Sunday, 24 August 2014

MSIBA:MASHABIKI WAMUUA MCHEZAJI ALGERIA..

MASHABIKI WAMUUA MCHEZAJI ALGERIA

MCHEZAJI kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya Ligi ya Algeria.
Albert Ebosse enzi za uhai wake.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyefunga mabao mengi katika Ligi ya Algeria msimu uliopita.
Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.

Marehemu ndiye aliyefunga bao hilo pekee kwa timu yake.
Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe kuhusiana na kifo hicho.

JE,HAO NI WALEVI AU ?MPAKA WAKAPOST HIYO PICHA

Sunday, August 24, 2014
 Picha ya Familia On Facebook;Vipi walilewa au ?

HABARI NA PICHA:VIPI MBUNGE WAKO YUPO KAMA HUYU???

Wananchi wa Kijiji cha Luvuyo Kata ya Madope wakimpokea Mbunge wao, Deo Filikunjombe kwa maandamano.
Wanachama wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi wa Kijiji cha Luvuyo kata ya Madope wakishirikiana jana na Deo Filikunjombe (kushoto) kuchimba mifereji ya maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe yenye urefu wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 50.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luvuyo mara baada ya  kuzindua ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe.
Deo Filikunjombe akisafirishwa katika mkokoteni wa kukokotwa na ng'ombe baada ya wananchi wa  Luvuyo ambao awali walitishia  kuhama  wilaya ya Ludewa kuhamia Njombe kusikilizwa kilio chao  cha ubovu wa  miundombinu kwa  kuanza kujengewa barabara na mbunge huyo

PICHA YA LEO:ALIKUWA ANAWAZA NINI HAPO FETTY?

SALIM ASAS SASA ANAFAA KUWA MBUNGE WA IRINGA MJINI,hutaki chechemea...

August 24, 2014

MWIGULU AMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA, MH. MWIGULU NCHEMBA AKIMSIMIKA KAMANDA WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM), MKOANI IRINGA SALIM ASAS, KATIKA VIWANJA VYA MWEMBETOGWA..
MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI IRINGA, TUMAINI MSOWOYA NA MWENYEKITI MWENZAKE WA MKOA WA KATAVI, WILLIAM MBOGO WAKIJADILI JAMBO WAKAZI WA ZOEZI LA KUMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM IRINGA SALIM ABRI
VIONGOZI WA UVCCM KUTOKA MIKOA MBALI MBALI WALIKUWEPO..ILIKUWA BURUDAAANI1...
MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI IRINGA TUMAINI MSOWOYA KIBIKI, MWENYEKITI WA UVCCM MKOANI KATAVI, WILLIAM MBONGO NA KATIBU WA UVCCM WILAYANI MUFINDI KANTALA, MAMBO YALIKUWA YAKIENDA SAWIA WAKATI KAMANDA ASAS AKIAPISHWA
KATIBU WA UWT MANISPAA YA IRINGA CHIKU MASANJA NA MNEC WA MBEYA JIJI WAKILI, SAMBWE SHITAMBALA NDANI YA VIWANJA VYA MWEMBETOGWA KUSHUHUDIA SALIM ASAS, KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA AKISIMIKWA RASMI 
MH MWIGULU NCHEMBA, NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA, AKISAINI KITABU CHA WAGENI KWENYE OFISI YA CCM MKOA WA IRINGA....KABLA YA KUANZA SHUGHULI RASMI...
KAMANDA ASAS AKIWA MAKINI KUSIKILIZA KINACHOJILI MKUTANONI
SAFARI NI SAFARI...TUNAENDA ENEO LA MKUTANO..WA KWANZA KUSHOTO; TULA TWEVE MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM MKOA WA IRINGA

PICHA ZOTE NA FRANK KIBIKI
KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA, SALIM ABRI  AMEAPISHWA RASMI KUANZA KAZI YAKE YA UKAMANDA IKIWA NI KIPINDI CHA TATU KUANZA KUTUMIKIA NAFASI HIYO.
 
VIJANA WANAMPENDA SALIM ASA KUTOKANA NA UTU WAKE, MAPENZI YAKE YA DHATI KWA CCM, UPENDO WAKE, USHAURI, UALIMU NA ULEZI WAKE USIOJALI ITIKADI, RANGI, DINI, KABILI, MASKINI WALA MATAJIRI..
UDUMU SALIMU ASASI.

