa Chama hicho Naoe Nnauye wakati akizungumza na waandishi kuhusiana na vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM vinavyoendelea mjini hapa.

Alisema chama hakina sababu ya kufanya hivyo keani lengo lilikuwa ji kuoatikaana kwa katiba na tayari imepatikana.

Alisema eanaofai  kwamba vikao hivyo vitajadili  watu waliokuwa wakitaka mchakato usitishwe wana uwezo mdogo wa kufikiri.

"Sisi hatuwezi kujadili watu,keani hakuna msingi wala tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla,sisi tunajadili hoja.

"Hakuna muda wa kujadili watu ,sisi tunajadili   hoja,chama hakina muda wa kujadili watu,bali kinatakiwa kujafili ni tulipotoka,tulipo na tunapikwenda,kujadili watu hakusaidii   nchi ,chama wala mchakato wenyewe wa katiba." alisema Nape

Alisema ,wanaogukiri vika hivyo vya juu vy achama hicho vitajadili watu, wanatumia akili ndogo kufikiri,ili mradi mchakato ulifanyika vizuri na katiba imepatikana  kwa nini tujadili  watu,hoja za msingi ni kujadili mambo ya kulijenga  taifa letu

"Kujadili watu hata sisi akili yetu itakuwa siyo nzuri sana, sula la nani alikataa na nani alikubali hiyo haina msingi kwa sasa." alisema Nape

Pia alisema kikao cha Kamati kuu kilichofanyika juzi kimefanya uteuzi Wa  makatibu wa wilaya 27  wa CCM.


Kuhusiana na ucahguzi wa serikali za mitaa,alisema pia chama hicho kumejipanga kuhakikisha kinashinda kea kishindo.

IRINGA::Akamatwa na bangi katika bakuri


Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Iringa kwa makosa
tofauti tofauti likiwemo la Rahedy Josephat (23) mkazi wa Ipogoro
kukutwa akiwa na bhangi kete 43.


Akizungumza ofisini kwake,
Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 13 Oktoba majira ya
saa 12 za jioni maeneo ya kata ya Ruaha.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa amezihifadhi kete hizo
katika bakuli la kuwekea chakula.

Tukio lingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la John Bosco alikutwa
akiwa na silaha aina ya shotgun yenye namba za usajili 66721 na risasi
zake 10 akizimiliki bila kibali.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo ambaye alikamatiwa maeneo ya kijiji cha
Mmbweleli kilichopo kata ya Migoli wilaya ya Iringa Vijijini pamoja na
kukamatwa na hivyo vitu pia alikutwa akiwa na nyama ya swala kilo nne.

Mbali na matukio hayo, kamanda alisema watu wasiofahamika walimvamia
Happy Ingasi (36) ambaye ni mfanyabiashara na kumnyang’anya fedha
taslimu shilingi Milioni 2.5, simu aia ya tecno pamoja na vocha
mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 3.5 baada ya kumshambulia
na panga.

Tukio hilo lilitokea tarehe 13 Oktoba majira ya saa 2 za usiku huko
maeneo ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambapo watuhumiwa bado
wanatafutwa na Jeshi la polisi.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIODAIMA.CO.TZ IRINGA

MAAJABU::ANGALIA PICHA MWANAMAMA MWENYE MATUKIO YA AJABU


 Kwa jina unaweza muita Leilani Franco(Backbend)  ana uraia wa nchi mbili (Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi umbali wa 20m  katika muda wadk  10.05  katika  tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, tarehe 11 Machi 2013.

  Backbend binadamu ambaye ana uwezo wa kutembealea mikono na miguu kwa umbali mrefu.
 Pia kama inavyodhaniwa kwa kawaida Mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine,

 lakini kwa mwanamke huyu imekuwa ni tofauti kabisa, Mwanamke huyu ana uwezo wa kutumia miguu yake  katika shughuli zake binafsi kama Kula na kadhalika.....
 Hatimaye, Leilani pia anashikilia rekodi ya Dunia kutokana na uwezo wake katika kuuzungusha  Mwili wake.

