Tuesday, 19 August 2014

MAREKAN NA UBAGUZI WA RANGI:Mapigano yazuka upya Missouri

Mapigano yazuka upya Missouri

 19 Agosti, 2014 

Rais Obama amehimiza kuwe na utulivu
Maafisa wa polisi huko Marekani walirusha mabomu ya machozi ili kutawanya halaiki ya watu waliokuwa wakiandamana , kwa usiku mwingine, katika mji wa Ferguson, jimbo la Missouri kupinga mauaji ya kijana mweusi.
Maandamano yalitibuka saa chache baada ya hotuba ya Rais Obama akisihi raia kuwa watulivu.
Chanzo cha maandamano hayo ni kuuawa kwa kijana mmoja mweusi, aliyepigwa risasi na maafisa wa polisi tarehe 9, mwezi huu.
Michael Brown, ambaye hakuwa na silaha yoyote, alipigwa risasi mara sita na polisi waliomshuku kuwa alikuwa ametekeleza wizi wa kimabavu katika duka moja mjini Ferguson.
Mwanasheria mkuu wa Marekani anatarajiwa kuzuru mji wa Ferguson atakapokutana na maafisa wanaopeleleza mauaji hayo.
Gavana wa Missouri Jay Nixon aliidhinisha kutumika kwa kitengo maalum cha polisi wa kuzima ghasia waliotumwa eneo hilo hapo jana ili kusaidia juhudi za polisi kurejesha amani, huku amri ya kutoruhusiwa kutoka nje iliyotangaza mwishoni mwa wiki iliyopita ikiondolewa.
Kuuwawa kwa Brown na askari mzungu kulizusha wasiwasi kati ya watu wa rangi tofauti katika eneo hilo, Ferguson, lililo na jamii yenye wakazi wengi weusi.
Afisa wa polisi Darren Wilson alimpiga risasi Michael Brown juma lililopita baada ya kumsimamisha kwa kutembea barabarani, kulingana na ripoti zilizotolewa.
Afisa mkuu wa polisi Ron Johnson, anayeendesha operesheni hiyo ya Ferguson, alisema maafisa wa polisi walilazimika kuingia mjini humo siku ya Jumanne, baada ya waandamanaji kuwashambulia kwa bunduki na kuwarushia mabomu ya petrol na machupa huku watu wawili wakipata majeraha ya risasi.
Alisihi waandamanaji kufanya maandamano yao nyakati za mchana ili kuzuia “baadhi ya wahalifu” kuanzisha vurugu kimakusudi.
"Yeyote ambaye amewahi kushiriki katika maandamano kama haya anafahamu kuwa kuna hatari nyakati za usiku: maandamano ya usiku huruhusu wahalifu wachache kujificha miongoni mwa halaiki ya watu na kujaribu kuleta vurugu,” Jonson alisema.
Maafisa wa polisi wakiwakamata waandamanaji Ferguson
Maafisa wa usalama pia waliamuru wanahabari kuondoka baada ya waandamanaji walikataa kutoa vizuizi barabarani.
Ushahidi wa video unaonyesha maafisa wa polisi wakiwakamata waandamanaji kadhaa, huku msururu wa maafisa wa polisi waliojihami wakiingia kukabiliana na umati wa watu waliojawa na hasira.