UJASIRIAMALI UNAOLIPA AFRIKA NI SIASA:TUNDAMAN NAE ANATAKA UBUNGE

Tundaman: Iddi Azan Ananiandaa kuwa Mbunge, 'Napata Ushauri kwa Mheshimiwa Lowasa..'

Sunday, August 24, 2014
Tundaman ameweka wazi mpango wa kuingia rasmi katika siasa na kukitafuta kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu baada ya 2015.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Tundaman ameeleza kuwa alipata moyo na wazo la kugombea kiti cha ubunge kutoka kwa mbunge wa Kinondoni, mheshimiwa Iddi Azan.

“Rafiki yangu sana Iddi Azan, sometimes nikikaa nae sehemu wananchi wananishangilia mimi anasema ‘Tunda unapendwa hivi, basi na wewe uje kugombania mambo haya’. Nikasema basi sawa na hilo suala nalifanyia kazi, kwa hiyo mimi ntachukua details nyingi kutoka kwake na yeye ndiye anaeniandaa mimi kuwa mbunge baadae (sio 2015).” Amesema Tunda Man.

Ameeleza pia kuhusu jinsi anavyopata ushauri wa siasa kutoka kwa wanasiasa wakubwa akiwemo waziri mkuu wa zamani Mheshimiwa Edward Lowasa.

“Kwa sababu niko karibu sana na waheshimiwa wananishauri, kwa hiyo najua nini cha kufanya na nini nisifanye. Sometimes nakaa na Lowasa ananiambia vitu vingi mheshimiwa kwamba siasa iko hivi… kwa hiyo kuna vitu fulani mimi ninapata bila wao kujua napata kutoka kwao. Lengo baadae nitakapovifanya nisiwe nakosea, niwe straight katika kuvifanya ili nifanikiwe.”

CHRIS BROWN ANUSURIKA KIFO

CHRIS BROWN ANUSURIKA KIFO, SUGE KNIGHT AKIJERUHIWA KWA RISASI

Cris Brown akiwa Klabu 1OAK kabla ya vurugu kutokea.
 
Prodyuza mkongwe, Suge Knight amejeruhiwa tumboni na mkononi katika shambulio hilo.
MWIMBAJI Cris Brown amenusurika kuuawa katika shambulio la risasi ndani ya klabu ya usiku jijini Los Angeles ambapo prodyuza Suge Knight amejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika klabu ya usiku iitwayo 1OAK iliyopo magharibi mwa Hollywood wakati wa shoo iliyokuwa ikiongozwa na Cris Brown kabla ya zoezi la utoaji Tuzo za VMA ambapo watu watatu wamejeruhiwa mmoja akiwa mahututi.
Suge Knight alipigwa risasi mara mbili tumboni na mkononi na kukimbizwa hospitali ambapo anaendelea na matibabu.
Mastaa wengine waliokuwepo kwenye klabu hiyo wakati tukio hilo likitokea ni pamoja na Justin Bieber, rappa The Game, Pia Mia, Tyson Beckford, Robert Ri'chard  na wengineo.
Indaiwa mlengwa mkuu katika shambulio hilo alikuwa Cris Brown.

Saturday, 23 August 2014

DJ FETTY NDANI YA MAHABA NIUEEEE NA MUL B'

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’ na DJ Muli B, wamenaswa wakiwa kwenye pozi la mahaba huku tena wakiwa wamejisahau utadhani mume na mkewe.
 
Mtangazaji wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty' akiwa na 'DJ Muli B’.
Ishu hiyo ilitokea Agosti 17, Mwaka huu ndani ya Uwanja wa Kahama, ambapo walienda kwa ajili ya kutazama burudani za Serengeti Fiesta 2014 zilizokuwa zikifanyika siku hiyo.
Wakiwa nyuma ya jukwaa, wawili hao walionekana kubebana wakati wamekaa jambo lililowafanya baadhi ya wasanii waliokuwa nyuma yao kukonyezana na wengine kuulizana maswali ambayo hayakuwa na majibu kama ni wapenzi au laa.
 
‘DJ Fetty' na 'DJ Muli B’ wakila ujana.
Paparazi wetu apowauliza kama wana uhusiano wowote, wawili hao walikanusha na kusema wamepozi kama mtu na mfanyakazi mwenzake Clouds FM.

TCRA:YATOA ONYO REDIO YA WATU...