Wednesday, 15 October 2014

USHAURI WA NDOA::MAUMIVU UNAPOFANYA TENDO LA NDOA (DYSPAREUNIA)

Tatizo hili huwasumbua baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, yaani kuanzia miaka 18 hadi 40. Tatizo huweza kuanza ghafla au taratibu pale mwanamke anapofanya tendo.
Maumivu haya hutokana na hali ya mabadiliko ukeni ambapo uke huwa mkavu daima au mwanamke anapata vipindi vya ukavu ukeni na katika mlango wa kizazi pia husababisha tatizo hili.
Maumivu yanaweza kuwa ndani ya kizazi, yaani wakati wa tendo unahisi kuna kitu kinasukumwa na ukahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kiuno wakati wa tendo.
Maumivu pia yanaweza kutokea baada ya tendo la ndoa, mwanamke akafanya tendo la ndoa vizuri lakini anapomaliza tu akijigeuza anahisi maumivu chini ya kitovu na kiuno na wakati mwingine hata kichefuchefu.
Chanzo cha tatizo
Tumeona vyanzo vitatu vya maumivu wakati wa tendo ambavyo ni ukavu ukeni. Huu unatokana na maandalizi hafifu kabla ya tendo. Endapo hakuna maandalizi yoyote basi uke unakuwa mkavu na unashindwa kufanya tendo au linafanyika kwa nguvu.
Ukavu unaweza kusababishwa na kutokuwa na hamu ya tendo au kutojisikia kufanya tendo, hili linaweza kusababishwa na matatizo ya kisaikolojia au katika mfumo wa homoni.
Michubuko ukeni na katika mdomo wa kizazi husababishwa na maambukizi, kansa au kufanya tendo la ndoa kwa nguvu bila maandalizi au ubakaji.
Maambukizi ukeni huambatana na kutokwa na uchafu wenye harufu na muwasho. Maambukizi yanaweza kusababishwa na fangasi, bakteria na magonjwa ya zinaa.
Maumivu ya ndani hutokana na maambukizi katika viungo vya uzazi mfano, ndani ya kizazi, mirija na vifuko vya mayai.
Maambukizi haya huanzia ukeni na kusambaa hadi ndani ya kizazi, lakini pia yanaweza kuanzia kwa ndani hasa baada ya kuharibika au kutoa mimba.
Dalili za tatizo
Maumivu wakati wa tendo la ndoa yanaweza kuanza mara tu tendo linapoanza, au tendo linapoendelea. Vilevile maumivu yanaweza kutokea baada ya tendo kumalizika.
Mwanaume pia anaweza kupata maumivu wakati wa tendo au baada ya tendo kutokana na michubuko katika uume, matatizo katika misuli ya uume, maambukizi ndani ya njia ya mkojo na matatizo ya korodani.
Maumivu ya kiuno kwa wanaume na wanawake pia ni mojawapo ya tatizo kubwa.
Uchunguzi
Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa huchunguzwa hospitali ambapo vipimo mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa. Vipimo vya kuangalia ukeni, damu, mkojo na Ultrasound hufanyika kutegemea na ukubwa wa tatizo.
Ushauri
Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi wa kina na tiba. Tatizo likiwa sugu yaani kukusumbua mara kwa mara husababisha upotevu wa hamu na raha ya tendo.
Kwa mwanaume hata uwezo wa kufanya tendo la ndoa hupotea. Waone madaktari katika hospitali ya mkoa na wilaya kwa uchunguzi na tiba.

SAIASA::Kinana awaasa makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa


 
Joyce Kasiki, Dodoma

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Abdulrahaman Kinana amewaomba  makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa nchini kufanya maandalizi mazuri kwa kuteua wagombea wazuri wanaokubalika,wanaopendwa na wanaoheshimika  katika jamii ili chama kiweze kushinda kwa kishindo katika chaguzi zijazo.

Kinana  alisema  hayo  mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku ya moja ya sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na makatibu hao.

Alisema kuwa, tukishinda vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa watakuwa wamejenga msingi mzuri kwa ajili ya uchaguzi mwaka ujao ambapo ushindi huo huo utasaidia ushindi mwingine mkubwa zaidi wa madiwani,wabunge na rais mwaka ujao.