Matukio Ferguson

  • 9 Agosti: Michael Brown apigwa risasi na afisa Darren Wilson.
  • 10 Agosti: Machafuko yaanza kutokota baada ya watu kukesha kwa ajili ya mauaji yake .
  • 11 Agosti: FBI yaanzisha uchunguzi wa mauaji ya kijana huyo.
  • 12Agosti:Wasiwasi yaenena, huku maafisa wa polisi wakitumia mabomu ya machozi na risasi za raba kutawanya.
  • 15 Agosti: Maafisa wa polisi watoa kanda ya video inayosemekana kuonyesha Brown akiibakatika duka Fulani.
  • Video hiyo ilikera waandamanaji hata zaidi na kusababisha mapigano mapya kati ya raia na polisi.
  • 16 Agosti: Missouri yatangaza hali ya tahadhari na kutoa amri ya kutotoka nje katika mji wa Ferguson.
  • 17 Agosti: Gavana Jay Nixon atuma kitengo maalum cha polisi wa kukabiliana na ghasia.
  • 18 Agosti: Uchunguzi ulioagizwa na familia ya Brown wadhibitisha alipigwa risasi sita, mbili za kichwani.
Mpigapicha anayefanyia shirika la Getty, ni mmojawapo ya waliotiwa nguvuni, hata hivyo aliachiliwa huru baadaye.
Katika taarifa ya hapo awali, mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder alisema “atazuru eneo hilo binafsi” hapo kesho ili kupatana na wapelelezi kutoka kwa ofisi ya uchunguzi FBI na waendesha mashtaka.
"Watu wanataka kufahamishwa yaliyojiri na kupelekea Michael Brown kuuawa, lakini nasihi raia wawe watulivu huku tukiendeleza upelelezi,” bwana Holder alisema.
Pia alisisitiza kuwa uchunguzi huo “ulikuwa hatua ya muhimu ili kurejesha imani kati ya watekelezaji wa sheria na jamii, sio tu katika eneo la Ferguson, bali hata katika maeneo mengine.”
wakati huohuo Rais Obama alielezea kuwa anaelewa “hisia za mapenzi na hasira” zinazozushwa kufuatia mauaji ya kijana huyo.
Matukio kulingana na nyakati
Lakini alisema,vitendo vya hasira, “kuiba au kujihami kwa bunduki, au hata kushambulia maafisa wa polisi, ni vichochezi vya ghasia zaidi.”
Rais Obama alisema alitambua kuwa katika jamii nyingi nchini Marekani “kulikuwepo na “ghuba la kutoaminiana” kati ya wakazi na watekelezaji wa sharia.
"Katika jamii nyingi, vijana wengi wa rangi huwachwa nyuma na hutazamwa kuwa watu wa kuogofya,” Rais Obama alisema.
Hapo awali, familia ya Michael Brown ilimtumia daktari mmoja, kufanyia uchunguzi wa mwili wa Micheal.
Daktari huyo, Michael Baden, alisema kuwa aliamini kuwa Brown alipigwa risasi sita.
“Brown angeweza kuishi hata baada ya majeraha hayo yote ya risasi, lakini risasi aliyopigwa kichwani ilisababisha kifo chake,” alisema.
Rais Obama amehimiza kuwe na utulivu
Daktari Baden alisema hakukuwepo na dalili zozote za mapambano, kwani huenda alipata chembe za kutu usoni alipoanguka kwenye veranda baada ya kupigwa risasi.
Aidha Baden aliamini kuwa afisa Wilson hakumpiga risasi Brown akiwa hatua za karibu naye, kwani hakukuwepo na masalio ya baruti kwa mwili wa Brown, ishara kuwa afisa huyo alikuwa zaidi ya futi mbili mbali na Brown.
Mashahidi wamesema kuwa Brown alipigwa risasi akiwa ameinua mikono yake juu akiwa amesalimu kwa amri, huku maafisa wa polisi na wanaomtakia mema Wilson wakisema kuwa Wilson alifyatua risasi wakipigana na Brown.
Afisa huyo aliyempiga bwana Brown risasi, Darren Wilson, aliachishwa kazi bila malipo kufuatia mauaji hayo, huku familia ya bwana Brown ikitoa wito akamatwe na kufunguliwa mashata .
Uchunguzi mwingine utafanyiwa mwili wa Brown na idara ya haki ya Marekani, kuongezea kwa makadirio ya Baden na maafisa wa County ya St. Louis.

Monday, 18 August 2014

ECONOMY WAR:U.S vs CHINA


DUMISHA AMANI KWA NAFASI YAKO....






hii ndo NCHI ILIYOJIWEKEA MIPAKA yenyewe kwa ridhaa ya wananchi.....IPENDE TANZANIA
Image result for Bendera ya tanzania

BONGO MOVIE UNITY...KIMENUKA TENA kisa MBUMBA...

Kimenuka Tena Bongo Movie, Steve Nyerere Adaiwa Kula Fedha za Club Hiyo

August 18, 2014
KIMENUKA! Klabu ya Bongo Movie Unity imedaiwa kuingia kwenye mpasuko mkubwa baada ya baadhi ya viongozi kutangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amechikichia mtonyo (fedha) mwingi wa klabu kwa masilahi yake

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya klabu hiyo, juzikati viongozi wote wa klabu hiyo walikaa kikao kilichoitishwa na katibu wao, William Mtitu ambacho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumwajibisha Steve Nyerere kwa madai hayo.

“Kuna fedha zilikuwa ni za maandalizi kwa ajili ya dua ya wasanii waliofariki dunia iliyofanyika Jumamosi.
“Pia kuna fedha nyingine zilitolewa hivi karibuni, walizitafuna akina Steve na baadhi ya viongozi, kilinuka kishenzi,” kilisema chanzo.

Imeelezwa kuwa katika kikao hicho, hawakufikia muafaka kwani mtuhumiwa (Steve Nyerere) hakutokea pasipo kujulikana sababu za kutofika kwake.
Chanzo kiliendelea kudai, baada ya Steve kutoonekana, baadhi ya viongozi walisusa na kuondoka ambapo Katibu Msaidizi wa Bongo Movie, Devotha Mbaga na Mwekahazina Msaidizi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ walitangaza kuachia ngazi endapo muafaka wa fedha zinazodaiwa kuliwa kinyemela hautapatikana.

“Bongo Movie ni kivumbi mtindo mmoja kwa sababu baadhi ya viongozi walio karibu na Steve wanadaiwa kuchikichia fedha nyingi tu, kitu ambacho kinazua mtafaruku kwani siyo mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho.