Clouds FM Yapewa Onyo na Kupigwa Fine Kwa Kukiuka Kanuni za Utangazaji

Udaku Specially on Saturday, August 23, 2014
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005. 

Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.

Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.

Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.

Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.

Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.

TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

habari na picha:OMMY D NA KIDOTI,VIPI WAMEPENDEZA?

USHAURI WA BUREEE

Mimi Binti wa Kitanga Niliyefundwa Mme Wangu Kwa Style Hizi Huwa Achepuki

Saturday, August 23, 2014
Admin Udaku Specially Kila siku nasikia vilio vya wanawake wakilia Waume zao wanachepuka kwa hilo naweza sema wanayataka wenyewe, natamani niwafunde siku moja kidogo mjue kuwa akili ya Mwanaume ni kama mtoto mdogo yaaani ni vitu vidogo sana unaweza ukawa unamfanyia mumeo na hata siku moja asifikirie kuchepuka , Mimi mme wangu akitoka kazini gia ya kwanza ni home na simlazimisha bali vijimambo vyangu vya uchokozi wa hapa na pale ndo vinamuwaisha, yaani namfanya mme wangu kama mtoto mdogo, kwa kupitia mavazi yangu na chakula nachompikia ni silaa moja wapo nayotumia ...Jamani Wanawake Wenzangu Amkeni ...Wacha Kulalamika
Consolata

Jux Afunguka:Kweli Jack Patrick Alikuwa ni Mpenzi Wangu

Jux Afunguka:Kweli Jack Patrick Alikuwa ni Mpenzi Wangu

Saturday, August 23, 2014
Na Musa Mateja
MALOVEE! Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.

Jux ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva, alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti Fiesta 2014.

Akijibu swali la mwandishi wetu lililomtaka afungukie penzi lake na Jack ambalo alikuwa akichengachenga kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari, Jux alianza kwa kukiri kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na walidumu kwa takriban miezi saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya kulevya.

Alisema tangu aanze kuyajua mapenzi, Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake ingawa wakati anapatwa matatizo walikuwa wametibuana kwa kipindi cha wiki mbili.

“Nilisikitika sana niliposikia amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama anafanya hiyo biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua yupo Bongo na nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.

Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema hana taarifa hizo.“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.

Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

USOME WARAKA WA MBUNGE GODBLESS LEMA..endeleaaaaa

Godbless Lema Amshushia Waraka Mzito Jakaya 'Heri Kuitwa Mpumbavu Kwa Ajili ya Haki Na Kweli'

Saturday, August 23, 2014

Mh Rais , bila shaka utakuwa unaifahamu vizuri historia ya Farao

Mh Rais nakusalimu .

Ni usiku wa manane wakati naanza kuandika waraka huu , nimetoka kuangalia historia ya maisha ya Dr Martin Luther Jr na nilipotaka kulala nilishindwa na nilipotafakari jambo jema la kufanya wakati huu nilipokosa usingizi ndipo wajibu huu muhimu wa kuandika waraka huu kwako ulipoanza .

Mh Rais , bila shaka utakuwa unaifahamu historia ya Farao na Wana wa Israel wakati Mungu alipotaka kuwatoa wana wa Israel utumwani Misri , kwa wale Wakristo wanaosoma Biblia wanajua kuwa , maandiko yanasema “ Na Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu ili apate kujitukuza mbele ya wana wa Israel . Mh Rais siwezi kuandika sana juu ya nini kilitokea kwa Farao na Watu wake ila nikuombe sana umuombe Mch G. Rwakatare hakueleze kwa ufasaha ili upate kujifunza jambo muhimu hapa .

Mh Rais , ukiona unafanya au unatenda hila au dhambi bila kipingamizi wala taabu , maana yake ni kuwa mauti kwako yamekaribia kwani mwizi aliyeambiwa kuwa siku zake ni arobaini kama angeacha uovu katika siku ya thelasini na nane pengine angeponywa na wito wa mauti…. Nchi hii haiko salama hata kidogo , hali ni tete sana na kwa bahati mbaya Watawala hamuoni kwani macho yenu yamepigwa upofu na shetani na ndipo andiko laGodbless Lema litatimia “ Na Mungu akaufanya Moyo wa Kikwete na ccm kuwa mgumu ili apate kuikomboa Tanzania “

Mh Rais sina mashaka na Uhuru wa kweli na wa pili wa Taifa ili katika siku chache zinazokuja ,, , hamtaweza kuzuia mabadiliko hata kama wanayoyataka sasa watakufa wote leo , ila kukosa hekima katika uongozi kunaweza kusabisha mabadiliko haya yakaja na hasara kubwa katika Jamii . Hata hivyo kiburi mlichonacho kinasababishwa na wajibu na mipango ya Mungu katika Nchi yetu .