Vile vile alisema ,  yeye binafsi anaamini mwaka ujao pia ushindi ni kwa CCM kutokana na kazi nzuri inayofanywa na watendaji na viongozi wa chama na kuwaomba kujtahidi kadri ya uwezo wao kuongeza juhudi maarifa na ufanisi.

Kinana alisema   kuwa mwaka 2009 katika uchaguzi wa seriklai za mitaa ushindi wa CCM ulikuwa ni kwa asilimia 96 ambapo asilimia 4 zilizobaki waligawana vyama vya upinzani kama sehemu ya wao kupumulia hivyo anaamini hawatapata asilimia zaidi ya hizo walizopata.

Akielezea kuhusu ziara zake anazozifanya katika mikoa mbalimbali hapa nchini amesema ameridhishwa na maandalizi yaliyopo mikoani na wilayani hivyo hana sababu ya kutokuwa na imani kwamba ushindi kwa CCM utakuwa mkubwa sana.

Amesema mpaka sasa imebaki mikoa 8 ambapo mpaka mwezi februari mwakani atakuwa amemaliza mikoa yote nchini lengo likiwa ni kuimarisha chama, kusukuma,kusimamia, kuhimiza utekelezaji wa ilani na  ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

UREMBO::USHINDI MTOTO WA MBUNGE, MISS TANZANIA YATIKISIKA

Stori:  Erick Evarist na Musa Mateja
OHOOOOH! Siku chache baada ya mtoto wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Sitti kujinyakulia U-Miss Tanzania 2014, tayari joto la ushindi huo limetikisa taji hilo na kuibua maswali ‘chungu mbovu’ kuhoji uhalali wa ushindi huo, Risasi Mchanganyiko linashuka na mchongo kamili.
Miss Tanzania Sitti Mtemvu akiwa mwenye nyuso ya furaha baada ya kushinda taji hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, vuguvugu za uhalali wa ushindi ziliibuka muda mchache kabla ya shindano hilo kuchukua nafasi katika Ukumbi wa Mlimani City, Ijumaa iliyopita ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji kulikoni wafuasi wa mrembo huyo waingie na vipeperushi vingi vyenye picha ya mshindi (Sitti).
“Tatizo lilianzia kwa watu wengi kuingia na vibendera vyenye picha ya Sitti vikionyesha dhahiri kwamba walijua kabla kwamba ni mshindi hivyo kuja wakiwa wamejipanga kabisa,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema hata katika suala zima la mshindi kuandaliwa gari maalum la Hammer ambalo baadaye lilimchukua na kumrudisha kivyake tofauti na washiriki wengine ambao waliondoka ukumbini hapo na basi waliloandaliwa.
Miss Tanzania aliyemaliza muda wake,Happiness Watimanywa akimvika Crown na Taji Miss Tanzania Sitti Mtemvu.
“Waandaaji wanapaswa kutueleza vizuri, haiwezekani watu waandae Hammer waje nalo ukumbini pasipo kuwa na uhakika wa ushindi, ule ni utani,” kilinyetisha chanzo hicho.
Aidha, vuguvugu hilo lilijiongeza zaidi baada ya watu kudai huenda ushindi huo ulitokana na mgongo wa baba yake (mbunge wa Temeke) madai ambayo kwa pamoja yalikanushwa na muandaji wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga.
“Hakuna kitu kama hicho, malalamiko kila siku hayakosekani, vipeperushi havikatazwi, majaji sita kati ya tisa waliwekwa na wadhamini (TBL kupitia kinywaji chao cha Red’s), haiwezekani akawahonga majaji wote hao.
“Kuhusu gari, hakuondoka ukumbini na Hammer, aliondoka na basi kama washiriki wengine, sijui hayo maneno yanatoka wapi,” alisema Lundenga.
Kwenye shindano hilo, Sitti aliwagaragaza washiriki wenzake 29 na kuondoka na kitita cha shilingi milioni 18. Mrembo huyo ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia (Miss World) hapo baadaye.

MBEYA::MWANAMKE AUAWA KWA KUSHINDWA KULIPA T.SH,3,000/=



Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.
 