Mtitu ambaye ni katibu wa klabu hiyo, alipohojiwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kutokea ambapo alisema hata yeye amejipanga kuachia ngazi endapo hatapewa ufafanuzi wa fedha zinazodaiwa kuliwa na mwenyekiti wao.

Steve Nyerere alipopigiwa simu kwa lengo la kuulizwa juu ya madai hayo, simu yake iliita bila majibu. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.

UNADHANI HUYU BINTI ANA MIAKA MINGAPI???

Rais Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha 4, Neema Mtwanga mwenye umri wa miaka 16 wa shule ya Sekondari Naboti iliyopo mkoani Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa Insha katika shindano lililoandaliwa na SADC.
Picha: Rais Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha 4, Neema Mtwanga mwenye umri wa miaka 16 wa shule ya Sekondari Naboti iliyopo mkoani Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa Insha katika shindano lililoandaliwa na SADC.

kama umefurahishwa na ushindi wa binti huyu, tupia 'HONGERA' yako hapa tumpongeze.

KUPATA KAZI NI KAZI:AJIFANYA WA KIKE ILI AWE HOUSEGIRL...

Mwanaume Aliye Jifanya Mwanamke na Kupewa Kazi ya House Girl Akamatwa

August 18, 2014
Mwanaume mmoja huko nchini Uganda Amekamatwa baada ya Kujifanya ni Mwanamke ili apate kazi ya House Girl, Zoezi lake hilo lilifanikiwa na kuweza kupata hiyo kazi lakini siku zilivyozidi kwenda Boss wake ambae ni Mama Mwenye Nyumba alishtukia mchezo na kugundua ni Mwanaume, Baada ya kugundulika jamaa alichukua kipigo kutoka kwa Majirani , alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo alijitetea akasema Maisha ni magumu na kupata kazi kama mwanaume ni ngumu...

UKIONA HIVO UJUE MWANAUME ULIYENAE HAKUPENDI au alichokitaka hajakipata.

Mwanaume Akishakupata Baada ya Muda Mfupi Upendo Wote wa Awali Huisha

August 18, 2014
Hiyo ni kauli kutoka kwa baadhi ya wanawake.

Je kauli hiyo ina ukweli kiasi gani?

Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi ya wanawake hawaijui. Hii ni ile yakudhani kwamba, mwanaume akishaanzisha uhusiano na mwanamke au wakioana, kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile kile milele. 

Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba, binadamu ana hisia na hisia hizi huweza kuchoka. watu wanapokaa pamoja au wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa muda mrefu, hufikia mahali ambapo kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa maana kwamba, zimechoka.

Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa yako ambaye umekuwa ukitamani aje kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa muda fulani kwako, zile cheche za hamu zinapungua, wala bila kukosana au tatizo lolote? 

Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani, ule 'mchecheto' wa awali kukihusu,hupungua au kwisha. Ni suala la hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu hukipendi tena. Kama mwanamke halijui jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba, mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo kauli kama:

''Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali huisha''

Haya ni malalamiko ya wanawake katika kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii. wanashindwa kujua kwamba, kabla ya kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa pamoja kwa muda mwingi

Ni mwongo anayeweza kusema kwamba, katika mahusiano yake au ndoa yake hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa mwenzake kushuka angalau kidogo. kuna kutofautiana tu katika viwango vya kushuka kwa hisia hizo. lakini kila binadamu hisia zake za upendo hushuka.

Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa huenda ni maumbile, sababu nyingine ni uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa kauli nzuri kwa mpenzi wake katika mahusino. lakini pia utayari kwa kila mmoja kuondoa zile tabia ambazo mwenzake anasema zinamkera.

Kushuka kwa hisia za upendo hakuna maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo unapoondoka umeondoka, lakini hisia za upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa na hali ikarejea kama zamani tu. wakati mwingine hurudi zenyewe kama zilivyopotea.

Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za upendo za wenzi wao zinapopotea,hubabaika na kuharibu mambo.

DIAMOND NA SEPETU ni KAMA CHRISS BWIZZO NA RIHANNA....


Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya

Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.

TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala la Wema kukashifiwa liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Wema wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa Instagram kwamba ni kwa nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno jukwaani (hivi karibuni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya kumfungulia biashara ya maana?

“Tujaribuni kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu Diamond. Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno namna ile kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye ni mfuasi wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa kumshauri ‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonesha Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata mauno jukwaani kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.

WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau hao walimtaka Wema kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy Sumari (2005), Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi kwa jinsi wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza kuendesha maisha yao bila kudhalilishwa majukwaani.

WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata mauno.

DIAMOND AWAJIBU
Baada ya wadau hao kumshauri Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo walidai yanamdhalilisha, kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond alishindwa kuvumilia ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka wake unaodaiwa kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond alieleza kwamba yeye kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu kama mpenzi wake na suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.

WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri ningewaona kweli mna akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu (Wema) kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe, mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. “Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo anatakiwa aamue kunywa maji!

“Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu, nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”

WAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya waraka huo, mashabiki na wadau waliopo kwenye mtandao huo walimgeukia Diamond kwa kumlaumu kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona amemfungulia dada yake Esma Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa akimtumia tu bila faida yoyote?

MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana na waraka huo, aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika wa kwake na kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.

MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada ya meneja huyo kubwanga manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na penzi hilo la mwanaye ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha hivyo anaacha ‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.

“Jamani sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao wazungushane wee mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo imemchanganya.

TUJIKUMBUSHE
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
GPL.

WAKIMBILIA MAHAKAMANI KUPINGA BUNGE LA KATIBA kuendelea

Sasa ni Bunge la katiba Mahakamani.

Screen Shot 2014-08-18 at 10.08.07 AM
Wakati kamati zikiendelea kufanya kazi yake kwenye bunge la katiba Dodoma, bado kumekua na mvutano kuhusu bunge hilo kuendelea au kutoendelea kutokana na Wajumbe wa UKAWA kukosekana.
Wakati hayo yakiendelea kuna ripoti imetoka kwenye gazeti la Mtanzania, ikisema  bunge hilo sasa kuburuzwa Mahakamani kesho August 19 2014 na chama cha Wanasheria Tanganyika kikitaka Mahakama kuzuia vikao vya bunge hili kuendelea hadi muafaka wa taifa utakapopatikana ili kupata katiba bora kwa Wananchi.

REST IN PEACE....

Watu 4 Wafariki Kwa Kuangukiwa na Jiwe Wakiwa Wamelala

Monday, August 18, 2014
Watu wanne wa familia mbiili tofauti wakazi wa mtaa wa Nyerere A, eneo la Mabatini jijini Mwanza wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala.
Tukio hilo limetokea majira ya saa Nane usiku wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha.
EATV imefika katika eneo la tukio na kushuhudia wananchi wakishirikiana na jeshi la uokoaji na zimamoto pamoja na askari polisi wakiendelea na kazi ya kufukua miili iliyonasa chini ya jiwe kubwa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza Hassan Maulid amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.
Kaimu kamanda wa jeshi la uokoaji na zimamoto mkoa wa Mwanza inspekta Augustino Magere amewashauri wakazi wa jiji la Mwanza waishio maeneo ya milimani kuchukua tahadhari ili kuepusha maafa kama yaliyojitokeza.
Wakisimulia tukio hilo katika hali ya majonzi na simanzi, baadhi ya wakazi wa mtaa huo wa Nyerere A, wanaeleza namna walivyoupokea msiba huo mkubwa.
Huyu ndiye mtoto pekee aliyenusurika kifo baada ya wazazi wake kufariki dunia kufuatia nyumba yao kuangukiwa na jiwe kubwa.

Rais Kikwete Amepoteza Dira......PROF:LIPUMBA

Lipumba: Rais Kikwete Amepoteza Dira

Monday, August 18, 2014
Profesa Lipumba alisema Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kusimamia ahadi zake, hali inayochangia kupwaya kwa utawala wake.

Akifafanua hoja yake, mwanasiasa hiyo alisema, “Katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2011 ambapo pia alianzisha mchakato wa Katiba, alisema kutakuwa na kituo cha kufua umeme cha megawati 300, kutakuwa na Kinyerezi (I) ya megawati 200, megawati nyingine 200 za makaa ya mawe na uzalishaji wa umeme kwa upepo.

“Hadi sasa imeshapita miezi 36, hakuna hata kimoja alichomaliza kukitekeleza, kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi (I) kinaendelea kujengwa.”

“Kwa jumla, Kikwete ameshapoteza dira ya maendeleo kwa kipindi cha miaka tisa alichokaa madarakani, hivyo sioni cha kumshauri. Alisema tangu Kikwete aingie madarakani, hakuwa na ajenda maalumu ya maendeleo, ndiyo maana nchi imeendelea kuwa maskini.

“Kwa sasa, Rais Kikwete amebakiza muda wa mwaka mmoja, hakuna la kutegemea. Kwanza, hakuwa na mtazamo au dira ya kufanikisha mambo, kwa hiyo kwa mwaka huu mmoja huwezi kutegemea kuwa ataleta mabadiliko makubwa,” alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba, akirejea utawala wa kiongozi wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alisema kuwa utawala wa Kikwete umeshindwa kuwa na nidhamu ya fedha kiasi cha kuzorotesha uchumi.

“Ili uweze kusimamia maendeleo ya nchi yetu, ni lazima uwe na matumizi mazuri ya fedha za umma na uwe na Serikali inayosimamia vizuri matumizi na malengo yaliyowekwa,” alisema msomi huyo wa nyanja ya uchumi.

“Rais Mkapa alikuwa na nidhamu ya utendaji wa Serikali kibajeti, kwa sababu alikuwa akitumia bajeti ya fedha taslimu. Ilitumika kuleta nidhamu kwa kuwa fedha zilizokuwapo, ndizo zilizotumiwa.