Mh Rais , Watu wameendelea kuteseka kila kona , maisha ni magumu , mfumuko wa bei umepoteza thamani ya fedha , Wagonjwa mahosiptalini wanakufa kwani panadol imekuwa dawa ya kutibu maradhi yote, jela kumejaa masikini na wanyonge na Watu wanaokwepa kodi na kulibia Taifa wamekuwa marafiki wa watawala , ajira hakuna na vijana wamekata tamaa , dada zetu wamekuwa malaya wa kutafuta chakula cha siku na ada ya kuendelea na masomo .

Mh Rais , pamoja na rasilimali tele tulizonazo kama vile dhahabu , Tanzanite , Gesi , Almasi , Mbuga za Wanyama , Madini ya Urani , Mlima Kilimanjaro , Kahawa , Pamba , Korosho , Bandari , Mito na maziwa na vitu vingine vingi , bado vimeshindwa kutoa mwanga wa maendeleo katika Taifa hili .

Mh Rais , Tuko katika kipindi ambacho tunaandika Katiba ambayo wakati Wananchi wanatoa maoni walikuwa na matumaini makubwa . Mtafaruku uliopo sasa ni kati ya UKAWA na ccm , sio vita rahisi hata kidogo lakini Watu wajinga wanaweza kukushauri vibaya na ukafikiri unyenyekevu kwenye jambo hili ni kujidhalilisha , Wewe ni Rais , ukishindwa kutambua Mamlaka yako na nguvu zako katika kusimamia ukweli na haki basi Nchi itakuwa imepoteza dira . Mh Rais unapaswa kushuka na kuwa mnyenyekevu kwani dhamira njema yenye malengo mazuri haiwezi kumdhalilisha binadamu . Wasira . Lukuvi na Werema na wengine watakushauri nakukuambia ukilihairisha Bunge utawapa Kichwa UKAWA na Nchi itaenda Upinzani .

Mh Rais ukiitwa mpumbavu kwa ajili ya haki na kweli , upumbavu huo una maana kubwa kuliko kusifiwa na watu wanaopenda dhuluma na hila hata kama ni wengi , ninahisi changamoto unazopitia kama Rais na Mwenyekiti wa Chama , lakini Mtu Hodari na shujaa ni yule anayeshinda majaribu na taabu wakati usio muaafaka .Nakuomba ufanye maamuzi kwa ajili ya Watoto wa watoto wa Rizwan na Watanzania na sio Chama chako . Chama chako kitakuwepo leo na siku moja hakitakuwepo lakini Watoto na Wajukuu zako watakuwepo . Hivyo basi isaidie Tanzania kupata Katiba ambayo itampa binadamu yeyote haki , usawa na fursa katika Taifa lake.

Mh Rais , karibu kila mtu mwenye akili timamu amesema juu ya jambo hili hakuna atakaye kulazimisha lakini wakati ukifika wakati utakulazimisha , Polisi wetu na Jeshi halitaweza kushindana na kulishinda Jeshi linaloitwa WAKATI , hali itakuwa ni mbaya , Watoto wataitafuta Tanzania na kuikosa , ndipo watu wazima watasema tulikuwa wapi wakati misingi ikiharibika ? zitakuwa ni siku za taabu na uchungu na UKAWA hawatakuwepo tena ila WAKATI watakuwepo na hawatamsilikiza mtu yeyote , nyumba za kifahari na magari yanayokusanywa sasa kwa hila na wizi hayatakuwa makazi ya Watu isipokuwa popo na mende , Marekani , Uchina na Ulaya watawageuka watawaita wahalifu wa demokrasia na wauaji , watawatafuta ,watawakamata na Maisha yenu yatakuwa ya Uchungu mkubwa wakati Nchi haitakuwepo , mimi sio mtabiri kama marehemu Sheikh Yahaya , lakini najua kwamba ukiwa na mwanamke mjamzito ndani ya nyumba ni bora na ni muhimu ukaanza kuandaa vifaa muhimu vya mtoto kama nguo nk .