WAKATI wajumbe maalum wa katiba wakiwa wamependekeza suala la haki za binadamu na mgawanyo sawa wa madaraka kati ya mwanamke na mwanaume, vitendo vya ukatili na mauaji kwa wanawake vimezidi kushika kasi mkoani Mbeya.

Katika tukio la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa kwa jina la Rutina Ng’ekele(75), mkazi wa kijiji cha Mabondeni, kata ya Bulyaga, tarafa ya Tukuyu mjini wilayani Rungwe, amefariki dunia katika hospitali ya Makandana wilayani Rungwe, akiwa anapatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa mateke na ngumi.

Taarifa zinasema kuwa, Bibi huyo alishambuliwa vikali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu aliyefahamika kwa jina la Nicolous Afyasisye.

Tukio hilo limeelezwa kutokea Octoba 4, mwaka huu, majira ya saa moja usiku na kupelekea marehemu kulazwa hospitalini hapo mpka mauti yalipomfika jana Octoba 14, mwaka huu, saa sita mchana.

Chanzo cha tukio hilo, kimeelezwa kuwa ni marehemu kumlipa mtuhumiwa Tsh.7,000/= badala ya Tsh.10,000/= aliyokuwa akidaiwa na mtuhumiwa, jambo ambalo lilisababisha mtuhumiwa aanze kumshambulia marehemu.

Baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana na Jeshi la polisi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisimkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema kuwa anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahala alipo mtuhumiwa wa tukio hilo, azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
 

TETESI>>AUNT: NILIONANA NA NYALANDU UKUMBINI

Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel .
Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo.
“Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo.

MUZIKI NA SHOW::DIAMOND AIBU NYINGINE DODOMA!

Stori: Richard Bukos, Dodoma
KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.
Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.
AIBU YENYEWE
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiendelea na shoo.
MAFUNDI MITAMBO WAHAHA
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.
Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.
Mafundi mitambo wakirekebisha nyaya ili shoo iendelee.
WEMA ATAKIWA
Katika zomeazomea ya safari hii,  mashabiki walikwenda mbele zaidi wakimtaka Wema apande jukwaani  kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.
Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.
MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.
Mashabiki wakisubiri shoo ilipobuma.
Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.
“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka betri mpya kwenye maiki?
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akisubiriri mitambo ikae sawa.
DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila mara huku maiki nazo zikikoroma.
“Braza huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye vigodoro lakini siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu wameingia kwa bei mbaya, ni kuwaibia watu.
“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akirejea kuendelea na shoo.
INTAVYUU FUPI
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo. alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana ni Diamond.
UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31, mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani.
Nchini Uingereza nako, Septemba 20, mwaka huu, Diamond alijikuta ndani ya aibu kubwa kwa mashabiki wake kufuatia mwandaaji kuingia mitini katika ukumbi wa LafACE club jijini Londan licha ya mashabiki kujaa.
KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana.
Nuhu Mziwanda na bebi wake Shilole wakitoa sapoti katika shoo ya Diamond.
Kwa kawaida, msanii anapokwenda kupiga shoo mahali, kuna utaratibu unaoitwa kwa Kiingereza kama Technical Rider ambapo wasimamizi wake, akiwemo meneja huenda kuukagua ukumbi, usalama, muziki wenye viwango na hata steji shoo ilivyo.
Kama mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo. Lakini mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa makubaliano.Meneja wa Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili kuulizwa kwa nini hakuwepo Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki na maandalizi mengine, hakupatikana hewani!

IRINGA::MKE wa mtu sumu , kikongwe afanya mauaji ya kihistoria Iringa

 Picha namba 01 Wananchi  wakiwasikiliza  mke  wa mtuhumiwa wa mauaji Bi  Melea Mtwanga akiwa na mtoto  wake  Manet Mtalima ( kushoto)  wakati  wakizungumza na mwandishi  wetu (hayupo pichani) nje ya eneo la tukio.
Mke  wa mtuhumiwa wa mauaji Bi  Melea Mtwanga akiwa na mtoto  wake  Manet Mtalima.
 