“Tatizo kubwa ambalo limejitokeza katika kipindi hiki… Bajeti kwa ujumla wake, ule mgawanyo wa kila wizara haukuwa na mwongozo mzuri wa nini Serikali itatekeleza. Tatizo hilo lilikuwa ni muhimu kwa awamu ya mwanzo kuleta nidhamu katika matumizi ya ujumla yalingane na mapato, lakini hilo jambo limeendelea mpaka leo.”

Chanzo: Mwananchi

KAULI YA UWOYA JUU ya DIAMOND na ndoa YAKE...

Diamond Hajavunja Ndoa Yangu-Irene Uwoya

Monday, August 18, 2014
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka  katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live na kusema kuwa yeye hajaachana na mumeo wa ndoa na wala msanii Diamond Platnum hajavunja ndoa yao kama ambavyo baadhi ya watu na vyombo vya habari walivyokuwa wakisema.
Uwoya ameweka wazi suala hilo baada ya mashabiki wengi kutaka kujua kama ameachana na mumeo ndikumana na ndipo hapo amekanusha kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Diamond Platnum wala Msanii Msami Baby kama ambavyo watu wamekuwa wakijua ni wapenzi bali amesema kuwa yeye na msanii Msami ni marafiki wa karibu na sasa wanafanya filamu ya pamoja.


MAREKAN KAMA BONGO TUI:GAVANA AWAAMURU POLISI KUTUMIA MABOMU

Missouri kuwatumia National Guard

 18 Agosti, 2014 

Missouri kuwatumia National Guard kuzima ghasia
Jimbo la Missouri Marekani limeamua kuwatumia maafisa wa kitengo maalum cha National Guard'' ilikuzima maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea mjini Fergusson kwa muda sasa tangu auawe kijana mmoja mwenye asili ya Kiafrika na polisi wa mji huo.
Gavana wa jimbo hilo Jay Nixon alitia sahihi amri ya kuwatumia kitengo hicho maalum kinachutumika tu wakati wa Vita na majanga ilikukabili utovu wa usalama katika jimbo hilo la Ferguson.
Maandamano yamezidi kwenye mji huo wa Ferguson, licha ya kuwepo kwa amri ya kutotoka nje ambayo imekiukwa kwa usiku wa pili mfululizo.
Missouri kuwatumia National Guard kuzima ghasia
Polisi katika jimbo hilo wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za raba ilikukabiliana na wenyeji waliokasirishwa na mauaji ya kijana mmoja ambaye anashukiwa kuwa alikuwa ni mwizi wa kimabavu.
Maafisa wa polisi wa Ferguson, katika kitongoji cha St Louis, walisema walishambuliwa na hawakuwa na “na jinsi mbadala” ila kujibu tu.
Cpt Ron Johnson anayeongoza operesheni hiyo huko Ferguson anasema kuwa waandamanaji waliwatupia mabomu ya kujitengenezea pamoja na chupa zaidi ya saa tatu kabla ya marufuku ya kutotoka nje kuanza rasmi.
Kitengo maalum cha National Guard kutumiwa Missouri
Mauji ya kijana huyo Michael Brown ambaye alikuwa amehitimu shule ya upili na ambaye alipigwa risasi na askari mzungu imetibua kovu la ubaguzi wa rangi katika karne ya 21.
Uchunguzi wa kwanza wa mwili wake unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa risasi mara sita ikiwemo risasi mbili zilizoingia kichwani kulingana na ripoti ya New York Times.
Mkuu wa sheria nchini Marekani Eric Holder ameagiza uchunguzi kufanyika upya kwa mwili ya mwendazake.

UBAGUZI:WAPINGA NDOA YA MUARABU NA MYAHUDI isifanyike

Wapinga ndoa kati ya Muarabu na Myahudi

 18 Agosti, 2014

Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha kuolewa na mwanamume Mwarabu raiya wa Israeli.
Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama.
Bwana harusi , Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikaha yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo.
Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo .
Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo.
Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.
Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.
Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.
Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo.
Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu.
"Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26.
Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.

HUYU NDO mwanamke MWENYE BICYCLE CONTROL..Tazama picha yake.



Picha: Huyu dada ni moja ya wanawake wanaojitafutia riziki zao, hapa amebeba mzigo wa chakula kwenye ndoo kwaajili ya kwenda kuuza. Je, wewe unampa maksi ngapi huyu mama kwa shughuli zake za kujitafutia riziki kupitia njia hii?

A: 100
B: 75
C: 50
D: 25
E: 0
huyo ni MAMALISHE AKIWA KABEBA CHAKULA

HUYU NDO MPENZI mpya wa LULU

Lulu Wajibu Wanaosema Hawezi Kumpata Justin Bieber, Asema Ukichukia Ukale Mbegu za Malimao

August 18, 2014
Muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu anaendelea kuonesha hisia zake kwa Justin Bieber na sasa ameeleza kuwa atakuwa anamuandikia ujumbe kila Jumatatu.