Mh Rais , sikutishi , ila Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho , najua watakuja wapambe hapa watakuambia umeona ujinga wa yule Mbunge wa Arusha ? watasema ameandika ujinga , watakebehi na kudharau kama kawaida yao . Hata mimi siandiki kutafuta sifa kwani mke wangu na watoto wangu wanatosha kunisifu na kila siku wanafanya hivyo asubuhi na jioni hasa pale ninapowaletea Ice Cream .

Mh Rais , nisikuchoshe sana , ila tafakari tena , natambua mara kwa mara huwa unakuja Arusha lakini sijawahi kuambiwa wala kutaarifiwa pengine ningekuambia haya mambo kwa mdomo na mara nyingi huwa nakutana na msafara wako barabarani na ndipo natambua kuwa huko Jimboni kwangu . Hata hivyo tunaendelea kupambana vizuri kujenga demokrasia ya kweli na Chama chako kinaendelea kudhoofika vizuri sana hapa Arusha na tunatarajia kumaliza uchaguzi Mkuu wa 2015 wa Jimbo letu hili mwaka huu mwezi wa kumi na mbili .

Mh Rais , naomba nitoke nje ya mada yangu muhimu kidogo , matukio ya Ugaidi na mauaji bado yanaendelea hapa Arusha , lakini sina taarifa za ndani sana kwani na siku nyingi kidogo sijatembelea matajiri wa Arusha ambao Rpc anawapa taarifa zaidi za matukio yanayotishia usalama wa Jimbo langu kuliko mimi Mbunge hata kama nikizihitaji kwa barua , ni jambo la kusikitisha lakini ni jaribu ambalo tumeweza kulisitahimili , nitajaribu kwenda kuwaona matajiri hawa siku chache zinazokuja ili nipate taarifa za hali ya usalama ya Jimbo langu na nitakuandikia waraka mwingine kukueleza ukweli , hata hivyo kuna watu waliokamatwa hivi sasa ila kwa vile sina taarifa za kutosha nina shindwa kujua vizuri kama watu ha ni wahalifu au la , isipokuwa ni na imani Mungu , Shetani na Polisi wa Arusha wanajua vizuri .

Mh Rais , nakushukuru na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu wakati unatafakari tena kuhusu mchakato wa Katiba , hata hivyo Watanzania wasiogope kwani “ Na Mungu akaufanya Moyo wa Kikwete na ccm kuwa mgumu ili apate kuikomboa Tanzania “

Godbless J Lema (MB)

KISIASA ZAIDI:HUU NDO MGOGORO WA UVCCM ARUSHA.

August 22, 2014

sakata la bifu ndani ya Uvccm Mkoa wa Arusha lachukua sura mpya

six1
 
Katibu mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda akiongea katika moja ya ziara yake Mkoani Arusha hivi karibuni  ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi kufanya Mkoani hapa
 
SAKATA la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha sasa kupatiwa muarubaini wake ambapo imedaiwa kuundwa timu maalumu itakayochunguza mgogoro huo  
 
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda ameeleza mtandao wa jamiiblog kuwa kutokana na kinachoendelea hivi sasa katika umoja wa vijana Mkoa wa Arusha kuwa tayari Makao makuu wameshatuma timu ya kuchunguza mgogoro huo
 
Alisema kuwa tayari timu hiyo imeshawasili jijini Arusha hivyo kuanza kazi rasmi kesho (leo)itakayopelekea kubaini ni nini hasa chanzo cha mgogoro huo ambao unaendelea katika umoja huo wa vijana
 
“Taarifa za kinachoendelea Arusha katika umoja wa vijana tayari ila tumeshatuma timu maalumu ya kuchunguza ni nini hasa kinasababisha vurugu hizo”Alisema Mapunda 
 
Aidha Mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku ameshangazwa na utaratibu uliotumika kuwaita katika kikao cha Sekretarieti unaotarajiwa kufanyika kesho ambapo alidai wajumbe walitumiwa mualiko kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno(sms)
 
Kuhusu kikao cha kesho (leo) kilichoitwisha na Sekretarieti ya mkoa chini ya Katibu wake Mary Chatanda, mwenyekiti Meitinyiku alisema utaratibu uliofanyika kuwajulisha wajumbe kuhusu kikao hicho ni wa ‘kihuni’ kwa kuwa walitumiwa taarifa kwa ujumbe wa simu badala ya kujulishwa kwa barua kama inavyotakiwa.
 