  Picha namba 02  mtuhumiwa wa mauaji Gwalino Ganga akiwa na mkewe  Melea  Mtwanga.


Na  Francis Godwin, Iringa
 
MKE ama mume  wa  mtu  ni  sumu si neno jipya  katika vinywa  vya wengi  japo baadhi yetu tumekuwa  tukichukulia juu juu neno ila kwa wakazi wa kijiji  cha Mbigili kata ya Mazombe wilaya ya Kilolo wameamini kuwa lina ukweli ndani yake baada ya kikongwe wa miaka 70 kumtwanga risasi mbili kijana ambae alimtuhumu kuingilia ndoa yake kwa  kuvunja amri ya sita na mama watoto wake.
 
Mbali ya kijana huyo Thadei Mbugu(40)ambae ni marehemu  kudaiwa kujihusisha kimapenzi na mke wa kikongwe huyo   Gwerino bado inaelezwa  kuwa chanzo cha mauti  yake alijisababishia  kutokana na maneo ya dharau ambayo  alikuwa akiyatoa mbele ya  watu  waliokuwa  wakinywa  pombe katika klabu cha pombe za  kienyeji kilichopo nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji ambacho kinaendeshwa na  mke wa mtuhumiwa  huyo wa mauwaji .
 
Imedaiwa  kuwa awali  mtuhumiwa huyo wa mauwaji alikuwa akimsaka mgoni  ama  dowezi  wake  ambae  amekuwa akiivuruga  ndoa yake bila  mafanikio  japo alikuwa na taarifa  kuwa  vijana  watoto  kijijini hapo  ndio  wanajihusisha kimapenzi  na mke  wake  huyo.
 
Akizungumza na mwandishi  wa  habari hizi  aliyefika  eneo la  tukio mke  wa  Maneti Mtalimbo (24) ambae ni  mtoto  wa kambo mtuhumiwa wa mauwaji hayo  alisema  kuwa chanzo  cha mauwaji hayo ni mke  wa marehemu kumtuhumu mama  yake  kuwa huwa na tabia ya  kukopa fedha kwa marehemu hali  iliyopelekea mama  yake  huyo  kwenda kumwita baba yake (mtuhumiwa) na kumshitakia maneno  hayo.
 
Baada ya  kufikishiwa malalamiko hayo mzee mtuhumiwa wa mauwaji  alifika  ndani ya klabu hicho na kuanza  kumuuliza marehemu  juu ya mahusiano  yake na mke  wake ndipo marehemu  alipoanza  kutoa  lugha chafu  mbele ya watu  kwa mwenye mke  kuwa ni masikini hana  uwezo wa  kutunza  wake wake  wawili hivyo anasaidia  kulea.
 
Alisema  kuwa  kufuatia madai hayo na majibu ya marehemu  kikongwe  huyo mtuhumiwa wa mauwaji alimtaka marehemu  kuondoka na katika  eneo hilo na mke wake mtuhumiwa kwa madai  kuwa wamependana  waende  wakaishi  wote ila marehemu aligoma na  kuendelea  kutoa  lugha chafu.
 
“Baba  alimtaka aondoke na mama kwa  kuwa  wamependana ila marehemu  alisikika akisema  siondoki  utanifanya  nini wewe  mzee  na baada ya  hapo akaanza  kumtukama  baba matusi kuwa   wewe ni masikini umeuza  ng’ombe nab ado  unaishi katika  vibanda ….baada ya  hapo  mimi nilitoka  kwenda  kutafuta msaada  wa watu kuja  kuamua  ugomvi  huo kwa kumtoa marehemu huyo ghafla  nyuma  nilisikia mlio  wa  risasi na baada ya  kurudi nilikutana na marehemu  huyo akitoka  nje  huku akivuja damu baada ya  kupigwa  risasi begani kushoto “
 
Alisema  baada ya  hapo  alilazimika  kuingia ndani na  kumuuliza baba yake  kulikoni  ila  kabla ya  kumuuliza  hivyo  Mbugu akiwa amelala  nje bila msaada .
 