Kupitia Instagram, Lulu amepost picha ya JB akiwa kifua wazi akipiga kinanda na kuandika ujumbe akiwajibu wale wanaodai kuwa anaota ndoto za mchana na kwamba hatampata.



Mapemaaaa...Kabla cku haijawa ngumu..! Haya ni hv wale wa kuandika ndoto za nn cjui...Mara cjui huwezi kumpata na cjui kimepanda kimeshuka...msinijazie comment😂😂😂Acha niwape ufafanuzi kdgo...ni hv Huyu Bwana swala ya yy kupenda....nimemwachia awapende kina @selenagomez na wengine wote anaotaka kuwapenda...ila swala la yy kupendwa Aniachie Mimi....yan hyo kazi yangu....!!!

Sasa Kama ni ndoto Wallah ctaki kuamka,Kama ni ufala...yani ninaukubali kwa asilimia 150%,na mengine mengine yote...sasa Kama nakuchefua,Nina uhakika Zile ndimu za @diamondplatnumz haziwezi kukutosha mana hiki kichefuchefu co cha kuisha,bora utafute mbegu ya Malimao au mbilimbi upande kwako kbsa....Na hili Zoezi ni endelevu...yani kila Jumatatu...Kama Mshahara vile....!!! #MCM...... #Nilikuwepo
Written by udaku specially.

HUYU NDO MMAKONDE ANAYEISHI UJERUMANI...MTAZAME ALIVYO

Azuiwa kuingia Dubai akihofiwa kuwa mchawi

 18 Agosti, 2014

Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe
Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake, Rolf Buchholz amekatazwa kuingia Dubai.
Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453 ikiwemo usoni mwake na ana pembe mbili juu ya paja la uso wake.
Rolf Bushholz aliyenyimwa ruhusa ya kuingia Dubai.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa ameratibiwa kuandaa onyesho katika klabu moja mjini humo.
Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.
Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake
Alieleza wanahabari wa Press News Agency kuwa hapo awali alikuwa amekubalika lakini baadaye akarejeshwa kabla ya kufika eneo la maafisa wa usafiri ndipo akarejeshwa katika ndege iliyokuwa ikielekea mjini Instabul Uturuki.
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.
Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz ulivyotogwa

Maafisa wa mgahawa huo wa Fairmont Dubai wamesema kuwa walifanya chochote kadri ya uwezo wao kumuingiza Buchholz nchini Dubai lakini hawakufua dafu.
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.

Sunday, 17 August 2014

katuni ya leo:RAFIKI YAKO NDO ADUI YAKO

ALIKIBA FOR REAL:"SINA UGOMVI NA DIAMOND MIE"

Alikiba: Nawaomba watu Wasinikosanishe na Diamond, Sina Ugomvi Naye!

Udaku Specially on Sunday, August 17, 2014
Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

Bongo5

ALIKIBA FOR REAL:"SINA UGOMVI NA DIAMOND MIE"

Alikiba: Nawaomba watu Wasinikosanishe na Diamond, Sina Ugomvi Naye!

Udaku Specially on Sunday, August 17, 2014
Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

Bongo5

JE,HII NDO NGUVU YA MWANAMKE KATIKA NDOA...?

Ndoa Nyingi za Kizazi Hiki Zinavunjika Kwa Sababu za Kijinga, Nguvu ya Mwanamke Katika Ndoa

Written By Udaku Specially on Sunday, August 17, 2014 
POWER OF A WOMAN IN MAKING THE MARRIAGE WORK!

1st Lesson SOMETIMES A WOMAN WINS BY LOOSING! Unaweza mwanamke ukajiona umepoteza kitu ila in reality umeshinda! Na unaweza kuona umeshinda ila in reality umepoteza. Usiendekeze hisia za moyo zinavokuongoza na wapambe! Tumia akili na busara zaidi! Mfano unapewa data mumeo yuko guest kafumanie, kuliko kwenda na kumuita shigongo kuvunja utu wako na wa mumeo na kutia doa maisha yenu shukuru tu taarifaa, mpe mumeo benefit of the doubt sali kwa Mungu wako. Kuchapiwa ni siri ya ndani indeed! Usimchunguze mumeo kama CIA au KGB sababu ukitafuta sanaa kitu utakipataaa! Manake wanawake kuna tabia unamfatilia una withold eveidence hiku unaikusanya hadi uhakikishe siku ukimsomea mashtaka hana pakutokea ushahidi unatosha kuconvict. Hahahaaaaaa!