 “Nashangaa kwa kweli nimetumiwa ujumbe mfupi wa maneno na Gerald Mwadalu tuliyemsimamisha kuwa kesho kutakuwepo na mkutano wa sekretarieti ya Mkoa sijajua kikao hicho kitahusu nini hasa ila pamoja na hayo haizuii mimi kutohudhuria”alisema Meitinyiku
.
Aidha alisisitiza kikao walichokifanyacha baraza la vijana mkoa na  kuwatimua Katibu wa UVCCM Mkoa Gerald Mwadalu kilikuwa sahihi licha ya kudaiwa kuwa kilikuwa kikao feki kwa kuwa idadi ya wajumbe walikuwa wametimia
 
Mwadalu akizungumza jana alisema kuwa kila kitu kitajulikana kwenye kikao cha (leo) cha Sekretarieti ya Mkoa kwamba hawa wanapata wapi nguvu za kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na taratibu za umoja wa vijana.
 
Kwa sasa aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa muda Daniel Kayongo kutoka Longido(Habari na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Diamond:Sasa Naoa Rasmi,HARUSI UWANJA WA TAIFA

Diamond:Sasa Naoa Rasmi, Harusi Naweza Ifanyia Uwanja wa Taifa Kila Shabiki Ashuhudie

Udaku Specially on Saturday, August 23, 2014
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.

“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.

Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.

“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.

“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”

Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”

Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.

Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.

“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.

Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.

“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.

“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.”

Friday, 22 August 2014

UCHAMBUZI WA LEO:IJUE CHUNYA NA UTAJIRI WAKE

SAUTI KUTOKA NYIKANI.... MULUGO, MWANASIASA MREFU KAMA UTAJIRI WA CHUNYA MBEYA

MBUNGE WA JIMBO LA SONGWE PHILLIPO MULUGO.