“ Kweli  nilitoka  mbio kwenda  kutafuta  msaada wa gari  kwa  Besti  ili  sikumkuta  ila wakati najiandaa  kurudi baba alikwenda kumuongeza  risasi nyingine ya  kifuani na kumuua kabisa “
 
Hata  hivyo  baada ya  kumuua kabisa  ndipo alianza  kumfukuza mama yake mzazi akitaka  kumpiga  risasi kabla ya  kumfukuza na kumpokonya bunduki  hiyo na  wananchi  kusogea na kumtia nguvuni.
 
Huku mke  wa  mtuhumiwa  huyo  wa mauwaji Bi  Melea Mtwanga  akidai  kuwa hajapata  kuwa na mahusiano  yeyote na marehemu  huyo  isipo  kuwa marehemu aliuwawa kwa ajili ya  lugha zake  chafu .
 
“Marehemu  alikuwa akinidai pesa za mahindi  debe  kumi na  wakati akinidai ghafla  mume  wangu  alitoke na  kuuliza kwanini unaongea na mke  wangu na kusema  sasa  leo nakumaliza ndipo alipompiga  rusasi huku akiwa amekaa katika  benji  akinywa pombe na  wenzake …..kweli  watu  walikimbia wote japo  mimi  sikuwa na mahusiano yoyote na marehemu zaidi ya kunidai pesa za mahindi “
 
Alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo na maehemu  wote  walikuwa  wanamiliki wake  wawili  kila mmoja na kuwa  hakuona  sababu ya kufanyiana unyama  huo.
 
Mmoja kati ya  wajane  wa marehemu  huyo  Bi Gloria  Ngailo  alisema  kuwa  wakati mauwaji  hayo yakitokea  alikuwa eneo la  tukio  pamoja na mke  mwenzake ila  yeye  kwa  wakati huo alikuwa ametoka  nje ya chumba hicho kabla ya  kusikia mlio  wa  risasi na kusogea kukuta mume  wake akivuja  damu.
 
“ Siwezi  kujua kama ni kweli  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtuhumiwa  japo tunaishi  jirani na mtuhumiwa  huyo ila ni kazi ya  nguvu ndie anayejua siri  iliyopo juu ya  tukio hilo”
 
Baba  mzazi wa marehemu  huyo  Antony  Mbungu alisema  kuwa haamini kama  mtoto  wake amekufa  na  kuwa hata kama alikuwa akimtuhumu  kutembea na mke wake  hukumu yake  haikuwa ni kifo .
 
Kwa  upenda  wao  mashuhuda wa  tukio hilo  walisema  kuwa wakati  linatokea  tukio  hilo  walikuwa ndani ya  chumba  hicho na kati yao  walikuwepo  vijana  wawili ambao  walikuwa  wakituhumiwa  pamoja na marehemu  kujihusisha na mapenzi na mke wa mtuhumiwa ambao baada ya  kuona mwenzao kapigwa  risasi walikimbia porini pamoja na walevi wengine   eneo hilo.
 
Mwenyekiti  wa  serikali ya  kijiji   hicho Bw  Chesco Lukosi  alisema  kuwa tukio hilo  limeacha  fundisho kubwa  kijijini hapo na kuwa ni  tukio la kwanza  kutokea kwa mtu  kuuwawa  kinyama  kiasi hicho.
 
Pia  alisema  iwapo  marehemu  asingekuwa na lugha  chafu  yawezekana  mauti  yasingemkuta ila kwa kawaida  wahehe  huwa  hawapendi kutukanwa  mbele ya wake  zao .
 
Alisema mauwaji hayo hayana tofauti mauwaji ya  aliyekuwa  mkuu wa mkoa  wa Iringa marehemu  Dr Kreluu aliyeuwawa miaka 40  iliyopita na mkulima Said Mwamwindi ambae  alimuua kwa mkuu  wa mkoa wa kumpiga  risasi na mwili  wake  kuupeleka polisi mwenyewe kabla ya  kukamatwa na kuhukumiwa  kifo .
 
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi amethibitisha  kutokea kwa  tukio hilo lililotokea Oktoba 9 majira ya saa moja za na  kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na  jeshi la polisi huku akidai  kuwa  bunduki  hiyo aina ya shotgun alikuwa akiimiliki kihalali .