2nd Lesson! BY NATURE MARRIAGE IS SELF DESTRUCTORY, LOOK FOR SOLN TO MAKE IT WORK! Yaani nature yenyewe mambo ya kumkinai mwenzio, kutamani vipya, ni natural tu, hayahitaki hata sababu, sasa baada ya kuwa mtu wa lawama, kulaani kwanini mambo kama hayo yawatokee, kumuona mwenzio hana shukrani, spend more time kudeal na situation kuliko mwenzio. Kama uzazi umekubongesha work out, acha kula hivo. Kuliko kudemand the impossible kuwa sababu umemzalia akupende hivo hivo kwenye jimwili jipya sio rahisi. Shirikiana kutafuta soln.

3rd Lesson USISAHAU HATA SIKU MOJA AT A POINT LIFE YOU WERE HIS NUMBER ONE NDO MAANA AKAKUOA! Hata kama anakunyanyasa saivi, heshima haipo, anachepuka, labda wewe upo number 100 saivi not even once dont let you forget once upon a time you were his number 1, he married you, yes you na mapungufu yote yako, not Lily the cutest, mima the big as.s, Rose the beauty queen etc, wote aliwaona yet still akakuona wewe ugly betty or whatever! Tatizo ni kujisahau, wakati anakuoa you might have been ugly still lakini una heshima, upo humble, etc sasa umo ndani ndo unajifanya king kong atakwambia nini si ushindani hamna! Ukiona mambo magumu rudi back in the days ujiulize ulimloga vipi wakati ule umloge tena!

4th Lesson UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILE ILE! Unakuta mtu unamuacha mumeo kisa muhuni ana michepuko? Mwanaume gani asie na michepuko? Hahahaaa! Utamuacha wa kwanza utatafuta 2, wembe ule ule, utahangaika mpaka basi! Kabla hujamuacha mumeo kisa michepuko jiulize nani hachepuki utaempata? Au mimeo hela hana! Hata unaemkuta nazo zaweza kusiha vile vile. Tulia vumilia unyolewe. Wenzio wote wametulia wewe unajilegeza! Ifike mahala fumba macho uombe Mungu siku ziende maana hata ukisema uende kwingine mwendo ule ule! Unamuacha mumeo unaanza kuiba wa wenzio! Akili matope hayo?

5th Lesson KABLA HUJAPANIC KWA JAMBO MOJA KUMBUKA MEMA YAKE ELFU MOJA NDO UAMUE KUHUSU HIKO KIMOJA! Mtu kakuoa miaka 5, anakupa yote utakayo, anakiabudu malkia wake, hakuna unachokosa, shabash kateleza kidogo shetani kampitia sisi wote binadamu kakusoea kachepuka one time! Basi wewe. Unasahau mema yoooooote ya 5 years huko kumshika ndo unafunga mabegi na kutokomea! Khaaaaa! Au mmeishi vizuri miak 7, mwaka huu ndo kabadilika, japo uvumilie na kuomba atambue makosa na kujirudi miaka yote 7 watia kwenye dustbin, unashupalia matendo yake mwaka huu na kudai talaka! Sasa na mwanaume mda mwengine nae anakereka anaona kama wema wake wa miaka 7 sio issue basi nendaa tu! Power of love sio kufaidi goodtimes ni kuhimili mikimikiki! Wapambe nuksi kina lara 1 tunakutia ndimu ondoka bwanaa, kwanini afanye hivo, ndo unakole kweli kweli. Usiruhusu tendo moja la kijinga likupotezee 7 yrs of your life n hard work! Kwani ukisamehe hilo fumanizi utababuka? Vitakuuma vitapoa mnaanza upya! Hatoki mtu inaitwa! Atafanya visa wee akikuona mkomavu atachoka mwenyewe!

6th lesson! JIFUNZE KULET THINGS GO! Sio basi ukimfumania mara moja kila akikosea kidogo unamshikia kooni ile ugoni wa mwaka juzi. Kitu kidogo unaretrieve file! Au ulimsaidia mwaka juzi alipokwama, akikunyima hela kidogo unakumbushia, mwaka juzi fyoko fyoko! Daaah! Sio issue. Inatakiwa uwe mkomavu ukisema umesamehe kitu basi ndo unakizika kooni forever! Haukitaji tena! Unamuepusha shaitwani kukaa kati kati yenu kila wakati! Unavomsamehe mara nyingi inaondoa hata ile ladha ya kukusoea tena! Sababu anajua utamsamehe na wala hutomuuliza tenaaa! Mwenyewe anajistukia. Ananza kuona kweli huyu si binadamu wa kawaida, labda namtendea ndivo sivo.

7th lesson! MUME NAE BINADAMU LOLOTE LINAWEZEKANA! Usiwe na expectations kubwa sanaaaaaa! Ukamuona yule malaika labda hawezi kukosa. Aaaaah! Wapi! Jua tu yule binadamu kupitiwa inawezekana pia, na hata akipitiwa unajua umejipanga kusort hizo issue out kuendeleza libeneke! Ila kama ndo ulikuwa unamuona mungu mtu, siku akiteleza waweza kuga kwa pressure! Wakati cha ajabu hamnaa mbona! Kwani ye wa kwanza kufanya hivo? Au wa mwisho? Hamnaaaaa!