NA GORDON KALULUNGA
MWAKA 2011, Mwandishi Mubelwa Bandio, aliwahi kuandika kuwa, anatamani angekuwepo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili ayaone yanayotendeka hivi sasa.
Alisema tamaa yake ni kuhusu uchumi wa dunia unakoelekea na namna mataifa yanavyochukua umiliki wa uendeshaji wa shughuli muhimu za kiuchumi kisha anaishia kujiuliza kama hii si sehemu ama aina mpya ya ujamaa?
“Kama Baba wa Taifa Mwl Nyerere angekuwepo, basi angeweza kurejea kusema mawili matatu ambayo alishawahi kusema miaka kadhaa iliyopita na ambayo yamekuwa katika hotuba zake na nukuhu zilizopo sehemu mbalimbali” anasema Mubelwa.
Anaendelea kwa kusema kuwa, anatamani angekuwepo akaona viongozi wetu wa sasa ambao hawawezi kusimamisha mapigano mpaka watishiwe na mataifa fulani, ama wawekewe vikwazo na fulani.
Katika andiko la makala yangu wiki iliyopita ukurasa huu, kuhusu baadhi ya wajumbe wa Bunge la katiba kutoka Chadema na kurejea Bungeni, lilileta maoni mengi na ninawashukuru wasomaji wote waliopiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.
Kabla ya Bunge hilo kuisha, nitaleta takwimu ambazo wengi hawataki kuzisikia ili mradi wahalalishe walichokisikia/wanachokitaka kuhusu serikali tatu, na hapo nitakumbusha neno “ukweli mchungu” la Mhariri wa Mtanzania Jumapili, Ratifa Baranyikwa.
Kwa leo sauti hii inatokea katika nyika ya wilaya ya Chunya mkoani Mbya.
Aliyekuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Philipo Mullugo, kabla hajaangukiwa na jumba bovu la uteuzi mpya, alikuwa akionekana mchapa kazi na jambo hilo halina ubishi, labda ubishi uwe kwenye siasa chafu zinazoendelea kuishi hapa nchini.
Mulugo ni Mbunge wa Jimbo la Songwe, wilayani Chunya mkoani Mbeya. Mwonekano wake ni kiongozi kijana, umbile lake ni mwembamba na mrefu wa kutosha.
Katika wilaya hiyo ya Chunya kuna majimbo mawili ambayo ni Jimbo la Lupa linaloongozwa na Mbunge, Victor Mwambalaswa na linaloongozwa na Mulugo, liitwalo Jimbo la Songwe.
Historia inaonesha kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya kubwa kuliko zote nchini Tanzania.
Wilaya hiyo ina kilomita za mraba zipatazo 29,219 tarafa 4, kata 30 vijiji 73 na idadi ndogo ya watu wapatao 290,478.
Chunya ilianzishwa kwenye miaka ya 1948 na wakati huo ikiwa kama makao makuu ya wilaya ya Mbeya.
Wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya za zamani au za mwanzo na zenye historia kubwa na ya pekee nchini.
Upekee wake unaazia kuwa ni wilaya ambayo imesahaulika kimaendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo misitu ya mbao na dhahabu.
Enzi za ukoloni wakati nchi ikijulikana kwa jina la Tanganyika, waingereza walichagua wilaya ya Chunya kuwa makao makuu ya jeshi la polisi katika eneo la mgodi wa Saza(mine).
Sababu kubwa ya kuchagua eneo la mgodi wa Saza au Saza Mine kuwa makao makuu ya polisi katika koloni la Tanganyika ilikuwa ni kulinda maslahi ya dhahabu.
Sehemu nyingine za machimbo ya dhahabu katika wilaya hiyo zilikuwa zinasimamiwa na wakoloni, na maeneo hayo ni Chunya mjini, matundasi na Makongorosi.
Wilaya ya chunya imepata umaarufu wa kuwa eneo la kwanza hapa nchini kuleta wachimbaji madini katika maeneo ya Saza na Matundasi kutoka nchi za Northern Rhodesi kwa sasa Zambia na South Africa yaani Afrika kusini.
Enzi za ukoloni kabila wa wawemba kutoka Zambia na makaburu(Boers) kutoka Afrika kusini, ndiyo watu waliokuwa wakifanya kazi za migodini kwasababu walikuwa ndiyo wataalamu.
Utaalamu wao unaelezwa kuwa ulitokana na sababu kwamba nchi zao zilikuwa na migodi mingi ya shaba, dhahabu, Almasi na makaa ya mawe.
Hadi leo hii ukienda Matundasi, Chunya mjini na Saza utawakuta Wawemba wengi ambao zama hizo walitoka Zambia na kwa sasa wamebakia kuwa walowezi.
Marais wa zamani wa Afrika kusini Frederick deKlerk na Pietha Botha wote walizaliwa katika eneo la mgodi wa Saza wilayani Chunya kati ya miaka 1938 na kuendelea.
Viongozi hao mashuhuri baadaye walisoma shule katika sekondari ya Iyunga iliyopo Jijini Mbeya, ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kwa jina la Mbeya European School(shule ya wazungu) kati ya miaka ya 50.
Rais wa Zamani wa Namibia Sam Nujoma na akina Thabo Mbeki, wamewahi kuishi Matundasi katika kambi ya wapigania uhuru iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Tumbu.
Wilaya hiyo ya Chunya, ndiyo wilaya ya kwanza kuwa na kiwanja cha ndege na huduma za benki Tanzania, lakini mpaka sasa ni wilaya ya inayoonekana change kati ya wilaya tisa za mkoa wa Mbeya na wananchi kukosa huduma za kijamii.
Hapa hakuna mchawi, bali mchawi wa wilaya hiyo ni serikali yenyewe ambayo inaelezwa kuwa viongozi wengi wa nchi hii ama kwa kuingia ubia na makampuni ya watu wengine, wanaendelea kuila Chunya.
Wananufaika na rasilimali za wilaya hiyo hasa upande wa madini aina ya dhahabu na mbao za asili.
“Kuliwa” kwa Chunya hakujaanza leo, bali ni miaka mingi tangu enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Sauti hii ya nyikani, ndiyo maana imeamua kufananisha urefu wa Mbunge Mullugo na utajiri wa mkoa wa Mbeya, ambapo serikali ikiamua, wilaya ya Chunya itakuwa na maendeleo marefu kama alivyo Mullugo.
Mwandishi anapatikana kwa simu 0754 440749

KATUNI YA LEO:CHAMA ukitoa HERUFI YA KWANZA Inabaki nini?

PICHA YA SIKU:WATU WALIVOJAA KUMUONA RAIS WAO KIKWETE

HABARI NA PICHA:KIKWETE NDANI YA JONGOO LA TAZARA MOROGORO

RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO‏

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini  Mhe Innocent Kalogeris na KAtibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro.
Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri (kulia) na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro . Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri zawadi ya picha ya jengo la makao makuu ya TAZARA akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na umati mkubwa wa watu baada ya kuwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika mkoa wa Morogoro.
PICHA NA IKULU