By Lara 1

Gari lililobeba Maiti Kumi za Mafunzo Laua Wawili Mikese

Gari lililobeba Maiti Kumi za Mafunzo Laua Wawili Mikese

Udaku Specially on Sunday, August 17, 2014

KUPITA peter msigwa 2015 IRINGA MJIN NI NDOTO....ONA UONGO WA CCM

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM )MKOANI IRINGA KIMEWEKA WAZI KAZI WALIZOZIFANYA KWA KUWA WAO NDIO WALIOLETA MAENDELEO YA MANISPAA YA IRINGA NA SIO MBUNGE WA JMBO HII MCH:PETER MSIGWA



Akihutubia wananchi wa mkoani iringa katika soko la kuu la manispaa ya iringa meya wa manispaa ya iringa AMANI MWAMWINDI alisema kuwa yeye ndiye anaye saini mikataba yote inayoleta maendeleo katka jimbo hili na sio kweli kama amabavyo mbunge wa jimbo hili peter msigwa kuwa maendeleo ya manispaa ya iringa.

MWAMWINDI kwa kuyaongelea maeneo ambayo serikali imeyafanyia kazi na yameleta maendelo katika manispaa ni pamoja na kutengeneza barabara zote kwa njia ya rami na kukalabati zile zote zilizokuwa zinahitajika kukalabatiwa kwa lengo la kuleta maendeleo katika manispaa.

pia MWAMWINDI alisema iringa inafanya vizuri upande wa elimu na usafi kwa kuwa wamejipanga toka zamani kwa kamati mabalimbali zilizokuwa zinakuja kukagua usafi katika maeneo ya manispaa wamekuwa wakiisifia kwa kuwa kila mwaka wanafanya mabadiliko ya kimaendeleo.
naye  katibu wa chama cha mapinduzi mkoani iringa HASANI MTENGA alimtaka mkurugezi kumuondoa halaka afisa SUMATRA KONDO kwa kuwa amekuwa akiwanyanyasa madereva wa daladala.bodaboda na bajaji hivyo hafai kuwa kiongozi kwakuwa anafanya kazi kwa faida yake mwenyewe.

HUYU NDO MWANAMKE MWENYE KIUNO KIDOGO DUNIANIIII?

Cathie Jung  ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. Yumo miongoni mwa watu kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness world hakika hii inashangaza kimtindo.

HILI NDO DONGO LA MASANJA kwa DIAMOND NA WEMA

Soma alichoandika Masanja Mkandamizaji kuhusu uhusiano wa Wema na Diamond
WEMA
Masanja mkandamizaji mchekeshaji kutoka kundi la Komedi Orijino kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake juu ya uhusiano wa Wema Sepetu na Diamond.
Hiki ndicho alichoandika,”Hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. Kama wangekuwa watu wa kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta????
Rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib unamapungufu yako. Na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika.
Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! Sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! Nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisikie vibaya.

Saturday, 16 August 2014

cheka na katuni:NIMEMISS MATUSI YA BUNGENI...Mjadala lini tena????

MAN UNITED YALAMBWA 2-1 KWA SWANSEA ' OT'

Matokeo ya Manchester Utd vs Swansea City haya hapa

IMG_6442.JPG
Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Barclays Premier League imeanza rasmi leo hii kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Manchester United dhidi ya Swansea City.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde katika dimba la Old Trafford, United imeendelea pale pale ilipoachia msimu uliopita kwa kupoteza mechi ya kwanza kwenye dimba la nyumbani kwa kipigo cha magoli 2-1.
Swansea ndio walikuwa wa kwanza kuona nyavu za United kwenye dakika ya 28 kipindi cha kwanza kupitia Ki Sung, kabla ya Wayne Rooney kusawazisha dakika 58.
Huku United wakiwa wanatafuta goli la pili, kinda Tylor Blackett akapoteza mpira kwa Wilfred Bony na kusababisha goli la pili lilofungwa na
Sigurdsson.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Swansea 2-1 Man uTD.
Hiki ndio kipigo cha kwanza kwa United katika mechi ya ufunguzi wa EPL tangu mwaka 1972.
Man Utd (3-4-1-2): De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Lingard (Januzaj (24min), Fletcher, Herrera (Fellaini 67), Young; Mata; Hernandez (Nani 46), Rooney.
Subs: Kagawa, Michael Keane, Amos, James.
Goal: Rooney 53.
Booked: Blackett, Young.
Swansea (4-2-3-1): Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor (Tiendalli); Ki, Shelvey; Routledge, Sigurdsson; Dyer (Montero 67), Bony (Gomis 77).
Subs: Tiendalli, Montero, Tremmel, Bartley, Richards, Sheehan.
Booked: Dyer, Taylor, Shelvey.
Goals: Ki 28, Sigurdsson 72.
Referee: Mike Dean (Wirral).

KATUNI ZA MICHEPUKO HIYO


CHEKA NA KATUNI